rmashauri
JF-Expert Member
- Jan 29, 2009
- 3,011
- 454
Mwaka 2006 kama siyo 2007 Kikwete akiwa ameambatana na waziri wa viwanda na bishara wakati huo Nazir Karamagi, katika mkutano wake na watanzania waishio Oslo, Norway mama mmoja kutoka Bukoba alimuuliza Kikwete swali kuhusu uhaba wa madaktari huko Bukoba. Kikwete hakujibu swali lile akamsukumia mbunge wao Karamagi ajibu swali lile. Karamagi alijibu kwa kifupi tu kuwa "Tatizo letu wahaya tunawakataa madaktari wanaopangiwa kazi huko kwetu ambao siyo wahaya hivyo inawalazimu kuondoka". Kwa maana nyingine analiyoyasema mtoa hoja hapa yana ukweli ndani yake.