Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,184
- 671
viti maalum Chadema vyazidi kupasua kichwa Send to a friend Saturday, 25 September 2010 22:38 0diggsdigg
Mgombea Urais kwa tiketi ya Chadema,Dk Wilbrod Slaa
Fredy Azzah na Frederick Katulanda, Mwanza
MKUTANO Chadema, uliotishwa kuwateua wabunge wa viti maalumu, uliingia dosari baada ya kumalizika bila mwafaka kutokana na kuibuka makundi mawili yanayopingana.
Mkutano huo ulishindwa kumaliza ajenda zake baada ya makundi hayo kushindwa kufikia njia sahihi ya kuwapata wabunge wa viti maalumu vya wanawake.
Vyanzo vya habari kutoka ndani ya mkutano huo, vililidokeza gazeti hili kuwa makundi mawili yanayovutana yaliibuka kwenye kikao hicho na kukifanya kipoteze mwelekeo.
Makundi hayo yalidaiwa kuegemea vigogo wawili wazito ndani ya chama hicho, jambo ambalo liliipasua pia meza kuu na kuiweka katika mazingira magumu katika kuokoa jahazi.
Ingawa watu wanaodhani kuwa katika makundi hayo hawakutaka kuzungumza, habari zilidokeza kuwa mmoja wa viongozi wa juu wa Chadema (jina tunalo), alitaka elimu kiwe kigezo cha kuwapata wabunge hao wateule.
Yeye anakazania kigezo cha elimu kitumike katika kuwapata wabunge,na anafanya hivyo kwa sababu kuna watu wake anaotaka waingie, kilisema chanzo kimoja na kufafanua:
Watu wengi wanataka utumike mfumo utakao wezesha kupata uwakilishi kutoka katika mikoa yote ili ile dhana ya kuwa Chadema viongozi wake wanatoka Kaskazini ifutike,.
Chanzo kingine kutoka ndani ya mkutano huo kilisema, baadhi ya wajumbe walipinga njia ya kupiga kura kutafuta wabunge hao kutokana na kile kilichoelezwa kuwa kinaweza kurudisha makundi yaliyokuwa tayari yamevunjwa.
Wanasema yatarudi yale makundi ya kina-Zitto na Mbowe kwa hiyo hawataki hiyo njia ya kupiga kura, kwa hiyo ngoma imelala mpaka kesho tena, kilisema chanzo kingine.
Habari zimeeleza kuwa vingezo vingine vya kuwapata wabunge hao ambavyo viliibua makundi katika mkutano huo ni kuangalia uzoefu na juhudi za mtu katika kujitoa kukitumikia chama.
Baadhi ya wajumbe waliokuwa katika mkutano huo ambao pia ni wagombea wa kinyanganyiro hicho walisema, kuna watu ambao wameshaandaliwa ili kutimiza vigezo hivyo.
Wameshawaandaa watu wao katika hizi siku za karibuni wamekuwa wakiwapitisha pitisha mbele ili waonekane ni watu muhimu na wanaojitolea katika kukihudumia chama, kilisema chanzo kingine.
Chanzo kiningine kilidai: Kwa mfano kama tukishinda katika uchaguzi huu, ni baraza gani la mawaziri tutaunda la watu wasiyo na elimu, lazima tuhakikishe tunajenga watu watakaoweza kuiendesha hii nchi kwa siku za baadaye .
Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema , John Mnyika alikataa kuzungumzia kilichojadiliwa katika mkutano huo kwa madia kwamba leo ataizungumza na vyombo vya habari.
Hata hivyo, baadhi ya vigogo waliotoka meza kuu walioombwa kutotajwa gazetini walisema wameamua kuahirisha kikao hicho ili leo wajipange upya kupata mwafaka.
Tumelaza ngoma mpaka kesho. Imeundwa timu maalumu ya ku-rank (kupanga) majina. Hakuna kura. Mzozo ulikuwa hapo wakati mjumbe kutoka Shinyanga alipinga vikali akitaka kura.
Hata hivyo, habari zilizolifikia gazeti hili zinaelezwa kwamba timu hiyo iliundwa na kuanza kuyapitia majina hayo ili kunusuru chama hicho ambacho kimeonekana kutoa upinzani mkali kwa CCM katika uchaguzi wa mwaka huu.
Hii ni mara ya pili kufanyika kwa mkutano wa viongozi wa Chadema kujadili kupata wagombea wa wabunge viti maalumu baada ya kile cha kwanza kuvunjika kutokana na wajumbe kushindwa kuelewana.
Wakati hayo yakiendelea makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam, mgombea ubunge wa chama hicho jimbo la Nyamagana Ezekiel Wenje, ameonja adha ya mkono wa dola baada ya kutiwa mbaroni na polisi na kuohojiwa kwa saa kadhaa.
Habari zimeeleza kuwa mgombea huyo wa ubunge ambaye hivi karibuni alinusurika kuenguliwa baada ya kuwekewa pingamizi na mgombea ubunge wa CCM, Lawrence Masha, alikamatwa juzi jioni wakati akizungumza na wananchi katika mtaa wa Kamanga jirani na Ikulu ndogo jijini Mwanza.
Wenje ambaye akiwa ameongozana na wapambe wake kumi, alikuwa akipita katika mitaa mbalimbali ya kati kati ya Jiji la Mwanza akitokea mitaa ya Sokoni.
Lakini alipokuwa amefika mitaani maarufu ya Makoroboi, alijikuta akianza kuzungukwa na watu wengi ambao walimfuata uku wakipiga miruzi na wengine kutoa maneno ya kejeli dhidi ya CCM.
Matembezi hayo yalianza majira ya saa 9:30 alasiri na kuhitimishwa na jeshi la polisi majira ya saa 11:17 baada ya maofisa hao wa polisi kumfuata na kumweka chini ya ulinzi.
Kutoka hapa nilipo ni umbali wa mita 100 sasa sidhani kama inafaa kwenda kwa gari. Nitatembea hadi hapo kituoni. Wenje aliwaeleza polisi hao ambao walitaka apande kwenye gari lao.
Wakati anaelekea kituoni kundi kubwa la watu liliendelea kumfuata jambo ambalo liliwafanya polisi hao kumbeba Wenje na kumwingiza kwenye gari lao kisha kuwaamuru wapambe hao kurudi.
Kumkamata na kumweka katika gari ni matumizi ya nguvu, lakini hajaonyesha kukaidi na anakwenda vizuri kituoni. Hawa wafuasi wake watarudi tu, alieleza mmoja wa mapambe hao.
Baada ya kumfikisha kituo cha polisi cha kati, mvutano mwingine uliibuka walipotaka kumweka ndani.
Lakini baadaye walikubaliana atoe maelezo ya kwanini alifanya mkutano nje ya utaratibu na ratiba za kampeni za uchaguzi.
Wenje aliliambia gazeti hili baada ya kuachiwa Wenje alisema: Nilipofika kituoni walikuwa wakibishana (polisi). Wengine walidai wakiniweka ndani watazua vurugu na wengine wakidai kuwa hakuna sababu ya msingi ya kuniweka ndani kisheria, baadaye waakaniachia huru".
Kaimu Kamanda wa jeshi la polisi Nonosius Komba alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema hana taarifa za kukamatwa kwa mgombea huyo.
source mwananchi