Elections 2010 Baada ya hatihati, Chadema yapendekeza wagombea viti maalum

chama cha magirl friend kama ya tangazo la fisadi wa chadema. walikua weshapanga kuwa kuna deal

hahaaa huyu girl friend wake mke wa mtu
 
weshapitisha kwa kuinyonga demokrasia

sasa subiri waliouawa waanze kuja juuuuuuuuuuuuuuuu
 
viti maalum Chadema vyazidi kupasua kichwa Send to a friend Saturday, 25 September 2010 22:38 0diggsdigg

_dk%20wilbord%20slaa.jpg
Mgombea Urais kwa tiketi ya Chadema,Dk Wilbrod Slaa

Fredy Azzah na Frederick Katulanda, Mwanza
MKUTANO Chadema, uliotishwa kuwateua wabunge wa viti maalumu, uliingia dosari baada ya kumalizika bila mwafaka kutokana na kuibuka makundi mawili yanayopingana.
Mkutano huo ulishindwa kumaliza ajenda zake baada ya makundi hayo kushindwa kufikia njia sahihi ya kuwapata wabunge wa viti maalumu vya wanawake.
Vyanzo vya habari kutoka ndani ya mkutano huo, vililidokeza gazeti hili kuwa makundi mawili yanayovutana yaliibuka kwenye kikao hicho na kukifanya kipoteze mwelekeo.

Makundi hayo yalidaiwa kuegemea vigogo wawili wazito ndani ya chama hicho, jambo ambalo liliipasua pia meza kuu na kuiweka katika mazingira magumu katika kuokoa jahazi.

Ingawa watu wanaodhani kuwa katika makundi hayo hawakutaka kuzungumza, habari zilidokeza kuwa mmoja wa viongozi wa juu wa Chadema (jina tunalo), alitaka elimu kiwe kigezo cha kuwapata wabunge hao wateule.

“Yeye anakazania kigezo cha elimu kitumike katika kuwapata wabunge,na anafanya hivyo kwa sababu kuna watu wake anaotaka waingie,” kilisema chanzo kimoja na kufafanua:

“Watu wengi wanataka utumike mfumo utakao wezesha kupata uwakilishi kutoka katika mikoa yote ili ile dhana ya kuwa Chadema viongozi wake wanatoka Kaskazini ifutike,”.
Chanzo kingine kutoka ndani ya mkutano huo kilisema, baadhi ya wajumbe walipinga njia ya kupiga kura kutafuta wabunge hao kutokana na kile kilichoelezwa kuwa kinaweza kurudisha makundi yaliyokuwa tayari yamevunjwa.
“Wanasema yatarudi yale makundi ya kina-Zitto na Mbowe kwa hiyo hawataki hiyo njia ya kupiga kura, kwa hiyo ngoma imelala mpaka kesho tena,” kilisema chanzo kingine.
Habari zimeeleza kuwa vingezo vingine vya kuwapata wabunge hao ambavyo viliibua makundi katika mkutano huo ni kuangalia uzoefu na juhudi za mtu katika kujitoa kukitumikia chama.

Baadhi ya wajumbe waliokuwa katika mkutano huo ambao pia ni wagombea wa kinyanganyiro hicho walisema, kuna watu ambao wameshaandaliwa ili kutimiza vigezo hivyo.
“Wameshawaandaa watu wao katika hizi siku za karibuni wamekuwa wakiwapitisha pitisha mbele ili waonekane ni watu muhimu na wanaojitolea katika kukihudumia chama,” kilisema chanzo kingine.

Chanzo kiningine kilidai: “Kwa mfano kama tukishinda katika uchaguzi huu, ni baraza gani la mawaziri tutaunda la watu wasiyo na elimu, lazima tuhakikishe tunajenga watu watakaoweza kuiendesha hii nchi kwa siku za baadaye” .
Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema , John Mnyika alikataa kuzungumzia kilichojadiliwa katika mkutano huo kwa madia kwamba leo ataizungumza na vyombo vya habari.

Hata hivyo, baadhi ya vigogo waliotoka meza kuu walioombwa kutotajwa gazetini walisema wameamua kuahirisha kikao hicho ili leo wajipange upya kupata mwafaka.
“Tumelaza ngoma mpaka kesho. Imeundwa timu maalumu ya ku-rank (kupanga) majina. Hakuna kura. Mzozo ulikuwa hapo wakati mjumbe kutoka Shinyanga alipinga vikali akitaka kura.”

Hata hivyo, habari zilizolifikia gazeti hili zinaelezwa kwamba timu hiyo iliundwa na kuanza kuyapitia majina hayo ili kunusuru chama hicho ambacho kimeonekana kutoa upinzani mkali kwa CCM katika uchaguzi wa mwaka huu.

Hii ni mara ya pili kufanyika kwa mkutano wa viongozi wa Chadema kujadili kupata wagombea wa wabunge viti maalumu baada ya kile cha kwanza kuvunjika kutokana na wajumbe kushindwa kuelewana.

Wakati hayo yakiendelea makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam, mgombea ubunge wa chama hicho jimbo la Nyamagana Ezekiel Wenje, ameonja adha ya mkono wa dola baada ya kutiwa mbaroni na polisi na kuohojiwa kwa saa kadhaa.

Habari zimeeleza kuwa mgombea huyo wa ubunge ambaye hivi karibuni alinusurika kuenguliwa baada ya kuwekewa pingamizi na mgombea ubunge wa CCM, Lawrence Masha, alikamatwa juzi jioni wakati akizungumza na wananchi katika mtaa wa Kamanga jirani na Ikulu ndogo jijini Mwanza.

Wenje ambaye akiwa ameongozana na wapambe wake kumi, alikuwa akipita katika mitaa mbalimbali ya kati kati ya Jiji la Mwanza akitokea mitaa ya Sokoni.

Lakini alipokuwa amefika mitaani maarufu ya Makoroboi, alijikuta akianza kuzungukwa na watu wengi ambao walimfuata uku wakipiga miruzi na wengine kutoa maneno ya kejeli dhidi ya CCM.

Matembezi hayo yalianza majira ya saa 9:30 alasiri na kuhitimishwa na jeshi la polisi majira ya saa 11:17 baada ya maofisa hao wa polisi kumfuata na kumweka chini ya ulinzi.

“Kutoka hapa nilipo ni umbali wa mita 100 sasa sidhani kama inafaa kwenda kwa gari. Nitatembea hadi hapo kituoni.” Wenje aliwaeleza polisi hao ambao walitaka apande kwenye gari lao.

Wakati anaelekea kituoni kundi kubwa la watu liliendelea kumfuata jambo ambalo liliwafanya polisi hao kumbeba Wenje na kumwingiza kwenye gari lao kisha kuwaamuru wapambe hao kurudi.

“Kumkamata na kumweka katika gari ni matumizi ya nguvu, lakini hajaonyesha kukaidi na anakwenda vizuri kituoni. Hawa wafuasi wake watarudi tu,” alieleza mmoja wa mapambe hao.

Baada ya kumfikisha kituo cha polisi cha kati, mvutano mwingine uliibuka walipotaka kumweka ndani.

Lakini baadaye walikubaliana atoe maelezo ya kwanini alifanya mkutano nje ya utaratibu na ratiba za kampeni za uchaguzi.

Wenje aliliambia gazeti hili baada ya kuachiwa Wenje alisema: “Nilipofika kituoni walikuwa wakibishana (polisi). Wengine walidai wakiniweka ndani watazua vurugu na wengine wakidai kuwa hakuna sababu ya msingi ya kuniweka ndani kisheria, baadaye waakaniachia huru".

Kaimu Kamanda wa jeshi la polisi Nonosius Komba alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema hana taarifa za kukamatwa kwa mgombea huyo.

source mwananchi

Big up mzalendo mwenzangu. Hii inathibitisha kuwa JF ni ukombozi kwa watanzania wote. Ninafanya research ya kuhakikisha kuwa watanzania asilimia zaidi ya 50% wanapata mawazo murua kutoka JF. Hapa mtu wa pwani umehabarisha hata wale ambao hawajapata habari hii.

