Augustino Mrema kurudi bungeni kwa kura nyingi baada ya kuainisha aliyowatendea wananchi wa Vunjo

Majasho

JF-Expert Member
Aug 4, 2009
413
220
MREMA NA MAENDELEO YA VUNJO 2010 - 2015

UTANGULIZI
Awali ya yote napenda kumshukuru mwenyezi mungu aliyenipa uhai, afya na nguvu kuweza kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Vunjo kwa kipindi cha miaka 5 iliyopita, napenda kuwashukuru wananchi wote wa Jimbo la Vunjo, kwa ushirikiano mkubwa walionipa ambao uliniwezesha kutekeleza majukumu yangu.

Nachukua nafasi hii kumshukuru mke wangu mpendwa Bi. Rose Mrema na familia yangu yote. Aidha, nawashukuru wananchi wote wa Jimbo la Vunjo walionichagua kuwa mbunge wao mwaka 2010, nawashukuru wanachama na viongozi wote wa TLP wakiwemo madiwani, viongozi wa Jimbo na Mkoa wa Kilimanjaro kwa ushirikiano wao

Kabla ya kuelezea kazi niizofanya kama Mbunge wa Jimbo la Vunjo kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, napenda kuchukua nafasi kuelezea ukweli kuhusu shutuma mbalimbali zinazotolewa dhidi yangu na baadhi wanasiasa. Shutuma hizo ni za uongo uliotungwa kwa makusudi kwa lengo ya kunichafua na kunidhalilisha kwa wapiga kura wa Jimbo la Vunjo ili nionekane kama sifai kuwa mbunge wenu. Baadhi ya tuhuma hizi ni kama ifuatavyo:


  1. TUHUMA KWAMBA DIGRII YANGU YA PHD NI FEKI
Kuna wanasiasa na wapambe wao wenye roho mbaya wananichafua kwa kueneza uongo kwamba shahada yangu ya PHD ni feki jambo ambalo sio kweli. Shahada yangu ya PHD ni halali na ya ukweli niliyoipata kutoka Chuo Kikuu cha OMEGA GLOBAL UNIVERSITY cha Afrika Kusini.

PHD hiyo niliipata baada ya kupata shahada ya awali Bachelor of Arts in Political Science ambayo nilisoma chuo cha WESTERN PACIFIC UNIVERSITY nchini Marekani. Chuo hicho kilichonitunuku shahada hiyo ya PHD kutokana na mchango wangu katika jamii na kazi nzuri niliyofanya kwenye uongozi kama ifuatavyo:

  1. Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini kwa miaka 10 (1985-1995)
  2. Mbunge wa Jimbo la Temeke kwa kipindi cha miaka 4 (1996 -1999)
  3. Waziri wa Mambo ya Ndani (1990 1994)
  4. Naibu Waziri Mkuu (1993 1994)
  5. Waziri wa kazi na Maendeleo ya vijana (1994 1995)
  6. Mgombea urais wa mwaka 1995 kutoka upinzani aliyepata 28% ya kura zote za urais, rekodi ambayo hadi leo haijafikiwa na mtu yeyote
  7. Mwenyekiti wa Taifa NCCR Mageuzi (1995 1999)
  8. Mwenyekiti wa Taifa Tanzania Labour Party (TLP)(1999 2019)

Hivyo shahada hiyo ni halali na imethibitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na ndio maana hata ninapokuwa ndani ya Bunge Spika wa Bunge ananitambulisha kwa hadhi ya Dkt. Augustino Lyatonga Mrema

  1. MADAI KWAMBA MIMI NALINGANGANIA JIMBO LA VUNJO NA KWAMBA SITAKI KUWAACHIA WATU WENGINE
Madai hayo si kweli kwa sababu mimi niligombea urais mwaka 1995 na wakati huo Mhe. James Mbatia alikuwa hajulikani kisiasa, mimi ndie niliyemnadi na kuwaomba wananchi wa Vunjo wampigie kura ili awe Mbunge, na wananchi walinisikiliza na kumchagua kuwa Mbunge wenu.

Lakini kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2000 Mhe. James Mbatia alikataliwa na wananchi na badala yake walimchagua Major Jesse Makundi kuwa Mbunge wa Vunjo. Hata hivyo, mwaka 2005 waliokuwa wagombea wa upinzani walishindwa kulitetea jimbo la Vunjo na badala yake likachukuliwa na Mhe. Aloyce Kimaro wa CCM.

Baada ya kuona kwamba wapinzani wenzangu wameshindwa kulitetea Jimbo la Vunjo na wamesababisha lichukuliwe na CCM, wananchi wa Vunjo waliniomba nirudi ili nilikomboe Jimbo la Vunjo kutoka kwenye mikono ya CCM. Kazi ambayo niliifanya kwa mafanikio makubwa mwaka 2010.

Sasa tujiulize hao wengine walikuwa wapi? Na kwa nini walishindwa kulikomboa Jimbo la Vunjo? Badala yake Mhe. James Mbatia mwaka 2010 alikimbilia kwenda kugombea Jimbo la Kawe jijini Dar es Salaam ambako aliambulia nafasi ya tatu, nyuma ya wagombea wa Chadema na CCM. Sasa baada ya kuona mambo ya Dar es salaam yamemshinda anarudi tena Vunjo, muulizeni alikuwa wapi na kwanini aliondoka?

Sasa jimbo limekombolewa kutoka CCM na lipo mikononi mwa mpinzani mwenzake ni kipi kinachomrudisha sasa? Mbona alishindwa mwaka 2000 na mbona hata alipoenda Kawe mwaka 2010 nako alishindwa. Labda atasingizia kwamba alishindwa kwa sababu sio mzawa wa Kawe, lakini mbona mimi mwaka 1996 niligombea ubunge Temeke na kushinda wakati sio mzawa wa Temeke?

  1. MADAI KWAMBA MIMI MREMA NIMEZEEKA
Madai hayo si kweli, kwani ujana sio kigezo cha uongozi bora. Kigezo cha uongozi ni uwezo wa kuwatumikia wananchi, kutatua kero zao na kusimamia maendeleo yao, kwa mfano, Rais Muhamad Buhari amechaguliwa kuwa Rais wa Nigeria mwaka huu akiwa na umri wa miaka 72 wakati mpinzani wake Rais wa zamani Godluck Jonathan ana miaka 55.

Hivyo uzee au ujana sio vigezo vya uongozi bali kigezo ni uwezo wa kuwaongoza na kuwatumikia wananchi. Hata yeye Mhe. James Mbatia alishindwa ubunge mwaka 2000 na Major Jesse Makundi wakati yeye Mhe. Mbatia ni kijana zaidi akilinganishwa na Major Jesse Makundi. Wananchi jiulizeni mbona mwaka 2010 mlinipa ubunge bila kujali umri wangu wakati nilikuwa nashindana na wagombea vijana wa Chadema na CCM? Lakini mliwakata. Mbona kuna majimbo mengi yanaongozwa na wabunge wazee kuliko mimi mbona hawaendi kuwangoa? Kwa nini wananingangania mimi tu? Watu wa namna hiyo wapuuzeni maana wamekosa hoja za msingi na badala yake wanatunga hoja za uongo kuwahadaa wananchi ili wawapigie kura.

  1. MADAI YA KWAMBA MIMI NI MGONJWA HIVYO SIFAI KUWA MBUNGE WA VUNJO
Madai ya kwamba mimi ni mgonjwa na sifai kuwa Mbunge wa Vunjo ni ya uongo. Kwanza napenda niseme kwamba hakuna binadamu asiyeugua, na mimi kama binadamu mwingine yoyote niliugua Mild Cancer na baadae nilipelekwa nchini India ambako nilitibiwa na kupona kabisa ugonjwa huo. Na kwa sasa mimi ni mzima, mwenye afya njema na nina uwezo wa kuwatumikia wananchi wa Vunjo kwa miaka mingine mitano ijayo.

