Babu wa Loliondo afungiwa kwa muda kutoa huduma...

Mlachake

JF-Expert Member
Oct 13, 2009
4,412
4,559
Mods:
Kuna Threads Nyingi sana zime/zinaaanzishwa juu ya Babu Loliondo, Hii ikiwa mojawapo.
Ningeomba kama kungekua na uwezekano wa kuziunganisha zote. Or just One thread with sub topics ie.
1.Ushuhuda wa walionda Loliondo
2.Maswali kuhusu Babu wa Loliondo
3.Wasemavyo viongozi kuhusu Babu loliondo.
4. etc etc...............
This Being an Extraodinary Event, it may deserve a special Treatment Here.

Natunguliza shukrani zangu kwa moderators
 
Kufuatia ujumbe uliotumwa na wizara ya afya na ustawi wa jamii kwenda Loliondo kwenda kuangalia uhalali wa matibabu yanayo tolewa na babu inasemekana babu hakuwa tayari kuruhusu wataalam hao kuipima dawa yake. ndugu wanajamii je hiyo imekaaje?
 
Babu amekwambia anatibu kwa dawa ya mti aliooteshwa pamoja na maombi. Sasa unaweza kuyapima maombi kwa kisayansi!
 
Kupima ufanisi wa kitu kuna njia nyngi: mfano, ufanisi wa mkandarasi unaweza kupimwa kwa kupima ubora wa jengo au barabara aliyojenga na si kukagua vyeti vyake au zana alizotumia. Nawashauri wapime wagonjwa kama wamepona au la.
 
Uko sahihi kabisa mkuu!!
 
Kufuatia ujumbe uliotumwa na wizara ya afya na ustawi wa jamii kwenda Loliondo kwenda kuangalia uhalali wa matibabu yanayo tolewa na babu inasemekana babu hakuwa tayari kuruhusu wataalam hao kuipima dawa yake. ndugu wanajamii je hiyo imekaaje?

Wawachukue wagonjwa wa ukimwi, kisukari na kifua kikuu kama "sample" wawapeleke na baada ya kunywa wawapeleke maabara kupima kama bado wanasumbuliwa na magonjwa yao. Hili halihitaji PHD kulithibisha, kupima dawa ni kutaka kuiba formular ya Babu bila idhini yake.
 
Hao waliotumwa nao walikuwa wanatumia kigezo cha kuipima ili wahudumiwe wa kwanza naibu waziri Nkya alishaenda kwa nini wasimuulize alipona au la .
Kama serikali inataka kujua hasira za watz wajaribu kuyumbisha tiba ya babu
 
babu ana msimamo c mchezo.... kwa hiyo hao wataalam waliishia kupaona tu bila mafanikio ya kufanya chochote lol......
 
Kupima ufanisi wa kitu kuna njia nyngi: mfano, ufanisi wa mkandarasi unaweza kupimwa kwa kupima ubora wa jengo au barabara aliyojenga na si kukagua vyeti vyake au zana alizotumia. Nawashauri wapime wagonjwa kama wamepona au la.

Uko sahihi wapime wagonjwa kama wamepona kweli au la. Lakini wasiishie hapo tu, kama hiyo dawa inaponya kweli ni vizuri sampuli zikachukuliwa kufanyiwa uchunguzi wa kina, kwa muda mrefu wanasayansi wamekuwa wakihangaika kupata dawa za magonjwa haya sugu. Yawezekana kuna kemikali fulani ambazo zinapatikana katika mmea huo ambazo zinaleta tiba, Dunia inahitaji matumaini na matumaini hayo yakichimbukia Tanzania hatutakaa tusahaulike katika historia ya dunia, Vilevile watu watamtukuza Mungu kwa kazi zake kama ni kweli ameoteshwa na Mungu.
Nikweli Babu anasema ni dawa ya kiimani na inamasharti, lakini kama binadamu na jumuiya ya wanasayansi kwa ujumla hatuna budi kujaribu kuchunguza tujue kulikoni.
 
Wawachukue wagonjwa wa ukimwi, kisukari na kifua kikuu kama "sample" wawapeleke na baada ya kunywa wawapeleke maabara kupima kama bado wanasumbuliwa na magonjwa yao. Hili halihitaji PHD kulithibisha, kupima dawa ni kutaka kuiba formular ya Babu bila idhini yake.
Hii ni sawa, lakini kama serikali inabidi/ni muhimu ijiridhishe pia kwamba dawa hiyo licha ya kuponya kama inavyodaiwa haina madhara mengine makubwa kwa mtumiaji (sasa na baadae). kumbuka ni maelfu ya watu wanapatiwa tiba hii na wengine wanatolewa mahospitalini kwenda huko kwa ajili ya tiba, sasa kama ina madhara ni watu wengi wataathirika na serikali ina jukumu la kulinda afya na maisha ya watu wake.
 
ha hahaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!

mkwere nae nasikia ataenda kuzindua jiwe la shule ya msingi huko loliondo!!!

mmhh!! nahisi lbd anataka apate gia ya kumpitia babu apate kikombe kimoja.
 
yani wanataka wakamchakachue babu hapo ss wataiona hasira za tz mbona vitu vya kuchunguzwa vipo vingi tz mfano rais ajui dowans, kuna mikataba mibovu mingi na mengine mengi hayo yanaitaji uchunguzi na sio kwenda kumsumbua babu wa watu bure
 
Ndugu yangu amerudi leo kutoka kwa Babu kupata dawa, amenipa hali halisi kuwa Babu yupo kwa ajili moja tu kusaidia watu na hapati hata senti tano. Ni kuwa mpaka sasa ana wasaidizi sita ambao wote ni wachungaji wanaomsaidia kutoa dawa na kwa siku anahudumia magari yapatayo elfu moja. Na mchanganuo wake kwa kila Tsh 500 inayotolewa ni kuwa; Tsh 300 inakwenda kwenye huduma za kanisa yote kama ilivyo bila kupungua hata senti na Tsh 200 wanachukua hawa wasaidizi wake sita kwa kazi ngumu wanayoifanya. Hivyo yeye hapati hata mbuni. :-(
 
ha hahaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!

mkwere nae nasikia ataenda kuzindua jiwe la shule ya msingi huko loliondo!!!

mmhh!! nahisi lbd anataka apate gia ya kumpitia babu apate kikombe kimoja.

teh teh teh teh kashaenda bana ni kat ya wa2 wa mwanzo mwanzo pamoja na baba yenu mwngne EL
 
ndiyo utaona tofauti ukilinganisha na haya makanisa yenu yanayojiita ya WOKOVU kwa kweli. sadaka mbele
 
Awaruhusu wamuugunguzie mtaji! Babu ndo kashaula hapo. Nchi ya ajabu sana hii utaruhusiwaje kuuza dawa ambayo haina vipimo?
Na Watanzania wanatetea, yale yale ya Desi, likija kulipuka wataanza kulia.
 
Back
Top Bottom