Askofu Thomas Laizer: "Uchaguzi wa Meya Arusha Urudiwe"

Siasa yetu sijui inachukua uso gani kwa sasa. Hadi makanisa ni CHADEMA?
 
Siasa yetu sijui inachukua uso gani kwa sasa. Hadi makanisa ni CHADEMA?

sasa wewe ulitaka asitoe maoni yake kisa ni askofu? Na kama kweli ccm walishinda kihalali uchaguzi wa meya Arusha kwanini hawataki urudiwe ili washinde tena? Si wana uhakika?

mkuu uwe unaona mbali, hawa ni wachakachuaji wakubwa na ndio maana wito unatolewa uchaguzi urudiwe tuone impact yake.
 
si swala la makanisa, bali wananchi wanapenda kuwa chama cha ukombozi wa mwananchi CDM, wamechoshwa na ufisadi na unyanyasaji raia wa wazi
 
Nguvu ya umma haina dini,kabila,rangi,lugha wala eneo.
PEOPLES POWEEEEEEEEEERRR!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Siasa yetu sijui inachukua uso gani kwa sasa. Hadi makanisa ni CHADEMA?

WEWE UNA MAWAZO MGANDO SANA.

Eti makanisa ni CHADEMa mbona hueleweki.

Mkanisa na Misikiti inaongozwa na binadamu kama ww na wao ni sehemu ya jamii tena inayoheshimika ukiachia tabia za mtu moja mmoja.

Hivyo si jambo la kushangaza kusikia Mapadri au mashehe wakitoa maoni yao katika masula ya kisiasa kwa sababu yanawagusa wote.

Ukumbuke, mapandri au mashehe wana ndugu zao ambao si viongozi wa dini na wanaathirika na upuuzi wa kisiasa unaoendelezwa na mafisadi sasa ulitegemea wakae kimya.

mambo mengine tusishabikie tu au kuandika bila fikra.
 
Siasa yetu sijui inachukua uso gani kwa sasa. Hadi makanisa ni CHADEMA?


Sio kwamba makanisa ni CHADEMA, ila hata makanisa na kila taasisi inawajibika kusema pale haki inapokuwa haikutendeka kwamba walionyimwa haki ni CHADEMA AU CCM. Hii inakuwa na uzito zaidi ikiwa kupotoshwa kwa haki huko kuna mwelekeo wa uvunjifu wa Amani. Nadhani kuna uchanga mkubwa wa uelewa kuhusu siasa.

Tatizo ni kwamba wengi (akiwemo Chatanda) wanadhani viongozi wa dini hawana au hawapaswi kutoa mawazo yao kuhusu mambo ya kisiasa. Eti ni kuchanganya dini ni siasa. Ni vyema tufahamu kuwa dini ni wadau wa siasa kama taasisi yoyote nyingine nchini. Siasa ya inchi ikiwa chafu dini huathirika kama wengine. Hivyo ni lazima waseme. Lakini pia viongozi wa dini ni wanadamu wenye fikra na uzalendo wa nchi zao kama wengine. Kuwa kiongozi wa dini hakumnyimi haki yake ya kiraia ya kutoa mawazo yake hasa kama kiongozi wa watu.
 
Bado maaskofu wanaendele kuongelea siasa tu wakati wamevaa majoho yao!!!!!!!! wapi CHATANDA!!!
 
watu wengine bwana.....badala achangie hoja, anaibusha hoja nyingine. ...........
..........Hata mi naona urudiwe tu, ofcoarse, kwenye mazingira huru na haki yenye kufuata misingi ya sheria
 
Hivi mnasahau kabisa kwamba askofu Laizer ameshirikiana sana na viongozi wa CCM kipindi cha Mwinyi na hata Mkapa ndio maana viongozi wakongwe wa CCM hawajasubutu kumpinga. Hii ni kwasababu wanajua historia ya Arusha: mahospitali, shule, maji na miradi mingi ya maendeleo imechangiwa na kanisa, na ccm ndio hao hao walikua wanakuja kuwa wageni rasmi kuzindua hiyo miradi. Leo akitofautiana nao hawataki. Serikali lazima ielewe kwamba haka kamchezo kakusema "Yes sir' kwenye kila kitu kipo CCM tu, watu wengine hasa viongozi wanaoheshimika kwenye jamii hawawezi kuwa wajinga on serious issues. Mtu mwenye akili zake hawezi ingiza politics kwenye huu udhalimu wa polisi unless kama yeye ndio amewatuma.


Siasa yetu sijui inachukua uso gani kwa sasa. Hadi makanisa ni CHADEMA?
 
Sijawahi kumsikia Laizer hata siku moja akihubiri kwa vile mimi ni mkatoliki. Ila leo nimegundua jambo kama Laizer ni Askofu mwenye busara na hekima nyingi sana kati ya viongozi wa dini. Kama kuna mwana jamii yeyote alikuwepo uwanjani leo atakubaliana nami kwamba hotuba na sala ya Laizer imejaa busara na hekima za kutosha. Ameonyesha wazi kama yeye sio tu kiongozi wa dini bali kiongozi wa jamii yote inayomzunguka. Kama viongozi wote wa Tanzania watapata hiyo clip nadhani wanaweza kubadilika sana. Mungu akulinde na kukupa maisha marefu baba Askofu laizer.
 
My motive and suspicion is Arusha wana kaukabila fulani huwa wanapenda sana Meya aitwe Laizer. It is very hidden motive. Anyone can lead us provided will lead us in righteousness na kujitolea kwa wananchi bila kuweka maslahi binafsi. Kuweka akilini haya yatatuwekea negative atitude na kutuvunja moyo pamoja na kutupofusha hata tusione na kushauri kuhushu michakato ya maendeleo. Sikuwa huko wanajamvi wanakohisi. Sometimes watu hu-abuse publicity waliyo nayo. hat kama ni miradi ya afya ni nini vile bado si ya kanisa kama askofu bali ya waumini kwani huchangishwa kufanya maendeleo wao kwa wao. Tusijisahau. Hawa viongozi ni watumishi wetu na sisi raia ndio maboss. Huwaita kwenye interview na kuwahoji kisha kuwachagua au kuwaandika kazi. Kam kila uongozi na mamlaka yanatopka juu. Hata uongozi mbaya hutoka juu ili kwa ajili ya ubaya. We can not have angels to lead Tanzania as we are not angels. Kwanza sote tuutafute uso wa Mwenyezi Mungu na mengine yatakuja kwa ziada. Naomba kuwakilisha.
 
Nimeipenda sana command yake,nategemea wamtii,any thing different wanatafuta vita!
 
Siasa yetu sijui inachukua uso gani kwa sasa. Hadi makanisa ni CHADEMA?
Katika wale waliokufa mmoja wa alikuwa ni muislamu na yale yalikuwa maandamano ya Chadema. Hiyo nayo imekaaje? Tusiingize udini kwenye maslahi ya Taifa letu sooote
 
kama kuna ukweli.... mnategemea askofu akae kimya halafu aendelee kuitwa askofu... huu ndio utakuwa usaliti wa wito... well done aksofu Laizer
 
Siasa yetu sijui inachukua uso gani kwa sasa. Hadi makanisa ni CHADEMA?

Don't put comment kuleta udini na kupotosha ukweli
Wakati unajua uhuni uliofanywa uchaguzi wa
Meya Arusha, acha upuuzi
 
Kwa hiyo misikiti ni ccm? pls think, think! Don't become a thick brainer! Ihate this notion of udini, utatuuwa!
 
Back
Top Bottom