Baada ya UKAWA kutoka nje,umeona tofauti ipi Bungeni ?

serikali mbili ukawa si wanajifanya haiwezekani wakt mambo yanaweza rekebishika.
Hayo sio maoni ya wana ukawa ni maoni ya wananchi kupitia tume iliyo undwa na raisi ,sasa hayo maoni ya serikali mbili yametoka kwenye tume gani iliyo undwa na raisi na kukusanya maoni ya wananchi?
 
Majibu ya kipima joto ITV kilichohoji "Je kitendo cha baadhi ya wajumbe wa bunge la katiba kutoka nje ya bunge kutasaidia kuboresha mchakato huo?
51% Wamesema ndio
47% Wamesema hapana
Swali kwa Takwimu hizo ni wazi wananchi wako nyuma ya Ukawa? Serikali 3
Au ccm serikali 2?
Tafakari Chukua Hatua.
 
" sample iliyotumika kupata tkwimu hizo ni ndogo sana,hivyo hayo si maoni ya watanzania,ni kikundi cha watu wachache tu" by: Magamba BMK
 
sitaki 3 wala 2 nataka 1 huu ndo muungano,kinyume cha hapo ni kuiogopa znz
 
1397756874381.jpg
Bunge la makundi limeacha Rasimu linajadili mawazo binafsi.
 
Huo ndio ukweli hata hapa kijijini kwangu wananchi wamejitambua kupitia tbc bungeni.wanasema maoni yao ndio katiba ya heshimiwe
 
Mimi bado najiuliza ni "turning point" ipi iliyosababisha wana-UKAWA kutoka nje ya Bunge. Kama ni msimamo imara wa CCM juu ya Serikali 2 wana-UKAWA wanaufahamu tangu wanaripoti pale Bungeni na wanaonekana walikuwa ready kupigana mpaka mwisho!
Tunajua wana-UKAWA walijenga hoja kuwa Muungano huu hauna Hati na ni BATILI! Hoja hii iliwapa morali wa kusonga mbele, liwalo na liwe! Sote tulishuhudia matusi ya nguoni ya "Mwanasheria Nguli" Tundu Lissu dhidi ya Waasisi wa Muungano! Huu ujasiri aliokuwa nao Tundu Lissu umewashangaza wengi, mpaka mwasisi wa CHADEMA Mzee Mtei alipomkemea Tundu Lissu kwa kukosa hekima na adabu!
Mara tukamwona Mzee Stephen Wassira, almaarufu kama Tyson, akanyanyuka pale mjengoni hivi majuzi akijigamba kuwa atawasilisha Hati ya Muungano ndani ya Siku 2!
Hatua hiyo imebadili kabisa upepo wa UKAWA na tumeshuhudia wakijitoa mjengoni ili kwenda "kushtaki kwa wananchi!"
Bado sitaki kuamini kuwa ni ile Hati ya Muungano halisia iliyowatoa mjengoni lakini kuna mazingira yanayounganisha matukio hayo mawili!
Hii ni kwa sababu UKAWA walijua msimamo wa CCM ambao hakuna asiyefahamu kuwa JK aliusisitiza wakati wa Hotuba ya Kuzindua Bunge Maalum la Katiba! Kama hivyo ndivyo basi, WHY NOW?
TUJADILI!
 
Pole sana ndugu yangu mwana ccm, nadhani Mungu ameamua kuwafanya vipofu ili msielewe chochote kinachoendelea. Sheria ya Mabadilikoya Katiba inazungumzia juu ya kuwepo haja ya Katiba mpya, moja wapomya mambo makuu ni pamoja na kuundwa Tume ya kukusanya maoni ya wananchi na Tume itengeneze rasimu na kisha rasimu ikabidhiwe kwa Bunge la Katiba ijadiliwe hiyo rasimu ili iboreshwe na kisha Bubge lije na Rasimu ya Katiba pendekezwa ambayo Wananchi wataipigia kura ya Maoni kuikubali ama kuikataa.

Sasa kinachoendelea Bungeni si kujadili Rasimu iliyoko mezani CCM na Mamluki wao wanajadili mfumo wa serikali mbili ambao haumo kwenye rasimu. Cha ajabu kuliko vyote Mwenyekiti wa CCM Taifa anadai ameisoma na kuisoma tena na tena, alipokabidhiwa na Tume ya Waryoba akaikubalia iende Bungeni sasa kwa nini wasiiboreshe hiyo na sasa wanaruhusiwa akina LUKUVI kuja na hofu zao na kuonyesha chuki dhidi ya Waislamu na Uislamu wa Zanzibar?
 
Back
Top Bottom