tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 21,847
- 18,254
Mchezo wa kukataa mchele kutoka Marekani ni zaidi ya mchezo maarufu wa kombolela unaochezwa na watoto. Mchezo wa kitoto haukeshi. Sote tunafahamu kuwa msaada ni kitu kinachotolewa kwa hisani (goodwill) bila mpokeaji kuhitaji kumpa masharti mtoaji. Taarifa za Bashe (Waziri wa Kilimo) kuukataa msaada wa mchele wenye virutubisho zimepokelewa kwa mshtuko na watanzania wazalendo wanaofahamu madhara ya kukataa msaada kutoka Marekani.
Na madhara haya yanaweza kuwa makubwa pale Bashe alipoonesha wasiwasi kuwa huenda mchele huu umetiwa sumu au kuwachanganyia homoni za kishoga kwa lengo la kuwadhuru watanzania. Bashe amesema haya kabla ya kufanya uchunguzi wa kina (food analysis) kuhusu chakula kilicholetwa kama kimebeba sumu au homoni za kishoga.
Kibaya zaidi, kabla vumbi hili halijatulia, shirika la viwango la Taifa (TBS) limetoa taarifa sahihi kuwa mchele huu wameufanyia uchunguzi na kugundua kuwa unakidhi vigezo vya kuliwa na binadamu na uingizaji wake hapa nchini umefuata taratibu zote zinazotakiwa.
Hapa tayari tumejenga ugomvi na Marekani. Tukumbuke kuwa Marekani haina rafiki wa kudumu na wakiamua kukushughulikia hawakosi sababu. Tazama jinsi walivyokuwa na urafiki na Osama lakini baadaye wakatofautiana na kumshughulikia hadi kumuua.
Pia tusijitoe ufahamu jinsi Marekani alivyotafuta sababu za kuingia Iraki na hatimaye kumuua Sadam Hussein kwa kisingizio ambacho hakikuwepo. Sembuse Tanzania ambayo imeonyesha dharau ya waziwazi na kuituhumu Marekani kuwa imewatilia sumu na homoni za kishoga kwenye chakula.
Hivi huyu mtu anajua gharama za vita kutoka nchi yenye vifaa vya kisasa na mifumo mizuri ya kupigana? Ikitokea Marekani wakakinukisha na Tanzania. Je, sisi raia tutakimbilia wapi?
Tunapaswa kufahamu kuwa nchi zinaishi kwa kutegemeana. Hakuna nchi iliyojitosheleza kwa kila kitu. Hata Marekani kuna wakati wanahitaji misaada kutoka China, Japan, Uingereza, Urusi na nchi nyingine. Itakuwa Tanzania, nchi hohehahe isiyokuwa na mbele wala nyuma!
Sisi tunategemea karibu kila kitu kutoka Ulaya na Marekani. Chanjo na dawa zote za binadamu zinatoka Marekani. Mfano mzuri ni chanjo ya COVID-19. Chanjo hii kwa kiasi kikubwa imetoka Marekani na bado tunayo dozi ya kutosha inayoendelea kutolewa kwa watanzania bure. ARVs zinazotolewa bure kwa wagonjwa wa UKIMWI zinatoka Marekani. Hivi Marekani leo hii wakigoma kutoa ARVs wagonjwa wetu si watakufa? Nani ana uwezo wa kugharamia dawa hizi? Sio serikali wala wananchi wanaoweza kugharamia dawa hizi.
Sasa huyu Bashe anayetaka kutugombanisha na Marekani anataka watu wetu wafe kwa kukosa dawa au anataka nini hasa? Ikiwa dawa na chanjo zote hizi tunazitegemea kutoka kwa wazungu, je wangekuwa na nia ya kutuua nani angebaki salama? Chanjo zote ambazo watoto wanachanjwa tangu wakiwa wadogo zingekuwa na madhara si kila mtanzania angekuwa zombie? Kungekuwa na mtanzania hata mmoja mwenye akili timamu? Acheni kutafuta matatizo na wazungu huku ukijua bado huna uwezo wa kusimama mwenyewe.
Kana kwamba hili halitoshi, bado 60% ya bajeti yetu inategema michango na mikopo kutoka kwa wahisani. Je, wahisani hawa wakigoma kutuchangia kwenye bajeti tutajiendeshaje? Watu wengine wanajitoa ufahamu na kudai eti tunazo rasilimali za kutosha kujiendesha wenyewe. Rasilimali hizi tunazo tangu dunia hii ilipoumbwa lakini hatuna uwezo wa kuzichakata na kuzitumia. Mambo madogo kama ujenzi wa barabara na reli tunawatumia wazungu na wachina. Tunashindwa kutengeneza vitu vidogo kama vijiti vya meno na sindano. Huo uwezo wa kuchimba madini na kuchakata rasilimali nyingine tulizo nazo tutaupata wapi ikiwa tunashindwa kufanya mambo madogo kama haya?
Kama tuna jeuri ya kukataa msaada wa chakula, basi tusiishie hapo tu. Tukatae pia michango ya bajeti kutoka kwa wahisani na tukome kukopa mikopo ya maendeleo kutoka benki za wazungu (WB, IMF, etc). Ikiwa hatuwezi haya, tukae chini tutulize matako tuache chokochoko za kijinga wakati bado hatuna uwezo wa kusimama wenyewe kama nchi inayojitegemea.
Nawasilisha.