Mombo Wetu
JF-Expert Member
- Aug 5, 2008
- 377
- 36
Babu amekwambia anatibu kwa dawa ya mti aliooteshwa pamoja na maombi. Sasa unaweza kuyapima maombi kwa kisayansi!
Alafu amesha sema hiyo dawa ukichemsha mwenyewe haitibu, yeye akitoka hapo kwenda kuwapelekea kwingine haitibu, mgonjwa asipoenda na kuipokea hapo yeye mwenyewe na kupewa na mikono ya babu haitibu so hiyo science itapima kitu gani hapo? But kiroho tunaweza ipima kwamba imani itakufanya wewe unyanyue mguu wako uende kule, unyenyekevu utakufanya wewe ukubali kuacha nyumba yako nzuri na magari na chakula huku ukiweka elimu yako pembeni umfuate babu asiye na jina wala elimu kwenye nyumba yake hiyo ndogo ya matope akakupe dawa inayoponya kwa neno alilopewa kwenye ndoto (Mungu mjanja maana alijua watamhonga babu awape upendeleo wachache wenye uwezo kwanza), but babu ni mtii huyu haongezi wala hapunguzi alichoambiwa (another character of a child of God)...so whats the healing power in that 'MUTI'...the word ofcourse which was given to babu by His God; who then is this God this is a spiritual question...Ukishahakikishiwa ndani ya dhamira yako na ukaipima kwa neno la Mungu tulilopewa (Biblia) ukaona halijapungua then umekiri uponyaji wahuyo mtoa ndoto and according to Babu ni Yesu maana yeye ni mchungaji...Kama kweli imo ndani yake basi ni neno ndilo linaponya hapo huo mti ni media ya kupitisha huo uponyaji kwani Mungu pia anajua cultural setting ya watanzania ni rahisi kuamini mti shamba/physical matter kuliko neno lakuambiwa...Hii ni based na analysis yangu mwenyewe na wala si ukristo nilionao lisije likatukanwa jina la Bwana yesu kwaajili yangu...
Then neno linasema kwa matendo yao mtawajua...kama kweli babu hapokei hata senti tano then yuko biblically correct kwamba umepewa bure na utoe bure..hapo anawaacha wenye dini kwa mbali sana...Tena neno la Mungu linasema God is not respector of person kila mwenye roho iliyotayari hupokea this is proved to both..babu aliyetamani kutibu hayo magonjwa (according to what is said in JF) na wale wote wanaoenda kunywa dawa ya babu huku wakiweka dini zao pembeni na kupokea uponyaji; this is also biblically proved kwamba Bwana Mungu wa majeshi ameleta wokovu kwa wote kwa myunani kwanza na kwa mataifa pia, again babu ni mtii hapunguzi wala haongezi neo sisi je tumeambiwa kila mwenye kulitaja jina la bwana na aache uovu je is this what we do?...niajabu sana wenye dini wameingia kwenye mtego wa kupeleka habari njema kwa wateja wao tu na kuiacha dunia ikiwaya waya kama machele...God promised if you wont take this good news to all nations then I will raise stones to do it on your behalf...so watumishi wajiulize mbona ukimwi bado unatesa dunia wakati wao wamebeba anointing kwenye makanisa huku watu wakiendelea kupukutika? Je yesu alikuwa mwongo aliposema mtapokea nguvu nanyi mtakuwa mashahidi wangu Galilea, Samaria na kwa mataifa yote? Ushuhuda wetu uko wapi? Je ni kipi hatukifanyi sawa? Babu is a challenge to the gospel we are preaching!