Baraza la mawaziri kutangazwa wakati wowote-Ikulu!!

Hayo yote yatafanywa lakini nionavyo mimi kinachotakiwa hapa ni uzalendo ambao utafufua maadili kwa viongozi wa ngazi zote wakiwemo hawa watakao tangazwa upya, ili watusaidie kuifikisha nchi hii sehemu ambayo Hayati baba wa Taifa,Mwl. J. K Nyerere alitarajia ifike. Wewe moyoni kwako tafakari nn kimefanyika kutoka katika Kipindi cha utawala wa Mwalimu JK mpaka sasa katika utawala wa JK (from JK to JK). Jiulize: Yaliyofanyika kwa kipindi hicho chote ndio mwl. JK aliyokusudia yafanyike. Tanzania imepotoka au inakwenda katika njia sambamba na wazo la mwl. JK? Wazo langu "UZALENDO WA VIONGOZI KATIKA NGAZI ZOTE NDANI YA NCHI YOYOTE HUZALISHA MAADILI NA HIVI KUWA NA UADILIFU WA KAZI WAZIFANYAZO." Ukiwa mzalendo utakuwa mwadilifu na hapo utakuwa na uchungu wa nchi na pia kuwa mbali na kukemea kabisa yule mwenye wazo la kuifisadi nchi. Kwa kutenda hivyo tutaondokana kabisa na kila msamiati unaozuka kila kunapoitwa leo, mara rushwa, mara takrima,mara ufisadi, mara uepa nk. Aidha masomo ya MAADILI yangeanza kufundishwa kutoka shule za msingi, sekondali na hata vyuoni ili kuwazalisha watanzania ambao watakuwa na uchungu wa nchi yao kwa namna yoyote ile. Taifa lingeelekeza nguvu zake katika kuwaandaa viongozi wa kesho katika kufanya hayo ili walau kuirejesha Tanzania katika utanzania wake halisia ambao Mwl. JK angetarajia auone kama Mwenyezi Mungu angemfufua leo hii.
Huo ndio mtazamo nambari moja katika kuleta maendeleo ya nchi yetu Tanzania.

Binti hakika umenena.
 
Weeee Polisi hakuna kitu kama hicho! Kwanza ukiona circular resolution inapitishwa ujue tayari manunuzi yameishafanyika ila tu Board inatumiwa kubariki tu. Kwanza huwa hakuna muda wa kufikiri wajumbe wanakuwa wamesimamiwa ili wasaini.

Hii tuongee kwingine manake nina mengi katika hili. Hapa tujikite tu kwenye subra ya baraza.

Asante kimbunga kwa uzoefu wako. Nitakutafuta unipe kidogo A,B, C za hii njia ya kupitisha manunuzi. Back to the topic, hivi inakuwaje watu wanafurahia sana wenzao kuondolewa uwaziri? Je wabaya ni mawaziri au mfumo uliopo ndo mbaya?. hivi kweli tumefikia mahali tunajadili watu badala ya kujadili mifumo? Hatuwezi kufika. Yaani people are eager to hear fulani katoswa!
 
Okay mkuu. Whoever aliyekaa awe mzungu, mmisiri ama mwarabu ila aligawa ili tupate kupeana muda muafaka. Ila Mkuu MAKOLE kumbuka mimi natumia Gregorian Calendar.

