Nakerwa na dhana potofu ya hawa ndugu zetu! Nakumbuka miaka kama 15 iliyopita kuna rafiki yangu ambaye ni mwislam aliulizwa na kakake kuwa "kwanini umefeli kwa mara ya pili tena mdogo wangu?" Yaani huwezi amini yule rafiki alimjibu kakake (mbele yangu) kuwa "kaka, unajua kule balaza la mitihani sisi wenye majini ya kiislam ngumu sana kufaulu, kwa wenzetu wakristu hata kama hajafanya vizuri inakuwa rahisi kuwekewa mark nzuri na kufaulu" Dah nilipata hasira sana kwa majibu majibu ya kibaguzi ya rafiki yangu na dhana potofu aliyokuwa nayo, kabla sikujua kama alikuwa mpumbavu kiasi hicho. Sasa baada ya kuona heading ya hilo gazetu hapo imekunikumbusha huyo rafiki yangu. Lakini wapo wengi pia ambao wanaamini hivyo, lakini mbona wapo waislam ambao wanafanya vizuri! Nadhani hao ambao inakuwa ngumu kujishughulisha na masoma wanakuwa na dhana mbaya kabisa hiyo. Ni akili mbaya sana hiyo. Yaani nilitamani nimpige kibao huyo rafiki yangu.
huyo dogo kama ndo dogo langu nalikata ngwala,,,jinga kabisa hilo,,,,yaani naudhiwa na wenye mawazo fake kama hawa,,,,,,