Wananchi kumbukeni kwamba kuugua sio kufa na hata viongozi wakuu wa nchi yetu waliwahi kuugua na kupelekwa nje ya nchi kwa matibabu na sasa wamepona kabisa na wanaendelea na majukumu yao kama kawaida wakiwa ni wazima wa afya njema. Hivyo ndivyo ilivyo kwa mimi pia. Kama madaktari wangu wanaonitibu wangeniambia kwamba ni mgonjwa na sina uwezo wa kufanya kazi tena ningewatii lakini wameniahakikishia kwamba nimepona na nina afya njema ya kuweza kufanya kazi.

  1. MADAI KWAMBA MREMA NI KIBARAKA WA CCM
Wanaoeneza maneno hayo kwamba mimi Dkt. Augustino Lyatonga Mrema ni kibaraka wa CCM, wanatoa sababu ambazo ni za uongo kama ifuatavyo:

  1. Wanadai kwamba wakati wa kampeni za uchaguzi wa mwaka 2010, mimi nilisema kwamba kura za Urais apewe Kikwete na mimi nipeni kura za ubunge

  1. Wanadai kwamba wabunge wa upinzani walivyotoka nje ya Bunge la Katiba, kupinga katiba mpya inayopendekezwa mimi nilikataa kutoka nje.

  1. Wanadai kwamba mimi nimekataa kujiunga na UKAWA kwa hiyo ni kibaraka wa CCM ili kugawa kura za upinzani kwa lengo la kusaidia CCM ishinde.

  1. Wanadai kwamba mara kwa mara nimekuwa nikiunga mkono hoja za serikali badala ya kuzipinga

Naomba kutoa ufafanuzi kuhusu madai haya ya uongo kama ifuatavyo:

  1. Sio kweli kwamba wakati wa uchaguzi wa mwaka 2010 nilimnadi Rais Kikwete, kama yupo mwenye ushahidi huo autoe hadharani. Hata kama ningekuwa nampenda Rais Kikwete kwa kiasi gani, nisingeweza kufanya hivyo kwa sababu chama changu cha TLP kilikuwa na mgombea wake, ambaye ni Mhe. Mutamwega Mughaya. Hivyo nilikuwa namnadi mgombea wa chama changu. Na kwa kudhihirisha hilo mgombea huyo alipata kura nyingi kutoka jimboni kwangu Vunjo kuliko jimbo lingine lolote, anayebisha hilo aende akaangalie takwimu za matokeo ya Tume ya Taifa ya uchaguzi.

  1. La pili, ni hili la kukataa kutoka nje wakati wabunge wa baadhi ya vyama vya upinzani walipotoka nje kupinga katiba mpya inayopendekezwa. Kwanza niseme kwamba vyama vya upinzani ni 21 lakini vilivyoamua kutoka nje ya Bunge la Katiba ni vinne tu.

Vyama vingine vya upinzani viliona vibaki ndani ya bunge ili vipambane kwa nguvu ya hoja badala ya kususa. Je unaposusa nani atakayewakilisha mawazo ya wananchi wa jimbo lako? Maana katiba mpya ilikuwa inajadili mambo mengi mazuri kama vile haki wa wanawake, haki za watoto, haki za wakulima na wafugaji na mambo muhimu kwa maendeleo ya taifa letu. Hivyo tuliobaki tuliona ni vizuri kuendelea ili kufikisha hoja zetu kwenye bunge la katiba. Hoja ambazo zilizingatia maslahi ya makundi yaliyotajwa.

Kwa maoni yetu waliosusa hawakuwatendea haki wapiga kura wao waliowachagua kuingia bungeni na pia hawakuyatendea haki makundi yaliyotajwa. Kwa mfano, kubakia kwangu ndani ya bunge kulisaidia kuondoa suala la mahakama ya kadhi lisiwemo kwenye katiba mpya inayopendezwa, bali mahakama ya kadhi ibakie kwenye sheria tu, lakini sio kwenye katiba. Nashukuru maoni yangu yalizingatiwa na mahakama ya kadhi ikaondolewa kwenye katiba mpya inayopendekezwa. Lakini bado kuna uongo unaoenezwa mitaani kwamba mahakama ya kadhi ipo ndani ya katiba iliyopendekezwa, jambo ambalo si kweli.

Watu wamesahau kwamba kuna baadhi ya vyama vya siasa viliweka mahakama ya kadhi kwenye ilani zao za uchaguzi ili kuwarubuni waislamu wapige kura kwa vyama hivyo. Kwa mfano, ilani ya uchaguzi ya NCCR Mageuzi ya 1995 hadi mwaka 2000 na ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005 mpaka 2010 zote zilikuwa zinapendekeza mahakama ya kadhi zianzishwe nchini.

Kwa hiyo sisi tuliobakia kwenye bunge la katiba tumesaidia kuboresha katiba inayopendekezwa kwa manufaa ya wananchi na taifa letu. Mwanasiasa shupavu hasusi vikao bali kuingia na kupambana hadi mwisho hata akishindwa, lakini ujumbe utakuwa umefika kwa wabunge wenzake na wananchi kwa ujumla, na hivyo watu wataendelea kutafakari hoja zake, kususa vikao vya bunge ni ishara ya kukosa hoja za msingi.

  1. KWA NINI SIKUJIUNGA NA UKAWA
Kuna watu wanaosema mimi ni kibaraka wa CCM eti kwa sababu nimekataa kujiunga na UKAWA ili kuimarisha upinzani lakini watu wao hawaelewi hali halisi na kama wangeelewa wasingenilaumu. Sikujiunga na UKAWA kwa sababu zifuatazo:

  1. UKAWA walitaka kambi ya upinzani tususie vikao vya bunge maalumu vya katiba. Sikuona busara ya kufanya hivyo kwa sababu niliona kufanya hivyo katiba mpya itakosa mchango kutoka kwa wananchi wangu ninaowawakilisha na itasababisha taifa kupata katiba mbovu. Mimi na wenzangu wa vyama 17 vya siasa vilivyobaki bungeni tuliona ni busara kuendelea kupambana kwa nguvu ya hoja badala ya kususa na mchango wetu ulisaidia sana kuboresha katiba mpya inayopendekezwa.
Kuhusu serikali tatu inayopigiwa debe na ukawa sio kipaumbele cha watanzania. Kipaumbele cha watanzani ni kuondoa umaskini, kuimarisha huduma za afya, elimu, maji, miundo mbinu na kupunguza tatizo la ajira kwa vijana.

  1. Ndani ya ukawa kuna vyama vya siasa vinavyotaka kuvifuta vyama vingine visikuwepo kwenye ramani ya siasa. Kwa mfano, chama cha NCCR Mageuzi kilitangaza rasmi kampeni ya kuifuta TLP. Kampeni hiyo ilijulikana kwa jina la DELETE TLP. Kwa kupitia kampeni hiyo chama hicho kiliwarubuni na kuwanunua viongozi na wanachama wa TLP jimboni Vunjo na nchi nzima, na hivyo kukidhoofisha chama changu cha TLP kwa lengo la kutaka kukiua kabisa. Kwa nini wasiwarubuni na kuwanunua wana CCM kama wao ni wapinzani wa kweli? Na ndio maana ukawa umevamia jimbo la Vunjo, nia yao ni ile ile ya kuifuta TLP na isiwe na Mbunge wala diwani.

Tujiulize kama kweli ukawa una nia ya kuimarisha upinzani, ni kwanini wasiwekeze nguvu zao kwenye majimbo ya CCM, mfano Same, Mwanga, Moshi Vijijini n.k. ni kwa nini wanawekeza nguvu nyingi kwenye jimbo la Vunjo ambalo tayari ni la mpinzani mwenzao. Je, huko ndiko kuimarisha upinzani? Sasa nitajiungaje na watu kwa makusudi kabisa wamedhamiria kukifuta chama changu.

Watu hao sio wapinzani wa kweli bali ni wapinzani maslahi, mimi ndiye mpinzani wa kweli kwa sababu nilikubali kupoteza uwaziri na ubunge na kujiunga na upinzani ili niweze kuwatetea na kuwatumikia vizuri wananchi kwa lengo la kuboresha utawala bora na maendeleo ya Taifa letu.

