kisu
JF-Expert Member
- Mar 31, 2009
- 1,005
- 382
[h=2]Baba ambaka binti yake, ampa 2,000/- atunze siri[/h]
Na Mwandishi wetu
17th October 2011
B-pepe
Chapa
Maoni
Mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Buzirayombo, Wilaya ya Chato mkoani Kagera, amebakwa na baba yake mzazi kisha kupewa zawadi ya Sh. 2,000 ili asivujishe suala hilo.
Tukio hilo la kikatili lilitokea Oktoba 13, saa 2:30 usiku kwenye kilima cha Kanisa la AICT Buzirayombo baada ya baba huyo kumrubuni binti yake kwamba anakwenda kumtafutia dawa ya kumaliza umalaya.
Inadaiwa kuwa mzazi huyo, Mathias Merick (50), alimchukua binti yake huyo mwenye umri wa miaka 12 (jina limehifadhiwa), nyumbani kwake na kwenda naye porini majira ya usiku kwa madai anakwenda kumtengenezea dawa ya asili itakayomfanya aache umalaya ili hatimaye afaulu mtihani wake wa darasa la saba.
Ilielezwa kuwa baba huyo alikuwa akimtuhumu binti yake kujihusisha na vitendo vya umalaya ambapo siku hiyo alimweleza kuwa amepata dawa ya kuzuia hali hiyo kutokea tena kwa madai alikuwa akisumbuliwa na mizimu ya mababu zake.
Hata hivyo, katika hali isiyo ya kawaida baada ya kufika kwenye vichaka vilivyopo eneo la kanisa hilo, alimwamuru binti yake kutandika chini upande wa khanga aliokuwa amevaa na kumtaka avue nguo zote kwa lengo la kumpatia dawa hiyo.
Lakini uamuzi huo ulimfanya binti kuogopa kuvua nguo huku akimtazama baba yake mzazi.
Hata hivyo, baba yake alilazimika kumfokea binti na kumsisitiza kuwa hakuwa na sababu ya kuogopa chochote kwa kuwa yeye ndiye baba yake mzazi.
Imeelezwa kuwa wakati majibizano hayo yakiendelea, baba huyo alikuwa ameshika panga mkononi.
Kutokana na hali hiyo, ilimlazimu binti huyo kutii amri ya mzazi wake na ndipo alipofanyiwa unyama huo.
Kwa mujibu wa habari hizo, baada ya baba yake kukamilisha kitendo hicho, alimpa binti yake Sh. 2,000 kama zawadi na pia atunze siri hiyo.
Ilidaiwa kuwa baada ya tukio hilo, baba huyo alimshinikiza binti yake kutamka baadhi ya maneno ya kuiasa mizimu imwachie ili asome na kama inamhitaji imfuate baada ya kumaliza masomo yake.
CHANZO: NIPASHE