Bajeti ijayo ni trilioni 15; nini maoni yako?

Wanajamvi kwa pamoja, heshima zenu.Nimeshwawishika kuandika uzi huu baada ya magazeti mengi ya leo kuandika bajeti ijayo ya 2012/2013 itakuwa 15trl na hapa nalinukuu gazeti la Mwananchi "BAJETI ya Serikali ya mwaka 2012/2013 inatarajiwa kutumia Sh15 trilioni katika vipaumbele saba ikilinganishwa na Sh13.5 trilioni zilizotengwa mwaka 2011/212"Suala la msingi katika uzi wangu ni hili. Hivi hii bajeti ni ya kuongeza figure tu au ina lengo la kumkomboa mwananchi wa chini? Mwaka jana wa fedha bajeti ya 13trl ni bajeti ilikuwa inaonekana kama mkombozi lakini katika bajeti hewa nadhani ile ilikuwa inaongoza.Mpaka hivi sasa taasisi nyingi za serikali zipo hoi yaani zinashindwa hata kujiendesha kwa vitu vidogo vidogo, almost kila kitu kinakwenda kwa mkopo!!!!Ukiacha hilo, miradi ya maendeleo ndiyo safari hii haikuguswa kabisa. Mingi ni kama imetelekezwa kutokana na uhaba wa fedha toka serikalini. Ikumbukwe bajeti hiyo haikutengenewa fedha ya mradi wa miaka 15 ambao ulizua balaa bungeni kwa nini uzinduliwe mwaka huu (2011/2012) lakini fedha yake isitengwe katika bajeti hiyo hali iliyoilazimu serikali kutoa majibu ya ziada.Kutokana na baadhi ya ushahidi huo nashawishika kusema bajeti ijayo ya 15trl isn just a figure but nothing.Nakaribisha maoni yenu wakuu.
Bajeti ya nchi yetu imekuwa kama kichekesho kutokana na ukweli kwamba tangu tupate uhuru nchi haijawa na kipaumbele maalumu, mara kipaumbele ni elimu baada ya mwaka mmoja kipaumble kinabadilika kinakuwa kingine. Ni wakati muafaka sasa wa kuiga wenzetu wa korea ambao waliweka kipaumble kimoja elimu kwa muda wa miaka kumi na tano mfulilizo matokea yake ni kwamba si tu korea imefuta ujinga ni kati ya mataifa bora kabisa duniani kwa kila kitu.
 
Upuuzi mwingine huo, hiyo ni bajeti ya kwenye makaratasi, serikali haina hiyo pesa, mbona bajeti ya 2011/2012 wameshindwa kutoa pesa, mpaka miradi mingi imesimama na taasisi na idara za serikali kuwa hoi mpaka karatasi wanakosa.
 
First and foremost, other than reading The Economist and Financial Times, I know very little about Economics. That said, I have more questions than answers in this topic.

Inflation rate as at July 2011 was about 11%, and as at May 2012 was about 18%. Therefore ongezeko halisi la budget ni around 0.105 trillion, i.e. 1.5 * (18%-11%). I stand to be corrected here.

Pia, ongezeko katika capital expenditure ni ONLY 0.1 trillion compared to 1.4 trillion ya revenue expenditure. It is evident we are spending very little on capital items, hivyo in the future there will be little return to finance our investments, hence a nation of beggars – indeed the apple doesn't fall very far from the tree (JK).

On the other note, how did we raise that 15 trillion? TRA wamekusanya ngapi? Mikopo kiasi gani na misaada kiasi gani?

Kwa upande wa ukusanyaji kodi, ni kiasi gani tumepoteza kutokana na misamaha ya madeni? Ni kampuni gani na watu gani waliosamehewa hayo madeni? Na kodi kubwa hukusanywa kutoka sehemu gani? Rasimali zetu zina mchango kiasi gani?

Upande wa mikopo, je tunakopa wapi? Kama ni mabenki, what is the interest rate charged? Nauliza hivyo kwa sababu, kwa mahesabu madogo tu, ukitumia the amount used to service our debts to the national debt, i.e 2.7/22 * 100 utapata around 12%. Tuseme tuchukue half of that to be the interest rate, which is 6%, utaona hii ni kubwa sana. Nchi ya ulaya inayokopa at that rate ni Spain ambayo ni bankrupt.

Pia kama tunakopa kwenye mabenki ya ndani (read commercial banks), can we please know these banks? Maana serikali inaweza kuwa inatumia ubabe kukopa pesa ambayo probability ya kurudi ni ndogo na mwisho wa siku hizi benki zitafeli – public will suffer, not CEOs nor the finance minister. Sasa can we know these "Bankias" zinazokopesha Serikali?

Upande wa misaada, kuna habari kwamba donors walifurahishwa na "utendaji na uwajibikaji" wa serikali, kwa hiyo hao donors ndio wamejipinda mpaka mwisho na kusaidia ongezeko la 1.5 trillion? $1bn?! Au zile zilikua stories tu..

Kitu kingine ninachohofia, tena sana, ni kwamba serikali ina matatizo ya pesa na wameombaomba mpaka wamechokwa, hivyo basi wameanza kula pesa za pensheni. This speaks volumes on how the pension funds have been spending their money lately. Hapo hapo, je ni kiasi gani cha fedha serikali inadaiwa na hizi pension funds in total? Juzi hapa NSSF imesema inaidai serikali 14bn kwenye ujenzi wa UDOM, most likely hiyo pesa haitarudi. Hili suala la kula pensheni solution kwa serikali itakua simple, wataongeza retirement age to 90 years, afu watatuambia tufunge mkanda. Hawashindwi! Hii ndiyo Tanzania, sijui ni Tanganyika, hata sijui but you get the drill..

Huko kwenye recurrent expenditure, jaribu kuuiliza "What are those recurrent expenditures?", the government is too big and careless. Hivi, hawa mawaziri waliotemwa na wanaoachia uwaziri wanapata benefits za wastaafu? Kidumu chama!!

Bado kuna wanaoongelea suala la EAC na matumizi ya sarafu moja. Huku gavana anasema uchumi umekua. Where is the firing squad?

Hakuna vision, ni bora liende na usanii tu. Hakuna future hapa.

Yes, I am a pessimist and I am abandoning ship!
 
Mheshimiwa Mzindakaya alipooondoka bungeni alilalama kuwa bajeti yenyewe ni yakuzinufaisha familia ziiisizofika 10!
kwa hali hii tumeliwa!ndiyo maana waona recurrent expenditure ni kubwa kama USA vile.Hakuna aliyekanusha tuhuma hiyo ya Mzinndakaya hadi leo,si SPIKA wala Salva REWYEMAMU wala Wizara ya Fedha.BAJETI?AU KIINI MACHO
 
Bajeti ya Tanzania ni ndogo sana; trilioni 15 ni sawa na dola bilioni kama 13 hivi ambazo kwa kweli hazitoshi kabisa. Yaani bajeti yetu haifikii bajeti ya Jiji la NY! Binafsi naamini tunahitaji bajeti isiyopungua bilioni 50 dola kwa mwaka na tutakuwa tunaweza kuona matokeo katika mabadiliko ya quality of life kwa watu wengi zaidi tutakapoanza kufikia bajeti ya bilioni 100 dola! Hii ya bilioni 13 ni bajeti ya wavivu wa kufikiri, wazembe wa kupanga na goigoi wa kutenda. Hatupendi kufikiri juu ya uwezo wetu!

Bajeti hii ya 13 billion inatushinda mpaka tunategemea misaada na mikopo kwa zaidi ya 50% ya bajeti sembuse hiyo ya bilioni 50?
 
How do we raise that amount of money? Mbona bajeti hii tumeshindwa kwa kiasi kikubwa kutoa hela la shughuli za maendeleo kama tulivyopanga kwenye bajeti? Tukiwa serious kukusanya kodi na kupunguza misahama na rushwa au kukwepa ulipaji kodi, labda we can achieve.

