Bajeti ijayo ni trilioni 15; nini maoni yako?

Wanabodi naomba tuijadili hii Bajeti ya Madeni


Serikali inapendekeza Bajeti ya TZS 15 trilioni(USD 8.75 Billion) katika mwaka 2012/13. Uchambuzi wa vitabu vya Bajeti unaonesha kwamba mafungu ya juu 5 kwenye Bajeti ni Kama ifuatavyo;

1 Huduma kwa Deni la Taifa Tshs 2.7 trilioni(USD 1.69 Billion)

2 Wizara ya Ujenzi. Tshs 1 trilioni (USD 625 Million)

3 Wizara ya Ulinzi Tshs 920 bilioni (USD 575 Million)

4 Wizara ya Elimu Tshs 721 bilioni (USD 451 Million)

5 Wizara ya Nishati na Madini Tshs 641 bilioni (USD 400 Million)

TOTAL
TZS 5.982 Trilioni(USD 3.74 Billlion)

Chanzo:
Vitabu vya Bajeti kwa Wabunge Jumla ya mafungu haya ni sawa na asilimia 40% ya Bajeti. Kwa hiyo asilimia 40% ya Bajeti yote imepangwa kwa mafungu 5 tu.Fungu lenye kiwango kikubwa
zaidi ya Bajeti kuliko vyote ni fungu 22 ambalo ni malipo kwa Deni la Taifa.
Pia sehemu kubwa
ya fedha zilizotengwa kwa Ujenzi na Nishati ni madeni kwa wakandarasi wanaotekeleza
miradi ya miaka ya nyuma.

Hii yaweza kuwa Bajeti ya kulipa madeni zaidi kuliko Bajeti ya kuchochea maendeleo. Bajeti hii
pia yaweza pia kuwa ni Bajeti ya kukopa maana jumla ya TZS 5.1 trilioni(USD 3.19 Billion)
zitachukuliwa kama mikopo kwa Serikali. Mikopo ya kibiashara ambayo ni mikopo ghali sana
itachukuliwa kwa wingi zaidi kuliko mwaka wa fedha uliopita. Wabunge wanapaswa kufanya
uchambuzi zaidi wa Bajeti ya mwaka huu inayopendekezwa na Serikali. Kuna haja kubwa
sana ya kuharakisha kuanzishwa kwa Ofisi ya Bajeti katika Bunge na Kamati ya Bunge ya Bajeti ili
kuweza kufuatilia kwa karibu, kuchunguza na kutoa taarifa kwa wabunge ili kuwezesha
kuboresha Bajeti.

Misamaha yote ya Kodi na Madeni yote ambayo Serikali inaingia inabidi sasa ithibitishwe na
Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi ili kuongeza udhibiti na usimamizi wa Misamaha ya Kodi
na pia Deni la Taifa.


hapo kwenye red,,,,hayo maden huwa wanapokopa ni kwa ajili yetuuu au kwa ajili yao na familia zao????mbona huwa hawatyambii kututaka ushauri,,,,,halafu kwenye kulipa husema TUFUNGE MIKANDA,,,,wao wanalegeza kwa kuvimbiwa
 
kuwa na bajeti kubwa au ndogo hakireflect maendeleo ya haraka ktk nchi au utatuzi wa matatizo yaliopo, mipango thabiti na usimamizi wenye tija ndio unaoweza kureflect reality of the budget otherwise full mbwembwe
 
Nyuma ilikuwa 9 trl
ikaja 11 trl
ikaja 13 trl
sasa ni 15 trl!

Wastani wa 2 trl kila mwaka.

Tatizo ni kuendesha serikali rasmi na ile isiyo rasmi. CCM ni serikali isiyo rasmi na wao huchukuwa kwenye recur. budget. Wanachota moja kwa moja huko hazina.

Ndo maana hakuna uwiano wa mahesabu. Angalia mapato ya TRA yanavyopotelea hewani bila kufika Hazina. Mapato ktk madini yasivyo endana na mahesabu halisi toka ktk makampuni. Yote hayo sehemu kubwa ni kuifidia CCM.

Bahati mbaya ni njia isiyo rasmi na kwa sababu hiyo sehemu ya pesa hiyo hupotelea hewani.
 
Hebu angalia tena ukuwaji huu wa bajeti. Hauendani na nadhalia ya ukuwaji wa uchumi unaotajwa kila mwaka;

Toka 9 trl, kwenda 11 trl, kwenda 13 trl, kwenda 15 trl!

Kwa wastani huo wa 2 trl ni sawa na ongezeko la
22% kwenda 18% kwenda 15% sasa itakuwa 13%

Tunapungua na kupungua bila kujali cumulative increase ya ongezeko la pato la taifa. Hebu Kikwete atueleze ni nini hicho?
 
Back
Top Bottom