Nakosa usingizi kwa kuwaza hili jambo, Wazoefu naomba ushauri wenu

Mcanada

JF-Expert Member
Jun 8, 2020
982
1,904
Jamani wanaume wenzangu mimi mcanada nimeoa tayari mwanamke wa kichaga tuna miaka 6 kwenye ndoa na tumefanikiwa kupata watoto wawili katika harakati zangu za maisha nikafanikiwa kuja canada na baadae nikamvuta mke wangu na mtoto wetu wa kwanza wakafika canada na baada ya miaka miwili baadae tukapata mtoto wa pili ambaye amejifungua kule kule canada sasa kitengo ambacho nipo pale kazini canada kimenifanya niwe mtu wa kusafiri safiri sana nchi tofauti..

Katika rotation zangu za kikazi miezi hii 6 nitakuwa finland na huu mwezi unaenda wa tatu ...sasa katika harakati za kazi huku na kule nimejikuta tu nimeingia mahusiano na mdada mfinland mmoja na akatokea kunielewa kweli kweli na kuniamini mno ila kwasababu wazungu huwa wanapenda transparency nikajiwekea ulinzi kwanza kwanza kwa kumwambia ukweli kuwa mimi nishaoa na familia yangu ipo Canada ila cha kushangaza alichonijibu ni kuwa hana tatizo juu ya hilo anachohitaji tu mimi kumpa penzi as friend kuhusu ndoa yangu hana tatizo nayo ataheshimu na hataiingilia kwa chochote.

Basi nikaona isiwe tabu wikiendi hii iliyopita bi dada huyu alikuja kwenye nyumba niliyopangiwa na ofisi tukafanya ya kufanya wee kama ilivyo wikiendi zingine ila tulipomaliza akanimbia kuwa pamoja na ujio wake ila pia amekuja kunipa taarifa kuwa tayari ana ujauzito wa mwezi mmoja na hayupo tayari kutoa huo ujauzito na kuhusu matunzo sijui takataka zingine zote zitakuwa juu yake mwenyewe anachohitaji tu kutoka kwangu ni mimi kuwa karibu naye mpaka atakapojifungua.

Sasa yaani toka amenipa hiyo taarifa yaani usingizi sipati kabisa yaani kwakuwa si kitu nilichotegemea kumsaliti mke wangu mpaka kuzaa nje ya ndoa yaani sasa naona hili suala linanitafuna taratibu nasikia hatia kubwa mno maana mke wangu mchaga yule ananiheshimu na kuniamini mno sasa sijui akigundua hii issue sijui itakuwaje.

Sitamani kuingiiza ndoa yangu matatani kwasababu ya hili suala maana litaniharibia mambo yangu mengi mno nyuma ya pazia wazoefu wa haya mambo naomba ushauri wenu nifanyeje ili hili suala nilizike chichini kwa chini yaani mke wangu asijue wala kunusa harufu yoyote kuwa tayari kuna mtoto nje maana mke wangu ni mchunguzi mchunguzi sana.

Nishaharibu mwanaume mwenzenu.
 
Si bora hata wew kukuambia atajihudumia mwenyewe. Huku uswahilini ukimpa demu mimba hata kama alikua na kikazi anaacha ili umuhudumie.na ndio Maana wengi wanakataa mimba sababu ya najukumu.
We cha msingi mkeo asijue,kitanda hakizai haramu
 
1682978487027.jpg
 
Hakukuwa na sababu ya kutaja kabila la mkeo.

Kauli hiyo imekaa kidharau dharau kama vile mkosaji. Wewe mkosaji ndio ingejitambulisha kwa kabila lako kama vile...mimi Muhaya wa Kashozi🤣🤣🤣🤣maana ni mkosaji na sio mkeo.

Hilo la usaliti pambana nalo sina uzoefu kama huo.
Nakuitia mtaalamu wetu wa IT za usaliti akusaidie
DeepPond njoo🤣🤣🤣🤣
 
Aisee!
Mkuu umejaribu kuharibu Maisha yako.

Inabidi uwe Transparent Kwa Mkeo piah!
Ila itakupasa uanzie mbali
nipe mwanga nifanyeje hili lisiniaribie ndoa kaka mkubwa dah yaani nimejikuta nipo tu mitandaoni humu jamii forum mara instagram mara facebook akili yangu naona inaweweseka kuna kazi natakiwa kesho kwnda kuifanya ila naona jambo litanipunguzia ufanisi
 
nipe mwanga nifanyeje hili lisiniaribie ndoa kaka mkubwa dah yaani nimejikuta nipo tu mitandaoni humu jamii forum mara instagram mara facebook akili yangu naona inaweweseka kuna kazi natakiwa kesho kwnda kuifanya ila naona jambo litanipunguzia ufanisi

Kikawaida Wanawake Hawana shida na mtoto ikiwa alikukuta naye lakini kumleta mtoto Baada ya Ndoa kwao ni usaliti wa Hali ya juu Mno.
Wengi hushindwa kusamehe na hunuia kulipa Kisasi kama hamtaachana,

Itakupasa uandae scenario ya kumuambia Mkeo ukweli hasa huyo Mzungu akishajifungua, Kwa sasa tulia tuu wala usimshauri aitoe. Huo sio ushauri mzuri.

Wakati mimba inaendelea kukua andaa tukio la kujifanya upo upset kila mara lakini usimpe sababu ya wewe kuwa hivyo, fanya hivyo lakini sio kila mara. Lakini sio kila Siku.
 
Kikawaida Wanawake Hawana shida na mtoto ikiwa alikukuta naye lakini kumleta mtoto Baada ya Ndoa kwao ni usaliti wa Hali ya juu Mno.
Wengi hushindwa kusamehe na hunuia kulipa Kisasi kama hamtaachana,

Itakupasa uandae scenario ya kumuambia Mkeo ukweli hasa huyo Mzungu akishajifungua, Kwa sasa tulia tuu wala usimshauri aitoe. Huo sio ushauri mzuri.

Wakati mimba inaendelea kukua andaa tukio la kujifanya upo upset kila mara lakini usimpe sababu ya wewe kuwa hivyo, fanya hivyo lakini sio kila mara. Lakini sio kila Siku.
asante mkuu ushauri wako nauzingatia
 
Ipe rikizo familia yako irudi nyumbani kwanza,ili umalize la huyu demu wa Kifalme

ASEE MKUU UMEOGA MAJI YA BARAFU BILA KUPENDA......sisi tukisimamisha tu hatujutii hadi tumalize dhambi ya asili.
 
Nataka nikuambia hivi...
Ogopa sana Mwanamke anayekuambia atalea Mimba mwenyewe na gharama zote za mtoto zitakuwa juu yake...Hasa mwenye kipato chake...

Ipo hivi;Kuna wanawake wengine wametafuta mtoto/watoto muda hawapati...wakipata ndiyo kama hivyo...hakuna unachoweza kumwambia akakuelewa....(Hii ilimtokea Mtu mmoja namfahamu,Nina Ushuhuda)

Na kitakachotokea baada ya Wewe kumuacha na hiyo mimba...Kama wewe ni Mzazi/Baba unayejali Damu yako kuna siku utamtafuta tu....Unachotakiwa kufanya Mwambie tu Mke wako....Hakuna namna...Ukinyamaza kuna siku atajua... Na akijua mwenyewe ni hatari zaidi kwako....

Nimemaliza.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom