Bajeti ijayo ni trilioni 15; nini maoni yako?

Ulinzi mbona kubwa sana? Vita hakuna, Idi Amini alishakufa. Shule za kata hazina walimu na nyumba. Tunashindwa kusomesha watoto wa mkulima (Akina pinda, hawatkuwepo tena). Naona cheche tupu. Kicwa kinauma sasa.Wizara ya Ulinzi Tshs 920 bilioni (USD 575 Million)

Waitoe hiyo Wizara ya Ulinzi na hapo Wa-replace Wizara ya Kilimo. au wanataka tena kwenda kununua mabomu yaliyo-expire yaje yalipuke tena?! Tuanze kuwa Serious na kilimo kama kweli tunataka kuendelea. Kwa nchi yetu ili iweze kuendelea inabdi pia na Kilimo kipewe kipaumbele. Ni Sehemu ambapo watanzania walio wengi wamejiajili (wengi wao productivity yao ni kidogo saaana).
 
hayo ni makaratasi tu,hii inayomalizika imetekelezwa kwa asilimia ngapi?

nonsense kabisa,na mwaka huu miaka 51 ya uhuru tunafanyia zanzibar,budget yake sasa,
 
Wapi Kilimo na Afya kwenye top five?
Kwa nini pesa nyingi sana kwenye wizara ya nishati na madini, madeal ya Tanesco nini?
Kwa nini all that amount kwenye wizara ya ujenzi? tunatishio gani la kiusalama kutoka nje, bora wangealot pesa nyingi kwa wizara ya mambo ya ndani.
 
Mwea, mbona sasa naona trilioni 5 tu? trilioni 10 zinaenda wapi? sababu wanasema zimetengwa trilioni 15.
 
Last edited by a moderator:
Ulinzi mbona kubwa sana? Vita hakuna, Idi Amini alishakufa. Shule za kata hazina walimu na nyumba. Tunashindwa kusomesha watoto wa mkulima (Akina pinda, hawatkuwepo tena). Naona cheche tupu. Kicwa kinauma sasa.Wizara ya Ulinzi Tshs 920 bilioni (USD 575 Million)

Tisho la alshabab na UAMSHO lazima tujiweke sawa kisilaha na kimbinu kukabiliana na llolote!
 
Ulinzi wanawapa hela nyingi mno wakati nchi ni kisiwa cha amani na utulivu
 
Waitoe hiyo Wizara ya Ulinzi na hapo Wa-replace Wizara ya Kilimo. au wanataka tena kwenda kununua mabomu yaliyo-expire yaje yalipuke tena?! Tuanze kuwa Serious na kilimo kama kweli tunataka kuendelea. Kwa nchi yetu ili iweze kuendelea inabdi pia na Kilimo kipewe kipaumbele. Ni Sehemu ambapo watanzania walio wengi wamejiajili (wengi wao productivity yao ni kidogo saaana).

Tehetehe tender hiyo ya mkuu wa kaya na familia yake. Unachezea maslahi ya watu wewe
 
Hii ndo bajeti mfu kabisa.

Unaweza kukumbuka bajeti ya mwaka gani iliwahi kuwa hai?

Chukua bajeti ilopita soma neno kwa neno kisha linganisha na hii neno kwa neno. Utagundua kilichobadilika ni tarakimu tu. Usisahau pia mfumiko wa bei uko zaidi ya 23%.
 
Naona wamewapa kipao mbele wajeshi ili wananchi wakigoma tu waadabishwe. Hii ndo Tanganyika wanaweka kipau mbele kwenye ulinzi badala ya elimu, elimu sijui ni ya ngapi. Daaaaaaaaaaa JK kaka mbona unapoteza mwelekeo? Ni kweli watoto wa masikini watasoma.
 
Unajua wameweka ulinzi ya tatu ili iwe rahisi kuchota mafungu si unajua kule huwa kuna bit (mambo ya ulinzi are unquestionable) uku wanaume wanapiga!
 
Tunaomba ukurasa unaonesha summary ya kazi na fedha iliyotengwa kwa wizara za Ulinzi na Nisahati. Ili tuwe na wigo mpana wa kuijadili.
 
only 30% ndo utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa 2011/2012?! Sasa kwa nini bajeti ya nchi imeongezeka kutoka Tirioni 13 za mwaka 2011/12 hadi Tirioni 15 kwa mwaka ujao wa fedha?! Kuna haja gani ya kuwa na 'figure' kubwa kwenye bajeti yatu wakati tukijua kabsa kuwa hatuna fedha za kutosha kutekeleza miradi iliyopangwa? sasa huwa tuna-mdanganya nani au huwa tunataka kumfurahisha nani?! kwa nini tusi-bajeti kile ambacho tuna uwezo nacho au kilichopo ndani ya uwezo wetu?! mbona sisi watanzania tunapenda sifa za kijinga namna hii?!
......??....?!:painkiller::angry::angry::angry:!! maswali mengi bila ya majibu.
 
Ulinzi mbona kubwa sana? Vita hakuna, Idi Amini alishakufa. Shule za kata hazina walimu na nyumba. Tunashindwa kusomesha watoto wa mkulima (Akina pinda, hawatkuwepo tena). Naona cheche tupu. Kicwa kinauma sasa. Wizara ya Ulinzi Tshs 920 bilioni (USD 575 Million)
TAARIFA NILIZOZISIKIA (SIO RASIMI) CHAMA CHA MAPINDUZI KITAHITAJI PESA NYINGI KWA AJILI YA UCHAGUZI WA 2015 NA KWA SASA HALIYAKE KIFEDHA SIO NZURI. WAFADHIRI WAKE (WAFANYABIASHARA WAKUBWA) WALITOA MCHANGO MDOGO KINYUME NA MATARAJIO KATIKA UCHAGUZI WA 2010 NA HUENDA WASITOE UFADHILI KABISA KATIKA CHAGUZI UJAO IKIZINGATIWA KUNDI KUBWA WANAMUUNGA MKONO EDWARD LOWASSA AMBAYE CHAMA HAKINA MPANGO WA KUMSIMAMISHA KAMA MGOMBEA URAIS KWA MJIBU WA MTOA TAARIFA SEHEMU KUBWA YA MATUMIZI YA WIZARA YA ULINZI HAYAKAGULIWI NA KWA VILE SIO RAHISI TENA KUCHOTA FEDHA BANK KUU KAMA ILIVYOFANYIKA 2005, SERIKALI IMEANZA MAANDALIZI YA KUKUSANYA FEDHA KWA NJIA HII YA KUTUNISHA MFUKO WA WIZARA HII. Kulingana na mahitaji yanayolikabili taifa kwa sasa na ikizingatiwa hatuna tishio la uvamizi maamuzi yaliyopelekea serikali kutoa kipaumbele kwa wizara ya ulinzi yanatia shaka
 
1 Huduma kwa Deni la Taifa Tshs 2.7 trilioni(USD 1.69 Billion)
2 Wizara ya Ujenzi. Tshs 1 trilioni (USD 625 Million)
3 Wizara ya Ulinzi Tshs 920 bilioni (USD 575 Million)
4 Wizara ya Elimu Tshs 721 bilioni (USD 451 Million)
5 Wizara ya Nishati na Madini Tshs 641 bilioni (USD 400 Million)

HATUWEZI KUSEMA NA KULIHUTUBIA TAIFA KUWA TUNA MPANGO MKAKATI WA KILIMO KWANZA NA TUNATAKA KULETA MAPINDUZI YA KILIMO AMBAYO INA AJIRI WATZ WENGI HUKU KIBAJETI SIO KIPA UMBELE.
HATUTAWEZA KULETA MABADILIKO HAYA TUKISUBIRI MIALIKO YA MIKUTANO YA G8 ILI TUPEWE MISAADA.

