Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,810
- 15,398
Hivi mnajua kwamba karibu wanaume watano kati ya kumi wanakabiliwa na uhanithi wa aina fulani? Fasihi mbalimbali za tafiti kuhusu hali hii kwa wanaume zinaonyesha kwamba, zaidi ya asilimia 52 ya wanaume wa umri kati ya 40 hadi 70 wanakabiliwa na uhanithi wa aina na viwango mbalimbali. Lakini idadi ya kutosha kati ya hao ni ya wale ambao wana matatizo ya maradhi kama shinikizo la damu, maradhi ya moyo na kisukari.
Wale ambao wana matatizo hayo na ambao wanavuta sigara wako kwenye hali mbaya zaidi na siyo ajabu kwao kuwa na uhanithi wa kudumu. Lakini hata wale ambao hawana maradhi ya aina yoyote, kuna wengi sana ambao wana matatizo haya, ingawa wenyewe wanajiona wako sawa. Uhanithi ni pamoja na na mwanaume kuimaliza haja mapema sana, kushindwa kumaliza na mengine, ambayo kwa mazoea hayaonekani kuwa ni uhanithi. Ongezeko la wauza miti shamba ya kuongeza nguvu za kiume na ukubwa wa maumbile ni ushahidi tosha wa kuthibitisha ukweli huu........... Bidhaa haiwezi kuwa sokoni kwa wingi kama haina wateja........................!