Bango laigombanisha serikali na Kampuni!

Barabara za Tanroads na Manispaa,

Siyo mjuzi sana wa hii kitu. Ila kwa UELEWA wangu ni kuwa, Dar es salaam kuna barabara ziko chini ya manispaa na nyingine (chache sana) ziko chini ya Tanroads. Hivyo kwa mabango mengi yaliyopo Dar, si kweli kuwa yako chini ya Tanrods. Hayo mabango na hela ya kodi nina uhakika wanachukua timu ya Kandoro. Ila yote yaliyoko kwenye barabara zinazoenda mikoani au nchi za jirani (kwa ujuzi wangu, naomba mnisamehe kuwa SINTAZIITA HIGHWAY, kwani Tanzania hatuna HIGHWAY), hizo ndiyo zipo chini ya Tanroads.

Ili MUELEWE tofauti ya barabara za MANISPAA na za TANROADS, siku zote za Tanroads (barabara za taifa/kimataifa) zinaitwa BARABARA au ROADS, na zile za MANISPAA huwa zinaitwa MITAA au STREET/Evenue. Nchi nyingi duniani, STREETS au MITAA huwa zinashughulikiwa na serikali za mitaa/wilaya/mkoa na ROADS & HIGHWAYS huwa zinakuwa chini ya chombo ya SERIKALI/TAIFA kinachodesign, kujenga na kutunza hizo barabara/highway zake na kwa Tz kinaitwa TANROADS.

Nafikiri sasa mtafahamu nani wa kulaumiwa katika mambango ya Dar.
 
Nadhani huu ni wakati muafaka wa kuzuzui uchafuzi wa mazingira! Uchafuzi wa mazingira ni pamoja na kuweka kitu hata kama ni kizuri mahali kisipostshili.
Uwekaji wa mabango hapa kwetu imekuwa ni holela. Mabango yanawekwa ovyoovyo tu bila hata kujali usalam. Hebu fikiria kimbunga au upepo mkali ualikumba jiji letu, hayo mabango mazito na makubwa yaliyotuzuguuka yatatusalimisha?
Hao AI Outdoor wanafanya biashara hiyo hata UINGEREZA, ila mabango wanayo weka na yanavyosimikwa ni tofauti na Bongo. Nimeshuhudia mwenyewe!
Sasa hivi hawa AI Outdoor wameingia mkataba wa kuweka taa za barabarani (streel lights) kwa maelewano ya kutolipia ushuru wa matangazo kwenye taa hizo kwa kipindi fulani! lakini kinachotia shaka ni ubora wa wa hizo nguzo za taa. Ukiziangalia nguzo zimengenezwakwa mabati mepesi ambayo yamefanywa kukunjwa kisanii kiasi kwamba ukizingatia haliya mazingira ya Dar es salaam nguzo hizo zitakuwa zimeishaoza wakati wa mkataba wa kutolipa ushuru kinaisha! Hizi nguzo na taa ni sawa na hizi zilizopo kuanzia makutano ya Morogoro Road na Bibi Titi na kuishia Maktaba! Ziliwekwa majuzi tu lakini zimeishoza chini tofauti na taa za barabara nyingine ambazo zina miaka zaidi ya 30ziko bado ukiachilia mbali zinazogongwa na madereva wazembe!
 
Mimi sioni sababu ya kulumbana sana kwenye hili nijuavyo mimi ni kwamba Hawa wenzetu (namaanisha makampuni ya matangazo) wamekuwa wakijali maslahi yao binafsi bila kutazama maslahi ya nchi na jamii kwa ujumla, unapoweka bango ilhali unajua kabisa kwamba pahala unapo liweka panaweza kusababisha madhara kwanini unasisitiza kuweka? kama si ubinafsi na ubabe nakumbuka mwaka fulani wamiliki wa A1 walisisitiza kwamba kampuni nyingine iliyokuwa ikiweka bango pale barabara ya salender kwenye njia panda upande wa salenda bridge club kuwa wanaharibu maliasili za taifa kwa kukata miti pale cha ajabu baada ya wiki mbili tukaona wao A1 wameweka maabango palepale walipowaondoa wenzao. ukiacha hilo pale karibu na zantel makao makuu kulikuwa kuwekwe bango la tv hao hao A1 wakawaondoa wwapinzani wao wakaweka la kwao. kimantiki haileti picha nzuri kampuni fulani kuwa wababe wa kutaka kila kitu kifanyike watakavyo bila kujali maslahi ya taifa hili. Siku hizi mabango yamegeuka uchafu jijini. wengi kati yetu wamewahi aidha kutembelea nchi za wenzetu ama kutazama luninga utakuta mabango yanapamba mji huku kwetu tunashindwa hatakujua majukumu ya watu wa ujenzi na maafisa mipango miji. Hawa A1 wanajua kabisa kuwa watapenyeza rupia na mwisho wa yote watabaki walipoliweka bango hilo yote hayooooooo ni RUSHWAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA
 
Tanroads Vis a Vis Manispaa. Ni nani anayelipwa kwa matangazo hayo? Nafikiri ni manispaa, na Tanroads wanaona wao ndio walipwe. Wasilete spinning zao hapa kwa kuzungumzia flimssy issues kama hizo temporary structures ambazo ziko duniani kote.

Hawa Tanroads wanaacha kushughulika maswala muhimu ya barabara zetu --ujenzi , repea, etc wanazungumzia maswala ya kima cha chini namna hii. F*** Angalia Meneja mzima anavyotoa taswira ya kipuuzi ---BANGO LAIGOMBANISHA SERIKALI NA KAMPUNI. I hate such too low f*** ing thinking and acting of some personalities in the government who think all Tanzanians are always mbumbumbu kama walivyo wao. STOP .

Kama bazabara ni ya manispaa, ok manispaa ndo wahusike but kama barabara iko under tanroads then manispaa hawana authority of any thing andif there is money paid 4 matangazo ambayo at the end of the they are not beneficial; for road users we dont need them! Weka reguratory signs,information signs and directional sign bwana acheni usanii Tanzania!
 
Aisee hao jamaa wa outdoor ni waajabu sana kama hawataki kutoka kwa amri ya serikali kuna kitu ambacho wanajivunia, lakini cha msingi hata kama wana mtu anawabeba wajitahidi kutii mamlaka husika ili mambo yaende vizuri.
 
Back
Top Bottom