Zitakusanywa toka kwetu sisi wenyewe watanzania hasa hasa PAYE (Pay As You Earn). PAYE ni zaidi ya 30% ya pato la mfanyakazi kwa mwezi lakini makampuni kama ya madini yanalipa 4% tu. Nadhani ulizipata taarifa kwamba kule Shinyanga (ambako kuna migodi kadhaa ya dhahabu), tumbaku inaingiza mapato zaidi serikalini kuliko dhahabu! Kwa kweli inatia aibu sana.
 
kwa kweli; tuna matatizo makubwa zaidi. Bajeti hii tunaweza kuiita "uchwara" maana ukifactor corruption... basi hata kukisia actual budget inakuwa ni mbinde
 
Bajeti ya Tanzania ni ndogo sana; trilioni 15 ni sawa na dola bilioni kama 13 hivi ambazo kwa kweli hazitoshi kabisa. Yaani bajeti yetu haifikii bajeti ya Jiji la NY! Binafsi naamini tunahitaji bajeti isiyopungua bilioni 50 dola kwa mwaka na tutakuwa tunaweza kuona matokeo katika mabadiliko ya quality of life kwa watu wengi zaidi tutakapoanza kufikia bajeti ya bilioni 100 dola! Hii ya bilioni 13 ni bajeti ya wavivu wa kufikiri, wazembe wa kupanga na goigoi wa kutenda. Hatupendi kufikiri juu ya uwezo wetu!


Mwanakijiji, sina uhakika kama hii bajeti ni kubwa au ni ndogo, na wala sina uhakika kama tunatakiwa kuwa na bajeti ya Tshs 50 trillion au Tsh 500 trillion. Na hii ni kwa sababu bajeti hanipi picha tunakwenda wapi? Hapa naamanisha hii bajeti hainiambii itatutembeze 'HATUA NGAPI' katika kufikia destination Vision 2025. Kwa mfano, kama tulisema by 2025 tunataka tuwe na 70% ya households wanaopata umeme (au number yoyote) basi annual bajeti inatakiwa inipe picha mwaka huu ni households ngapi zitapata umeme na hii idadi ya households ya mwaka huu ni asilimia ngapi ya 70% ya Vision 2025. Na hii iwe ni kwa kila sector kama ilivyo kwenye dira ya taifa yaani vision 2025 na his short-term plans i.e MKUKUTA na 2011-2016 plans.

Kwa kifupi, bajeti ni sehemu ya dira ya taifa, hivyo nataka kujua kila mwaka unatakiwa utekeleze what % na mwaka huu % yake ni ngapi. Nikijua hilo ndio naweza kusema bajeti ni ndogo au kubwa. Lakini kwa miaka nenda rudi tumekuwa tunasomewa bajeti za "zima moto" hazina kichwa wala miguu na kwa bahati mbaya upinzani nao unaanza kuongea vipande ndani ya bajeti badala ya kuangalia 'development framework ya nchi.

At this stage both CCM & opposition party are feeding rubbish. Mmoja anasema jenga kilometa 5 mwingine anasema ulitakiwa 10. But hakuna anayesema mwaka huu unatakiwa ujenge kilometa X kama share yako ya kufikia malengo ya 2025. Huu ni uwendawazimu and I am really looking foward kuwasikia wote wakisoma bajeti zao.
 
Mwanakijiji, sina uhakika kama hii bajeti ni kubwa au ni ndogo, na wala sina uhakika kama tunatakiwa kuwa na bajeti ya Tshs 50 trillion au Tsh 500 trillion. Na hii ni kwa sababu bajeti hanipi picha tunakwenda wapi? Hapa naamanisha hii bajeti hainiambii itatutembeze 'HATUA NGAPI' katika kufikia destination Vision 2025. Kwa mfano, kama tulisema by 2025 tunataka tuwe na 70% ya households wanaopata umeme (au number yoyote) basi annual bajeti inatakiwa inipe picha mwaka huu ni households ngapi zitapata umeme na hii idadi ya households ya mwaka huu ni asilimia ngapi ya 70% ya Vision 2025. Na hii iwe ni kwa kila sector kama ilivyo kwenye dira ya taifa yaani vision 2025 na his short-term plans i.e MKUKUTA na 2011-2016 plans.

Kwa kifupi, bajeti ni sehemu ya dira ya taifa, hivyo nataka kujua kila mwaka unatakiwa utekeleze what % na mwaka huu % yake ni ngapi. Nikijua hilo ndio naweza kusema bajeti ni ndogo au kubwa. Lakini kwa miaka nenda rudi tumekuwa tunasomewa bajeti za "zima moto" hazina kichwa wala miguu na kwa bahati mbaya upinzani nao unaanza kuongea vipande ndani ya bajeti badala ya kuangalia 'development framework ya nchi.