  1. Ndani ya UKAWA kuna baadhi ya vyama ambavyo vinafadhiliwa na vyama vya siasa vya ulaya na Marekani ambavyo vinashabikia ushoga na ndoa za jinsia moja jambo ambalo ni kinyume cha imani za dini zetu zote za kiislamu na kikristo na pia, ni kinyume cha mila na desturi za kiafrika. Binafsi, mimi pamoja na chama changu hatuwezi kukubali ufadhili wa namna hiyo, kwa sababu ni dhambi mbele ya Mungu.

  1. Kuna watu wengine wanaodai kwamba mimi ni kibaraka wa CCM kwa sababu nimekuwa nikiunga mkono baadhi ya hoja za serikali ndani ya bunge. Napenda niwaelimishe watu hao kwamba maana ya upinzani sio kupinga kila kitu, hata jambo lenye maslahi kwa Taifa. Hata huko ulaya na Marekani ambako Demokrasia ya vyama vingi ndiko ilikoanzia wapinzani hawapingi kila kitu, bali hufanya uchambuzi iwapo suala husika lina maslahi kwa wananchi na kwa Taifa, na mimi ndivyo navyofanya. Kama suala lina maslahi kwa wananchi na Taifa siwezi kulipinga eti kwa sababu tu limeletwa na serikali ya CCM. Mimi natanguliza mbele maslahi ya wananchi na taifa badala ya maslahi ya vyama vyetu vya siasa. Lakini serikali inapoleta hoja zisizofaa ambazo hazina maslahi kwa taifa siku zote nimekuwa mstari wa mbele kuzipinga

Kwa mfano, majuzi nilipinga bajeti ya serikali ya mwaka 2015 /2016 kwa sababu imepandisha kodi ya mafuta ya taa, petrol na dizeli jambo ambalo ni mzigo kwa wananchi na litasababisha bei za vyakula kupanda na hatimaye ongezeko la umaskini.

  1. MAJIBU KWA KATIBU MKUU WA CCM, MHE. KINANA
Mhe. Abdularahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM alipofanya mikutano ya hadhara jimboni Vunjo aliwaambia wananchi wa Vunjo wasinichague kwa sababu nimekula T.shs milioni 400, fedha ambazo alidai ni ruzuku za mfuko wa Jimbo la Vunjo ndani ya kipindi cha miaka minne. Aliwaambia wananchi wasinichague kwa kuwa mimi ni mpinzani, sina serikali, sina waziri wala Rais, hivyo sitoweza kuwaletea maendeleo. Naomba kueleza ukweli kuhusu madai ya Mhe. Kinana kama ifuatavyo:

a. Kwamba fedha, halisi zilizotolewa kwenye mfuko wa maendeleo ya jimbo la Vunjo tangu 2010 mpaka leo ni T.shs milioni 150 na wala sio Tshs milioni 400 kama Mhe. Kinana anavyodai. Pia, fedha ziko chini ya kamati ya Maendeleo ambayo Makamu Mwenyekiti wake ni diwani, Mhe. Chongi wa CCM, na katibu wake wa huo mfuko ni Afisa Mipango wa Halmashauri ya Moshi Vijijini. Fedha hazitoki bila idhini ya kamati hiyo na zinaidhinishwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi Vijijini na huwa zinapelekwa moja kwa moja kwa watendaji wa Kata zinazohusika.

Ukijumlisha fedha zote kwenye jedwali lililopo kwenye kitabu hichi, fedha zilizosimamiwa na Mbunge kuleta maendeleo na kutoa huduma kwenye jimbo la Vunjo ni T.shs 416,880,000/=. Ukiondoa fedha za ruzuku za mfuko wa Jimbo T.shs milioni 150, zinabaki T.shs 266,680,000/= ambazo zinatokana na mchango wangu binafsi na marafiki zangu. Kwa hiyo madai hayo ni ya uongo na ya kunipakazia uliotungwa makusudi na Mhe. Kinana kunichafua ili wananchi waninyime kura kwa lengo la kumnufaisha mgombea wa chama chake. Nawaombeni wananchi wa Vunjo mpuuze uongo huo.

b. Kuhusu madai kwamba wapinzani hatuwezi kuleta maendeleo kwa vile hatuna serikali, hatuna Rais wala waziri, madai hayo sio sahihi na yana harufu ya ubaguzi, ni kuwabagua watanzania ambao si wanachama wa CCM. Kwa sababu kwa mujibu wa katiba ya nchi, diwani, mbunge, waziri na Rais wa kisha chaguliwa wanakuwa viongozi wa wananchi wote kwa ujumla na hawatakiwa kubagua wala kufanya upendeleo kwa misingi ya vyama vya siasa.

Madai ya Mhe. Kinana si ya kweli kwa sababu kuna baadhi ya majimbo yanayoongozwa na wabunge wa upinzani yamepata maendeleo makubwa kuliko yanayoongozwa na wabunge wa CCM.Maendeleo ya jimbo yanatokana na uzalendo, moyo wa kujituma, uchapakazi na ubunifu wa Mbunge husika haijalishi kama yuko CCM au upinzani. Kwa mfano, mambo makubwa ya kimaendeleo niliyosimamia kwenye jimbo la Vunjo na kutatua kero za wananchi ni kama ifuatavyo:

  1. Nimefuatilia kwa ukaribu mgogoro kati ya walimu wa Moshi vijijini na Maafisa wa Halmashauri ya Moshi kuhusu maslahi yao kuanzia mwaka 2012 ambao serikali iliwalipa stahiki mbalimbali walizokuwa wakidai na mpaka kufikia Februari 2015 jumla ya shilingi milioni 676.7 zimelipwa kwa walimu, shilingi millioni 579 kwa ajili ya malimbikizo ya mishahara. Pia, milioni 646.8 zimelipwa kwa walimu kwa ajili ya uhamisho, likizo, matibabu, gharama za mazishi na masomo.

  1. Kuomba na kufanikiwa kupata ufadhili kutoka Marekani T.shs. 50,000,000 nikishirikiana na Diwani David Koka wa Mamba Kusini, kusomesha watoto 34 katika shule za sekondari Nronga O level, Vunjo Sekondari A level na Agape Seminari za Mamba Kusini na ufadhili huo unaendelea mpaka Vyuo Vikuu. January 2016 tutaingiza vijana, yatima na watoto ambao wako kwenye mazingira magumu wajimbo zima la Vunjo ili wapate fursa ya kusoma mpaka Vyuo Vikuu.

  1. Nimefanikisha upatikanaji wa ukanda wa nusu maili kwa ajili ya wananchi kukata majani na kukusanya kuni zilizokauka. Walionufaika na mradi huo ni wananchi wa Kirua Vunjo Magharibi, Kirua Vunjo Mashariki, Kilema Kaskazini, Marangu Magharibi, Marangu Mashariki, Mamba kaskazini na Mwika Kaskazini

  1. Nimeasisi wazo la kuwa na soko la kimataifa LOKOLOVA ili kuinua uchumi wa Vunjo, Kilimanjaro na Taifa kwa ujumla. Kilichobaki ni kushirikiana na wana Lokolova na Rais ajaye ili kukamilisha na kuhakikisha soko hilo linajengwa

  1. Katika kipindi changu cha ubunge nimefuatilia kwa ukaribu kwa ushirikiana na Wizara ya Miundombinu kuhakikisha barabara muhimu zimetengenezwa. Ambazo ni:

  1. Barabara ya MARANGU MTONI mpaka KILEMA SOKONI kwa kiwango cha lami

  1. Barabara ya KAWAWA kwenda NDUONI, KIRUA VUNJO MAGHARIBI kwa kiwango cha lami

  1. Barabara ya UCHIRA kwenda KISOMACHI, KWALARIA kiwango cha changarawe

1) KATA YA MWIKA KASKAZINI

MSAADA
KIASI
1
Mrimbo uuwo - Ukarabati wa Madarasa shule ya msingi Kirimeni
1,500,000
2
Maringa-Ukarabati wa Madarasa shule ya msingi Maringa juu
2,000,000
3
Msae nganyeni Ujenzi wa bweni Lyakirimu sekondari
3,000,000
4
Kupanua chumba cha kuhifadhia maiti - Msae
2,000,000
5
Ujenzi wa kanisa la Baba Askofu - Lole
2,000,000
6
Lole Marera - Ujenzi wa barabara ya Kokipura
1,000,000
7
Ujenzi wa mahabara ya Lyakirimu sekondari
500,000

JUMLA
12,000,000

2) KATA YA MWIKA KUSINI

MSAADA
KIASI
1
Ukarabati wa madarasa shule ya msingi - Kiruweni
1,000,000
2
Ujenzi wa zahanati - Kiruweni
2,000,000
3
Ujenzi wa kivuko cha Marero Mecha - Kondeni
2,000,000

Kivuko cha More - Kimangaro
1,000,000
4
Japron Zakayo Macha - Mwananchi aliyeunguliwa na Nyumba, kimangaro, More
500,000
5
Daraja la Kwamorera - Kimangaro
1,000,000
6
Ukarabati wa darasa - Mawanjeni
1,000,000
7
Shule ya msingi - Kirueni
1,000,000
8
Kikundi cha kinamama Kirueni
1,000,000
9
Kikundi cha kinamama Kondeni
1,000,000

JUMLA
11,500,000


3) KATA YA MAMBA KASKAZINI

MSAADA
KIASI
1
Kokirie - ujenzi wa nyumba ya walimu Kokirie sekondari
3,000,000
2
Ukarabati wa madarasa
1,000,000
3
Komakundi-ukarabati miundo mbinu ya maji
500,000
4
Ukarabati wa uwanja wa mpira
2,990,000
5
Mchango wa maabara Kokirie sekondari
1,000,000
6
Ujenzi wa paa Kotela
1,000,000
7
KKKT - Kotela
500,000
8
Shule ya Ufundi - Mwangaria
500,000

JUMLA
10,490,000

4) KATA YA KILEMA KASKAZINI

MSAADA
KIASI
1
Ujenzi wa choo cha shule msingi Kilai - Ruwa
1,000,000
2
Ujenzi wa choo cha shule ya msingi - Makame juu
1,500,000
3
Ukarabati wa madarasa shule ya msingi - Makame chini
500,000
4
Ujenzi wa choo cha shule ya msingi - Kyou
500,000
5
Ujenzi wa ofisi ya kijiji - Makame juu
1,000,000
6
Ujenzi wa ofisi ya kijiji - Makame chini
1,000,000
7
Fedha za mkopo za kikundi cha Mkombozi
1,000,000

JUMLA
6,500,000

5) KATA YA MAMBA KUSINI

MSAADA
KIASI
1
Ujenzi wa choo cha shule ya msingi Kimbogho
2,000,000
2
ujenzi wa choo cha shule ya msingi Mseroe - Mkolowoni
1,500,000
3
Ukarabati wa madarasa na kuweka umeme shule ya Sekondari Mamba Day
1,000,000
4
ujenzi wa mfereji shokoni - Kiria
1,000,000
5
Ukarabati kanisa Rauyamamba KKKT
1,000,000

JUMLA
6,500,000

6) KATA YA KILEMA KATI

MSAADA
KIASI
1
Mkyshi-ujenzi wa choo shule ya msingi Kisuluni
1,000,000
2
Ujenzi wa choo shule ya msingi Kichilioni
500,000
3
Ununuzi wa jokofu la kuhifadhia maiti Kilema hospitali
5,000,000

Kusaidia kituo cha watoto yatima
1,000,000
4
Ujenzi wa maabara sekondari kisuruni
1,000,000
5
Novatus Mbando - mkopo wa kuanzisha M-pesa - Mkyashi
1,000,000
6
Mkopo wa kuimarisha M-pesa inayoitwa Lyaruu family-Kimaroroni
1,000,000

JUMLA
10,500,000

7) KATA YA MARANGU MASHARIKI

MSAADA
KIASI
1
Mshiri - ukarabati wa tenki la maji Ashira
3,500,000
2
Samanga - msaada wa kununua baiskeli ya walemavu
1,000,000
3
Arisi - kununua vifaa vya manesi Marangu hospitali
500,000
4
Samanga- ukarabati wa madarasa shule ya msingi Palangeni
1,000,000
5
Lyasongoro - ujenzi wa shule ya msingi Andrea
1,000,000
6
Harambee shule ya sekondari darajani
1,000,000
7
Ujenzi wa choo cha walimu Mrokora
2,000,000
8
Ujenzi wa maabara Rasesa sekondari
1,000,000
9
Msaada kwa Mmasai mlemavu - Mshiri
100,000

JUMLA
11,100,000

8) KATA YA KILEMA KUSINI

MSAADA
KIASI
1
Kilototoni-ujenzi wa shule ya msingi Kilototoni
1,500,000
2
Marawe kyura-ujenzi wa choo shule ya msingi Ngangu
2,500,000
3
Legho Mulo-ujenzi wa zahanati Legho Mulo
1,000,000
4
Ukarabati wa bweni lililoungua moto Muungano Sekondari
21,000,000
5
Legho Mulo- ukarabati wa shule ya msingi Legho
500,000
6
Ukarabati wa shule ya msingi Mulo
500,000
7
Ujenzi wa bwalo St. Amediusi sekondari
2,000,000
8
Kilema chini-ujenzi wa kanisa RC Kilema Chini
1,000,000
9
Kutengeneza ghala la kuhifadhi nafaka Muungano sekondari
1,000,000
10
Kutengeneza viwanja vya mpira shule ya Njia Panda, uwanja mpira wa umma Njia Panda na uwanja wa sekondari Muungano
1,610,000
11
Ununuzi wa viti vya kanisa Kilema Pofo
1,000,000

JUMLA
33,610,000

9) KATA YA MAKUYUNI

MSAADA
KIASI
1
ujenzi wa choo cha shule ya msingi Saghana Himo Makuyuni
2,000,000
2
Mradi wa umwagiliaji maji Makuyuni
1,000,000
3
ukarabati wa vyoo Meresini sekondari - Himo
1,000,000
4
Kulipia ada watoto yatima shule ya sekondari Himo
1,000,000
5
Ujenzi wa madarasa ya watoto wa chekechea KKKT Himo
3,500,000
6
Kutengeneza kiwanja cha mpira Himo
2,500,000
7
Ujenzi wa chekechea ya Msikiti wa Himo
1,000,000
8
Lotima-kununua mabomba ya maji
500,000
9
Himo-mchango wa ujenzi wa madarasa Hope Academy
1,500,000
10
Ujenzi wa kivuko na kuweka karavati-Kiriche
1,100,000
11
Mchango wa Maendeleo - Lokolova
1,000,000

JUMLA
16,100,000

10) KATA YA KIRUA VUNJO MASHARIKI

MSAADA
KIASI
1
Laso-ukarabati wa madarasa shule ya msingi Laso
750,000
2
Kileuo-ujenzi wa choo cha walimu shule ya msingi Msufini
750,000
3
Kileuo-ukarabati wa zahanati Karumeli
1,000,000
4
Ukarabati wa shule ya chekechea Urenga
1,000,000
5
Mfereji wa umwagiliaji Nganjoni (ukarabati)
1,000,000

JUMLA
4,500,000

11) KATA YA KIRUA VUNJO MAGHARIBI

MSAADA
KIASI
1
Nduoni-ujenzi wa jiko shule ya msingi Nduoni
500,000
2
Iwa-ukarabati wa madarasa na choo
500,000

Ujenzi wa sekondari ya Iwa
1,000,000
3
Kwa Mare-ujenzi wa choo shule ya msingi Kokira
1,000,000
4
Iwa-mchango wa ujenzi wa maabara
1,000,000

JUMLA
4,000,000

12) KATA YA KIRUA VUNJO KUSINI

MSAADA
KIASI
1
Uchira - ujenzi wa jiko sekondari ya Mashingia
1,000,0000
2
ujenzi wa bwalo na ukarabati wa madarasa shule ya msingi - Makaa
1,000,0000
3
Kukamilisha ujenzi wa madarasa shule ya msingi Nanga
500,000
4
Uchira -mchango wa ujenzi wa maabara Mashingia sekondari
500,000
5
Kikundi cha vijana ZECA - Uparo
500,000
6
Shule ya Msingi Azimio - Madawati ya NMB
3,500,000

JUMLA
7,000,000

13) KATA YA KAHE MASHARIKI

MSAADA
KIASI
1
Kyomu- kukamilisha ujenzi wa ofisi ya Kata
2,000,000
2
Kukarabati madarasa shule ya msingi Majengo
1,000,000
3
Ghona ujenzi wa vyoo shule ya msingi Ghona
1,000,000
4
Mchango wa maabara Ghona sekondari
1,000,000
5
Ujenzi wa ofisi ya kijiji - Mkameni
1,000,000

JUMLA
6,000,000

14)
KATA YA KAHE MAGHARIBI

MSAADA
KIASI
1
Ngasinyi- ukarabati wa madarasa Mangoto sekondari
500,000
2
Ukarabati wa madarasa shule ya msingi Kahe
500,000
3
Mwangaria ukarabati wa madarasa na vyoo Mwangaria
1,000,000
4
Ujenzi wa kanisa la Mwangaria Kimala KKKT
500,000
5
Rau River-ukarabati wa madarasa
500,000
6
Msaada kwa mtu mwenye ulemavu
500,000
7
Ukarabati wa madarasa shule ya msingi Oria
1,000,000
8
Ujenzi wa madarasa Maendeleo shule ya msingi
1,000,000
9
Ujenzi wa kanisa KKKT Mkonga
500,000
10
Kisangesangeni- ukarabati wa darasa shule ya msimgi Kisangesangeni
1,000,000
11
Mawala-ujenzi wa chekechea Mawala KKKT
1,000,000
12
Ujenzi wa chekechea Kimala KKKT
500,000

JUMLA
8,500,000

15) KATA YA MARANGU MAGHARIBI

MSAADA
KIASI
1
Kununua kiwanja cha soko la akina mama - Kiraracha
5,000,000
2
Ujenzi ngazi ya ghorofa shule ya msingi - Kiraracha
2,000,000
3
Makomu-ujenzi wa Makomu sekondari
1,500,000
4
Nduweni-ukarabati wa madarasa shule ya msingi Nduweni
1,000,000
5
Ukarabati wa madarasa Mlanga sekondari
1,000,000
6
Ukarabati wa mabomba ya maji - Kyala
1,000,000
7
Kyala ukarabati barabara Tangusa Uomboni
1,000,000
8
Kiraracha-ujenzi wa ofisi ya kijiji Kiraracha
2,500,000
9
Ujenzi wa sekondari - Kiraracha
1,000,000
10
Augusti Bazili Temu Msaada wa ujenzi wa nyumba yake
500,000
11
Makomu - Ujenzi wa Kanisa
1,000,000
12
Mbahe ukarabati wa Barabara
1,000,000
13
Uomboni - Mchango wa Kanisa
2,000,000
14
Kiraracha - Mfuko wa Sungusungu
2,000,000
15
Zahanati ya Uomboni
1,000,000
16
Mkopo wa wajasiriamali kwa ajili ya kuanzisha mradi wa Nguruwe kupitia kwa Israel Mtui (M/kiti wa kijiji Komalyagoe)
1,000,000

JUMLA
24,500,000

Pia, nimesaidia vikundi vya wakina mama,vijana na wazee ili viweze kufanya kazi za uzalishaji mali ili kujiongezea kipato, Vikundi hivyo ni:-

MAHALI KINAPATIKANA
KIASI
1
WAWALYA GROUP Marangu Mashariki
1,000,000
2
NEEMA GROUP Mwika Kaskazini
1,000,000
3
MREMA GROUP
Marangu Mashariki
1,000,000
4
UWT GROUP MwikaKaskazini
1,000,000
5
MTARONI GROUP Kahe Magharibi
1,000,000
6
WAWARA GROUP
Rawiya, Marangu Mashariki
1,500,000
7
EBENEZA GROUP
Marangu Mashariki
500,000
8
FARAJA GROUP
Lyasongoro, Marangu Mashariki
500,000
9
TUMAINI GROUP
Marangu Mashariki
1,000,000
10
UPENDO GROUP Mamba Kusini
1,000,000
11
FARAJA GROUP Marangu Mashariki
1,000,000
12
UKOMBOZI GROUP Marangu magharibi
1,000,000
13
NGUVU KAZI GROUP Mwika Kusini
1,000,000
14
WAZEE WASTAAFU GROUP Marangu Magharibi
1,000,000
15
FURAHA GROUP Kilema Kati
1,000,000

16
HATUDANGANYIKI GROUP Mwika Kaskazini
1,000,000
17
MUUNGANO GROUP
Marangu Mtoni
3,000,000
18
AMANI GROUP
Kilema Kati
1,000,000
19
TUJIKOMBOE GROUP
Kahe Magharibi
1,000,000
20
NGUVU KAZI GROUP
Kahe Mashariki
1,000,000
21
UPENDO GROUP
Kilema Kusini
1,000,000
22
MWANGAZA GROUP
Kilema Kaskazini
1,000,000
23
NEEMA GROUP
Himo Makuyuni
1,000,000
24
EBENEZA GROUP
Himo Makuyuni
1,000,000
25
TUTARAMANE GROUP
Mashariki
1,000,000
26
AGAPE GROUP
Kirua Mashariki
1,000,000
27
COMFORT GROUP
Kilema Kusini
1,000,000
28
JIKOMBOE GROUP
Mwika Kaskazini
1,000,000
29
MBOGA MBOGA GROUP
Karisia, Kiraracha
1,000,000
30
WAJANE GROUP
Marina, Mwika Kaskazini
1,000,000

JUMLA
27,000,000

VUNJO DEVELOPMENT CHARITY FOUNDATION
Kulikuwa na vikundi vya wajasiriamali wadogo wadogo kama wafuatavyo:-

MAHALI KINAPOPATIKANA
KIASI
1
MBOGA MBOGA GROUP
Njia Panda
1,000,000
2
UPENDO GROUP
Kilema Chini
1,000,000
3
FARAJA GROUP
Legomulo
1,000,000
4
KIWANU GROUP
Legomulo
1,000,000
5
MAMALISHE GROUP
Himo-Makuyuni
1,000,000
6
KILEO GROUP
Njia Panda
1,000,000
7
FURAHA A GROUP
Himo
1,000,000

JUMLA
7,000,000

Hata hivyo, nimetoa mikopo kwa Wenyeviti wa Vijiji ni kama ifuatavyo:

MAJINA
KIASI
1
ANDREW A.LEKULE
Kijiji cha Kiraracha
1,000,000
2
ALOISIA E.LYARUU
Kijiji cha Maroroni
1,000,000
3
ISRAEL E. MTUI
Kijiji cha Angoe
1,000,000
4
ANTONIA E. KITALY
Kijiji cha Kyala
1,000,000
5
GABRIEL N. MALEO
Kijiji cha Mbahe
1,000,000
6
ELIAS S.LYIMO
Kijiji cha Arisi
1,000,000
7
EDWARD S. LYIMO
Kijiji cha Maringa
1,000,000
8
JACOB KIMARO
Kijiji cha Lole
1,000,000

JUMLA
8,000,000



Uendeshaji wa Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Vunjo 2010 - 2015
65,600,000

MAFANIKIO YANGU NA MALENGO YANGU
Naamini katika uwekezaji katika huduma za jamii. Elimu na afya bora, mazingira, makazi safi na maji salama ndiyo mihimili ya maendeleo ya watu.

