Baada ya UKAWA kutoka nje,umeona tofauti ipi Bungeni ?

Huyu anaga point kabisa tupuuze thread zake kama tunavyompuuza yeye mwenyewe
 
Mimi bado najiuliza ni "turning point" ipi iliyosababisha wana-UKAWA kutoka nje ya Bunge. Kama ni msimamo imara wa CCM juu ya Serikali 2 wana-UKAWA wanaufahamu tangu wanaripoti pale Bungeni na wanaonekana walikuwa ready kupigana mpaka mwisho!
Tunajua wana-UKAWA walijenga hoja kuwa Muungano huu hauna Hati na ni BATILI! Hoja hii iliwapa morali wa kusonga mbele, liwalo na liwe! Sote tulishuhudia matusi ya nguoni ya "Mwanasheria Nguli" Tundu Lissu dhidi ya Waasisi wa Muungano! Huu ujasiri aliokuwa nao Tundu Lissu umewashangaza wengi, mpaka mwasisi wa CHADEMA Mzee Mtei alipomkemea Tundu Lissu kwa kukosa hekima na adabu!
Mara tukamwona Mzee Stephen Wassira, almaarufu kama Tyson, akanyanyuka pale mjengoni hivi majuzi akijigamba kuwa atawasilisha Hati ya Muungano ndani ya Siku 2!
Hatua hiyo imebadili kabisa upepo wa UKAWA na tumeshuhudia wakijitoa mjengoni ili kwenda "kushtaki kwa wananchi!"
Bado sitaki kuamini kuwa ni ile Hati ya Muungano halisia iliyowatoa mjengoni lakini kuna mazingira yanayounganisha matukio hayo mawili!
Hii ni kwa sababu UKAWA walijua msimamo wa CCM ambao hakuna asiyefahamu kuwa JK aliusisitiza wakati wa Hotuba ya Kuzindua Bunge Maalum la Katiba! Kama hivyo ndivyo basi, WHY NOW?
TUJADILI!
kama kweli umekerwa naomba uyataje gato matusi ya nguoni ambayo Tundu amewatukana the so called waasis wa Taifa hilo. Hata mwenyekiti wako bila aibu anasema baba wa Taifa ametukanwa, tajeni hayo matusi acheni uzushi. Leo ukweli umegeuka kuwa matusi kwa kuwa tu umemgusa Nyerere? Shame on you
 
Mhe: T. Lissu kasha sema hati ni feki. Ana vitabu vina saini za A. Aman Karume na JKN. Au kama una hela za zamani kalinganishe sahihi hizo ni Full Magumashi (Bambo hewani). Ww unadhani CCM ni wehu waende kuumbuka Bungeni? Umeona waipeleka Bungeni? Itaishia Ofisi ya JK tu.
 
attachment.php
 
Tatizo la ukawa bangi ndiyo wameziweka mbele kabisa.

Kweli kabisa mkuu!
Kura za wazi wao unga unga ndio chakula chao unga nouma kweli mkuu!
Me bangi siogopi sana ila unga mateja nouma wanauzaga adi sindano ya kujidungia nouma kweli kura ya wazi duh kwaunga nouma ata wee siunajua mkuu unga nouma
 
Umoja wa katiba ya wananchi bungeni -Ukawa- umegoma kabisa kuhudhuria mkutano wa bunge maalum baada ya kutoka katika mkutano uliofanyika Aprili 16 kwa madai ya mkutano huo kugubikwa na matusi, kashfa na vitisho vinavyofanywa na baadhi ya viongozi kwa wananchi.

Akizungumzia masikitiko yake mwenyekiti wa kamati ya bunge maalum, Mhe. Samweli Sita amesema licha ya bunge hilo kumwita bungeni Mhe. William Lukuvi kutoa ufafanuzi wa tuhuma za zinazomkabili ameitaka ameutaka ukawa kuja katika kamati ya uongozi kueleza kwa undani nini hatma ya maamuzi yao.

Akihitikia wito wa kuitwa bunge hilo,waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera uratibu na bunge, Mhe. William Lukuvi ameeleza hofu yake kuhusu muundo wa serikali tatu na kulieleza bunge dhamira ya vyama vikuu vya upinzani vya kugawana Tanganyika na Zanzibar.

Wakitoa maoni ya nje ya bunge baaadhi ya wabunge wameutaka umoja huo kuitikia wito wa wenyekiti wa bunge hilo wa kuhudhuria mikutano kama kawaida na kupeleka malalamiko yao kwa kamati ya uongozi ili kutafuta njia bora ya kufikia mwafaka na kuwapatika wananchi katiba mpya.

ITV imeutafuta uongozi umoja wa katiba ya wananchi-Ukawa iliokuwa ukifanya mkutano wake wa ndani na kuzungumza na mwenyekiti wa umoja huo Mhe Freeman Mbowe ambae amepinga kauli ya kiongozi huyo wa serikali kudai kuwa ni hofu yake binafsi na kusisitiza baadhi ya vinongozi wengine wameshawahi kutoa kauli kama hiyo ambapo chanzo:ITVametoa msimamo wa umoja huo.
 
Kwa nini UKAWA watoke mida hii na sio muda mwingine wowote? Na huyo Tundu Lissu wenu kasomea wapi utaalamu wa hati? Au anafikiri ukiwa Mwanasheria basi unakuwa mtaalamu wa kila kitu?
 
Ohh nchi yangu Tanzania!!! ndani yako yupo tanganyika na ndugu yake zanzibar lakini ndani ya zanzibar kuna unguja na pemba nini kina tokea nchi yangu?

Hata wale tulio kuwa na imani nao kuwa wataweza kuwatenga watoto wako hao wawili wakuu tanganyika na zanzibar naona na wao wameshindwa, hawana tena la kufanya wanakuja kwetu kushitaki na kutuambia kile ambacho tunakiona na kusikia kwenye radio na luninga zetu.

Ila na fahamu fika jambo mnalo taka kulifanya kwa wakati huu kuja kwetu haliwezekani kwa kuwa wakati wa kuja kupigia debe rasimu hii ya katiba bado ni sura mbili tuu zimejadiliwa na bado hazijafika mwisho hivyo sheria itachukua mkondo wake kwanza hata vibali vya kufanya mikutano yenu hamtoweza kupata.

Nafikiri bado mngeweza kutujulisha hicho mnachotaka kutuambia mkiwa huko dodoma, hapakuwa na haja ya kuja kutuambia huku nje.

Tafakari na chukua hatua
 
Serikali 3 ni balaa mkuu, asikuambie mtu!
 
Mhe: T. Lissu kasha sema hati ni feki. Ana vitabu vina saini za A. Aman Karume na JKN. Au kama una hela za zamani kalinganishe sahihi hizo ni Full Magumashi (Bambo hewani). Ww unadhani CCM ni wehu waende kuumbuka Bungeni? Umeona waipeleka Bungeni? Itaishia Ofisi ya JK tu.

Kwa hiyo akisema Tundu Lissu tu ni sahihi?
 
kama kweli umekerwa naomba uyataje gato matusi ya nguoni ambayo Tundu amewatukana the so called waasis wa Taifa hilo. Hata mwenyekiti wako bila aibu anasema baba wa Taifa ametukanwa, tajeni hayo matusi acheni uzushi. Leo ukweli umegeuka kuwa matusi kwa kuwa tu umemgusa Nyerere? Shame on you

Muulize Mzee Mtei, mwasisi wa CHADEMA atakueleza!
 
Back
Top Bottom