Leo kibao kimemgeukia sana ndugu Zitto na akina Ole Sendeka na wabunge Kadhaa wa CCM walipewa hongo ili kuitetea menejimenti ya tanesco, this is another setback deadlock kwa zitto ajiangalie Mara mbili anapotoa matamko hata wenzake poac wamemruka kabisa hawajawahi kuitetea menejimenti ya tanesco.
Hapo ndo nashindwa kabisa kuelewa faida ya elimu ktk siasa.
Mh. Sifahamu kama una elimu kubwa lakini kwa kuwa nimesikia unasoma Ph.D. somewhere, nimeamini unataka kuongeza elimu, lakini kwa haya niliyoyasikia Bungeni na kwa kuwa siku za nyuma tuliwahi kukuzoza hapa JF kwa support yako juu ya Tanesco na mpango wao wa kununua majenereta, nashindwa kuamini umakini wako. Utaharibu sifa ya Ph.D, ni bora u-download cheti kama wengine walivyofanya.
Which reasonable asset of ideas do you still have to offer to the public following all these revelations? Are you the same person you once struggled to outweigh Hon. (then) Slaa?
Is it true that you are a typical example of majority who fail to separate power and prostitution?
I believe, this is a fissure in your political ambition. You are likely to fall somewhere, obtusely.
Tunakunyooshea mkono kuliko yeyote kwa sababu wewe ni CHADEMA. Chama ambacho wengi wamekiona ni kama regulator wa matatizo ya wanyonge. What other bad words should make you understand our dissatisfaction? Mbunge kijana gani wewe?
Ni hivi mwenzetu,
Kwa wiki kadhaa sasa kumekuwa na tatizo ktk Wizara ya Nishati na madini. tatizo lenyewe ni la umeme, Tanesco. Baada ya waziri mpya kuingia kafumua mambo mengi sana lakini kubwa ni kwamba kumbe Tanesco wamekuwa wakiunda upungufu wa umeme kwa makusudi ili waanze kutumia pesa za shirika vibaya ktk kununua mafuta mazito ya kuendeshea mitambo ya ziada, ili kufidia upungufu huo. Pesa wanazozitengeneza ktk manunuzi hayo wanagawana.
Hadithi zinaeleza pesa hizo zinafahamika hata ndani ya kamati ya bunge ambayo inaongozwa na Mh. huyu. Bunge leo limesema na kuzomeya "Zitto", pale Mh. mmoja alipolaani mafisadi walioshirikiana na Tanesco.
Siku chache zilizopita pia Mkurugenzi mkuu wa Tanesco alisimamishwa kwa ufisadi. Ajabu Mh. huyu ndo wa kwanza kusema kaonewa. Tulitegemea yeye awe wa kwanza kufahamu undani wa ufisadi huo.
Lisemwalo lipo. Wiki hizi za bajeti ilisikika kwamba kuna wabunge walishajipanga kuwakataa viongozi wa Wizara hii kwa sababu tu eti wameigusa Tanesco. Yaweza kuwa kweli maana magazeti yameandika yakieleza kwamba Rais ana imani na uongozi wa wizara, ikiashilia kuna kundi fulani halina imani nao. Kama ni hivyo baadaye kuna jambo au mawasiliano yaliyofanyika kati ya wabunge maana jioni ya leo sasa bunge limekuwa kama uwanja wa Taifa. kwa pamoja kila aliyesimama kulaani uongozi wa Tanesco, alishangiliwa kama gori la ushindi.
Sisi JF tuliwahi kuhoji uhalali wa Mh. Zitto kuitetea Tanesco ilipokuwa inapanga kununua majenereta (nadhani ni yale ya Dowans) ili kufidia upungufu wa umeme. Sasa kumbe hata upungufu huo umekuwa ukitengenezwa!
Tuseme nini juu ya Mh huyu? na hasa gharama ya imani aliyokuwa amepewa na watu?