CHADEMA wajue kuwa mapambano yanaendelea...na CCM ni lazima itoke madarakani....na vyama vingine vya kisiasa kama CUF pia vipo...hivyo waangalie tusijeona ndani yao u-CCM wa aina yeyote...kwa mfano kukimbilia madaraka.

Tanzania kwanza.....siasa baadaye.

Big up sana mtu wa pwani....Big up sana vyama vya upinzani. SHAME ON YOU CCM.
 
Kama mnazungumzia ushwari, basi kuna shwari zaidi katika Chadema kuliko hicho chama chenu CCM kinachoonekana waziwazi kutokomea kinakostahili!!!!
 
viti maalum Chadema vyazidi kupasua kichwa Send to a friend Saturday, 25 September 2010 22:38 0diggsdigg

_dk%20wilbord%20slaa.jpg
Mgombea Urais kwa tiketi ya Chadema,Dk Wilbrod Slaa

Fredy Azzah na Frederick Katulanda, Mwanza
MKUTANO Chadema, uliotishwa kuwateua wabunge wa viti maalumu, uliingia dosari baada ya kumalizika bila mwafaka kutokana na kuibuka makundi mawili yanayopingana.
Mkutano huo ulishindwa kumaliza ajenda zake baada ya makundi hayo kushindwa kufikia njia sahihi ya kuwapata wabunge wa viti maalumu vya wanawake.
Vyanzo vya habari kutoka ndani ya mkutano huo, vililidokeza gazeti hili kuwa makundi mawili yanayovutana yaliibuka kwenye kikao hicho na kukifanya kipoteze mwelekeo.

Makundi hayo yalidaiwa kuegemea vigogo wawili wazito ndani ya chama hicho, jambo ambalo liliipasua pia meza kuu na kuiweka katika mazingira magumu katika kuokoa jahazi.

Ingawa watu wanaodhani kuwa katika makundi hayo hawakutaka kuzungumza, habari zilidokeza kuwa mmoja wa viongozi wa juu wa Chadema (jina tunalo), alitaka elimu kiwe kigezo cha kuwapata wabunge hao wateule.

"Yeye anakazania kigezo cha elimu kitumike katika kuwapata wabunge,na anafanya hivyo kwa sababu kuna watu wake anaotaka waingie," kilisema chanzo kimoja na kufafanua:

"Watu wengi wanataka utumike mfumo utakao wezesha kupata uwakilishi kutoka katika mikoa yote ili ile dhana ya kuwa Chadema viongozi wake wanatoka Kaskazini ifutike,".
Chanzo kingine kutoka ndani ya mkutano huo kilisema, baadhi ya wajumbe walipinga njia ya kupiga kura kutafuta wabunge hao kutokana na kile kilichoelezwa kuwa kinaweza kurudisha makundi yaliyokuwa tayari yamevunjwa.
"Wanasema yatarudi yale makundi ya kina-Zitto na Mbowe kwa hiyo hawataki hiyo njia ya kupiga kura, kwa hiyo ngoma imelala mpaka kesho tena," kilisema chanzo kingine.
Habari zimeeleza kuwa vingezo vingine vya kuwapata wabunge hao ambavyo viliibua makundi katika mkutano huo ni kuangalia uzoefu na juhudi za mtu katika kujitoa kukitumikia chama.

Baadhi ya wajumbe waliokuwa katika mkutano huo ambao pia ni wagombea wa kinyanganyiro hicho walisema, kuna watu ambao wameshaandaliwa ili kutimiza vigezo hivyo.
"Wameshawaandaa watu wao katika hizi siku za karibuni wamekuwa wakiwapitisha pitisha mbele ili waonekane ni watu muhimu na wanaojitolea katika kukihudumia chama," kilisema chanzo kingine.

Chanzo kiningine kilidai: "Kwa mfano kama tukishinda katika uchaguzi huu, ni baraza gani la mawaziri tutaunda la watu wasiyo na elimu, lazima tuhakikishe tunajenga watu watakaoweza kuiendesha hii nchi kwa siku za baadaye" .
Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema , John Mnyika alikataa kuzungumzia kilichojadiliwa katika mkutano huo kwa madia kwamba leo ataizungumza na vyombo vya habari.

Hata hivyo, baadhi ya vigogo waliotoka meza kuu walioombwa kutotajwa gazetini walisema wameamua kuahirisha kikao hicho ili leo wajipange upya kupata mwafaka.
"Tumelaza ngoma mpaka kesho. Imeundwa timu maalumu ya ku-rank (kupanga) majina. Hakuna kura. Mzozo ulikuwa hapo wakati mjumbe kutoka Shinyanga alipinga vikali akitaka kura."

Hata hivyo, habari zilizolifikia gazeti hili zinaelezwa kwamba timu hiyo iliundwa na kuanza kuyapitia majina hayo ili kunusuru chama hicho ambacho kimeonekana kutoa upinzani mkali kwa CCM katika uchaguzi wa mwaka huu.

Hii ni mara ya pili kufanyika kwa mkutano wa viongozi wa Chadema kujadili kupata wagombea wa wabunge viti maalumu baada ya kile cha kwanza kuvunjika kutokana na wajumbe kushindwa kuelewana.

Wakati hayo yakiendelea makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam, mgombea ubunge wa chama hicho jimbo la Nyamagana Ezekiel Wenje, ameonja adha ya mkono wa dola baada ya kutiwa mbaroni na polisi na kuohojiwa kwa saa kadhaa.

Habari zimeeleza kuwa mgombea huyo wa ubunge ambaye hivi karibuni alinusurika kuenguliwa baada ya kuwekewa pingamizi na mgombea ubunge wa CCM, Lawrence Masha, alikamatwa juzi jioni wakati akizungumza na wananchi katika mtaa wa Kamanga jirani na Ikulu ndogo jijini Mwanza.

Wenje ambaye akiwa ameongozana na wapambe wake kumi, alikuwa akipita katika mitaa mbalimbali ya kati kati ya Jiji la Mwanza akitokea mitaa ya Sokoni.

Lakini alipokuwa amefika mitaani maarufu ya Makoroboi, alijikuta akianza kuzungukwa na watu wengi ambao walimfuata uku wakipiga miruzi na wengine kutoa maneno ya kejeli dhidi ya CCM.

Matembezi hayo yalianza majira ya saa 9:30 alasiri na kuhitimishwa na jeshi la polisi majira ya saa 11:17 baada ya maofisa hao wa polisi kumfuata na kumweka chini ya ulinzi.

"Kutoka hapa nilipo ni umbali wa mita 100 sasa sidhani kama inafaa kwenda kwa gari. Nitatembea hadi hapo kituoni." Wenje aliwaeleza polisi hao ambao walitaka apande kwenye gari lao.

Wakati anaelekea kituoni kundi kubwa la watu liliendelea kumfuata jambo ambalo liliwafanya polisi hao kumbeba Wenje na kumwingiza kwenye gari lao kisha kuwaamuru wapambe hao kurudi.

"Kumkamata na kumweka katika gari ni matumizi ya nguvu, lakini hajaonyesha kukaidi na anakwenda vizuri kituoni. Hawa wafuasi wake watarudi tu," alieleza mmoja wa mapambe hao.

Baada ya kumfikisha kituo cha polisi cha kati, mvutano mwingine uliibuka walipotaka kumweka ndani.

Lakini baadaye walikubaliana atoe maelezo ya kwanini alifanya mkutano nje ya utaratibu na ratiba za kampeni za uchaguzi.

Wenje aliliambia gazeti hili baada ya kuachiwa Wenje alisema: "Nilipofika kituoni walikuwa wakibishana (polisi). Wengine walidai wakiniweka ndani watazua vurugu na wengine wakidai kuwa hakuna sababu ya msingi ya kuniweka ndani kisheria, baadaye waakaniachia huru".

