Balozi wa Romania nchini Kenya, awafananisha Wakenya na nyani mkutanoni

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,894
155,917

Romania kumuondoa balozi wake nchini Kenya kwa matamshi yake ya ubaguzi​

Matamshi ya balozi huyo kuwaita waafrika Nyani yameshutumiwa vikali
Afisa mmoja wa Kenya anaelezea majaribio ya ubalozi wa Romania kuficha tukio hilo kama ‘fedheha’. Photo: TRT Afrika

Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari, wizara ya mambo ya nje ya Romania imesema tayari imeanzisha utaratibu wa kumuondoa balozi wa Romania kutoka Kenya.
Wizara hiyo imesema maoni yoyote au maoni ya asili ya rangi hayakubaliki kabisa.

" Wizara ya Mambo ya nje ya Roma inajuta sana hali hiyo na inatoa pole kwa wale wote walioathiriwa," waziri wa mambo ya nje wa Romania amesema katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari, " tunalaani vikali na kulaani tabia na mitazamo yote isiyoendana na kuheshimiana."

Wizara hiyo imeendela kusema kuwa " tabia na mitazamo kama hiyo haionyeshi kwa njia yoyote thamani ya kitaasisi na kibinadamu ambayo hatua ya kidiplomasia ya wizara ya kigeni ya Kiromania inasimamia."
Balozi wa Romania nchini Kenya Dragos Viorel Tigau anatuhumiwa kutumia matamshi ya kibaguzi wakati wa mkutano wa kundi la Ulaya mashariki ambapo aliwataja waafrika kama "nyani".

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya Macharia Kamau alisema matamshi hayo "hayavumiliki na hayakubaliki katika umri wowote achilia mbali Karne ya 21 mjini Nairobi".

Katika ujumbe wake wa Twitter, Kamau alikashifu kile alichokitaja kama majaribio ya kuficha tukio hilo.
"Nimeshtushwa na kuchukizwa kusikia matamshi ya Balozi wa Rumania mjini Nairobi katika kuwarejelea wanachama wa Kundi la Afrika kama nyani wakati wa mkutano wa kundi la Ulaya Mashariki. Ni aibu kubwa kujaribu kuficha aibu hii. Hii haivumiliki na haikubaliki katika wakati wowote achilia mbali karne ya 21 jijini Nairobi," ameandika kupitia ukurasa wa twitter.

Appalled &disgusted at learning of remarks by Romanian Amb in Nairobi in reference African Group members as monkeys during Eastern European group meeting. Utter shame attempts to cover up this disgrace. This intolerable &unacceptable in any Age let alone 21 Century in Nairobi!
— Amb. Macharia Kamau (@AmbMKamau) June 8, 2023
Balozi na ubalozi wa Romania hawajazungumzia shutuma hizo. Haijulikani ni wapi na lini tukio hilo lilitokea.
Tukio hilo linaungana na orodha ndefu ya mizozo ya kidiplomasia iliyochochewa na matamshi ya wanadiplomasia wa Magharibi yanayo chukuliwa kuwa ya kibaguzi dhidi ya Waafrika.

Mwezi Januari, ofisi ya mambo ya nje ya Ujerumani iliomba msamaha baada ya kutumia emoji ya chui kurejelea ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Urusi barani Afrika.

Iliandika kwenye Twitter kwamba ziara ya Sergey Lavrov haikusudiwa kutafuta chui, bali kutumia safari hiyo kujaribu kuhalalisha vita vya Urusi dhidi ya Ukraine.
 
Nakumbuka ubalozi wa Romania Tanzania ulikuwa rafiki sana na Watanzania.

Kwa watu waliosoma shule ya msingi Oysterbay miaka ya 1980s enzi za Ceausescu wanaweza kukumbuka balozi wa Romania alivyokuwa rafiki wa shule.

Now this may sound elitist and Oysterbayish, but that is where tje ambassador lived.

Kuna matatizo mengi, racism is real, nilitaka kusema tu, kwa kumbukumbu zangu, kutoka miaka yangu ya Oysterbay, ubalozi wa Romania ulifanya kazi nzuri sana ya kutupa matumaini kwamba kunaweza kuwa na mahusiano mazuri kati ya Romania na Tanzania.

Na kwa mahusiano hayo, ambayo nakumbuka mpaka parties za nyumbani kwa balozi na kuongea na balozi na mke wake, kabla Ceausescu hajapinduliwa, mimi mwenyewe sikuona ubaguzi kuyoka muwakilishi wa watu wa Romania Tanzania.

I just wanted to stick out for the good people of Romania, na kusema kwamba, from my personal experience, this is not representative of the Romania-Tanzania relationship.

Najua watu wa Ulaya wanaweza kutupa expwriences zao.

Inawezekana kabisa Romania ilikuwa na balozi mbaya, ambaye karudishwa kwao na serikali ya Romania, na watu hawa wapo kila nchi, na Africa tunaweza kuwa na mahusiano mazuri na Romania baada ya habari hii ambayo ni mbaya sana.

Nimeandika kwa kumbukumbu zangu tu za kazi nzuri za Ubalozi wa Romania Tanzania.
 
images (2).jpeg
 
Romania kumuondoa balozi wake nchini Kenya kwa matamshi yake ya ubaguzi​

Matamshi ya balozi huyo kuwaita waafrika Nyani yameshutumiwa vikali
Afisa mmoja wa Kenya anaelezea majaribio ya ubalozi wa Romania kuficha tukio hilo kama ‘fedheha’. Photo: TRT Afrika

Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari, wizara ya mambo ya nje ya Romania imesema tayari imeanzisha utaratibu wa kumuondoa balozi wa Romania kutoka Kenya.
Wizara hiyo imesema maoni yoyote au maoni ya asili ya rangi hayakubaliki kabisa.

" Wizara ya Mambo ya nje ya Roma inajuta sana hali hiyo na inatoa pole kwa wale wote walioathiriwa," waziri wa mambo ya nje wa Romania amesema katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari, " tunalaani vikali na kulaani tabia na mitazamo yote isiyoendana na kuheshimiana."

Wizara hiyo imeendela kusema kuwa " tabia na mitazamo kama hiyo haionyeshi kwa njia yoyote thamani ya kitaasisi na kibinadamu ambayo hatua ya kidiplomasia ya wizara ya kigeni ya Kiromania inasimamia."
Balozi wa Romania nchini Kenya Dragos Viorel Tigau anatuhumiwa kutumia matamshi ya kibaguzi wakati wa mkutano wa kundi la Ulaya mashariki ambapo aliwataja waafrika kama "nyani".

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya Macharia Kamau alisema matamshi hayo "hayavumiliki na hayakubaliki katika umri wowote achilia mbali Karne ya 21 mjini Nairobi".

Katika ujumbe wake wa Twitter, Kamau alikashifu kile alichokitaja kama majaribio ya kuficha tukio hilo.
"Nimeshtushwa na kuchukizwa kusikia matamshi ya Balozi wa Rumania mjini Nairobi katika kuwarejelea wanachama wa Kundi la Afrika kama nyani wakati wa mkutano wa kundi la Ulaya Mashariki. Ni aibu kubwa kujaribu kuficha aibu hii. Hii haivumiliki na haikubaliki katika wakati wowote achilia mbali karne ya 21 jijini Nairobi," ameandika kupitia ukurasa wa twitter.

Balozi na ubalozi wa Romania hawajazungumzia shutuma hizo. Haijulikani ni wapi na lini tukio hilo lilitokea.
Tukio hilo linaungana na orodha ndefu ya mizozo ya kidiplomasia iliyochochewa na matamshi ya wanadiplomasia wa Magharibi yanayo chukuliwa kuwa ya kibaguzi dhidi ya Waafrika.

Mwezi Januari, ofisi ya mambo ya nje ya Ujerumani iliomba msamaha baada ya kutumia emoji ya chui kurejelea ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Urusi barani Afrika.

Iliandika kwenye Twitter kwamba ziara ya Sergey Lavrov haikusudiwa kutafuta chui, bali kutumia safari hiyo kujaribu kuhalalisha vita vya Urusi dhidi ya Ukraine.
Bado yupo hai hapo Nairobi?
 
Back
Top Bottom