Bora Farao kuliko Viongozi hawa Wa Afrika

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,214
3,587
Afrika imekwama siyo kwasababu ya ujinga, sayansi na teknolojia duni wala kukosa rasilimali (watu, muda, malighafi nk) bali kwasababu viongozi wake (kuanzia kizazi cha pili cha uongozi) ni makahaba-wa-kisiasa wa wazungu ambao wanapandikizwa kwenye uongozi kwa mbinu chafu za chaguzi na mifumo mibovu ya kile wanachokiita demokrasia.

Hata kiongozi jahili Firauni wa 40 wa Misri alikuwa na dira ya kulijenga taifa lake ambalo lilikuwa la pili nyuma ya Israel ktk sura ya dunia (hata Urumi ilikuwa bado); akaajiri watumwa toka taifa kubwa duniani na Mbinguni lililonasibiwa kama taifa la MUNGU lililokuwa na rasilimaliwatu bora duniani kwa akili na mitulinga.

Kwahiyo jahili Firauni wa 40 (kiongozi wa kiarabu wa kiafrika kabisaaa...) akaweza kuajiri (kama watumwa) raia wa MUNGU (raia wa Mbinguni) kumjengea mapiramidi. Duniani hadi Dahari hakuna kiongozi wa taifa ataweza kuvunja rekodi ya Firauni.

Leo Misri inaishi kwa fedha za utalii wa mapiramidi aliyojenga jahili Firauni miaka 3000 BC, huyu alikuwa ni kiongozi wa kawaida Mwafrika (au hata duniani) kulinganisha na hawa wa leo kweli!?

Jahili Firauni alikuwa na akili ya juu hata kumpa hifadhi mtoto Yesu aliyetaka kuuawa na kabila lake mwenyewe Wayahudi, yeye Firauni (mtu-baki) akawa na akili ya kumpa hifadhi ya kisiasa ili asigundulike kwenye hesabu ya sensa.

Jahili Firauni akamuajiri (akamteua) Waziri Mkuu Myahudi-mfungwa ili kuijenga Misri. Jahili Firauni alisaka talents (vipawa) hadi ndani ya jela kabisaaa... na kufanya teuzi.

Jahili Firauni alimlea, akamkuza, akamsomesha, Muebrania Musa ambaye akaja baadaye kupora nyara za taifa la Misri kama fidia kwa Waebrania wenzake waliokuwa wanadai mishahara, posho na pensheni ambazo ktk dhana na mfumo wa kazi za kitumwa tangu uumbaji huwa hazipo kwenye skimu ya malipo ya kazi; zaidi ya chakula tu.

Yokebedi (Muebrania aliyezaliwa na Mlawi) mamake Musa aliolewa na mtoto wa kakake, hivyo Amram akamuoa Yokebedi shangazi yake na kumzaa Musa, hivyo Amram babake Musa ni binamu yake Musa pia. Wakati Musa anazaliwa tayari Miriam na Haruni waliishazaliwa kwa jinsi hiyo.

Jahili Firauni aliwalisha raia wake na wageni (wahamiaji ktk nchi) yaani Waebrania na kuwatumia kujenga Misri kwa miaka 430.

Afrika ishirikiane na Waarabu badala ya Wazungu (japo Waarabu nao waliwauza Waafrika kama watumwa).

Mwarabu na Mwafrika ni ndugu, Mwafrika na Mzungu siyo ndugu wala Mwarabu na Mzungu siyo ndugu. Misri ni mtoto wa Hamu aliyewazaa pia Kushi, Puti na Kanaan. Hamu ni mmoja wa watoto wa Nuhu wakiwemo Shem na Japhet. Hivyo Mwarabu na Mwafrika ni ndugu.

Viongozi vibaraka hawa wanastahili wawapo kwenye kikao cha AU pale washushiwe bomu wote 54 ili Afrika ianze upya. MUNGU alipowachoka Wafalme (Marais) 450 wa Baali kama hawa wa Afrika wanaomtumikia Baali Mzungu, aliruhusu Nabii Eliya akawachinja wote 450.

Dunia ina nchi zinazotambuliwa na UN 193 ukiachilia Kosovo na Vatican ambao siyo wanachama wa UN, hivyo basi, kama Nabii Eliya angelikuwepo leo, angelihitaji sayari ya dunia ziwepo kwa idadi ya 2.3 ili kupata Wafalme wa Baali 450 wa kuchinja ili mfumo mpya uanze upya.

Rai yangu:
Afrika itafute ushirika na Mwarabu siyo na Mzungu. Ushirika unaojengwa hivi sasa baina ya Urusi, Uchina, India na Brazil (Afrika Kusini naye anavutwa humo) hautoufaidisha Afrika bali unalenga kuanzisha aina mpya ya mkutano kama ule wa Berlin wa kuligawa upya bara la Afrika baina yao na Wazungu.

Wazungu wameishawastukia Waarabu kuwa ni wajanja wanaotafuta kuweka mipango kamambe ya karne 1 kuitawala dunia, tayari wametawala US (Obama) kwa utambulisho wa dini yao ya Uislamu, Mhindi naye anatawala Uingereza hivi sasa kwa utambulisho wa dini yao ya Uhindu. Haya hayakufikiriwa na Wazungu kama yangeweza kuwakuta.

Hivi leo sehemu inayomvutia Mzungu kutalii duniani licha ya tahadhari za kiusalama (ughaidi) ni Uarabuni, kufuatia kiwango cha juu cha ustaraabu wa kisasa.

Wazungu ili kujinasua kwenye mipango makini ya Waarabu, nao wanajifua kuondoa kile kinachoitwa "Oil Age" ambayo ndiyo wanadhani ni jeuri ya Waarabu; ili walete mbadala wa mafuta ambao huo mbadala utatoka kwao wao Wazungu na kuifanya dunia kuwategemea.

Wote hao Wazungu, Waarabu, Warusi, Wahindi, Wachina, Wabrazil hawalali wanakesha kushughulisha bongo zao namna gani wataishi (nchi zao zitavyokuwa) zaidi ya karne 1 ijayo.

Sisi viongozi wetu wa Afrika wameendelea kuchagua kuwa mazuzu. Eti wanahubiri Demokrasia badala ya Magufulikrasia. Wanakula mpaka vya wajane na wagane kupitia kodi, ushuru na tozo. Wanakomba hadi masazo ya maskini.

Asilimia kubwa ya Watalii wa kizungu hawaji kuona wanyama (maana wanao kwao pia) bali Watu weusi wanaoendelea kuishi zama za kwanza za mawe wakiwa na elimu ya sasa ya kizungu vichwani mwao.

Mabaali hawa wa Afrika wanakusanya kwa ziada, wanakula, wanavembewa, wanatapika na kurudishia kupitia kodi na tozo kwenye mishahara ya vibarua wao waliowaajiri kwenye vitegauchumi vyao walivyowekeza kupitia state capture.

Wamekwama kwenye ulinzi mkali wa maisha yao, mali zao na ndugu zao wa damu badala ya ulinzi wa Afrika na rasilimali zake.

Wao na vizazi vyao hawataki nafasi za ajira bali nafasi za teuzi nono tu ambazo hizi hazinaga umri wa kustaafu. Wamefarakana na Meritocracy na hawataki kabisa Hakaindecracy (Hichilemacracy)

Bola Tinubu mojawapo ya mbinu chafu na ovu za kushinda uchaguzi alizotumia ni kusambaza magreda usiku mnene chini ya ulinzi mkali wa kikosi cha Navy cha jeshi la Nigeria kubomoa madaraja na kuchimbua barabara za lami zilizojengwa kwa ela za mikopo (ambayo haijamaliziwa kulipwa) ili tu magari ya Tume ya Uchaguzi yashindwe kusambaza vifaa vya uchaguzi kwenye ngome za wapinzani.