At this stage both CCM & opposition party are feeding rubbish. Mmoja anasema jenga kilometa 5 mwingine anasema ulitakiwa 10. But hakuna anayesema mwaka huu unatakiwa ujenge kilometa X kama share yako ya kufikia malengo ya 2025. Huu ni uwendawazimu and I am really looking foward kuwasikia wote wakisoma bajeti zao.
If only people could understand where you are coming from, then we would be discussing the politics of growth. Lakini ukweli wenyewe unapoteza muda tuu bruff (brother).

Anyway that is may take i could be wrong maana naamini tuna mijitu mingi iliyosoma na yenye miakili isipokuwa imechukuliwa na system ya mijizi, kiasi kwamba uzalendo au hata kuja na argument za ukweli haitaki hiyo ndio Tanzania.
 
cheyo.jpg






Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC), John Cheyo
Serikali imetoa mwelekeo wa Bajeti ya mwaka ujao wa fedha 2012/2013, ambapo imependekeza kutumia Sh. trilioni 15,

huku reli, viwanja vya ndege na umeme vikipewa kipaumbele katika matumizi ya bajeti hiyo mpya.
Bajeti hiyo ni ongezeko la asilimia 11.1 la bajeti yake ya mwaka wa fedha wa 2011/2012 unaoisha mwishoni mwa mwezi huu, ambapo ilitumia Sh. trilioni 13.5.

Vipaumbele hivyo, ni miongoni mwa hatua ambazo serikali inatarajia kuchukua katika bajeti ijayo ili kuboresha miundombinu katika sekta za usafirishaji na nishati.

Mapendekezo ya serikali ya bajeti hiyo mpya ni kwa mujibu wa habari zilizopatikana ndani ya kikao cha Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi.

Kikao hicho kilichofanyika katika ofisi ndogo za Bunge, jijini Dar es Salaam jana, kilihudhuriwa na Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhan Khijjah.

Wengine waliohudhuria ni Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Juma Reli, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya na baadhi ya maofisa waandamizi wa wizara, BoT na TRA.

Kwa mujibu wa habari hizo, kati ya Sh. trilioni 15 ambazo serikali imependekeza kutumia, Sh. trilioni 5.3 ni za mkopo.
Waziri Mgimwa anatarajiwa kutangaza mapendekezo hayo ya Bajeti mpya ya serikali katikati ya mwezi huu, atakapowasilisha bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali katika mwaka mpya wa fedha wa 2012/13.

Kwa mujibu wa habari hizo, Dk. Mgimwa alitoa mwelekeo wa Bajeti hiyo alipowasilisha kwa kamati hiyo maelezo kuhusu mfumo wa mapato na matumizi ya serikali katika kikao hicho jana.

MASHANGINGI SERIKALINI MWISHO JULAI MOSI

Akiwasilisha maelezo hayo, Dk. Mgimwa alisema kuanzia Julai Mosi, mwaka huu, magari ya kifahari ya serikali maarufu kama ‘Mashangingi' yatapigwa marufuku, ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa azma ya siku nyingi ya kubana matumizi ya serikali."Ila waziri atatangaza bungeni mpango mzima," kilieleza chanzo chetu kutoka ndani ya kikao cha kamati hiyo jana.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake, ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge, ilipitisha bajeti hiyo jana na kwamba mjadala kuhusu bajeti hiyo utaendelea kesho.
Wiki iliyopita, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC), John Cheyo, aliiomba serikali kuandaa bajeti iliyokamilika na inayotekelezeka pamoja na fedha zitakayotolewa katika bajeti itumike katika matumizi sahihi katika mipango ya maendeleo iliyokusudiwa.

Alisema kinachofanyika sasa ni bajeti inayopangwa inaweza kutekelezwa kwa asilimia 90, lakini si katika maeneo ya maendeleo ambayo wananchi wanataka watekekelezewe ikiwemo sekta ya miundombinu na huduma za jamii.
Cheyo alisema baada ya bajeti fedha nyingi hutumiwa kwa ajili ya kulipa mishahara kama matumizi ya kawaida badala ya maendeleo ya wananchi jambo ambalo baadaye serikali inapokea lawama kutoka kwa wananchi kwa kutotimiziwa mahitaji yao.