MSAADA BINAFSI

  1. Nimesaidia kwa hali na mali na kwa kadri ya uwezo niliokuwa nao kuhakikisha baadhi ya familia zilizopata matatizo ya msiba katika Jimbo langu la Vunjo, niliweza kusaidia kwa kutoa rambirambi kwa wafiwa na jumla ya kiasi cha T.shs milioni
32, 650, 000 kimetumika.

  1. Nimetoa msaada kwa Mwananchi aliyeunguliwa na nyumba Bwana Paul Justin Ngowi T.shs 1,000,000/=
  2. Nimenunua gari aina ya Coaster (Bus), T.shs 45,000,000/= kwa ajili ya kusaidia wana Vunjo kwa ajili ya kwenda kwenye mazishi, shambani, sokoni ndani na nje ya Jimbo la Vunjo

SEKTA YA ARDHI

  1. Nimetetea wana LOKOLOVA kuhakikisha ushirika wao ambao ulikuwa umefutwa umerejeshwa.
  2. Nimetetea heka 2,000 za wana ushirika wa Lokolova zilizotaka kuporwa zisiporwe. Nimeshirikana na wana Lokolova kubadili aina ya ushirika kutoka ushirika wa kilimo na wafugaji kuwa ushirika wa makazi, nyumba na biashara.
  3. Nimewatetea wafugaji wa Mawala, Kata ya Kahe Magharibi eneo lao la ufugaji lisiporwe na matajiri
  4. Nimetetea eneo la Meresini lisiporwe na matajiri na badala yake lipatikane eneo la kujenga shule ya sekondari ya Meresini kidato tano (5) na cha sita (6), vipatikane viwanja vya michezo na ujenzi wa masoko. Nimeshauri serikali ifute hati zote za matajiri walionyakua ardhi ya Meresini bila kuzingatia vipaumbele vya jamii. `
  5. Nimewatetea na kuwasemea wakulima wa zao la kahawa ili kuzuia rasilimali zao zisipigwe mnada kufidia ulaji uliofanywa na vigogo wa KNCU, mfano mzuri nyumba za TCCCO Limited na shamba la Gararagua lenye ukubwa wa hekari 3,000 ambalo lilitakiwa kuuzwa kwa T.shs shillingi bilioni 10.

SEKTA YA ELIMU
Napenda kusisitiza kuwa elimu ndiyo muhimili wa maendeleo, ndiyo mkombozi wa kweli wa binadamu. Mama akiwa na elimu atajua umuhimu wa kumpeleka mwanae shule, anapata lishe bora na chanjo stahili na kuwa anaishi katika mazingira safi. Elimu ndilo jibu la umaskini, maradhi na ujinga.Taifa lililo elimika ni taifa lenye maendeleo

  1. Nimesaidia kulipa ada za watoto, kununua madaftari, uniform na viatu kwa familia wasiokuwa na uwezo katika kipindi changu cha ubunge 2010 2015 kiasi cha T.shs 12,500,000/=zimetumika kwa kazi hiyo
  2. Nimechangia na nitaendelea kuchangia sehemu ya mshahara wangu wa kila mwezi kwenye masuala mbalimbali ya elimu. Mojawapo ni kuwapa walimu kiasi cha T.shs milioni 10 kwa ajili ya Saccos ya waalimu wa Moshi Vijijini.

SEKTA YA AFYA

  1. Nimeweza kusimamia na kumalizika kwa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya, Himo Mjini na kuhakikisha watoto walio chini ya umri wa miaka mitano, wajawazito na wazee wanatibiwa bure. Nitaendelea kuhakikisha huduma hizo zinaendelea kupatikana
  2. Pia, kuhimiza serikali kuwalipa wazee kiinua mgongo chao kama walivyoahidiwa
  3. Nimewasaidia wananchi wangu wenye shida mbalimbali kama matibabu, usafiri, wajawazito, wajane kiasi cha T.shs 7,330,000/=

SEKTA YA AJIRA

  1. Nimesimamia na kuhakikisha soko la LOKOLOVA linajengwa ili vijana wapate ajira, wakulima wanapate sehemu ya kuuzia mazao yao na bidhaa za viwanda vidogo vidogo zinapata soko
  2. Nimefuatilia kwa ukaribu ujenzi wa soko la Mwika ili nalo lilete ajira kwa wananchi wa Vunjo
  3. Nitaendelea kusaidia kuwezesha upatikanaji wa mitaji kwa vijana na wanawake kuweza kujiajiri. Orodha ya vikundi vilivyopatiwa mikopo na mitaji mpaka sasa katika Jimbo la Vunjo ni kama ilivyoorodheshwa hapo awali.
  4. Nitatetea wafanyabiashara wadogo kuendelea kutengewa maeneo ya biashara na hatua zitaendelea kuchukuliwa kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo wadogo ambao hawajapata maeneo mpaka sasa.

SEKTA YA MIUNDO MBINU
Nimekuwa nikifuatilia ujenzi wa Miundombinu jimboni kwangu kwa sababu naamini Miundombinu ambayo ni barabara, maji, umeme ikiwa mizuri uchumi unakuwa vizuri


  1. MAJI

  1. Nimefanikiwa upatikanaji wa mradi wa maji ya kunywa Himo, wenye thamani wa T.shs 450,000,000 katika fedha hizo nilimwomba Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete kiasi T.shs.150,000,000/= ili kukamilisha usambazaji wa maji katika mji mdogo wa Himo.
  2. Kwa upande wa Njia Panda tulipata T.shs 820,000,000 kutoka serikali ya Ujerumani kwa ajili ya kusambaza maji Njia Panda
  3. Nimekuwa nikifuatilia mkopo wa T.shs bilioni tano kutoka Benki ya dunia kwa ajili ya kusambaza maji safi ya kunywa katika vijiji vya Makame juu, Makame chini, Lotima, Himo Makuyuni na Mawanjeni
  4. Nimemwandikia Rais mchanganuo (proposal) kwa ajili kusambaza maji Mwika Kaskazini na Mwika Kusini


  1. MIRADI YA UMWAGILAJI MAJI

  1. Umwagaliaji maji kutoka mto Ghona kupita mfereji wa Mchomba kwa ajili ya umwagiliaji mashamba ya Sembeti, Rauya na Matala mradi uliofadhiliwa na serikali wa T.shs 300,000,000/=
  2. Skimu ya Mawala heka 3,000 za umwagiliaji mpunga na serikali imetoa T.shs 249,000,000 kwa ajili ya kurekebisha mifereji mitatu ili kukamilisha skimu hiyo, inatarajia kuisha mwezi Agosti
  3. Mfereji wa Kimangamao umejengwa kilomita 2.3 bado kilomita 4.3 haujajengwa. Tunahitaji angalio T.shs 250,000,000 ili tuweze kujenga kilomita 2. Nashukuru wananchi kwa nguvu kazi


  1. BARABARA
Nitaendelea kushirikiana na Wizara ya Miundombinu kuhakikisha barabara muhimu zifuatazo zinatengenezwa katika kipindi kijacho.