Ni sawa, nimekusoma rafiki Kimbunga. Falsafa ya Kiafrika kuhusu suala la wakati iko hivi: Waafrika hawawezi kuisaliti asili yao kama ambavyo rangi ya ngozi ya mwafrika isivyoweza kusalitiwa. Vivyo hivyo katika hofu yao juu ya jambo fulani. Kwa Mfano; Falsafa ya Kiafrika kuhusu mwanamke iko hivi, Mwanamke siku zote anatazamwa kama kitulizo cha mwanamume, hata wenyewe wanalijua hilo. Mwanamume anatazamwa kama ndio kichwa cha nyumba, kama nyumba ina wanawake wengi wakubwa, halafu ikatokea kuwa mwanamume ndiye mwenye umri mdogo kuliko wote, pakitokea nyoka mahali hapo tegemea kuwa mwanaume ndiye atakayeitwa kumuua nyoka. Kuhusu muda, Waafrika tunautambua muda kwa matukio. Kuna wakati uatambulika kama Mafungulia Ng'ombe, kuna wakati tunaangalia Jua, Hii inamaanisha kuwa huo ndo wakati kwa asili ya Mwafrika. Ndio maana hatuna muda maalum. Nikikwambia nitakuja mafungulia ng'ombe, namaanisha ni kuanzia saa 3-4 na nusu asubuhi, Hivyo nitarajie muda wowote kati ya 3-4 asubuhi. Nikichelewa hupaswi kunilaumu kwani hiyo ndio asili yangu; wala hupaswi kunilaumu kwa kusema " Waafrika Bwana.....hawajali muda" Hiyo ndio asili yetu na hatuwezi kuisaliti. Huo ni mtazamo wangu Finyu sana Rafiki yangu Kimbunga, kama niko op naomba yeyote yule anisahihishe.
 
Ngoja tusubiri huo upya wa baraza la mawaziri na huo ubora wa hari yajuu.
Lakini kwa swala la ubora wa hari ya juu si tegemei kabisa labda siyo baba riz
 
Huyo Mama Hana Jipya!! Naona kama Vuvuzela Tu!! Tunayo maeneo Machache ambayo Mungu ametujalia yakawa planned!! Kama sinza na Mikocheni!! Huyu Mama ameshindwa hata kwenda kufanya Law reinforcement ili watu wote walioziba njia kwa kuweka Groceries na biashara nyingine wapishe Njia!! Sasa anachofanya wala mbona Hatukioni? Bora apingwe Chini!!
msisahau system ya utawala wa Bongo ilivyo. Kwa bongo na nchi nchi nyingi zinazoendelea, Raisi ndiye kila kitu. Raisi ndio ambae akitaka kitu kifanyike kitafanyika, hakuna cha waziri wala nani. waziri ameteuliwa tu na raisi na kuna wavunja sheria ambao wapo katika channel ya bosi mkubwa ambao hawezi kuwagusa. bomoabomoa imemshinda hata huyo magufuli, unadhani ni kwa nini.
 
Hakuna jipya watu ni walewale bendera ni ile ile itikadi ni ile ile chama mbele utaifa nyuma km kauli yao sitegemei upya ktk utendaji kazi wa mfumo wa uwizi ulio na mizizi zaidi ya mti wa mbuyu. Sina moyo wala ari na hilo baraza la mawaziri la mafisadi. Ngoja niendelee kupambana kutafuta kipato nisije nikafa njaa.

we cant solve our problems with the same thinking we used when we created them.
 
Hivi wapinzani manataka kuingia kwenye baraza hili. Mimi nilidhani wapinzani wanajiaandaa kutwaa dola mwaka 2015?

wanaochukua dola ni cdm,ila nccr,tlp na cuf ruksa kuwemo kwenye hilo baraza,ss hatuna shida na uwaziri.
 
Elisha Ray Ule wakati wa Ikawa Asubuhi Ikawa Jioni? Sawa Mkuu

Sawa kabisa mkuu. Tatizo sisi hatujui au tunapuuza jinsi ya kutumia wakati. Mie naendelea kuusubiri huo wakati wowote waliosema Ikulu hata siujui ni upi mkuu. Si ajabu kashatengeza ila amepeleka kwa 'mababu/mizimu' Bagamoyo apate 'baraka' zao ndo maana ya huo wakati wowote!!
 
Watanzania bwana tuna kazi kweli kweli. Wazungu walikaa wakatumia ubongo wao wakagawanya mwaka katik miezi, mwezi katika wiki, wiki katika siku, siku pia ikagawanywa katika saa, saa katika dkk na dkk katika sekunde. Hii yote ni katika kurahisisha kupeana muda sahihi lakini leo tunasema WAKATI WOWOTE. Hiyo wakati wowote hauna mwezi, siku wala saa?
Afadhali umesema, nilivyoiona hii haraka nikakumbuka ule utabiri wa mvua na ngurumo za hapa na pale.
 
Hakuna mtu bora anayeweza kutoka ccm!
Si makufuli, Sitta, wala Chiligati, wote ni walewale tu!
Habari ya siku mkuu!
Vp wanasemaje ARUSHA kuhusu hii country?
Maana nina tetesi kwamba magamba yameamua kutoa mshiko kwa vijana wa Arusha ili muwapotezee cdm is it true?Maana kwa kuanzia nasikia kuna sherehe inaandaliwa pale 7x7 na itahudhuliwa na vijana tuu?Ebu tujuze mkuu ili nasi tutie timu huko.Maana kuna vyuku wa kufa mtu,mvinyo kwa kwenda mbele na nyama choma kama ile ya pale maeneo ya"JOGOO HOUSE NA PICNIC"
Hii imekaaje mkuu?ila msinunulike kwa bei ndogo........sii mnajua tena chukua chako mapema?
 
Mama Migiro yupi unaemuulizia? huyuhuyu kilaza aliyeshindwa kwa Ban Ki Moon?

Nadhani its time to change, hao walishapewa nafasi na hatukuona walichofanya.
Timu ikishindwa kwenye fainali ya klabu bingwa ya dunia haina maana itakuwa kilaza kwenye ligi ya nyumbani.
 
Sawa Mkuu OSOKONI Vipi kuhusu kuwa Waziri?

(4) Mawaziri na Naibu Mawaziri wote watateuliwa kutoka
miongoni mwa Wabunge.

56.
Waziri au Naibu Waziri hatashika madaraka yake ila mpaka

awe ameapa kwanza mbele ya Rais kiapo cha uaminifu na pia
kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake
kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge
 
ubora huo labda na mimi niwepo,,,tena,nipewe wizara ya maliasili na utalii,,,,week tu wtt wangunmmarekani,,na nahama uswahilin nenda uzungun,,


hahahaaa... tutakufilisi hadi watoto waishie 'kujilipua' huko marekani wakati wewe tumekusweka ndani. Kama itawezekana maana hao TAKUKURU watakaotakiwa kukushughulikia ni kiini macho tu kama Kilimo Kwanza..
 
Hivi Anna Tibaijuka yupo kweli?

Manake aliingia na bomoa bomoa yake halafu ghafla akawa hasikiki kama ilivyokuwa awali.

Siku zote mnafiki atabaki na ataendelea kuwa mnafiki, na atakufa kinafiki! Hii ni tabia kuu ya wale wote wenye magamba, hawawezi badilika kifikira, kimtazamo na kiutendaji!
 
Tetesi ni kwamba wengi wenye uwezo waliopendekezwa wanakataa hizo position....

Hao watakuwa wanajua namna system ilivyo na utendaji wa huyu 'faza-house' na hawaupendi ndio maana wanaona wakae mbali. Mimi nafikiri isiwe lazima mawaziri watokane na wabunge bali kuwe na mfumo unaoruhusu watu wengine kupewa hizo kazi kama ilivyo kwa wakurugenzi. Ila shida itakuwa rais anaweza kuwapa uwaziri watu wa ukoo wake wote waliosoma badala ya kufuata utaratibu.
 
CCM CCM CCM

KIDUMU CHAMA TAWALA CHA CCM!

wimbo:CCM CCM AAA........CHAMA CHA MAPINDUZI CCM NAMBA ONE.

CCM OYEEEEE....................................................
 
Back
Top Bottom