Kaimu Kamanda wa jeshi la polisi Nonosius Komba alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema hana taarifa za kukamatwa kwa mgombea huyo.

source mwananchi

Nawaomba Chadema wawe wakomavu kwenye suala hili. Kwanza wasipoteze muda mwingi na fedha kwa ajili ya viti maalum, watumie muda mwingi katika kuandaa mawakala makini, kutumia mbinu za kulinda kura za Karatu, Tarime, Kigoma Kaskazini, Mpanda, Moshi. Central Committee ikae na kutatua shida hii mara moja na kwa muda mfupi. Kwa nini msitumie vigezo vya mwaka 2005? Je, hilo baraza la wanawake halina vigezo vya kupata viti maalumu? Wasiwasi wangu kuna vibaraka ndani ya Chadema. Pia nina wasiwasi kuwa jambo hili linawezeka kupoteza kura zenu hasa vyama vingine watakapolitumia kama silaha ya kuwashambulia ninyi kisiasa!
 
bado chadema ni chama kichanga sana kukabidhiwa nchi,.. ona mambo madogo kama haya yanawashinda
 
bado chadema ni chama kichanga sana kukabidhiwa nchi,.. ona mambo madogo kama haya yanawashinda

Na mambo makubwa na ya maana, kama vile kulinda rasilimali za nchi na masilahi ya wananchi CCM wameonyesha kupata ZERO!!!!!! nao walijifundisahia wapi kuendesha serikali? Miaka 50 bado mambo hovyo hovyo, kugombana wao kwa wao hakuishi katika kila uchaguzi, wa ndani mwao na ule Uchaguzi Mkuu!!!
 
Hatimaye Chadema imepitisha majina ya wabunge 105 wa viti maalumu huku ikiwaacha
wanachama wake 42 walioshindwa kukidhi vigezo vya chama hicho.

Majina ya wabunge hao hayakuwekwa hadharani na badala yake yatapelekwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kabla ya Septemba 30 mwaka huu.

Uteuzi wa majina hayo ulifanywa na mshauri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Mkumbo Kitila, ambaye ni mwanachama wa chama hicho na kuthibitishwa na Kamati Kuu katika kikao chake cha Septemba 25 na 26 jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Katibu Mkuu wa Chadema ambaye pia mgombea urais, Dk. Willibrod Slaa, alisema baada ya matokeo ya wabunge hao ya Julai kufutwa kutokana na mizengwe, Baraza Kuu lilikasimu madaraka kwa Kamati Kuu kufanya uteuzi huo.

“Kamati Kuu ikaunda Kamati Ndogo ambayo ilimtumia mshauri kufanya uteuzi huo akizingatia vigezo vya elimu, uzoefu wa uongozi kisiasa, uzoefu wa uongozi nje ya siasa; ugombea jimboni mwaka huu; mchango katika operesheni za chama na kampeni zinazoendelea na umri ndani ya chama,” alisema Slaa.

Katika vigezo hivyo, aliyeongoza alipata asilimia 94 na wa mwisho 16 ambapo moja ya sababu za kutumika utaratibu huo ambao Dk. Slaa aliuita wa kisayansi, ni kuondoa uswahiba, wagombea kutoka kanda moja na urafiki.

“Tumeondoa dhana ya mtu kuchagua ‘girlfriend (rafiki wa kike)’ wake, na majina haya hatutayatoa hadharani, kwani wengine waliopitishwa wanagombea majimboni,
hivyo kunaweza kuwachanganya wapiga kura,”
alifafanua.

Dk. Kitila alisema katika uandaaji wa vigezo, waliangalia suala la umahiri wa mgombea na kwambambunge atakuwa anawakilisha nchi na kupanua wigo wa ushiriki wa wanawake.

Katika Bunge lililopita, wabunge wa Chadema walikuwa 11 wakiwamo wa majimbo na viti
maalumu na mwaka huu imesimamisha wabunge wa majimbo 185.

I love this. Mmekwisha kutegua bomu mlilokuwa mnataka kulikanyaga. Sasa vigezo hivyo viwe vya kudumu na ikiwezekana viingie kwenye katiba yenu.
 
bado chadema ni chama kichanga sana kukabidhiwa nchi,.. ona mambo madogo kama haya yanawashinda

Mambo madogo kwa sababu kwenu hata uraia wa mtu mnauvua huku kwenye chama. Mnajipa mamlaka ambayo siyo yenu. Heri yenu
 
Haya masuala ya vipaji maalum kwa chadema nawapa big up lakini ccm nafasi hizo zimekwisha milikiwa na wamiliki wamekwisha pewa hati miliki angalia wanavipaji maalum wa mkoa mara ni wale wale hawabaliki.
 
Kwenye chama makini ufisadi lazima uwepo. Ndiyo maana yule Mwenyekiti kakopa mamillioni NSSF halafu hataki kuyarudisha. :becky:

Kusema ukweli huyu KUDADEKI natilia shaka uelewa wake.

Ni vyema ukaelewa kukopa si UFISADI, pili unapokopa ktk taasisi za fedha mnaingia mkataba kuhusiana na masharti ya mkopo huo, tatizo lolote likitokea baina ya mdai na mdaiwa utatuliwa kwa mujibu wa makubaliano ya mkataba wenu, tafsiri ya masharti ya mkataba yasipo kubaliwa na upande moja ktk mgogoro huo na kupelekea muafaka kutofikiwa, suala hilo umalizwa mahakamani ili masharti ya mkopo ndani ya mkataba yatafsiriwe na kubaini ni nani kati ya mdai na mdaiwa anatatizo, na haki utolewa kwa yule aliyeathirika kwa ukiukwaji wa mkataba huo.

Hivi umejaribu kufuatilia suala la MBOWE kukopa NSSF hatma yake ni imeishia wapi? au inaendelea vp? ndugu yangu "NO RESEARCH NO RIGHT TO SPEAK"
 
Well done LAKINI,
Huyo msomi mwenye Master yeye amezoea kutumia uma na kisu na pengine kijijini labda kufika kwake amepata msiba wa mtu wa karibu, kweli anafahamu watu wa vijijini wanataabika na kitu gani?
 
Huyo jamaa aliyesema chadema ni ya wachagga na kutaja majina ya wachagga kaniboa vibaya sana, hana maana

Mhonga ni mchagga? Hivi huu ulemavu utaisha lini, unajua mtu ukiwa na akili inayoongoozwa na ngvu zako za kiume ndio unaongea mavi kama hivi. Unakaa kwenye computer yako tena labda ya mwajiri wako unakunya kwenye key board yako hadi mavi yanamwagika sakafuni. Why dont you write something else. Well kwa taarifa yako kigezo cha elimu ndicho kigezo kikubwa kimetumika, sasa kama elimu yako darasa la saba, cool off Utawakilishaje watu wenye Phd kwenye jimbo/nchi yako. Chadema is not CCM so be happy and enjoy the show, loser-- lets be serious kwenye hili nyie watumwa wa JK. Hata huyo kiwete wenu kaona deal kujipachika Udaktari sembuse mbunge wa viti maalumu. Hao watu wanaofurika kwenye mikutano ya kampeni ya chadema kule Musoma ni wachagga? Idiot!! Mdomo wako unahitaji wipers kuondoa minyama ya jana iliyoziba kwenye meno na sasa inaruka left and right from your mouth!!

But umeniudhi sana, hii issue ya uchagga ilishapigwa marufuku hapa jamvini wewe bado unaiongelea tu!! Stop it now, unaturudisha kuzimu wewe ala!! Kaoge manake sasa unanuka mavi uliyojipaka!! Crap!!!!
 
