Baraza la mawaziri kutangazwa wakati wowote-Ikulu!!

Ikulu imetoa taarifa rasmi kwamba baraza jipya la mawaziri liko jikoni na sasa litatangazwa muda wowote kuanzia sasa..taarifa hiyo imeongeza kwamba baraza hilo litakua lina ubora wa hali ya juu sana.

Chanzo:gazeti mwananchi.

Matumaini ni kitu muhimu sana kwa mwanadamu kwani humfanya mwanadamu aendelee kuamini kuwa kesho itakuwa siku njema kuliko leo au jana hata kama hajawekeza chochote. Hivi ni kipi ambacho kitaletwa na baraza jipya la Mawaziri kama taratibu, mifumo ya utawala, katiba na nguvu za utawala bado ziko chini ya mtu yule yule?
 
Bora tu aache hawahawa, angalau tayari wana magorofa na nyumba mbezi beach. Wakija wapya wanaanza upya kujenga magorofa na kununua apartments...

Mkuu umenichekesha. Nikikumbuka Maige alivyokuwa akibembeleza pale Bungeni na kumtanguliza Mungu nadhani akiachwa atakuwa ameogopa kweli hatafanya mchezo!
 
Watanzania bwana tuna kazi kweli kweli. Wazungu walikaa wakatumia ubongo wao wakagawanya mwaka katik miezi, mwezi katika wiki, wiki katika siku, siku pia ikagawanywa katika saa, saa katika dkk na dkk katika sekunde. Hii yote ni katika kurahisisha kupeana muda sahihi lakini leo tunasema WAKATI WOWOTE. Hiyo wakati wowote hauna mwezi, siku wala saa?

Mzee mzima Kimbunga, mzungu mwenyewe aliukuta wakati. Mungu ndiye aliyeweka majira na nyakati zilizopo. Ila nakubaliana na wewe in sense that wazungu wanajua kutumia muda na sie tunauchezea tu....
 
Ikulu imetoa taarifa rasmi kwamba baraza jipya la mawaziri liko jikoni na sasa litatangazwa muda wowote kuanzia sasa..taarifa hiyo imeongeza kwamba baraza hilo litakua lina ubora wa hali ya juu sana.

Chanzo:gazeti mwananchi.

Kama hiyo Cabinet, itakuja na Prof. Lipumba kama Waziri wa Fedha na Dr. Magufuli kama PM, ubora wake bado utakuwa mashakani. Prof. Lipumba japo si Mbunge, lakini anaweza kuteuliwa na kisha kuapishwa June 12 kwenye Bunge la Bajeti.
 
Mkuu Polisi una maana ile ya tender board!!! Manake watu wakitaka kupitisha manunuzi yao ya kimagumashi wanatumia circular resolution; inanikera hii.

Kwenye manunuzi, circular resolution mimi huwa naiona ni nzuri zaidi kuliko kikao. Pamoja na kuwa na gharama kidogo pia inatoa uhuru zaidi kwa mjumbe kutoa mawazo yake akiwa ametulia na ikiwezekana kutafuta vifungu kwenye vitabu
 
....mama migiro atateuliwa kuwa waziri na ataanza kazi mwezi wa saba...wizara yake itabaki wazi mpaka atakaporudi...kwani wizara ya mwandosya inaongozwa na nani kwa muda wote ambao ni mgonjwa?....
 
Kama hiyo Cabinet, itakuja na Prof. Lipumba kama Waziri wa Fedha na Dr. Magufuli kama PM, ubora wake bado utakuwa mashakani. Prof. Lipumba japo si Mbunge, lakini anaweza kuteuliwa na kisha kuapishwa June 12 kwenye Bunge la Bajeti.

Nafikiri utaratibu ni kuteuliwa UBUNGE ndipo unaapishwa katika kikao cha bunge, kinachofuata ni kuteuliwa kuwa waziri na vinginevyo. Naomba kuelimishwa zaidi juu ya utaratibu
 
Tetesi ni kwamba wengi wenye uwezo waliopendekezwa wanakataa hizo position....
 
Unaapa kwenye kikao cha kwanza cha mkutano wa kwanza wa bunge baada ya kuteuliwa. Siyo ukae na spika tu akuapishe Mkuu.
Kiapo cha
Wabunge
Sheria ya
1984 Na.15
ib.13
68
". Kila Mbunge atatakiwa kuapishwa katika Bunge kiapo cha
uaminifu kabla hajaanza kushiriki katika shughuli za Bunge; lakini
Mbunge aweza kushiriki katika uchaguzi wa Spika hata kabla
hajaapishwa"

Kwenye manunuzi, circular resolution mimi huwa naiona ni nzuri zaidi kuliko kikao. Pamoja na kuwa na gharama kidogo pia inatoa uhuru zaidi kwa mjumbe kutoa mawazo yake akiwa ametulia na ikiwezekana kutafuta vifungu kwenye vitabu

Weeee Polisi hakuna kitu kama hicho! Kwanza ukiona circular resolution inapitishwa ujue tayari manunuzi yameishafanyika ila tu Board inatumiwa kubariki tu. Kwanza huwa hakuna muda wa kufikiri wajumbe wanakuwa wamesimamiwa ili wasaini.

Hii tuongee kwingine manake nina mengi katika hili. Hapa tujikite tu kwenye subra ya baraza.
 
Last edited by a moderator:
Kiapo cha
Wabunge
Sheria ya
1984 Na.15
ib.13
68
". Kila Mbunge atatakiwa kuapishwa katika Bunge kiapo cha
uaminifu kabla hajaanza kushiriki katika shughuli za Bunge; lakini
Mbunge aweza kushiriki katika uchaguzi wa Spika hata kabla
hajaapishwa"

Sawa Mkuu OSOKONI Vipi kuhusu kuwa Waziri?
 
Last edited by a moderator:
as long as serikali ni ile ile ya ccm wala sivutiwi na porojo za baraza jipya wakati chama ni kile kile mijitu ile ile itakuwa recycled tu km zee la gombe aka wassira, lukuvi hawa ghasia yaani full mazingaombwe
 
Ni vema akatangaza mapema, maana sasa havi kazi hazifanyiki katika mawizara... nimetembelea wizara mbili tatu jana watu wako restless na mawaziri wa sasa pia.
Halafu, hivi kwa nini Rais amiamue yeye mwenyewe kufanya mabadiliko ya baraza kimya kimya badala ya kufanya advert kwa mba atafanya mabadiliko!!! hii inanishangaza sana
 
Mzee mzima Kimbunga, mzungu mwenyewe aliukuta wakati. Mungu ndiye aliyeweka majira na nyakati zilizopo. Ila nakubaliana na wewe in sense that wazungu wanajua kutumia muda na sie tunauchezea tu....
Elisha Ray Ule wakati wa Ikawa Asubuhi Ikawa Jioni? Sawa Mkuu
 
Last edited by a moderator:
Hayo yote yatafanywa lakini nionavyo mimi kinachotakiwa hapa ni uzalendo ambao utafufua maadili kwa viongozi wa ngazi zote wakiwemo hawa watakao tangazwa upya, ili watusaidie kuifikisha nchi hii sehemu ambayo Hayati baba wa Taifa,Mwl. J. K Nyerere alitarajia ifike. Wewe moyoni kwako tafakari nn kimefanyika kutoka katika Kipindi cha utawala wa Mwalimu JK mpaka sasa katika utawala wa JK (from JK to JK). Jiulize: Yaliyofanyika kwa kipindi hicho chote ndio mwl. JK aliyokusudia yafanyike. Tanzania imepotoka au inakwenda katika njia sambamba na wazo la mwl. JK? Wazo langu "UZALENDO WA VIONGOZI KATIKA NGAZI ZOTE NDANI YA NCHI YOYOTE HUZALISHA MAADILI NA HIVI KUWA NA UADILIFU WA KAZI WAZIFANYAZO." Ukiwa mzalendo utakuwa mwadilifu na hapo utakuwa na uchungu wa nchi na pia kuwa mbali na kukemea kabisa yule mwenye wazo la kuifisadi nchi. Kwa kutenda hivyo tutaondokana kabisa na kila msamiati unaozuka kila kunapoitwa leo, mara rushwa, mara takrima,mara ufisadi, mara uepa nk. Aidha masomo ya MAADILI yangeanza kufundishwa kutoka shule za msingi, sekondali na hata vyuoni ili kuwazalisha watanzania ambao watakuwa na uchungu wa nchi yao kwa namna yoyote ile. Taifa lingeelekeza nguvu zake katika kuwaandaa viongozi wa kesho katika kufanya hayo ili walau kuirejesha Tanzania katika utanzania wake halisia ambao Mwl. JK angetarajia auone kama Mwenyezi Mungu angemfufua leo hii.
Huo ndio mtazamo nambari moja katika kuleta maendeleo ya nchi yetu Tanzania.
 
Back
Top Bottom