Zijue faida za kuwa na mke

Kambi ya Fisi

JF-Expert Member
Feb 3, 2018
13,514
21,996
Faida za kuwa na mke ni nyingi sana.

Nakala ya 2023 ya Ufadhili wa Utafiti wa Afya (HRF) ilionyesha kuwa wanaume walioowa wanaishi miaka 17 zaidi ya wanaume wasio na wenzi.

Wanaume wasiowa hawako salama kiafya kwa sababu wanakabiliwa na ulaji chakula kisicho bora, ulevi wa kupindukia, uzinzi na uasherati na tabia zingine hatari.

Utafiti mwingine wa 2023 wa wanaume 6,800 wenye umri wa kati ya miaka 45 na 84 uliofanywa na Chuo cha Marekani cha Cardiology ulionyesha kuwa wanaume waseja wana uwezekano mara mbili wa kukumbwa na mfadhaiko na kushindwa kwa moyo.

Faida iliyo kuu ya kuoa ni hii, "mkeo atakulinda na watu wanaokutumia vibaya. Atalinda sifa yako. Atakufanya uheshimike zaidi".

Na kuna upendeleo maalum kutoka kwa Mungu kwa yeye apataye mke (Mithali 18:22).

Kwa ujumla, wanaume wanapoowa, huwa wanafanya vyema maishani. Ndiyo maana Mungu anawaonya wanaume wasimsahau mke wa ujana wao ambaye aliwasaidia kusimama kwa miguu yao (Mal 2:14-16).

Kwa nini upige punyeto wakati Mungu amekuumbia mwenzako kwa kazi bora ya kibinadamu?

Biblia inasema ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa (1Kor 7:9). Jipatie msichana mzuri, hata kama ni ni 'lishangazi' we oa tu utaenjoy maisha marefu. Wekeza kwenye ndoa yako.

NB : wale team kataa ndoa wengi wao wana matatizo ya afya ya akili, usisikilize ufyatu wao.

Pata mke ufurahie uumbaji wa Mungu.

#Wanawake msome comments tu za wanaume, comments zenu hazihitajiki kwa huu uzi.

Barikiwa.
 
Back
Top Bottom