Babu wa Samunge - ambao hawajapona warudie dawa

Babu wa Samunge amewaasa waliokunywa dawa na bado hawajapona basi warudi Samunge wanywe tena kikombe.Ameelezea kuwa yeye sio mganga wa kienyeji hivyo imani ni muhimu sana.

Source ;
EA-Radio (anahojiwa muda huu na Michael B & Zembwele -Bado mahojiano yanaendeleo)

Na waliotangulia mbele za haki je?
 
Babu wa Samunge amewaasa waliokunywa dawa na bado hawajapona basi warudi Samunge wanywe tena kikombe.Ameelezea kuwa yeye sio mganga wa kienyeji hivyo imani ni muhimu sana.

Source ;
EA-Radio (anahojiwa muda huu na Michael B & Zembwele -Bado mahojiano yanaendeleo)
Watu wengine waliokunywa kikombe chake walishakufa. Sasa anataka wafu wamfate akawatoe upepo tena? Au ile nyumba yake haijaisha, sasa anatafuta pesa za kumalizia milango na madirisha?
 
Ila kuna baadhi walipona.... jaman!! Na wengine tuko nao na wana afya bomba! Kwan wanaotibiwa hospit. Wanapona wote!!!??!?
 
Si alishasema kikombe chake unatakiwa kunywa mara moja tu? Huyu babu vipi? Mbona kigeu geu sana?

Jamani hata mimi nakumbuka hili, tena alisisitiza NI MWIKO KURUDIA KIKOMBE! sasa imekuwaje tena? au anataka sasa kujenga hekalu badala ya kujenga nyumba, anunue na ndege ! Mola atunusuru na imani potofu kama hii Amin
 
Jamani jaribuni kuwa na busara ya upembuzi. Babu aliposema watu wasirudie alikuwa na maana kuwa mtu ukinywa uondoke eneo lile, uendelee na dawa zako ukiwa na imani kuwa itakusaidia kupona.

Angeruhusu kurudia na jinsi binadamu anavyopenda kupona haraka, watu wasingebanduka kule mpaka wahakikishe wamepona ndo warudi makwao.

Lakini basi kwa kuwa kuna waliopona kwa kufuata utaratibu, na waliokufa kwa kutokufuata taratibu; wanaotaka kupona kwa sasa ni ruksa kwenda tena lakini kwa utaratibu ule ule kwamba kikombe kimoja halafu unachapa yebo.

Mnaombeza babu kuwa dawa yake ni hatari, ulizieni taarifa ya utafiti ya NIMRI juu ya dawa hiyo. Mbona mpaka leo hawajathibitisha wala kuipinga. Kwa utaratibu mtu ukikaa kimya inamaana umekubali.

Nawasilisha.
 
hahahahahaha babu kushney...mwambieni wajinga ndo waliwao haendi m2 hapa
 
Hv wale wengine nao walioibuka kuwa na vikombe waliishia wapi wamezimika ziii!!!
 
Tafadhali jifunze kiswahili vizuri - Samunge - Kienyeji - Hawakupona. hii ndio tafsiri sahihi.

Ndallo aisee umenichekesha saana umegunduaje.Nimecheka hadi nimekula kofi la kisogo kutoka kwa dia wng.
 
Back
Top Bottom