Asante Donald Trump kwa kuwavua nguo Wazungu!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,786
Chaguzi zote za Wazungu huwa zinaibiwa au kwa maana nyingine huwa zimeshapangwa na Rais au Kiongozi huwa tayari ameshateuliwa wanachofanya Wananchi ni kutimiza wajibu wao tu, lkn Wazungu wamekuwa wakizunguka Dunia nzima kuwaambia wengine kwamba chaguzi zao siyo free and fair!

Sasa mwaka huu D.Trump anawaumbua Wazungu, kwamba wao ndiyo waibaji kura wakubwa ukiangalia nchi ya Uingereza Waziri Mkuu wake ajulikanaye kama Tereza May hakuna aliyempigia kura lkn ndiyo kiongozi wa Uingereza, sasa demokrasia iko wapi hapo?

Huyo may amewekwa tu na maelite kuwaongoza Wananchi ambao hawajamchagua, najua Mwafrika utakuja hapa kumtetea Bwana ako Mzungu lkn ukweli ni kwamba huyo May hajachaguliwa na wananchi wa Uingereza bali amesimikwa madarakani!

Fikiria nchi ya Kiafrika iweke Raisi wa nchi bila ya uchaguzi halafu Raisi awekwaye kama alivyofanya May akatae kuitisha Uchaguzi watu wangeita ICC, lkn Mzungu kwa kuwa ni mnafiki na ametumia miaka zaidi ya 100 kumbrain wash Mwafrika kwamba yeye ni superior being basi Mwafrika huamini chochote afanyacho Mzungu!

Lkn ukweli ni ukwamba chaguzi zote Ulaya na USA huibiwa na Wananchi kamwe hawaamui nani awe Rais!

Sasa mwaka huu D.Trump anaianika live system ya Kimafia ya Kizungu na USA hapatatosha kwa maana Wazungu wameshachoka na wanaitaka nchi yao iliyoharibiwa na akina Obama, Clinton &Co.!
 
Chaguzi zote za Wazungu huwa zinaibiwa au kwa maana nyingine huwa zimeshapangwa na Raisi au Kiongozi huwa tayari ameshateuliwa wanachofanya Wananchi ni kutimiza wajibu wao tu, lkn Wazungu wamekuwa wakizunguka Dunia nzima kuwaambia wengine kwamba chaguzi zao siyo free and fair!

Sasa mwaka huu D.Trump anawaumbua Wazungu, kwamba wao ndiyo waibaji kura wakubwa ukiangalia nchi ya Uingereza Waziri Mkuu wake ajulikanaye kama Tereza May hakuna aliyempigia kura lkn ndiyo kiongozi wa Uingereza, sasa demokrasia iko wapi hapo?
Huyo may amewekwa tu na maelite kuwaongoza Wananchi ambao hawajamchagua, najua Mwafrika utakuja hapa kumtetea Bwana ako Mzungu lkn ukweli ni kwamba huyo May hajachaguliwa na wananchi wa Uingereza bali amesimikwa madarakani!

Fikiria nchi ya Kiafrika iweke Raisi wa nchi bila ya uchaguzi halafu Raisi awekwaye kama alivyofanya May akatae kuitisha Uchaguzi watu wangeita ICC, lkn Mzungu kwa kuwa ni mnafiki na ametumia miaka zaidi ya 100 kumbrain wash Mwafrika kwamba yeye ni superior being basi Mwafrika huamini chochote afanyacho Mzungu!

Lkn ukweli ni ukwamba chaguzi zote Ulaya na USA huibiwa na Wananchi kamwe hawaamui nani awe Raisi!
Sasa mwaka huu D.Trump anaianika live system ya kimafia ya kizungu na USA hapatatosha kwa maana Wazungu wameshachoka na wanaitaka nchi yao iliyoharibiwa na akina Obama, Clinton &Co.!
Hahahaha
 
Uingereza wana system yao ya ku transfer power na iko kikatiba. Ndo maana hukuona wananchi wameingia mtaani kupinga uteuzi wa Theresa May. Na wanaamini katika kushindwa, ndo maana David Cameron akajiuzuru.
 
Are you trying to justify the Rigging ...................!!

Waziri Mkuu wa Wingereza hachaguliwi na Watu anachuguliwa na Bunge!! Chama chenye viti vingi vinampendekeza ... !!
 
Nuilijua tu mtakuja kumtetea Mzungu, vyovyote vile lkn ukweli unabakia kuwa huyo Bibi May hajachaguliwa na Mwananchi yoyote yule wa Uingereza bali amesimikwa na hiyo siyo Demokrasia kwani siyo chaguo la watu, kwani hata kama ikitokea kama ilivyotokea huko Uingereza basi Waziri Mkuu mpya huwa ni wa mpito na hupaswa kuitisha uchaguzi haraka iwezekanavyo lkn T.May amekataa kuitisha uchaguzi hivyo ataongoza hivyo mpaka mwisho ingawaje hajachaguliwa!