Mabaali hawa wa Afrika wana mamlaka makubwa yanayotambuka mipaka ya mihimili na kujinasib kama munguvivuli (kumbe ni Baali 100%), bora jahili Firauni kujinasib kama pacha-wa-mungu lakini aliipenda nchi yake na kuiachia urithi wa Mapiramidi yanayoilisha Misri tangu 3000 BC hadi Dahari. Misri taifa kubwa leo, ndoto hiyo ya ukubwa wake iliatamiwa na jahili Firauni 3000 BC.

Waarabu wamewaajiri Wazungu, Wachina na Wahindi wengi Uarabuni kama Jahili Firauni alivyowaajiri Waisraeli. Waarabu baada ya kutengenezewa migogoro na vita na Wazungu, nao wamegundua mbinu na fursa ndani ya vita hizo kwa kuwajazia Wazungu wakimbizi wa Kiarabu na wamepewa ela za mafuta za kumiliki vitegauchumi vikubwa Ulaya na wamepewa amri ya kuzaliana hovyo kama utitiri na kuoa hovyo kama beberu la mbuzi ili baada ya karne 1 Ulaya itakuwa na Waarabu wengi kuliko Wazungu na kujipatia akidi ya kutengeneza mfumo wa kufanya maamuzi ikiwemo kujipatia idadi kubwa ya kura kwenye chaguzi na kutawala Ulaya.

Tena wanapandikiza mimba za mapacha watupu ili wengine walelewe na serikali za Wazungu hao hao. Mbinu hii imewasaidia sana Waarabu kuwadhibiti Wazayoni (Waisraeli) ambao ni 9.4 ml tu kati ya Waarabu 411 ml walioko Uarabuni na Waarabu-wahamiaji 13 ml.

Hata Wazayoni nao walisambaa duniani na matajiri wakubwa wa duniani ni Wayahudi. Asilimia takriban 75 ya Washindi wa tuzo ya Nobel duniani wana vinasaba vya Kiyahudi akiwemo Albert Einstein ambaye ni wa pili duniani kwa IQ kubwa ya 160 nyuma ya William James Sidis (Mmarekani) mwenye IQ kati ya 250 - 300. Huyu alibuni lugha mpya akaiandikia kitabu akiwa na umri wa miaka 8.

Baadhi ya Hesabu anazoringia Mzungu leo zimebuniwa na Waarabu mfano:-

1. Simultaneous Equations zilitumiwa na Wababeli (Wairaq) 1800 BC.

2. Geometry iligunduliwa na Babeli (Iraq) 3000 BC. Maghorofa yote duniani hata vyombo vya usafiri vimejengwa kwenye kanuni za Geometry.

3. Algebra iligunduliwa karne ya 9 na Al-jabri na Muhammad Bin Musa a.k.a Kwarizmi.

Afrika hii ya wahenga wa rika zifuatazo itaponaje?

1. Paul Biya 90.
2. Yoweri Museveni 78.
3. Bola Tinubu 70.
4. Cyril Ramaphosa 70.
5. Emmerson Mnangagwa 80.
6. Denis Sassou Nguesso 79.
7. Hage Geingob 81.
8. Jasusi Salva Kiir Mayardit 71.
9. Isaias Afwerki 77.
10. Ismail Omar Guelleh 75.
11. Sahle-Work Zewde 73.
12. Tom Thabane 83.
13. Teodoro Obiang Nguema Mbasogo 80.
14. Abdelmadjid Teboune 78.
15. Brahim Ghali 73.

Musa alikomboa Waebrania toka utumwani Misri katika umri mkubwa wa miaka 80.

NB.
Mishahara ya viongozi wa Afrika inatisha. Mfano, Mshahara wa Mfalme Mohammed VI wa Morocco ni mkubwa kuliko mshahara wa Joe Biden ambaye nchi yake US inamiliki 14% ya GDP ya dunia nzima. Mfalme Mohammed VI kwa mujibu wa jarida la Forbes mwaka 2015 mshahara wake ulikuwa USD 5.7 bl.

Mshahara wa rais wa US kwa miongo mitatu mfululizo umegota kwenye USD 200K kwa mwaka.

