Babu wa Loliondo afungiwa kwa muda kutoa huduma...

Babu wewe tibu watu serikali ya hovyo hii iliyoshindwa kila kitu wala isikupe shida hawana lolote
 
huo mti kama unajulikana si wachukue sample waifanyie utafiti ina kitu gani? tatizo kuna nguvu za maombi ndio dawa ifanye kazi sasa hapo sijui wizara ya afya ina role gani.. kwa kua wanatumia kodi zetu kwa ajili ya hiyo safari cha maana waweke vizuri mazingira ili kujiandaa kwa ajili ya magonjwa ya mlipuko ambayo yanaweza kulipuka huko kutokana na uwingi na mikusanyiko wa watu

Samora,

Mimi naona cha muhimu ni kwa serikali kujiridhisha kuwa hayo maji/dawa wanayopewa wagonjwa hayana madhara kwa watumiaji (sasa na hata baadae). Kwangu mimi hili ndilo kubwa na la muhimu. La pili ni hilo la kuponya ama la. Serikali ni lazima ifanye utafiti wake wa kisanyansi ili wananchi na watu wengine wajue ukweli na wafanye maamuzi huku wakiwa na/wakijua taarifa sahihi.

Kama uchunguzi wa kisanyansi ukionesha kuwa hiyo 'dawa' haina madhara na pia inaponya kama inavyodaiwa then serikali inaweza hata kusadia katika kumwekea utaratibu mzuri huyo Babu wa kuendelea kutoa tiba yake kama alivyooteshwa. Badala ya sasa, serikali kuanza kutumia kodi za wananchi kusaidia utoaji wa dawa ambayo pengine ni hatari kwa watumiaji au hata haiponyi kama inavyodaiwa. Si miaka mingi imepita tangu DECI ilipozua kizazaa na serikali kuanza kulaumiwa....na sadly hata katika DECI viongozi wa dini walihusika kwa kiasi kikubwa kuwapotosha waamini wao!

Kama uchunguzi wa kisanyansi ukionesha kuwa hiyo 'dawa' ina madhara makubwa kuliko manufaa yake then serikali ni lazima izuie utoaji wake.

Kama uchunguzi wa kisanyansi ukionesha kuwa hiyo 'dawa' haina madhara na pia haiponyi kama inavyodaiwa...watu waambiwe ukweli huo na serikali isiendelee kujihusha kwa kitu ambacho hakina manufaa. Kama watu wataendelea kuiamini na kuitumia waachwe wafanye hivyo kwa utashi wao wenyewe na kwa kujua ukweli wa kisanyansi.
 
Jamani mi nimeona vitu lakini hiki cha loliondo kimenishtua sana, kwasababu Mzee huyu ni wa ajabu na ameweza kujipatia njia nzuuurii ya kutafuta Pesa bila kutumia unyang'anyi wala Ndumba, bali kwa kutumia Akili yake.
Hakuna uthibitisho wa kisayanxzi kwamba dawa hiyo inaponesha, na kimachoshangaza Eti Dawa hiyo huponi ukichota mwenyewe mpaka achote kwa mkono wake.
naomba tuwege makini, na naomba uthibitisho ili na mimi niende bana

Eti wadau ni njia ya kutafuta Ela au Dawa kweli?
mkuu yule mzee haponyi NI IMANI YAKO WEWE NA MUNGU WAKO, KUMBUKA NYOKA WA SHABA WA MOSES WALIOITAZAMA WAKAPONA!
 
Jaribu na wewe kutafuta hiyo pesa kama wadhani watu wote wanafanya hivyo ili kujipatia pesa.Na kama we unaona sayansi vina uhusiano na mungu basi we fuata ya sayansi usiwababaishe watu na sayansi yako
 
Mimi na wasi wasi na hawa Wizara ya Afya wanaojidai kupeleka wataalam kupima eti ubora waa dawa kama ina tibu au vipi, hawa wanaweza wakasababisha fujo kubwa sana na amani ikapotea ni bora wawatafute wagonjwa waliopona wakawapima upyaa kuona kama wamepona au vipi kuliko kupima dawa ambayo mwenyezi mungu katushushia na si ya kutengeneza kwenye MAABARA
 
Felister,

1. Wagonjwa wenye shida ambao hawana nauli watafikaje kwa babu kama yeye peke yake
ndie anayetoa hiyo dawa na si mwingine?

2. Southern countries ndio zilizoathirika sana kwa ugonjwa wa UKIMWI, are you telling me all
those people should come to TZ to get this treatment from him ONLY?

3. Kama kweli hii dawa Mungu ndiye aliyemfunulia, vipi kuhusu wagonjwa ambao wanafia
njiani wakielekea huko Loliondo? Hawakustahili kupata hii dawa ili wapone?

4. How come we only hearing story from people but we havent actually see someone who got
healed, utasikia tu mtoto wa rafiki yangu, mama yake rafiki yangu, mjomba wangu
anayekaa mbeya etc?

Mbona hayo maswali yako zaidi upande wa serikali kuliko Babu? kwani watalii wanapokuja kutembelea wanyama mbugani na Ngorongoro crater mbona hatulalamiki kuzihamishia Dar ambako kuna facilite zote? Kumbuka babu kapewa karama ya kutibu katoa utaratibu ambao mimi nauona wakimungu zaidi...uwe na imani, uwe mnyenyekevu (nipamoja na kukubali hadharani kwamba babu ndiye aliyekusaidia na ndoto yake) and na yeye ili aweze kuhold anointing utii ndo agizo pekee so yeye amsikilize nani? Ninyi walalamikaji ambao hamtaki ku facilitate utaratibu wa babu uendelee kufuatwa bila yeye kukosa utii au yeye awasikilize ninyi na hiyo anointing iondoke watu waendelee na shida zao kama mwanzo? Babu is not a panacea but a contributor to problem ruduction kwa magonjwa sugu kumtupia lawama ya watu wanaokufa is not fair wengine wanatakiwa wasaidie kuweka coordination office sehemu kama Arusha na wagonjwa waliozidiwa wapewe priority badala ya kujaza FFU kule basi watu wangeruhusiwa kwenda kumwona babu kama wanavyopanda Mt. Kilimanjaro..ili babu awe free na tuhuma zenu za rushwa kama mtapenda kuingiza rushwa kama ilivyo desturi yetu hapo nyumbani kwani amekataa hayo kufanyika?
 