SIJAIPENDA.
 
Zitto na Demokrasia

Uchambuzi/Analysis: Bajeti ya Madeni

leave a comment »
Bajeti ya Mwaka huu 2012/2013 ni Bajeti ya Madeni

Serikali inapendekeza Bajeti ya TZS 15 trilioni(USD 8.75 Billion) katika mwaka 2012/13. Uchambuzi wa vitabu vya Bajeti unaonesha kwamba mafungu ya juu 5 kwenye Bajeti ni Kama ifuatavyo;
1 Huduma kwa Deni la Taifa Tshs 2.7 trilioni(USD 1.69 Billion)
2 Wizara ya Ujenzi. Tshs 1 trilioni (USD 625 Million)
3 Wizara ya Ulinzi Tshs 920 bilioni (USD 575 Million)
4 Wizara ya Elimu Tshs 721 bilioni (USD 451 Million)
5 Wizara ya Nishati na Madini Tshs 641 bilioni (USD 400 Million)
TOTAL TZS 5.982 Trilioni(USD 3.74 Billlion)
Chanzo: Vitabu vya Bajeti kwa Wabunge
Jumla ya mafungu haya ni sawa na asilimia 40% ya Bajeti. Kwa hiyo asilimia 40% ya Bajeti yote imepangwa kwa mafungu 5 tu. Fungu lenye kiwango kikubwa zaidi ya Bajeti kuliko vyote ni fungu 22 ambalo ni malipo kwa Deni la Taifa. Pia sehemu kubwa ya fedha zilizotengwa kwa Ujenzi na Nishati ni madeni kwa wakandarasi wanaotekeleza miradi ya miaka ya nyuma.
Hii yaweza kuwa Bajeti ya kulipa madeni zaidi kuliko Bajeti ya kuchochea maendeleo. Bajeti hii pia yaweza pia kuwa ni Bajeti ya kukopa maana jumla ya TZS 5.1 trilioni(USD 3.19 Billion) zitachukuliwa kama mikopo kwa Serikali. Mikopo ya kibiashara ambayo ni mikopo ghali sana itachukuliwa kwa wingi zaidi kuliko mwaka wa fedha uliopita.
Wabunge wanapaswa kufanya uchambuzi zaidi wa Bajeti ya mwaka huu inayopendekezwa na Serikali. Kuna haja kubwa sana ya kuharakisha kuanzishwa kwa Ofisi ya Bajeti katika Bunge na Kamati ya Bunge ya Bajeti ili kuweza kufuatilia kwa karibu, kuchunguza na kutoa taarifa kwa wabunge ili kuwezesha kuboresha Bajeti.
Misamaha yote ya Kodi na Madeni yote ambayo Serikali inaingia inabidi sasa ithibitishwe na Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi ili kuongeza udhibiti na usimamizi wa Misamaha ya Kodi na pia Deni la Taifa.
Zitto na Demokrasia
Ni jambo la muhimu kuacknoledge source mkuu!
Maajabu ni kwamba wizara nyeti kama afya na kilimo hazijapewa kipaombele. Kwenye MDGs bado tupo mbali kupunguza vifo vya mama na mtoto ( maternal and child dearhs......kilimo kwanza bado hakijapewa kipaumbele......kweli hii ni bajeti ya kulipa madeni...
 
Ulinzi mbona kubwa sana? Vita hakuna, Idi Amini alishakufa. Shule za kata hazina walimu na nyumba. Tunashindwa kusomesha watoto wa mkulima (Akina pinda, hawatkuwepo tena). Naona cheche tupu. Kicwa kinauma sasa. Wizara ya Ulinzi Tshs 920 bilioni (USD 575 Million)

Wakiweka ndogo unadhani amiri jeshi na marafiki zake akina Shimbo watakulaje?
 
Back
Top Bottom