  1. Barabara ya KILEMA POFU kwenda KILEMA HOSPITALI kujengwa kwa kiwango cha lami.
  2. Barabara ya KILEMA SOKONI kwenda KIRUA VUNJO MAGHARIBU itajengwa kwa kiwango cha lami
  3. Kujengwa na kupanuliwa kwa Madaraja yaliyoko barabara ya MARANGU MTONI kwenda KILEMA SOKONI
  4. Kuunganisha bararabara ya NDUONI kwenda KILEMA SOKONI kwa kiwango cha lami
  5. Kufuatilia awamu ya pili ya ujenzi wa barabara ya lami kutoka KILEMA SOKONI kupitia MAUA SEMINARI mpaka NJIA PANDA
  6. Barabara ya KOCHAKINDO kwenda KIOMU kwa kiwango cha Changarawe
  7. Barabara ya MAMBA SOKONI kwenda MAMBA KASKAZINI kwa kiwango cha Changarawe
  8. Kuhimizi ujenzi wa barabara ya Fongageti kupitia Mabogini kwenda Kahe kwa kiwango cha changarawe
  9. Kufuatilia na kufungua barabara ya kilema kwa ajili ya kuteremshia watalii


  1. NISHATI YA UMEME
Usambazaji wa umeme Jimbo la Vunjo (REA) 2013/2014
Nimeweza kupambana na tatizo la umeme ndani ya Jimbo langu la Vunjo. Nimefanikiwa kuomba Shirika la kusambaza umeme vijijini {REA} kusambaza umeme katika maeneo yafuatayo:
1. Kilema Pofo Neema
2. Kilema Pofo Upendo
3. Kilema Kusini Njia Panda A
4. Kilema Kusini Njia Panda B
5. Kilema Kusini Kilototoni 1-2
6. Kahe Mashariki- Ghona
7. Marangu MagharibiKarisini
8. Marangu Magharibi Kitowo
9. Makuyuni -Lotima 1,2,3 na 4
10. Mwika Kusini Matala
11. Mwika Kusini Karoro
12. Mwika Kusini Mariale
13. Mwika Kusini Mawanjeni
14. Mwika Kusini Madukani
15. Mwika Kusini Mawanjeni II
16. Kirua Vunjo Yamu Juu
17. Kirua Vunjo Yamu Chini
18. Ngasinyi Miwaleni

Gharama za kuingiza umeme wa ndani ya nyumba T.shs 27,000, kadi T.shs 59,000. Kwa wale wenye maisha duni kuunganisha umeme ni T.shs 36,000.


  1. Taarifa Ya Maendeleo Ya Miradi Ya Umeme Katika Jimbo La Vunjo2014/2015
Katika kuboresha huduma ya umeme katika Jimbo la Vunjo, Shirika la Umeme TANESCO linamiradi mbalimbali ya Umeme iliyokamilika na inayoendelea.


  1. Ujenzi wa Kituo Kipya cha Makuyuni Himo
Mojawapo ya miradi muhimu na mkubwa uliokamilika ni kujengwa kwa kituo kipya cha chenye ukubwa wa 20MVA (2X10MVA) katika eneo la Makuyuni Himo. Kituo hiki kipya cha Makuyuni unasambazwa umeme kupita njia kuu nne:-

  1. Njia ya Marangu - Maeneo yanayofaidika na umeme ni Marangu mpaka Mwika
  2. Njia ya Himo - Maeneo yanayofaidika na umeme ni Himo mjini na Holili
  3. Njia ya Kilema - Maeneo yanayofaidika na umeme ni Kilema yote, Kirua Vunjo na maeneo ya Pumuani
  4. Njia ya Rombo - Maeneo yatakayofaidika na umeme ni Lotima, Rombo mkuu mpaka Tarakea

Kutokana na ujenzi wa kituo hiki kimeboresha sana upatikanaji wa umeme mzuri katika maeneo yote ya Jimbo la Vunjo na kuwa chachu ya maendeleo ya wananchi katika Jimbo hili


  1. Miradi inayofanywa na Tanesco
Katika budget ya mwaka jana wa 2014/2015 katika Jimbo la Vunjo, TANESCO wamepewa jumla ya Tshs. 129,360,132.00/= za miradi mbalimbali ya kuendelea kuboresha miundombinu katika Jimbo la Vunjo. Tanesco inaendelea kutekeleza na kukamilisha miradi katika eneo moja baada ya jingine hii yote ni kutaka kuhakikisha wateja wao wanapata umeme wa uhakika ili kukidhi malengo yao ya kiuchumi na maisha kwa jumla.


  1. Miradi Ya Umeme Vijijini (REA)
Katika maeneo ya Jimbo la Vunjo kuna miradi ya umeme vijijini (REA) yenye thamani ya Tshs 3,562,475,999.65/= inayoendelea katika maeneo mbalimbali, ifwatayo ni taarifa fupi ya maeneo na maendeleo ya miradi hii:-


ENEO
(KIJIJI)
LINE
KUBWA
TRAN-
SFOMA
LINE NDOGO
WATEJA
WALIOU-
NGA-
NISHIWA
MAONI
1
Neema village
100%
1
100%
12
Utakamilika Juni 30
2
Upendo village
100%
1
100%
NIL
Utaanza Juni 01
3
Njia panda-1 village
100%
0%
0%
NIL
Utaanza Juni 01
4
Njia panda-2 village
100%
0%
0%
NIL
Utaanza Juni 01
5
Kilototoni-1 village
100%
1
100%
77
Utakamilika Juni 30
6
Kilototoni-2 village
100%
1
100%
84
Utakamilika Juni 30
7
Ghona VTC village
100%
1
100%
28
Utakamilika Juni 30
8
Karisia village
100%
1
75%
NIL
Utaanza Juni 01
9
Kitowo village
0%
0
0%
NIL
Utaanza Juni 01
10
Lotima-1 village
100%
1
100%
31
Utakamilika Juni 30
11
Lotima-2 village
100%
1
100%
79
Utakamilika Juni 30
12
Lotima-3 village
100%
1
100%
39
Utakamilika Juni 30
13
Matala village
100%
1
100%
103
Utakamilika Juni 30
14
Karoro village
0%
0
0%
NIL
Utaanza Juni 01
15
Mareale village
0%
0
0%
NIL
Utaanza Juni 01
16
Mawanjeni Madakuni
0%
0
0%
NIL
Utaanza Juni 01
17
Mawanjeni "B" village
0%
0
0%
NIL
Utaanza Juni 01
18
Mawanjeni kati village
0%
0
0%
NIL
Utaanza Juni 01
19
Mawanjeni kkkt church
10%
0
0%
NIL
Utaanza Juni 01
20
Yamu juu village
75%
0
0%
NIL
Utaanza Juni 01
21
Yamu chini village
75%
0
0%
NIL
Utaanza Juni 01
22
Miwaleni village
100%
1
100%
85
Utakamilika Juni 30
23
Mauru village
100%
1
100%
89
Utakamilika Juni 30
24
Sangesangen Village
100%
1
100%
44
Utakamilika Juni 30
25
Mkonga village
100%
1
100%
41
Utakamilika Juni 30
26
Holili pre-school & village
100%
1
100%
67
Utakamilika Juni 30

Kwa sasa Mkandarasi aitwae SPENCON SERVICE LTD yuko site na anaendelea kufanya kazi za miradi hii na Tanesco wanaendelea kuhamasisha wananchi kulipa kwa wakati hasa katika maeneo ambayo miradi imekamilika ili waweze kuunganishiwa umeme na kuanza kunufaika na huduma hii.

MICHEZO

  1. Nimewasaidia vijana wa Jimbo la Vunjo kwenye michezo kwa kuanzisha mashindano yanayoitwa MREMA CUP yaliyogharimu kiasi cha T.shs 12,000,000/=.
  2. Nitaendelea kuwasaidia watoto, vijana na wanawake kwenye michezo mbalimbali katika Jimbo langu.

NMB BENKI HIMO NA CRDB MARANGU MTONI
Nimefanikiwa kuhimiza ujenzi wa benki ya NMB Himo, nitahimiza kutoa mikopo kwa wafanya biashara ndogo ndogo, wafanya biashara wakubwa, vikundi vya akina mama, vijana na wazee ili waweze kupata mkopo kutoka Benki ya NMB Himo na CRDB Marangu Mtoni. Nitahimiza vyama vya msingi vya ushirika wa zao la kahawa kuuza kahama wenyewe kupitia benki hizi mbili ili wakulima waweze kupata bei nzuri ya kahawa ili kupunguza gharama zilizokuwa zinatokana na K.N.C.U

MFUKO WA JIMBO
Nitatumia mfuko wa jimbo nikishikiriana na wazazi pamoja na wafadhili kama kichocheo cha maendeleo kuhakikisha shule zote za msingi na sekondari katika jimbo la Vunjo zinakarabatiwa. Pia, kuwawezesha wananchi kujua haki zao, kutumia fursa zilizopo na namna ya kujiendeleza, haswa kwa akina mama, vijana na walemavu. Mfano; haki za mirathi kwa wajane na kukuza vipaji kwa vijana

UWAJIBIKAJI
Nimefanya mikutano na wananchi katika kata zote za Jimbo la Vunjo na kwenye maeneo mbalimbali ya kiserikali na ya kichama kwa ajili ya kutimiza wajibu wa uwakilishi kabla na baada ya vikao vya bunge

  1. Nimehakikisha halmashauri/ mawakala wanakusanya ushuru vizuri na unatumika kwa manufaa ya wananchi wote.
  2. Nimefuatilia kuhusu ujenzi wa kiwanda cha Njia Panda kilichojengwa kwenye makazi ya watu, mjenzi wa kiwanda hicho amepigwa faini.
  3. Nimehakikisha vizuizi(barrier) vinaondolewa ndani ya Jimbo la Vunjo viliyowekwa kwa kisingizio cha kukamata mali za magendo kama mahindi. Hivyo vizuizi vinabugudhi wananchi wa Vunjo kwa sababu, kwa mfano, mahindi yanalimwa Kata za Kilema lakini wananchi wanapo yapeleka mahindi hayo sokoni, Kata za Mwika wanakuta vizuizi Marangu Mtoni, wakati ni haki yao kuyapeleka sokoni kuuzwa
  4. Pia, nimewajibika katika kuisimamia serikali bungeni na kushiriki katika kutunga sheria. Lakini wakati huo huo sheria zinazo wakandamiza wananchi nazipinga, kwa mfano, katika bajeti ya mwaka huu iliyopandisha kodi ya mafuta ya taa kutoka T.shs 50 mpaka T.shs 150 kwa lita. Nilipinga kwa sababu kodi hiyo ni kubwa kwa wananchi wa kawaida.
  5. Nitahakikisha agizo la Waziri wa Maliasili na Utalii ambao linaagiza kwamba mbao za magendo zote zilizokamatwa zinatumike kujenga maabara na madawati ya shule.


MAELEZO BINAFSI

Naamini kwamba uongozi wangu katika nafasi ya Ubunge si kazi ya lelemama na inahitaji utashi. Na katika hilo, rekodi yangu inazungumza na kulithibitisha hilo.

Binafsi nina hazina ya uzoefu na rekodi njema ya matokeo ya kazi nilizozifanya katika uongozi na utumishi wa umma ndani ya Serikali, kwa mfano, kujenga vituo vya polisi na kufuta kodi za wanawake

Miongoni mwa mafanikio ninayojivunia katika uongozi na utumishi wangu, na ambayo wana Vunjo wanayatambua na naamini wanayathamini, ni pamoja na: kuwa Mbunge wa Moshi vijijini kwa miaka kumi (1985 1995), Mbunge wa Temeke miaka minne (1996 1999), Mbunge wa Vunjo miaka mitano (2010 2015), Naibu Waziri Mkuu, Waziri wa Mambo ya Ndani na Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana

Kutokana na rekodi yangu hii, naamini ninazo sifa za kuongoza Jimbo la Vunjo kwa miaka mingine mitano ijayo. Afya yangu imeimarika na nipo fiti kuwatumikia wana Vunjo. Naamini ninao uwezo wa kuwapa Wana Vunjo uongozi imara kwa ajili ya ujenzi wa Taifa imara.

Hata hivyo, maendeleo ya jimbo na taifa kwa ujumla yanaletwa na kiongozi ambaye ni muadilifu, mcha Mungu na mpenda haki kwa kushirikiana na wananchi wake

Naamini pia, kwamba wananchi wa Vunjo wanataka Mbunge ajaye wa Vunjo awe na sifa kuu zifuatazo:


  • Aweze kuja na sera na mikakati ya kuzalisha ajira kwa vijana wetu
  • Aweze kutokomeza mianya ya rushwa kwa vitendo
  • Aweze kuwa mfano wa kuchapa kazi na kuwajibika
  • Asimamie nidhamu ya matumizi ndani ya Manispaa na Serikali
  • Aweze kusimamia ukusanyaji wa mapato ya manispaa na Serikali
  • Aweze kuja na sera na mikakati ya kuinua uchumi wa Jimbo lake na kukuza pato la Mtanzania; ikiwemo kupunguza tofauti ya kipato kati ya aliyekuwanacho na wasiokuwanacho.
  • Mbunge anayeweza kuwadhibiti matajiri wanaoshirikiana na viongozi wa serikali kuwadhulumu ardhi wananchi wa Vunjo, kwa mfano, kujenga viwanda vyenye kemikali kwenye makazi ya watu bila kujali afya zao. Kujenga nyumba zao kwenye maeneo ya wazi bila kuhojiwa na mtu yeyote


Curriculum Vitae

Jina: Dkt Augustino Lyatonga Mrema

Elimu
Jina la Shule/ Sehemu
Digrii/ Tuzo
Tarehe
Chuo Kikuu cha Omega Global, South Africa
Digrii ya Uzamili katika Uongozi wa Siasa (PhD Holder)
2011
Chuo Kikuu cha Pacific Western, USA
Digrii ya Sayansi na Jamii
(B.A in Political Science)
2001
2003
Chuo Kikuu cha Sofia, Bulgaria
Diploma ya Sayansi ya Jamii na Utawala
1980
1981
Chuo Kivukoni CCM, Tanzania
Diploma ya Sayansi na Uchumi
1970
1971
Private candidate
Mitihani ya O Level, Chuo Kikuu Cambridge
1968
1972
Singa Chini Teachers
Training College
Cheti cha Kufundisha
1964
1965
Shule ya Msingi, Makomu, Marangu
Elimu ya Msingi
1956
1963

Kazi
Jina la Shirika
Wadhifa
Tarehe


Bunge la Tanzania
Mbunge Jimbo la Vunjo
2010
2015
Mwenyekiti wa Kamati ya Serikali za Mitaa
2010
2013
Mjumbe wa Kamati ya Ulinzi /Kamati ya Maadili na Nidhamu
2013
2015
Mbunge Jimbo la Temeke
1996
1999
Wizara ya Kazi na Maendeleo ya Vijana
Waziri
1994
1995
Wizara ya Mambo ya Ndani
Waziri
1990
1994
Naibu Waziri Mkuu
1993
1994
Bunge la Tanzania
Mbunge Jimbo la Moshi Vijijini
1985
1995
Usalama wa Taifa
Afisa Usalama wa Wilaya,
Wilaya ya Kahama, Shinyanga
1986
1987
Chama cha Mapinduzi (CCM)
Katibu Msaidizi Tume ya Ulinzi na Usalama, Makao Makuu, Mkoa wa Dodoma
1984
Usalama wa Taifa
Afisa Dawati na Kaimu Afisa Usalama wa Taifa, Mkoa wa Dodoma
1983
Chuo cha Usalama wa Taifa, Dar es Salaam
Mkufunzi
1982
Chama cha Mapinduzi (CCM)
Mwalimu wa Siasa

  • Wilaya ya Bunda
  • Wilaya ya Serengeti
  • Wilaya ya Hai
1974
1979

Wizara ya Elimu
Mratibu wa Elimu wa Kata
1970
1972
Mwalimu Mkuu (Wilaya ya Same) na Mwalimu Shule za Msingi, Mwembe Chini, Chabaru, Mkanyeni,

  • Kirongwe
1966
1974

Uzoefu kwenye Siasa
Chama cha Siasa
Wadhifa
Kutoka
Mpaka
Tanzania Labour
Party (TLP)
Mwenyekiti wa Taifa
1999
2019
Mgombea Urais:Uchaguzi Mkuu
wa 2000 and 2005
NCCR Mageuzi
Mwenyekiti wa Taifa
1995
1999
Mgombea Urais: Uchaguzi Mkuu wa 1995
 
Mbatia atosha,muda uliobakia akae na wajukuu aina Mrema na Wassira wameshapitwa na wakati kwenye siasa za kileo.
 
Back
Top Bottom