NoNoNonononono wadau naona mumeninukuu vibaya, ni nacho kifanya hapa ni kutoa angalisho maana wagonjwa wa Ukimwi wanawatukana Manurse na Madactari bila kuthibitisha sasa haya yana Effects kubwa ukitaka kurud tena
 
Kupima ufanisi wa kitu kuna njia nyngi: mfano, ufanisi wa mkandarasi unaweza kupimwa kwa kupima ubora wa jengo au barabara aliyojenga na si kukagua vyeti vyake au zana alizotumia. Nawashauri wapime wagonjwa kama wamepona au la.

UMENENA MKUU,ungekua karibu ningekupa zawadi
 
Jamani mi nimeona vitu lakini hiki cha loliondo kimenishtua sana, kwasababu Mzee huyu ni wa ajabu na ameweza kujipatia njia nzuuurii ya kutafuta Pesa bila kutumia unyang'anyi wala Ndumba, bali kwa kutumia Akili yake.
Hakuna uthibitisho wa kisayanxzi kwamba dawa hiyo inaponesha, na kimachoshangaza Eti Dawa hiyo huponi ukichota mwenyewe mpaka achote kwa mkono wake.
naomba tuwege makini, na naomba uthibitisho ili na mimi niende bana

Eti wadau ni njia ya kutafuta Ela au Dawa kweli?

kaka You are miinformed huyu babu hachukui hata shilingi yako unaambiwa 300 ni ya kanisa na 200 ya wale wachungaji wanaomsaidia kazi sasa sijui wewe habari za yeye kutafuta pesa umezitoa wapi
 
We sasa humu ndani ya JF unatuletea imani zako za kisayansi wakati watu wamepona kwa Maji (Damu ya Yesu). Kamuombe shehe Yahaya akufanyie utafiti wa kisayansi wa hiyo dawa
 
vibosile bwana wameona wao washakunywa na kupata nafuu ya vigonjwa vyao sugu sasa wanataka walalahoi washike adabu zao wasipate ki2
 
kwani watawalazimisha? Si watafute ambao wako tayari kufanyiwa vipimo? Kama wanaweza kushuhudia wamepona kwenye vyombo vya habari wataacha ku colaborate na serikali?
Mkuu kwani wewe unadhani serikali inafanya hivyo kujua kama dawa hiyo inacontents za kutibu tu au inaangalia pia kama hizo dawa hazina madhara kwa mtumiaji?
Kuna swala la kutibu na kuna swala la madhara kwa mtumiaji, serikali inaangalia madhara kwa mtumiaji na kama inazo hizo contents si vibaya zikafanyiwa kazi.
Kama serikali itaona ni maji ya kawaida na babu akadai ni mambo ya miujiza serikali haiwezi kufanya kitu, issue ni je hiyo dawa ina usalama gani kwa watumiaji?
 
Si umesha sema anawapa wachungaji sasa we vipi kaka? ujue nini huo ni usemi tu kwamba yeye anawapa wachungaji kwani yeye hali? hataki kuenjoy? na hao wachungaji wanamuachaje? jiulize kisha nipe jib
 
Hii ndio nchi ya mazuzu na viongozi wake mazuzu. Inawezekanaje ukaenda kupima dawa ambayo kabla aujapewa unaombewa ndio unakunywa so hii inaonesha tosha imani ndio inazofanya kazi. So ushauri wa bure kwa hawa viongozi ni kuwachukua wale wagonjwa waliopatiwa tiba na kuwapima kujua wamepona ama hawajapona. Ndipo watoe tamko kuhusu iyo dawa.
 
Kula kala kwa miaka 76 aliyonayo kaka iliyobaki haitamsaidia saaana hata mbele ya mungu akifanya hivyo atahukumiwa.So yule babu hana sababu ya kulaghai watu kwa kipindi kifupi chamaisha.Sio kama shehe yahaya anaedanganya hadi sasa
 
Jamani kwani Shehe yahaya ninani? kwani yeye ni mwana Sayansi mbona munataja watuwasio na macho wala miguu katika tasnia za watu bhana, munapeeeenda kuwatukuza watu, Shehe yahaya si kama wewe tu, ana nini cha ajabu,
 
Naona wanatafuta machafuko!! Watu tayari walikuwa na matumaini, then yanakatishwa gafla kwa upuuzi wa watu wachache!!!
 
Utafiti huo utachukua miaka mingi, na huenda matokeo yasitolewe hadharani..
..Serikali inajichanganya juzi walikuwa wanamuhoji mkuu wa wilaya ya ngorongoro akadai kuwa huyo mzee alianza kutoa hiyo tiba tangu mwaka jana ingawaje si watu wengi waliokuwa wakijua na wao kama uongozi wa wilaya baada ya kupata hizo taarifa walifatilia na sample ya hiyo dawa ilipelekwa Muhimbili kitengo cha madawa asilia tangu mwaka jana na hadi hii leo hawajatoa majibu...sijui kimebadirika nini mpaka wanataka kuifanyia utafiti kwa mara nyingine hiyo dawa.
 
Back
Top Bottom