Dr. Kitila huku ni kiongozi wa CHADEMA aliyesimamia uchaguzi wa hivyo viti maalumu ulioshindikana na leo wanamwita kama mshauri, hivi wanaelewa maana ya conflict of interest? Ni wakati gani anakuwa kiongozi na wakati gani mshauri?

Afadhali wangesema tu haya majina yameamuliwa na kiongozi wa CHADEMA ambaye ni msomi.

Hilo la kuficha majina ni kwasababu wamechakachua majina na hawataki wahusika wajue kwamba wameachwa.

Kwa vigezo walivyoweka ni wazi wale ambao wamekuwa viongozi kwa muda mrefu watapita kwani wana uzoefu na wamekuwa wakichangia chama hata kama hawatakiwi na wananchi.

Sio muda mrefu hiyo list itatoka tu maana itatolewa na hao hao CHADEMA waliochukia.
 
hivyo vigezo vinaweza kusaidia lakini vigezo ni kitu kimoja na mpangaji matokeo (kwa kutumia vigezo hivyo) ni kitu kingine. kwa sasa inaweza onekana ni njia murua kabisa lakini nahisi huko mbeleni kuna matatizo yatajitokeza. demokrasia iko wapi hapa?
kama viti maalumu ni wawakilishi wa makundi fulani kwa nini makundi hayo yanayowajua watu wao yasishiriki kuchagua? suala ya rushwa na upendeleo linaweza kuthibitiwa kwa kusimamia chaguzi vizuri na si hili la kutumia vigezo tu ambapo mtu anaweza kuwa na vigezo lakini hafai kuwakilisha kundi fulani
 
Mkuu wangu nadhani unapitwa na picha kamili ya uchaguzi wa viti maalum kwa sababu Unashindwa kwanza kutambua nafasi ya Chadema kama chama leo hii.

lakini nitakwambia vizuri, Chadema inategemea kwenda IKULU na kama watafanikiwa hawawezi kuweka majina ya watu hawa wazi leo hali bado kabisa mtihani mkubwa haujakwisha, kwani chukulia tu mfano wa Umoja wa Wanawake. Kama Dr.Slaa atakwenda Ikulu ina maana Chadema hawatasimamia tu chama cha wanawake wanachama wa Chadema na majimbo waliyoshinda ila kutakuwa na uwakilishi wa jumuiya hii Tanzania nzima, tofauti na mpango wa CCM kuwa na jumuiya ya wanawake wanachama wa CCM tu (UWT) kisha watindiga wengine wanajikomba wizarani.

Hivyo hivyo ktk taasisi nyinginezo Chadema hawatarajii kuwatenga wananchi kuendesha taasisi hizo kichama chama, bali kama tunapozungumzia vijana basi itawashirikisha vijana wote nchini bila kuwatenga hivyo ni lazima kuwepo na mtu wa Uhakika tofauti na CCM ambao kwanza hutazama maslahi ya chama kisha wengine mnachomekwa wizarani..Kwa mfano Umoja wa Wanawake nchini UWT ya CCM kina Sophia Simba wana nguvu kubwa kwa wanawake na watoto (wa chama) kuliko hata wizara iliyopewa jukumu hilo hilo kitaifa..Kinachopimwa hapa ni uanachama wa Mtanzania mhusika na huyu mama (kiongozi wa UWT) ana nguvu za ajabu kitaifa (Ukomunist).

Hivyo hakuna sababu ya kuwa na wizara ambazo zina taasisi ya kitaifa zikifanya kazi ile ile. Mimi nadhani ipo kila sababu Dr.Slaa na Chadema kutotangaza majina haya ila pale itakapo takiwa kama vile kutangaza baraza la Mawaziri.. Dr.Slaa na Chadema wakitangaza leo hii mtawaona vichaa wenye kufikiri wao wanajua zaidi ya Mwenyezi Mungu kupanga matokeo.. Mkuu mjuzi ni Mungu pekee, waacheni wajiandae na kukamata Ikulu.....Ikifika wakati wake watatangazwa, nyie hofu yenu ipi haswa ili hali watu hao watakuja tangazwa tu!
 
Back
Top Bottom