Aidha, Cheyo alipendekeza katika bajeti inayotarajiwa kuanza kupitishwa mwezi ujao na wabunge ielekezwe katika miundombinu ya barabara kutokana na kuwa ndiyo kiungo kikubwa cha maendeleo ya kijamii.
Aliongeza kuwa katika bajeti ya 2012/2013 fedha za ndani zitumike zaidi kuliko kutegemea wafadhili kwa sehemu kubwa kama ilivyokuwa kwa bajeti za miaka iliyopita.

"Tukitumia fedha yetu wenyewe tunaongeza thamani ya Shilingi, hivyo serikali inapaswa kuipa kipaumbele Shilingi kuliko Dola, pia itatusaidia katika kubana matumizi ya serikali ili kufanikisha mipango ya maendeleo," alisema Cheyo.
Pia hivi karibuni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, alitangaza uamuzi wa

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuzuia vibali vya ununuzi wa mashangingi ambapo wakurugenzi wote waliopo katika ofisi yake walianza kutumia magari aina ya RAV4 ukiwa ni mkakati wa kubana matumizi ya serikali.
Lukuvi alisema hayo wakati akihojiwa na kituo cha Televisheni cha ITV katika kipindi cha dakika 45.

Alisema serikali imeanza kutekeleza mpango wake wa kubana matumizi yasiyokuwa ya msingi tangu Waziri Mkuu alipozuia vibali vya ununuzi wa mashangingi na kama ni lazima kununua gari kinatolewa kibali cha kununua gari aina ya Double Cabin au Hard Top.

"Gari lenye gharama ya Sh. milioni 200 Waziri Mkuu amefuta ambapo kwa muda mrefu sasa magari mengi yenye thamani kubwa hayanunuliwi, lakini pia matumizi ya mafuta kwa ajili ya kurandaranda yamepungua sana," alisema Lukuvi.

Alimtolea mfano Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu kwamba ameanza kutekeleza agizo la serikali ambapo wakurugenzi wote wa ofisi hiyo wameanza kununua magari ya RAV4 ambayo gharama yake ni pungufu ya asilimia 20 ya gharama ya shangingi.

Lukuvi alisema magari hayo ya kifahari yakishafikia kilometa 100 matengenezo yake kwa mwezi yaweza kuwa karibu Sh. milioni 10 na yanapokuwa makongwe matumizi yake yanakuwa gharama kubwa zaidi.
Aliongeza kuwa serikali inatarajia kuona maofisa kuanzia wakurugenzi na makatibu wakuu kila mmoja anaangalia mbinu

na mikakati ya kupunguza gharama kwenye sekta yake bila kusubiri kupewa maelekezo ili kuokoa fedha ambazo zitapelekwa kwenye shughuli za maendeleo.
Lukuvi alifafanua kuwa matarajio ya serikali ni kuona Matibu Mkuu na Mkurugenzi wanabana matumizi hadi kwenye halmashauri na kuwataka Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa wawabane Wakurugenzi ambao baadhi yao wanasafiri sana nje ya vituo vyao vya kazi.

"Ukienda kuchukua vitabu vya wageni unashangaa Mkurugenzi hajaenda hata vijiji viwili, lakini anatoka nje ya wilaya kila siku," alisema.
Habari zilizopatikana wakati tunakwenda mitamboni, zinaeleza kuwa taarifa zaidi kuhusu bajeti hiyo mpya, zinatarajiwa kutolewa leo kwa waandishi wa habari.



CHANZO: NIPASHE
 
Wanabodi naomba tuijadili hii Bajeti ya Madeni


Serikali inapendekeza Bajeti ya TZS 15 trilioni(USD 8.75 Billion) katika mwaka 2012/13. Uchambuzi wa vitabu vya Bajeti unaonesha kwamba mafungu ya juu 5 kwenye Bajeti ni Kama ifuatavyo;

1 Huduma kwa Deni la Taifa Tshs 2.7 trilioni(USD 1.69 Billion)

2 Wizara ya Ujenzi. Tshs 1 trilioni (USD 625 Million)

3 Wizara ya Ulinzi Tshs 920 bilioni (USD 575 Million)

4 Wizara ya Elimu Tshs 721 bilioni (USD 451 Million)

5 Wizara ya Nishati na Madini Tshs 641 bilioni (USD 400 Million)

TOTAL
TZS 5.982 Trilioni(USD 3.74 Billlion)

