Baba ambaka binti yake, ampa 2,000/- atunze siri

kisu

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
1,000
380
[h=2]Baba ambaka binti yake, ampa 2,000/- atunze siri[/h]


Na Mwandishi wetu



17th October 2011


email.png

B-pepe



printer.png

Chapa



comment_bubble.png

Maoni









Mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Buzirayombo, Wilaya ya Chato mkoani Kagera, amebakwa na baba yake mzazi kisha kupewa zawadi ya Sh. 2,000 ili asivujishe suala hilo.
Tukio hilo la kikatili lilitokea Oktoba 13, saa 2:30 usiku kwenye kilima cha Kanisa la AICT Buzirayombo baada ya baba huyo kumrubuni binti yake kwamba anakwenda kumtafutia dawa ya kumaliza umalaya.
Inadaiwa kuwa mzazi huyo, Mathias Merick (50), alimchukua binti yake huyo mwenye umri wa miaka 12 (jina limehifadhiwa), nyumbani kwake na kwenda naye porini majira ya usiku kwa madai anakwenda kumtengenezea dawa ya asili itakayomfanya aache umalaya ili hatimaye afaulu mtihani wake wa darasa la saba.
Ilielezwa kuwa baba huyo alikuwa akimtuhumu binti yake kujihusisha na vitendo vya umalaya ambapo siku hiyo alimweleza kuwa amepata dawa ya kuzuia hali hiyo kutokea tena kwa madai alikuwa akisumbuliwa na mizimu ya mababu zake.
Hata hivyo, katika hali isiyo ya kawaida baada ya kufika kwenye vichaka vilivyopo eneo la kanisa hilo, alimwamuru binti yake kutandika chini upande wa khanga aliokuwa amevaa na kumtaka avue nguo zote kwa lengo la kumpatia dawa hiyo.
Lakini uamuzi huo ulimfanya binti kuogopa kuvua nguo huku akimtazama baba yake mzazi.
Hata hivyo, baba yake alilazimika kumfokea binti na kumsisitiza kuwa hakuwa na sababu ya kuogopa chochote kwa kuwa yeye ndiye baba yake mzazi.
Imeelezwa kuwa wakati majibizano hayo yakiendelea, baba huyo alikuwa ameshika panga mkononi.
Kutokana na hali hiyo, ilimlazimu binti huyo kutii amri ya mzazi wake na ndipo alipofanyiwa unyama huo.
Kwa mujibu wa habari hizo, baada ya baba yake kukamilisha kitendo hicho, alimpa binti yake Sh. 2,000 kama zawadi na pia atunze siri hiyo.
Ilidaiwa kuwa baada ya tukio hilo, baba huyo alimshinikiza binti yake kutamka baadhi ya maneno ya kuiasa mizimu imwachie ili asome na kama inamhitaji imfuate baada ya kumaliza masomo yake.



CHANZO: NIPASHE
 
Dunia imeisha hii....baba kutamani bintiyo wa miaka 12?!
 
labda ilikua ni kama investment fulani hivi...alaaaniwe
 
Sijui tunaelekea wapi, kama mzazi unafanya hivi kweli!?!? Ulaaniwe kabisa na upuuzi wako, kama una akili timamu kabisa basi uende kutumikia hiyo miaka 30 jela na kazi ngumu sama kama kuponda mawe n.k
 
Sasa hiyo ndio dawa ya umalaya aliyompa? Duh! Mibaba mingine, ameshindwa hata kutafuta changudoa anamchukua mtoto wake?
 
Dunia imeisha hii....baba kutamani bintiyo wa miaka 12?!

angekuwa wa jirani, tungesema labda mila zao zinaruhusu lakini kwa binti yake wa kumzaa? ni zaidi ukatili wa kijinsia, ni mwiko karibu jamii zote tanzania. napenda nijue kafanywa nini huyo mshenzi
 
Hapa ingekua ni mtu mwingine amemfanyia binti huyo Baba angemindi sana lakini yeye mwenyewe kaamua kula
tunda yaani
astakafirular mara 3475675036.....................................
 
Inawezekana huyu Baba shetani alikuwa akimmendea Bint yake muda mrefu
hivyo akatafuta mbinu ya kungoneka nae,
na pengine pia alimuona bintie akienda na wanaume wengine (maana mabint wengine huanza mapema haya mambo) akawaonea wivu
hivyo akataka kula mwenyewe!
Na alaaniwe alalae na Bintie!
Wote tuseme Amen!
 
kha!! yaani huyo baba ni kwakuhasiwa kabisa maana kumfunga kifungo cha maisha haisaidii ahasiwe kama mbuzi au ngombe ama mbwa ili awe anakumbuka maisha yake yote kuwa alihasiwa kama wanavyohasi mifugo *&%^$#@$%^&**)&%^$@# kabisa hana abadu na hafai kuwekwa kwenye kundi la ubinadamu huyo!!!
 
kha!! yaani huyo baba ni kwakuhasiwa kabisa maana kumfunga kifungo cha maisha haisaidii ahasiwe kama mbuzi au ngombe ama mbwa ili awe anakumbuka maisha yake yote kuwa alihasiwa kama wanavyohasi mifugo *&%^$#@$%^&**)&%^$@# kabisa hana abadu na hafai kuwekwa kwenye kundi la ubinadamu huyo!!!
mKUU uKO sAWA kABISA...AHASIWE tena kwa BISIBISI....
 
kipululu chake angekipeleka kwa wazee wenzake
hivi mtoto huyu mdogo anaenuka maziwa bado
anamfurahisa nini huyu mzee mzima??????
nashindwa kuamini .ila kama yule jamaa wa redio
family alivyotabiri nadhani anytime parapanda
italia


lulu...[/QUOTE]
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom