Asanteni wote kwa ushauri wenu, Nimefanikiwa kupata ujauzito

hakunipa masharti ni kitu ambacho alivyoniambia hata mimi ni dharau ila nilijipa moyo tuu ni maini robo na nyama ya ng'ombe sehemu ya nundu iliyojaa mafuta unapika pamoja bila maji coz maini yatatoa maji nundu itatoa mafua itaiva then kuna dawa ya kimasai jina niliandika kwenye diary nikiisoma nitakuandikia unachananya unakula baada ya siku 15 unarudia tena na inakuwa basi

Mrs Xian ubarikiwe Mtoto mwma. Hivyo kama ulivyokirimwa njia ya kutengeza Dawa, Nawe wakirimu wengine utengenezaji wa dawa hiyo, kwani wapo wengi wanatamani ujauzito na waoto...ili mzunguko wote utimie! Hongera na ujitunze tuje kukaona kaBaby !!
 
JF ni kama daladala kila mtu anaingia, mwenye akili zake, mwenye akili za kumtosha mwenyewe, wakurupukaji, mpaka mapunguani wamo! usikubali furaha yako iharibiwe na asiyejua maana.
 
Kila la heri na baraka katika safari yako, uwe unatuhabarisha kila nafasi inapokuruhusu kufanya hivyo. Hongera zako nyingi sana.
 
habari, wapendwa nakumbuka ilikuwa tarehe 14 ya julai mwaka huu nilivyofanya vipimo baada ya kukaa muda mrefu bila kupata ujauzito nilienda hospital kubwa kama tano hapa dar na nilionana na madaktari bingwa wa magonjwa ya wanawake tofauti tofauti ila wote majibu yao yalikuwa sawa kuwa sitaweza kupata ujauzito kwa njia ya kawaida, labda nijaribu kupandikiza.
kiukweli niliumia sana na nilikuja kuomba msaada wa mawazo hapa nawashukuru wote waliovaa uhusika na kuumia pamoja nami pia nawashukuru hata wale walionitolea maneno mabovu.

basi, baada ya kuleta hapa nilitajiwa dawa mbalimbali ila niliona nianze na dawa ya dada mmoja ambaye yuko singida kwa kuwa ilikuwa ni chakula tuu huyo dada nakumbuka jina lake ni Hornet, toka mwezi wa saba nilivyotumia ikawa kimya nikakata tamaa. mwezi huu wa novemba ndiyo nimegundua kama mimi ni mjamzito.

Julai nilitoka machozi ya uchungu na Mungu amenifuta machozi hayo na kunitoa yenye furaha, nawashukuruni wote kiukweli mlikuwa wengi siwezi kutaja majina ila yaani nimekuwa kama sijielewi kwa furaha, naomba muendelee kuniombea nifike salama safari hii yaa kuelekea kuwa mama

Mungu awabariki sana, dada HORNET NITAKUAFUTA KESHO KWENYE SIMU.

Hongera! tatizo lilikuwa nini dada hadi madokta bingwa wakwambie kwa kauli zinazofanana?
 
Hongera! tatizo lilikuwa nini dada hadi madokta bingwa wakwambie kwa kauli zinazofanana?

nilishawahi kufanyiwa operationa ya sisti( sorry siwezi kuandika kwa kizungu hiyo sisti) nikiwa fm four 2005 na niliambiwa ovary yangu iliharibika na kutolewa ikabaki moja nayo ikawa nusu mbovu, miaka imeenda nimeolewa naafua mtoto hakuna ndio nikashauriwa kupima, mrija mmoja nilio baki nao ukaonekana umeziba wote tena karibia na kizazi, doctors wakasema haifai kusafisha wala kunifanyia operation itakuwa wananisumbua tuu kwani imekaa vibaya sana.

Ndiyo nikashauriwa kupandikiza na gharama yake ilikuwa 12 - 15 m julai ile hiyo hela kwangu ilikuwa kama mitihani ya board ilikuwa ngumu sana hivyo nikaja kuomba msaada hapa wa mawazo, ndiyo ilivyokuwa hivyo kaka
 
Kila la heri na baraka katika safari yako, uwe unatuhabarisha kila nafasi inapokuruhusu kufanya hivyo. Hongera zako nyingi sana.

I wish nijue kupost picha hapa maana kuna watu wanaona nafanya promo ningeweka vyeti na vipimo vyote vile vya kwanza na nilivyopimwa sasa, na niakapoendelea ili wajua siko kipromo. ni kushukuru na ninajua wengi wanatatizo kama hili langu.
 
JF ni kama daladala kila mtu anaingia, mwenye akili zake, mwenye akili za kumtosha mwenyewe, wakurupukaji, mpaka mapunguani wamo! usikubali furaha yako iharibiwe na asiyejua maana.

asante sana
 
Mrs Xian ubarikiwe Mtoto mwma....Hivyo kama ulivyokirimwa njia ya kutengeza Dawa, Nawe wakirimu wengine utengenezaji wa dawa hiyo, kwani wapo wengi wanatamani ujauzito na waoto...ili mzunguko wote utimie !! Hongera na ujitunze tuje kukaona kaBaby !!

Asante sana nimeshafanya hivyo kwa wengine na baadhi wameshafanikiwa haraka wengine naendelea kuwa tia moyo labda nao watachelewa kama mimi ila itawasaidia
 
ooh Xian polesana

Wang walimwita anajaza choo,, akuna kama Mungu alipokuja was kwanza just after mmoja nanusu mwaka kingine kikafwata nakupatia upakoo huu in Jesus name ukapate wa. pili ndani yanmiaka miwiili ijayo baada ya kuzaa ,,hongera shemeji huo ndio uanaume nasema daily ndoa nwawili ukiingiza wa Tatu Si ndoa tena..nasikitika ndugu mmoja rafiki yet nae alichelewa kuzaa Mkewe baada ya three yrs kamtimua binti akapata jamaa next yr akabeba kama alivyo binti akuficha kilichomtokea kwa mume wa kwanza

Ili jamaa aamue kuvua ama kuvaa akamweleza nimekupenda we we kama we we...same yr anaapata ujauzito
 
Hongera mpz n Mungu akujaalie uje ujifungue salama, na mie mgen humu ndan jaman nna tatizo hilo pia nsaidie kuijua hyo dawa yakuchanganyia na maelekezo mengine kama yapo
 
SimamaNA Mungu sana sana sana.

Wakati wa kumdhirisha Mungunatoenkiumbe chake wakati muafaka...dini yetu wanasema kuna vitu vinaitwa kisasi. Kemea nankataa kwa dini unayoiamiji...wapo wasioifurahia jambonhili ila kwa damu ya Yesu.

Namhifadhi mama na mtoto na visasi vya ukoo,familia,ndugu,jamaa,majirani,marafiki wala visiwaguse. Mpaka atakapokuja duniani

Mungu natangaza mtoto kuja mud a muafakanmiezi Tisa sharp,,,lolote bay a liliongelewa juu yakee nageuza kwa dameu ya Yesu
 
SimamaNA Mungu sana sana sana
Wakati wa kumdhirisha Mungunatoenkiumbe chake wakati muafaka...dini yetu wanasema kuna vitu vinaitwa kisasi.

Kemea nankataa kwa dini unayoiamini..wapo wasioifurahia jambonhili ila kwa damu ya Yesu
Namhifadhi mama na mtoto na visasi vya ukoo,familia,ndugu,jamaa,majirani,marafiki wala visiwaguse. Mpaka atakapokuja duniani

Mungu natangaza mtoto kuja mud a muafakanmiezi Tisa sharp,,,lolote bay a liliongelewa juu yakee nageuza kwa dameu ya Yesu
 
uliisoma vizuri? aliniambia nikifanikiwa

Nimesoma vizuri, nilikurupuka. Kumbe ilikuwa dawa kwanza malipo baadae.

Asante kwa kunielewesha.

Nimejiridhisha kwamba uko genuine na lengo sio kutangaza biashara.

Mungu awe nawe.
 
Back
Top Bottom