Chanzo:
Vitabu vya Bajeti kwa Wabunge Jumla ya mafungu haya ni sawa na asilimia 40% ya Bajeti. Kwa hiyo asilimia 40% ya Bajeti yote imepangwa kwa mafungu 5 tu. Fungu lenye kiwango kikubwa
zaidi ya Bajeti kuliko vyote ni fungu 22 ambalo ni malipo kwa Deni la Taifa. Pia sehemu kubwa
ya fedha zilizotengwa kwa Ujenzi na Nishati ni madeni kwa wakandarasi wanaotekeleza
miradi ya miaka ya nyuma.

Hii yaweza kuwa Bajeti ya kulipa madeni zaidi kuliko Bajeti ya kuchochea maendeleo. Bajeti hii
pia yaweza pia kuwa ni Bajeti ya kukopa maana jumla ya TZS 5.1 trilioni(USD 3.19 Billion)
zitachukuliwa kama mikopo kwa Serikali. Mikopo ya kibiashara ambayo ni mikopo ghali sana
itachukuliwa kwa wingi zaidi kuliko mwaka wa fedha uliopita. Wabunge wanapaswa kufanya
uchambuzi zaidi wa Bajeti ya mwaka huu inayopendekezwa na Serikali. Kuna haja kubwa
sana ya kuharakisha kuanzishwa kwa Ofisi ya Bajeti katika Bunge na Kamati ya Bunge ya Bajeti ili
kuweza kufuatilia kwa karibu, kuchunguza na kutoa taarifa kwa wabunge ili kuwezesha
kuboresha Bajeti.

Misamaha yote ya Kodi na Madeni yote ambayo Serikali inaingia inabidi sasa ithibitishwe na
Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi ili kuongeza udhibiti na usimamizi wa Misamaha ya Kodi
na pia Deni la Taifa.

 
Zitto na Demokrasia

[h=2]Uchambuzi/Analysis: Bajeti ya Madeni[/h] leave a comment »
Bajeti ya Mwaka huu 2012/2013 ni Bajeti ya Madeni

Serikali inapendekeza Bajeti ya TZS 15 trilioni(USD 8.75 Billion) katika mwaka 2012/13. Uchambuzi wa vitabu vya Bajeti unaonesha kwamba mafungu ya juu 5 kwenye Bajeti ni Kama ifuatavyo;
1 Huduma kwa Deni la Taifa Tshs 2.7 trilioni(USD 1.69 Billion)
2 Wizara ya Ujenzi. Tshs 1 trilioni (USD 625 Million)
3 Wizara ya Ulinzi Tshs 920 bilioni (USD 575 Million)
4 Wizara ya Elimu Tshs 721 bilioni (USD 451 Million)
5 Wizara ya Nishati na Madini Tshs 641 bilioni (USD 400 Million)
TOTAL TZS 5.982 Trilioni(USD 3.74 Billlion)
Chanzo: Vitabu vya Bajeti kwa Wabunge
Jumla ya mafungu haya ni sawa na asilimia 40% ya Bajeti. Kwa hiyo asilimia 40% ya Bajeti yote imepangwa kwa mafungu 5 tu. Fungu lenye kiwango kikubwa zaidi ya Bajeti kuliko vyote ni fungu 22 ambalo ni malipo kwa Deni la Taifa. Pia sehemu kubwa ya fedha zilizotengwa kwa Ujenzi na Nishati ni madeni kwa wakandarasi wanaotekeleza miradi ya miaka ya nyuma.
Hii yaweza kuwa Bajeti ya kulipa madeni zaidi kuliko Bajeti ya kuchochea maendeleo. Bajeti hii pia yaweza pia kuwa ni Bajeti ya kukopa maana jumla ya TZS 5.1 trilioni(USD 3.19 Billion) zitachukuliwa kama mikopo kwa Serikali. Mikopo ya kibiashara ambayo ni mikopo ghali sana itachukuliwa kwa wingi zaidi kuliko mwaka wa fedha uliopita.
Wabunge wanapaswa kufanya uchambuzi zaidi wa Bajeti ya mwaka huu inayopendekezwa na Serikali. Kuna haja kubwa sana ya kuharakisha kuanzishwa kwa Ofisi ya Bajeti katika Bunge na Kamati ya Bunge ya Bajeti ili kuweza kufuatilia kwa karibu, kuchunguza na kutoa taarifa kwa wabunge ili kuwezesha kuboresha Bajeti.
Misamaha yote ya Kodi na Madeni yote ambayo Serikali inaingia inabidi sasa ithibitishwe na Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi ili kuongeza udhibiti na usimamizi wa Misamaha ya Kodi na pia Deni la Taifa.
Zitto na Demokrasia
Ni jambo la muhimu kuacknoledge source mkuu!
 
Bunge la Taifa linaanza kikao chake cha bajeti kuanzia tarehe 12/6/2012 kazi mojawapo ni kupitia na kupitisha mpango wa bajeti wa 2011/12 na bajeti ya 2012/13.

Bajeti ya mwaka 2011/12 serikali ilikadiria kutumia 13Trilion kwa shughuli zote za maendeleo na matumizi ya kawaida. Bajeti ya 2012/13 serikali inakadiria kutumia 15 Trilion kwa shughuli zote za maendeleo na kawaida.

Katika bajeti ya 2011/12 ni 30% ya miradi ya maendeleo imetekelezwa na shughuli nyingi za kawaida hazikutekelezwa kama inavyotakiwa. Kama ni 30% ya miradi yote ya maendeleo haijataekelezwa ni kwamba itachukua miaka 3 kukamilisha miradi ambayo ilipangwa kwenye mpango kwa 2011/12.Kama ndivyo kuna haja gani kuleta miradi mipya wakati miradi ya zamani na yenye maslahi haijakamilika au kutekelezwa.

Itakuwa ni logical kama serikali itapanga bajeti ya mwaka huu kukamilisha miradi viporo yote ya 2011/12 badala ya kuibuka na miradi mipya. Lakini kuna haja ya kubaini sababu za kuongezeka kwa deni la taifa kwa kipindi kifupi ambapo sasa limefikia TZS 22 Trtilion.Kama TRA inakusanya mapato na kuvuka malengo kwa kila mwezi madeni makubwa hayo yanatoka wapi?

Rais wetu pamoja na cv yake kwamba amemaliza degree ya uchumi mie na wasiwasi na weledi hasa wa elimu yake kwa manufaa ya taifa ili.Kupigia chapuo ukopaji wa serikali kwenye mabenki ni kukaribisha kufa kwa serikali na kuongeza mfumko wa bei.

Kama urais ungeweza kubinafisishwa nafuu wakati huu tungeweza kubinafisisha ofisi ya rais wetu kwa watu kama Tonyy Blair au Gordon Brown
 
Ulinzi mbona kubwa sana? Vita hakuna, Idi Amini alishakufa. Shule za kata hazina walimu na nyumba. Tunashindwa kusomesha watoto wa mkulima (Akina pinda, hawatkuwepo tena). Naona cheche tupu. Kicwa kinauma sasa. Wizara ya Ulinzi Tshs 920 bilioni (USD 575 Million)
 
Ulinzi mbona kubwa sana? Vita hakuna, Idi Amini alishakufa. Shule za kata hazina walimu na nyumba. Tunashindwa kusomesha watoto wa mkulima (Akina pinda, hawatkuwepo tena). Naona cheche tupu. Kicwa kinauma sasa. Wizara ya Ulinzi Tshs 920 bilioni (USD 575 Million)

Hii ndo bajeti mfu kabisa.
 
Mungu Ibariki Tanzania, naona bajeti ya ki magamba na itapitishwa tu na magamba wenzao. Tatizo kubwa pia, mawazo mazuri ya wapinzani hayachukuliwa kama chachu ya maendeleo, wanajifungia huko na kuja na bajeti zao ambazo hata hazina uelekeo wa kumsaidia Mtamzania masikini kuondokana na umaskini na ujinga. :A S thumbs_down:
 
Acheni watu wale, Ni maisha tu hii ndiyo serikari yetu na ni watu tu kama wewe walioiandika hiyo Badget. Hii inchi imejaa ubabaishaji sana
 
Ulinzi imewekewa bajet kubwa maana wanajua 2014/2015, CHADEMA watakuwa mwiba. CCM wanajiandaa kukabiliana na vurugu zitakazotokana na wizi wa kura 2015.
 
Back
Top Bottom