APHFTA: Tutasitisha huduma za NHIF kuanzia saa sita usiku, wagonjwa mahututi tutawaongezea saa 48

Bima Tanzania? Nchi ambayo serikali inachota pesa kila sehemu na hatujui huwa zinapelekwa wapi. Watakwambia tunajenga barabara, Siko Report ya CAG ikitoka unaambiwa hiyo barabara imefadhiliwa na Bank ya Dunia.

Unaanza kujiuliza zile pesa zilienda wapi, walisema walijenga barabara, hapo sasa utapata mvi na vipara ukiwa kijana mdogo kabisa kwa kutaka kuwaelewa ccm.

Serikali kazi yao kulazimisha tu, utasikia pokeeni wagonjwa, Hospitali zinapokea na kutoa huduma. Hospitali zikipeleka bill huko NHIF unaanza kusikia ohoo, tunahakiki, mara bill kubwa utadhani huduma walitoa wao.

Mkitaka vitu rahisi wapelekeni wagonjwa wenu wa NHIF wote hospitali za serikali, huko mdaiane wenyewe, mlipe msilipe sawa.

Mkitoa huduma hafifu, mtajuana huko huko na siasa zenu. Pesa mchukue nyie huduma watoe wengine, mkiambiwa mnaleta ujanja ujanja, na mapambio ya Anaupiga mwingi.

Serikali iboreshe huduma hospitali za umma ili na wao viongozi watibiwe huko, ndio nchi itapendeza. lakini hili la class A na class Z, tutashuhudia mengi sana.
 
Serikali imetoa sera mpya za bima, ikaziita maboresho. Madaktari wanaovutana na serikali nao wamekariri, wanatumia neno hilo hilo maboresho! Unapinga maboresho! Basi huna akili kichwani kama unapinga kitu ambacho wewe mwenyewe unakiita maboresho... Waandishi wa Kayumba nao wamemeza, wakakitema, kama kilivyo, vile vile kilivyotangazwa na serikali, maboresho! Watu wasomi, madaktari, waandishi wazima, logic vichwani zero. Hawana sense ya kutumia neno mabadiliko ya sera!
 
Serikali imetoa sera mpya za bima, ikaziita maboresho. Madaktari wanaovutana na serikali nao wamekariri, wanatumia neno hilo hilo maboresho! Unapinga maboresho! Basi huna akili kichwani kama unapinga kitu ambacho wewe mwenyewe unakiita maboresho... Waandishi wa Kayumba nao wamemeza, wakakitema, kama kilivyotangazwa na serikali, maboresho! Watu wasomi, madaktari, waandishi wazima, logic vichwani zero. Hawana sense ya kutumia neno mabadiliko!
Wewe umeongea point
 
Julius akirudi leo hii atashangaa sana jinsi watoto na wajukuu zake walivyobadilika na kuwa mamangimeza zaidi ya alivyokuwa mkoloni!

Watu wanaendekeza tamaa binafsi za kuchuma hata wasipostahili hata kwenye uhai wa binaadam!
 
Serikali imetoa sera mpya za bima, ikaziita maboresho. Madaktari wanaovutana na serikali nao wamekariri, wanatumia neno hilo hilo maboresho! Unapinga maboresho! Basi huna akili kichwani kama unapinga kitu ambacho wewe mwenyewe unakiita maboresho... Waandishi wa Kayumba nao wamemeza, wakakitema, kama kilivyotangazwa na serikali, maboresho! Watu wasomi, madaktari, waandishi wazima, logic vichwani zero. Hawana sense ya kutumia neno mabadiliko!
Hiyo sio sera mkuu..
Ungekuwa Mfatiliaji tu ukajua ni nini..
Hicho ni kitita ambacho huwa kinatoa Mwenendo wa bei za Bidhaa na huduma kwa Hospitali
 
Kazi imeanza
Screenshot_20240301_075940_Gallery.jpg
Screenshot_20240301_075920_Gallery.jpg
Screenshot_20240301_075855_Gallery.jpg
 
CHEAP IS EXPENSIVE.

Ukiona kitu cha bure kimbiaaaa!!!!! Ni moto!!!

Bure is business in disguise! A tiger in the shadows!

Ukiruka na bure unajikuta uko kwenye MIONZI YA KANSA, TIBA YA BEI NAFUU!

A psychological game to entrap the masses in a medical net!

Kuja huku, kuna chanjo ya bureee!!! 🤣

Au njoo na Bima ya Afya, utahudumiwa BUREEE!
Sio Bure Wanakatwa mshahara wao kila mwezi..
UKiangalia makato mwaka inaweza kufika laki sita mpaka laki saba...
Kwa sio mtu anakatwa laki sita kwa Mwaka ili atibiwe
 

Imeelezwa vituo vyote Binafsi vya Afya vitasitisha kutoa huduma kwa Wagonjwa wapya wanaotumia Kadi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)kuanzia Usiku wa Saa Sita kuamkia Machi 1, 2024 huku wale ambao watakuwa katika Uangalizi Maalum (ICU) wakiongezewa muda wa Saa 48 kuendelea kupata huduma.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Vyama vya Watoa Huduma Binafsi za Afya Tanzania (#APHFTA), Dkt. Egina Makwabe ambaye amesisitiza maamuzi hayo yameafikiwa katika kikao chao Bodi ya APHFTA kilichofanyika Februari 29, 2024.

Amesema “Watakaohitaji huduma watalazimika kulipa fedha Taslim kuongezea pale ambapo gharama za kadi zao za bima zinapoishia, wale wa ICU baada ya muda huo tutafanya mchakato wa kuwahamishia Hospitali za Serikali.”

Uamuzi huo umefikiwa baada ya NHIF kufanya maboresho ya Kitita cha Mafao kwa Wanachama wake na kutangaza utekelezaji wake utaanza rasmi Machi Mosi.

Pia soma - Wenye Hospitali binafsi wakataa kuwahudumia wateja wa NHIF kutokana na vifurushi vipya
mzee MAGU angekuwepo huyu jamaa 2ngemuokota kwenye kiroba!!
 
Back
Top Bottom