Askofu Basileus Ezekiel Mabumba: Lowassa asipokuwa Rais 2015 mniue!

Hizo harakati anazofanya sasa uku akisaidiwa na ROSTAM waTanzania tutakuja juta....kwanza imagine kwanini anautafuta urais kwa ari na mali? weunafikiria hizo fedha anazotumia unafikiri zitalipwaje? Jamani URAIS km upo upo tu haina haja ya kuangaika mpaka kwa mafree marson wa nIGERIA haina haja....Jamani tuhuma tu zinamtosha mtu kukaa pembeni kwanini YEYE tu? imagine jana kasaliti ata chama chake kwakutoudhulia sherehe kubwa za chama chake akaudhulia MAULID kwanza haimuhusu? YES! TUNAMUHITAJI RAIS KAMA LOWASSA LAKINI SIO SIO SIO HUYU LOWASSA....
 
Ndugu,

Kuhama nchi si sululisho, ni kama vile nyoka ameingia nyumbani kwako alafu wewe unahama nyumba. Utahama nyumba mpaka lini, utajuaje kwamba nyoka ametoka. Suala ni dogo kuwaambia watu wako wote kwamba afai kwa vigezo basi. Kama kweli ameishajipanga na anapitapita na kugawa pesa, pesa hiyo atairudishaje? Ikumbukwe kwamba ni wachache sana wanaoweza kutumia pesa ZAO kwa manufaa ya wengine.
 
mimi nitahama nchi kwani maendeleo yatakuwa ndoto tena

Ndugu,

Kuhama nchi si sululisho, ni kama vile nyoka ameingia nyumbani kwako alafu wewe unahama nyumba. Utahama nyumba mpaka lini, utajuaje kwamba nyoka ametoka. Suala ni dogo kuwaambia watu wako wote kwamba afai kwa vigezo basi. Kama kweli ameishajipanga na anapitapita na kugawa pesa, pesa hiyo atairudishaje? Ikumbukwe kwamba ni wachache sana wanaoweza kutumia pesa ZAO kwa manufaa ya wengine.
 
Kwa nini unauliza kuwa itakuwaje asipokuwa Rais badala ya kuuliza itakuwaje asipokuwa mgombea wa CCM? Mgombea wa urais yeyote yule wa CCM mwaka 2015 na kwa vyovyote vile hatashinda kiti cha urais wa JMT. Najua itakuwa ni rahisi zaidi kumshinda Lowasa kwenye uchaguzi wa Rais kuliko hawa wengine. siye tunasubiria gari yetu T2015CDM, waache Magamba watoane macho na ngeu
mkubwa kumbuka El hategemei huruma ya wanaccm kuwa mgombea bali anatafuta kwa kutumia ukwasi wake. Na hili limedhihirika jana kwa kutohudhuria kwenye ubwabwa wa Nape.llihali anazunguka nchi nzima akihadaa watz kupitia nyumba zao za ibada.
 
Mimi mpaka sasa nachanganyikiwa na jinsi watanzania tulivyo, wengi mmesema huyu jamaa hafai sasa kwanini tumjadili kwa kila angle na kila siku? huku kumjadili sana kunampa uhalali wa kufaa hata kama kweli hafai, mimi ninashauri tuachane naye kama hafai kuwa rais wa Tanzania.

Kwa serikali hii ya ccm ni wachache sana wenye sifa njema ya kuweza kumnyooshea EL kidole (hata hivyo wakipewa nafasi hawawezi kufanya vyema kama bado watabaki ndani ya ccm), wengi ni mafisadi kama hawajafanikiwa kutajirika kwenye huo ufisadi ni matatizo yao wenyewe, mwenzao (EL) kafisadi (kama ni kweli) na katumia vizuri kujijenga kibiashara na sasa ni tajiri, sasa kwakuwa mafisadi wengi wa ccm hawajafanikiwa kuwa matajiri wanafikiri hiyo ni rahisi kuwaaminisha watanzania kwamba wao hawakuwa mafisadi.

Kwa mafanikio ya Tanzania hatuna budi kuijadili ccm kama ccm na sio kiongozi mmoja mmoja, lengo liwe kuing'oa madarakani na sio vita ya EL anafaa au hafai maana hapa janga sio EL ila ccm na mfumo wake wa kifisadi. Tukifikia hatua hiyo ya kupambana na ccm huyo EL hataumiza vichwa vyetu tena, lakini inaonekana bado tuna mawazo ya kuipeleka ccm madarakani baada ya JK.. ndio maana anajadiliwa sana humu, hiyo ni hatari kubwa kuliko tunavyofikiri.
 
EL akiwa rais Tanzania tutakwenda mbelle kwa spidi kubwa huyu jamaa yupo makini sana ana sifa za kiongozi bora,haya ya Richmond asihukumiwe peke yake waliingizwa mjini na wafanyabiashara wazoefu.
 
NDUGU ZANGU WA JF; MMESHAHI KUISOMA HII?

[h=1]Lowassa asipokua rais 2015, mniue – Askofu[/h][h=3] [/h][h=3]Kiongozi mkuu wa kanisa la Last Glory Church la hapa nchini Basileus Ezekiel Mabumba, amesema amepokea ujumbe kutoka kwa Mungu unaoeleza kuwa Waziri Mkuu aliyejiuzuru, Edward Ngoyay Lowassa, atakua rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya uchaguzi wa mwaka 2015.[/h][h=3]Katika mahojiano na gazeti hili (Nyakati), Mabumba alieleza kuwa atawajibika iwapo unabii wake hautatimia. Kwa mujibu wa Torati kile ambacho kilikuja kubainika baadaye kuwa unabii wa uongo, adhabu kwa mtoaji unabii ilikua ni kupigwa mawe hadi afe.[/h][h=3]Jumatano iliyopita, Mabumba alitinga katika ofisi za gazeti hili na kueleza kuwa, kwa muda mrefu sasa amekua akipokea ujumbe kutoka kwa Mungu ukieleza kuwa Lowassa ndiye atakuwa rais wa nchi hii ya awamu ya tano.[/h][h=3]Sehemu ya mahojiano ya gazeti hili na Askofu Mabumba, ambaye hujulikana pia kama Mtume, ilikua kama ifuatavyo:[/h][h=3]Mwandishi: Umesema kwa muda mrefu umekuwa ukiletewa huo ujumbe. Tuambie ni tangu lini? Tuambie pia mtu wa kawaida kabisa anaelewa nini kuhusu unabii?[/h][h=3]Mabumba: Tangu mwanzoni mwa mwaka huu. Kwa uhakika unabii huu nimepata kuwaeleza waumini pale kanisani. Sasa nimeona niufikishe kwa watu wengi zaidi.[/h][h=3]Unabii ni tofauti na kutabiri. Kuna unabii wa aina mbili. Kwanza, ni ule unabii ambao Mungu anakuruhusu kuona mambo yajayo. Ni pale Mungu anapokuonyesha kutakua na nini siku zijazo. Ni karama za ufunuo. Aina ya pili ya unabii ni pale mtu aliyekusudiwa kufikisha unabii huo anaweza kutamka jambo kwa msukumo wa Roho Mtakatifu. Sasa hapo ndio ujue kwamba kuna msukumo wa kibinadamu, wazo la mwanadamu mwenyewe, msukumo wa shetani na msukumo wa Mungu.[/h][h=3]Mwandishi: Sasa Mtu anaweza kutofautisha vipi kama jambo fulani lina msukumo wa mwanadamu, kwa Shetani au wa Mungu?[/h][h=3]Mabumba: Unajua kama ni la Mungu kuna msukumo unaolazimisha kulitafakari kila mara kabla hujalikubali. Unakua kama una mzigo fulani ukikubaliana na Mungu ndipo utapata amani ya kulisema.