Raila kwa Balozi wa Marekani: Kenya Sio Koloni la Marekani, Funga Mdomo wako, jiepushe na Siasa za Kenya

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,616
Kiongozi wa Muungano wa Azimio la Umoja, Raila Odinga, amemjibu Balozi wa Marekani Mchini humo, Meghan Whitman, kuwa Kenya sio koloni la Marekani na kumtaka Whitman kujiepusha na siasa za Kenya, la si hivyo Watafanya mazungumzo ili arudishwe Marekani

Hii ni Siku moja baada ya Whitman kusema kuwa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2022 ulikuwa Huru na wa Haki, na Rais William Ruto alimshinda Odinga kwa njia ya haki

Akizungumza katika Mkutano huko Eldoret amesema, "Mwishowe, nataka kumwambia balozi huyu. Acha Wakenya waendelee na mambo yao. Ikiwa Maandamano yanaweza kuleta mazungumzo kati ya Serikali na Upinzani basi kila kitu kiko sawa na Maandamano. Mwambie balozi huyu Kenya sio Marekani, Kenya sio Koloni la Marekani, funga mdomo wako au tutakurudisha Nchini kwako,"

Chanzo: Tuko Kenya
 
πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚
Omera wach matich mar akaripia emerica!πŸ€ͺπŸ€ͺπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Tungepata viongozi hata 10 Kama Hawa
Mabeberu wangejitafajari na kutuheshim sn
 
Najaribu tu kupima ubora wa Katiba zetu

Kiongozi mkuu wa Upinzani nchini Kenya mh Raila Odinga amemuonya Balozi wa Marekani nchini humo kwa kumwambia " Kenya siyo Koloni la Marekani Funga mdomo wako la Sivyo tutaomba urudishwe nchini kwenu"

Mbowe au Zitto Kabwe Kule Zanzibar wanaweza kutoa warning kama hii?

Sema Viongozi wa Chama tawala ( Muungano) Kenya Kwanza wamemkemea Raila Odinga

Au namna gani?πŸ˜„πŸ˜„πŸ”₯

Jumaa Mubarak!
 
Halafu tuchukulie kimenuka kweli huko Kenya. The same Odinga atakua wa kwanza kukimbilia pale Village Market pande za United Nations Avenue, kuomba Mwamvuli wa KidiplomasiaπŸ˜ƒ.
 
Najaribu tu kupima ubora wa Katiba zetu

Kiongozi mkuu wa Upinzani nchini Kenya mh Raila Odinga amemuonya Balozi wa Marekani nchini humo kwa kumwambia " Kenya siyo Koloni la Marekani Funga mdomo wako la Sivyo tutaomba urudishwe nchini kwenu"

Mbowe au Zitto Kabwe Kule Zanzibar wanaweza kutoa warning kama hii?

Sema Viongozi wa Chama tawala ( Muungano) Kenya Kwanza wamemkemea Raila Odinga

Au namna gani?πŸ˜„πŸ˜„πŸ”₯

Jumaa Mubarak!
That's democry and he fought for it
 
Kiongozi wa Muungano wa Azimio la Umoja, Raila Odinga, amemjibu Balozi wa Marekani Mchini humo, Meghan Whitman, kuwa Kenya sio koloni la Marekani na kumtaka Whitman kujiepusha na siasa za Kenya, la si hivyo Watafanya mazungumzo ili arudishwe Marekani

Hii ni Siku moja baada ya Whitman kusema kuwa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2022 ulikuwa Huru na wa Haki, na Rais William Ruto alimshinda Odinga kwa njia ya haki

Akizungumza katika Mkutano huko Eldoret amesema, "Mwishowe, nataka kumwambia balozi huyu. Acha Wakenya waendelee na mambo yao. Ikiwa Maandamano yanaweza kuleta mazungumzo kati ya Serikali na Upinzani basi kila kitu kiko sawa na Maandamano. Mwambie balozi huyu Kenya sio Marekani, Kenya sio Koloni la Marekani, funga mdomo wako au tutakurudisha Nchini kwako,"

Chanzo: Tuko Kenya
odinga bwana, juzi si alikua analalama ICC waje kenya kuchunguza mauaji ya polisi?
leo anamkemea balozi kwa sababu ameuweka wazi unafiki wake!

anyway, odinga ni moja ya watu wanafiki sana, demokrasia ni yeye kushinda!
 
Back
Top Bottom