DOKEZO Wenye Hospitali binafsi wakataa kuwahudumia wateja wa NHIF kutokana na vifurushi vipya

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Umoja wa Watoa Huduma Sekta ya Binafsi APHTA, Mashirika ya Dini (CSSC), na Bakwata wanapenda kutaarifu umma kuwa mazungumzo yaliyokuwa yakifanyika baina ya umoja huo na Wizara ya Afya. Kamati ya Waziri na NHIF yameshindwa kupata muafaka katika suala zima la kitita cha bei mpya zilizopendekezwa na Wizara kupitia kamati iliyoundwa na Waziri.

Kwa kuwa Wizara pamoja na NHIF wameamua kudharau maagizo yaliyotolewa na Bunge la Jamhuri ya Muungano ya namna bora ya kumaliza suala hilo na kuamua kutangaza kitita hicho bila maridhiano, basi umma unatangaziwa kuwa vituo binafsi vya huduma za afya vitashindwa kutoa huduma hizo kwa wanachama wa Mfuko huo kuanzia tarehe 1 mwezi Machi 2024.

Ili kuepuka usumbufu, wanachama wa NHIF wanaombwa kuwasiliana na Mfuko wapi wataweza kupata huduma hizo.

Suala la hili limekuja baada ya Wizara ya Afya kutoa barua ya kuendelea na vifurushi vyao kwenye barua iliyoandikwa 27/02/2024.

Barua ilisema "Hivyo, Mfuko unapenda kukufahamisha kuwa utatumia Kitita cha Mafao cha Mwaka 2023 kuanzia tarehe 01.03.2024. Vilevile, unafamishwa kuwa, orodha ya huduma na bei katika Kitita hicho zinapatikana katika ofisi zote za Mfuko, tovuti ya Mfuko na kupitia mfumo wa Service Porta/. Aidha, Mfuko utaendelea kupokea maoni, ushauri na mapendekezo mbalimbali yenye lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma bora za matibabu kwa wanufaika wake na kuendelea kuishauri Serikali ipasavyo."
WhatsApp Image 2024-02-28 at 10.51.50.jpeg

Screenshot 2024-02-28 at 11-18-38 BAKWATA letter-1.pdf.png



Pia soma - APHFTA: Tutasitisha huduma za NHIF kuanzia saa sita usiku, wagonjwa mahututi tutawaongezea saa 48
 
Wakati serikali kupitia wizara ya afya leo ikitangaza maboresho kwenye kitita kwa watumiaji wengi wa NHIF na kusema maboresho haya yataanza hivi karibu.

Kwa upande mwingine sekta binafsi ambao ni wamiliki wakubwa wa hospitali binafsi na ambazo zina hudumia watanzania wengi wamesema wameshindwa kufikia muafaka na serikali na hivyo watanzania wengi watakosa huduma kwenye hospitali binafsi na itabidi wawaulize NHIF cha kufanya kwani wao hawataweza kuwa hudumia!

Hivi serikali kupitia Ummy Mwalimu kwanini wanafanya mzaha na afya za watanzania?
 

Attachments

  • IMG_1934.jpeg
    IMG_1934.jpeg
    324.9 KB · Views: 7
  • IMG_1935.jpeg
    IMG_1935.jpeg
    388 KB · Views: 5
  • IMG_1936.jpeg
    IMG_1936.jpeg
    335.8 KB · Views: 4
  • IMG_1937.jpeg
    IMG_1937.jpeg
    232.2 KB · Views: 5
  • IMG_1933.jpeg
    IMG_1933.jpeg
    317.3 KB · Views: 6
Nawaunga Mkono Mia fill 100..
Huwezi kuboresha kitita na ukaacha Kuboresha maslahi ya Watoa Huduma pamoja na Bidhaa husika na Baada ya kuambiwa bado unashupaza shingo..

Amoxyline iliyokuwa inalipwa kwa Bima miaka 10 iliyopita sh 80 kwa kidonge still bado baada ya miaka 10 bei ni hiyo.hiyo..Bila kuangalia Soko la Bidhaa la sasa unapanga bei bila huruma ya watu wenye Hospitali ambao wao hawaletewi dawa na MSD..
as one among the interested personel nasema wako sahihi na hatutapokea Mtu mwenye Bima Yoyote. Mpaka pale serikali itakapo thamini Mfumuko wa bei na maslahi ya pande mbili
 
Nawaunga Mkono Mia fill 100..
Huwezi kuboresha kitita na ukaacha Kuboresha maslahi ya Watoa Huduma pamoja na Bidhaa husika na Baada ya kuambiwa bado unashupaza shingo....
Hii ndio maana ya mfuko kujiendesha kitathmini na tafiti ,kuongeza pale inapohitajika ,sio kila kitu kinapanda bei kadri siku zinavyokwenda vingine bei inashuka kutokana na upatikanaji wake, inawezekana upatikanaji wa amoxilin umeongezeka kuliko ilivyokuwa awali hakuna haya ya kuongeza bei na hii ni lengo zuri la kupunguzia mzigo wanachama wake, lakini ni mfuko huuhuu ambao umekuwa ukiwezesha watoa huduma kwa fedha(loan) kuboresha miundombinu pale inapohitajika ili kuviongezea uwezo ,mfuko haugemei upande mmoja unajali wadau wake wote
 
Maboresho haya yanasaidia huduma za kibingwa na bingwa bobezi kama matibabu ya moyo, saratani, figo kupatikana kwenye ngazi za Kanda pia na sio lazima mwanachama aende mpaka hosp za ngazi taifa.
 
Nadhani tungeangalia Kwanza Manufaa ya ya Maboresho haya kabla ya kuingia kwenye lawama na Migogoro.

Kwa Mfano Maboresho haya Wanachama wanaotumia dawa za pressure na sukari sasa wanaweza kupata dawa ngazi za chini
 
Back
Top Bottom