[/h][h=3]Mwandishi: Lakini kuna nabii nyingi zimetolewa na watumishi hazikutimia. Kuna mtumishi aliwahi kusema angesigina Biblia iwapo unabii wake usingetimia. Haukutimia na hakusigina, leo yuko kimya. Mwingine akasema kutakua na vita…ziko nabii nyingi tu.[/h][h=3]Mabumba: Unabii wangu lazima utimie nimekua nikioneshwa mambo mengi lakini siyatamki. Kuna vitu vidogo vidogo nimeoneshwa na ikawa kweli. Yako na mambo makubwa labda kwa sababu sikuwa ninayasema kama ninavyofanya leo kwa hili. Hili ninasukumwa sana kulitamka.[/h][h=3]Mwandishi: Usipotimia?[/h][h=3]Mabumba: Niko tayari kuwajibika. Manabii waliwajibika kwa unabii wao. Hata nisipopondwa mawe, watu hawataniamini tena, hayo tayari ni ‘mawe’[/h][h=3]Mwandishi: Kwa mazingira ya sasa ambayo watu wamepunguza imani wapo ambao wanaweza kufikiri kuwa umetumwa na unatumia nafasi yako ya utumishi wa Mungu kutumikia wanasiasa? Wengine wanaweza kufikiria kuwa unatafuta umaarufu.[/h][h=3]Mabumba: Kwanza kabisa sitaki kuwa karibu na wanasiasa, hata chama sina, sijishughulishi kabisa na wanasiasa. Sifahamiani na Lowassa. Na ninafikiri kama ni hivyo Lowassa mwenyewe angeenda kwa wahubiri wakubwa. Mimi ninasema nilicholetewa.[/h][h=3]Kama kuna watakaofikiria ninatafuta umaarufu, watakuwa wamekosea. Sihitaji umaarufu zaidi ya hapa. Naandika vitabu watu wengi wananifahamu kupitia huduma hiyo. Ninaandika vitabu na vinapendwa, inatosha. Siwezi kutumia unabii feki kujijenga.[/h][h=3]Mwandishi: Unaweza kuzungumza chochote kuhusu dhana ya kujivua gamba ndani ya CCM ambacho Lowassa ni mwanachama na kiongozi?[/h][h=3]Mabumba: Sifuatilii mambo ya vyama. Kwa habari ya unabii Mungu anakuonesha kidogo tu. Hayo mengine siyajui bwana. Kama kuna kuna kuvuana gamba mi sijui.[/h][h=3]Lowassa Waziri Mkuu aliyejiuzuru kutokana na kashfa ya Kampuni ya umeme ya Richmond hajapata kutangaza hadharani kuwa ana nia ya kugombea urais mwaka 2015, lakini harakati za kisiasa ndani na nje ya chama chake cha CCM zinaashiria kuwa ni mmoja wa wanasiasa walioko katika ‘vita’ ya urais.[/h][h=3]Hivi karibuni Lowassa alionekana katika televisheni akishiriki kwenye ibada katika kanisa linaloongozwa na mhubiri maarufu wa nchini Nigeria, TB Joshua.[/h][h=3]Kushiriki kwa Lowassa katika ibada hiyo kulizua minong’ono, wengine wakihusisha na harakati za urais 2015 na kwamba alienda kuombewa ili ‘nyota yake ing’ae’.[/h][h=3]Hata hivyo baadhi ya watumishi wa Mungu walikerwa na kitendo cha baadhi ya watu kushangazwa na uwepo wa Lowassa katika Ibada hiyo, wakisema ni kuingilia uamuzi binafsi wa mtu anayemtafuta Mungu wake.[/h]Source: NYAKATI, Julai 10-16, 2011
 
Bado natafakari mara mbilimbili hivi, kitatokea nini ndani ya CCM iwapo hawatamsimamisha EL kuwa mgombea wa nafasi ya Urais hapo 2015?
 
