Asilimia 52 ya wanaume hapa nchini siyo rijali……….!

hivi uhanithi na kutokuwa na nguvu za kiume ni sawa??? lol i just think kusema kutokuwa na nguvu za kiume ni heshima zaidi???hilo lingine tumezoea kutukanana mitaani lol
 
Weka data evidence humu na si blah blah kama hii. Tungependa kujua utafiti huu ulifanywa lini, wapi na vipi? sehemu zilizofanyiwa utafiti zilipatikanaje, waliofanyiwa utafiti huo (Sample) walipatikanaje? Utafiti uliendeshwaje ? Ulinganifu wa matokeo na utafiti wa namna hiyo uliofanywa sehemu nyingine; na jarida lililochapisha. Hizi ni baadhi tu ya dondoo zinazoweza shawishi conclussion yako na si hiyo yako ambayo haina tofauti sana na ya wagagnga wa kienyeji.

Ndugu, ukiona moshi ujue moto upo. Kama dawa za kuongeza nguvu soko lake linaongezeka ujue tatizo lipo.
 
Hivi mnajua kwamba karibu wanaume watano kati ya kumi wanakabiliwa na uhanithi wa aina fulani? Fasihi mbalimbali za tafiti kuhusu hali hii kwa wanaume zinaonyesha kwamba, zaidi ya asilimia 52 ya wanaume wa umri kati ya 40 hadi 70 wanakabiliwa na uhanithi wa aina na viwango mbalimbali. Lakini idadi ya kutosha kati ya hao ni ya wale ambao wana matatizo ya maradhi kama shinikizo la damu, maradhi ya moyo na kisukari.

Wale ambao wana matatizo hayo na ambao wanavuta sigara wako kwenye hali mbaya zaidi na siyo ajabu kwao kuwa na uhanithi wa kudumu. Lakini hata wale ambao hawana maradhi ya aina yoyote, kuna wengi sana ambao wana matatizo haya, ingawa wenyewe wanajiona wako sawa. Uhanithi ni pamoja na na mwanaume kuimaliza haja mapema sana, kushindwa kumaliza na mengine, ambayo kwa mazoea hayaonekani kuwa ni uhanithi. Ongezeko la wauza miti shamba ya kuongeza nguvu za kiume na ukubwa wa maumbile ni ushahidi tosha wa kuthibitisha ukweli huu........... Bidhaa haiwezi kuwa sokoni kwa wingi kama haina wateja........................!

Huu ni upuuzi mtupu! Tafadhali acha kupotosha ndugu. Unajua maana ya "uhanithi" wewe? Nyambaaf!
 
Jitafiti kabla Hujatafitiwa...

Ushauri, Nenda kwa kila mjumbe wa 10 houses, mwabie unahitaji utafiti kwa wanaume wa kila kaya ukiongozana na Walimbwende kadhaa kama testa, plus Lots of Condoms kwa utafiti wako.(kama kupima Ngoma ). natumai utapata jibu, na c porojo hizi..
 
Weka data evidence humu na si blah blah kama hii. Tungependa kujua utafiti huu ulifanywa lini, wapi na vipi? sehemu zilizofanyiwa utafiti zilipatikanaje, waliofanyiwa utafiti huo (Sample) walipatikanaje? Utafiti uliendeshwaje ? Ulinganifu wa matokeo na utafiti wa namna hiyo uliofanywa sehemu nyingine; na jarida lililochapisha. Hizi ni baadhi tu ya dondoo zinazoweza shawishi conclussion yako na si hiyo yako ambayo haina tofauti sana na ya wagagnga wa kienyeji.

ishu siyo data kazipata wapi ishu ni je ni kweli haya yasemwayo?
binafsi nathibitisha hayo kwani idadi ya watu wanaonunua dawa hizi simba power plus, na za kufanana na hizo ni wengi. kilichonishangaza ni kwamba kwenye yale magazeti ya makorokocho matangazo 20 yanayokuwemo ndani yake basi ni ya dawa hizo sasa je tuseme hazina soko? kama hazina zinawezekanaje kutangazwa?
 
Back
Top Bottom