Kama ni swala la Katiba hata Nkuruzinza pia Katiba inampa uwezo wa kubadilisha Katiba kwa nini Wazungu wanamuwekea vikwazo?
 
Mie Trump nampenda tu katika kampeni zake badala ya kuongelea sera zake, amekomalia kumshambulia Bwana na Bibi Clintion hahahahahahahah.
 
Are you trying to justify the Rigging ...................!!

Waziri Mkuu wa Wingereza hachaguliwi na Watu anachuguliwa na Bunge!! Chama chenye viti vingi vinampendekeza ... !!

Lakini amekataa kuitisha Uchaguzi, kwani anatakiwa akisha kaa baada muda mfupi kuitisha uchaguzi Mkuu, lkn amekataa!
 
Are you trying to justify the Rigging ...................!!

Waziri Mkuu wa Wingereza hachaguliwi na Watu anachuguliwa na Bunge!! Chama chenye viti vingi vinampendekeza ... !!

Ni wapi nime justify rigging? Kusema Mzungu anaiba kura ndiyo kujustify rigging? Na hapo ndipo tatizo lilipo akili zenu mmeshikiwa na Wazungu kwa kuwa Wazungu wanaiba kura haimanishi kwamba kila mtu anaiba, ni wao ndiyo waibaji kura wakubwa lkn kuna sehemu nyingi Dunia hii ambao kuna free and fair elections!
 
Trump bwana uelewa wa mambo uko chini sana..! Anafanya cheap politics mno wamarekani ukikosa uelewa wa mambo ya kiusalama kwa nchi yao hufai kuwa rais.
 
Sasa mbona hatujasikia waingereza wakilalamika au wewe ni muingereza.... Acha kufaninisha chaguzi za wenzetu na mambo ya kijinga ya wakina JECHA NA YULE MZEE MPARE
 
Trump bwana uelewa wa mambo uko chini sana..! Anafanya cheap politics mno wamarekani ukikosa uelewa wa mambo ya kiusalama kwa nchi yao hufai kuwa rais.

Wewe ndiyo una uelewa wa juu kuliko Mamilioni wa Wamarekani wanamsupport? Kama angekuwa na uelewa mdogo ni kwa nini ana support base kubwa tena siyo low class uneducated Americans, bali middle class highly educated Americans wanamsupport sasa wewe ni nani hata uhoji? Hivi wewe unaweza hata kuqualify kuwa lower middle class USA mpaka uhoji uelewa wa middle na upper middle wanaomsupport Trump
 
Sasa mbona hatujasikia waingereza wakilalamika au wewe ni muingereza.... Acha kufaninisha chaguzi za wenzetu na mambo ya kijinga ya wakina JECHA NA YULE MZEE MPARE

Ni nani amekwambia kwamba Waingereza hawalalamiki? Tatizo lako akili zako zimeshikwa na Mzungu na huwezi kuona chochote nje ya Mzungu anachokwambia, Wazungu wengi sana tu wanaprotest corrupt system yao na ndiyo maana D:Trumo anasupport base kubwa, hata Ulaya kuna Wazungu wengi hawataki tena main stream political parties!
 
Uingereza wana system yao ya ku transfer power na iko kikatiba. Ndo maana hukuona wananchi wameingia mtaani kupinga uteuzi wa Theresa May. Na wanaamini katika kushindwa, ndo maana David Cameron akajiuzuru.
Hii system kwao inawafaa sana. Wanajitambua pale wanaposhindwa au hawatakiwi wapo tayari kujiuzulu.

Wasingekuwa na hii system ingewa gharimu sana. Mfano, UK uchaguzi mkuu ulifanyika 2015 ambao Cameron alishinda na kama hawangekuwa na power transfer ndani ya mwaka mmoja wangekuwa na uchaguzi mkuu mwingine ambao ungewagharimu mabilioni ya pesa kutoka na Cameron ku resign.
 
Lakini haibadilishi ukweli kwamba huyo Tereza May hajachaguliwa na Wananchi wa Uingereza, hivyo siyo Kiongozi wa kidemokrasia kwa maana halisi ya neno!
 
Huyu Trumph hana tofauti na Gambo, wote wanatumia kuropoka ili kupata madaraka, ya uingereza yanamuhusu nini?! Aseme atachowafanyia America aache mambo ya kuingilia maisha ya wengine.
 
Back
Top Bottom