NDUGU ZANGU WA JF; MMESHAHI KUISOMA HII?

Lowassa asipokua rais 2015, mniue – Askofu



Kiongozi mkuu wa kanisa la Last Glory Church la hapa nchini Basileus Ezekiel Mabumba, amesema amepokea ujumbe kutoka kwa Mungu unaoeleza kuwa Waziri Mkuu aliyejiuzuru, Edward Ngoyay Lowassa, atakua rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya uchaguzi wa mwaka 2015.

Katika mahojiano na gazeti hili (Nyakati), Mabumba alieleza kuwa atawajibika iwapo unabii wake hautatimia. Kwa mujibu wa Torati kile ambacho kilikuja kubainika baadaye kuwa unabii wa uongo, adhabu kwa mtoaji unabii ilikua ni kupigwa mawe hadi afe.

Jumatano iliyopita, Mabumba alitinga katika ofisi za gazeti hili na kueleza kuwa, kwa muda mrefu sasa amekua akipokea ujumbe kutoka kwa Mungu ukieleza kuwa Lowassa ndiye atakuwa rais wa nchi hii ya awamu ya tano.

Sehemu ya mahojiano ya gazeti hili na Askofu Mabumba, ambaye hujulikana pia kama Mtume, ilikua kama ifuatavyo:

Mwandishi: Umesema kwa muda mrefu umekuwa ukiletewa huo ujumbe. Tuambie ni tangu lini? Tuambie pia mtu wa kawaida kabisa anaelewa nini kuhusu unabii?

Mabumba: Tangu mwanzoni mwa mwaka huu. Kwa uhakika unabii huu nimepata kuwaeleza waumini pale kanisani. Sasa nimeona niufikishe kwa watu wengi zaidi.

Unabii ni tofauti na kutabiri. Kuna unabii wa aina mbili. Kwanza, ni ule unabii ambao Mungu anakuruhusu kuona mambo yajayo. Ni pale Mungu anapokuonyesha kutakua na nini siku zijazo. Ni karama za ufunuo. Aina ya pili ya unabii ni pale mtu aliyekusudiwa kufikisha unabii huo anaweza kutamka jambo kwa msukumo wa Roho Mtakatifu. Sasa hapo ndio ujue kwamba kuna msukumo wa kibinadamu, wazo la mwanadamu mwenyewe, msukumo wa shetani na msukumo wa Mungu.

Mwandishi: Sasa Mtu anaweza kutofautisha vipi kama jambo fulani lina msukumo wa mwanadamu, kwa Shetani au wa Mungu?

Mabumba: Unajua kama ni la Mungu kuna msukumo unaolazimisha kulitafakari kila mara kabla hujalikubali. Unakua kama una mzigo fulani ukikubaliana na Mungu ndipo utapata amani ya kulisema.

Mwandishi: Lakini kuna nabii nyingi zimetolewa na watumishi hazikutimia. Kuna mtumishi aliwahi kusema angesigina Biblia iwapo unabii wake usingetimia. Haukutimia na hakusigina, leo yuko kimya. Mwingine akasema kutakua na vita…ziko nabii nyingi tu.

Mabumba: Unabii wangu lazima utimie nimekua nikioneshwa mambo mengi lakini siyatamki. Kuna vitu vidogo vidogo nimeoneshwa na ikawa kweli. Yako na mambo makubwa labda kwa sababu sikuwa ninayasema kama ninavyofanya leo kwa hili. Hili ninasukumwa sana kulitamka.

Mwandishi: Usipotimia?

Mabumba: Niko tayari kuwajibika. Manabii waliwajibika kwa unabii wao. Hata nisipopondwa mawe, watu hawataniamini tena, hayo tayari ni ‘mawe’

Mwandishi: Kwa mazingira ya sasa ambayo watu wamepunguza imani wapo ambao wanaweza kufikiri kuwa umetumwa na unatumia nafasi yako ya utumishi wa Mungu kutumikia wanasiasa? Wengine wanaweza kufikiria kuwa unatafuta umaarufu.

Mabumba: Kwanza kabisa sitaki kuwa karibu na wanasiasa, hata chama sina, sijishughulishi kabisa na wanasiasa. Sifahamiani na Lowassa. Na ninafikiri kama ni hivyo Lowassa mwenyewe angeenda kwa wahubiri wakubwa. Mimi ninasema nilicholetewa.

Kama kuna watakaofikiria ninatafuta umaarufu, watakuwa wamekosea. Sihitaji umaarufu zaidi ya hapa. Naandika vitabu watu wengi wananifahamu kupitia huduma hiyo. Ninaandika vitabu na vinapendwa, inatosha. Siwezi kutumia unabii feki kujijenga.

Mwandishi: Unaweza kuzungumza chochote kuhusu dhana ya kujivua gamba ndani ya CCM ambacho Lowassa ni mwanachama na kiongozi?

Mabumba: Sifuatilii mambo ya vyama. Kwa habari ya unabii Mungu anakuonesha kidogo tu. Hayo mengine siyajui bwana. Kama kuna kuna kuvuana gamba mi sijui.

Lowassa Waziri Mkuu aliyejiuzuru kutokana na kashfa ya Kampuni ya umeme ya Richmond hajapata kutangaza hadharani kuwa ana nia ya kugombea urais mwaka 2015, lakini harakati za kisiasa ndani na nje ya chama chake cha CCM zinaashiria kuwa ni mmoja wa wanasiasa walioko katika ‘vita’ ya urais.

Hivi karibuni Lowassa alionekana katika televisheni akishiriki kwenye ibada katika kanisa linaloongozwa na mhubiri maarufu wa nchini Nigeria, TB Joshua.

Kushiriki kwa Lowassa katika ibada hiyo kulizua minong’ono, wengine wakihusisha na harakati za urais 2015 na kwamba alienda kuombewa ili ‘nyota yake ing’ae’.

Hata hivyo baadhi ya watumishi wa Mungu walikerwa na kitendo cha baadhi ya watu kushangazwa na uwepo wa Lowassa katika Ibada hiyo, wakisema ni kuingilia uamuzi binafsi wa mtu anayemtafuta Mungu wake.

Source: NYAKATI, Julai 10-16, 2011
Huyo Askofu anaonekana ana malengo yake, labda anamfurahisha huyo Lowasa ili amaulike kwenye Harambee ya kuchangia kanisa lake!!!! Lakini kusema Mungu amamwambia au amaemuonyesha siamini kwa kuwa Mungu aliye hai Jehova hawezi kuwa mnafiki kama anavyo dhani!!!!Kwanza Marehemu Nyerere alimfukuza kwa kukosa uadilifu kipindi hicho, ikaja zamu hii akajiudhuru mwenyewe kwa kukosa uadilifu kwenye sakata la RICHIMOND!!!! Sasa tena Mungu wake huyo atuletee mchoraji Lowasa ili alifilisi taifa la TANZANIA!!!! Tunaomba tusije kuwa kama wana wa Israel walipo mkataa Mungu aliwapa Sauli awatawale kwa hasara zao wenyewe!!!!!

 
Bado natafakari mara mbilimbili hivi, kitatokea nini ndani ya CCM iwapo hawatamsimamisha EL kuwa mgombea wa nafasi ya Urais hapo 2015?
CCM wakimsimamisha kugombea tutatumia resources tulizo nazo kidogo Mungu wetu akiwa Jemedari kuhakikisha Lowasa hachaguliwi na wananchi wa Tanzania!!!! Labda atumie majeshi kama alivyotaka kufanya Arusha, mkuu wa Polisi akamkatalia!!!! Hii kampeini anayotumia makanisa haimsidii maana si wakristo wote watakao kubaliana na Wachungaji na Maaskofu!!!!!

 
Back
Top Bottom