Ufalme wa Eswatini unaendelea na mjadala mkali kitaifa wa kuondoa mfumo wa Ufalme kwa sababu ni gharama kubwa kwa uchumi wa nchi.

Afrika inaliwa kulia na Mzungu, kushoto na Mchina, katikati na viongozi wake yenyewe.

Ili ipone, tuanze na mapinduzi ya viongozi ndipo mapinduzi ya uchumi yafuaye. Kwa sasa mapinduzi ya uchumi hayazai matunda kwa sababu yanahujumiwa kwa njia ya mapato yake kuvujishwa na miunguvivuli hawa. Mchawi wa Afrika ni viongozi wake.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Ila hata hao waarabu walioendelea ni hao Yemeni na Siria? Mbono waarabu wanakimbilia Ulaya na Marekani? Hivi mleta mada ukiulizaw yuor dream country of ua children utasema Uarabini kweli au Marekani au Ulaya? Halafu hata technologia kuchimba maguta ni makampuni ya Ulaya na US? Hivi unajuwa Kuwaiti ni 40% ya wananchi wanajua kusoma na kuandika? Wanasema ukienda porinitafuta simba awe rafiki yako na wala sii swala! ULAYA NA MAREKANI ni simba!
 
Ila hata hao waarabu walioendelea ni hao Yemeni na Siria? Mbono waarabu wanakimbilia Ulaya na Marekani? Hivi mleta mada ukiulizaw yuor dream country of ua children utasema Uarabini kweli au Marekani au Ulaya? Halafu hata technologia kuchimba maguta ni makampuni ya Ulaya na US? Hivi unajuwa Kuwaiti ni 40% ya wananchi wanajua kusoma na kuandika? Wanasema ukienda porinitafuta simba awe rafiki yako na wala sii swala! ULAYA NA MAREKANI ni simba!
Yawezekana makala ni ndefu sana kwamba wasomaji wanapoteza muktadha njiani na kufikia hitimisho lisilo.

Asma Fawaz al-Assad mke wa Bashar al-Assad amezaliwa na kukulia London, kilichompeleka Syria ni ndoa tu.

Suha Arafat mjane wa Yasser Arafat alikuwa na uraia pachatatu wa Palestina, Tunisia na Ufaransa.

Kwanini Wazayoni walisambaa duniani kama Warumi? Ukipata hizo sababu utajuwa kwanini Waafrika hawatakiwi kujikataa kwamba hawawezi na hawataweza hadi Dahari.

Kuhusu idadi kubwa ya watu kuwa nguzo kuu ya uchumi ni hivi:

Wachina hivi sasa wanazalisha binadamu viwandani 30,000 kwa mwezi ili wawasambaze huko duniani na wanajengewa bongo za uwezo wa juu wawapo kwenye incubators viwandani, wale wasioonyesha kuwa ma-genius wanapigwa sindano za kusimamisha moyo na kutupwa mochuari.

Warusi wana programu kabambe ya miaka 20 ya kuzaliana toka 149 ml. Ukubwa wa Urusi ni sawa na kuchukuwa Afrika kuchanganya na Australia (11% ya sayari ya dunia) lkn Nigeria ambayo ni kama kijiji kwa Urusi ina watu 200 ml.

India wanaendelea kuzaliana. Nigeria ni uchumi mkubwa Afrika kwa sababu ya idadi kubwa ya watu.

Mabara kama siyo taifa moja moja hivi leo yanatafuta kujinasua kwenye mikono-fedhuli ya Wazungu. Kenya hiyo tu juzi imerusha kwenye space satellite ya pili ya masuala ya teknolojia, ya kwanza ilikuwa ya masuala ya tafiti za kilimo.

Djibouti ile (hailingani na Tz kwa chochote) lkn imewekeza USD 1 bl kujenga satellite kwa msaada wa Hong Kong.

Sasa mnataka sisi turidhike tu kwamba Mzungu ameshindikana tumuache tu atufanye atakavyo? Baghosha!

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom