Mbunge Aisha Ulenge akizungumza katika Mkutano wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Geneva Uswissi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945
MHE. ENG. AISHA ULENGE, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga Akizungumza katika Mkutano wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Geneva Uswissi.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga, Mhandisi Mwanaisha Ulenge ameshiriki katika Mkutano wa 148 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unaofanyika jijini Geneva Switzerland.

Katika Mkutano huo, Mhandisi Ulenge ameshiriki pia mikutano ya Umoja wa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara (SADC) na Jukwaa la Afrika vikao ambavyo vimeangazia mambo ya dharura yanayohitajika kujadiliwa katika Mkutano wa Dunia unaojadili Diplomasia ya Bunge kupelekea kujenga Amani na Maelewano.

Pia, Mhandisi Ulenge ameshiriki katika majukwaa ya wabunge Wanawake na vijana ambapo amepata nafasi ya kuchangia mada za Mkutano huo kuhusu mifumo ya usalama na Amani.


WhatsApp Image 2024-03-25 at 00.42.10.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-25 at 00.42.40.jpeg
 
So what???
Kama kuna mambo mazuri basi tunataka yazungumzwe kwenye Bunge la nchi hii kule Dodoma, siyo huko kwenye hilo Bunge ambalo sisi hatuna faida nalo yoyote ile.
 
Matatizo ya hapa ndani yamewashinda. Vikokotoo, bima ya afya,nishati,mfumuko wa bei,mkwamo wa ajira nk. Sasa huko nje wakifika wanatoa mchango gani? Hata hao wanaowapa maiki wanakonyezana mnapoongea.
 
Back
Top Bottom