Ni kwanini sasa hivi Wazanzibari hawataki kuitwa Wazanzibari?

Lituye

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
1,862
5,680
Rais Samia, Waziri Mabarawa na katibu mkuu wao ktk wizara anayo ongoza Mbarawa ni kutoka Zanzibar na ndio waliouza bandari za Tanganyika wakaacha kuuza za Zanzibar.

Nyakati zote Wazanzibar wamekuwa wakijiita na kujivunia Uzanzibari wao kama taifa. WazanzibarI wanacho kitambulisho cha ukaazi cha Uzanzibari na Watanganyika tuna kitambulisho cha Tanzania. Wazanzibar wana serikali yao, bunge, Katiba na ukiwauliza Zanzibar ni nchi au sehemu ya Tanzania wanakwambia Zanzibar ni nchi yenye mipaka yake.

Wazanzibar baada ya kuuza bandari za Tanganyika wanataka wasiitwe wazanzibar kwa nini? Na tena kuna wajinga wachache wanawaunga mkono eti kuwaita Wazanzibari ni kuwabagua. Mbona miaka yote wazanzibar wamekuwa wakijiita hivyo na serikali yao ipo? Huu upendo wa ghafla kujiita Watanzania umeanza lini? Au mnafikiri Watanganyika ni mazuzu?

Huwezi ukawa na taifa moja katika nchi mbili ni kichaa peke yake anayeweza kuamini hivyo kama Magufuli anavyo sema. Mimi sijawahi amini na sitaamini kuwa kuna Wazanzibari ni Watanzania. Huwezi ukaunganisha nchi mbili halafu upate mataifa mawili.

Na ukiwa na akili timamu huwezi kuamini kuwa kuna raia wa Tanzania. Urai wa Tanzania ni wa kufikirika tuu bali kuna raia halali wa Tanganyika na wa Zanzibar. Afadhari kidogo Watanganyika wanaweza kujikomba kizuzu kuwa raia wa Tanzania kwa kulipoteza taifa lao kijinga jinga tuu lakini hiyo nchi wanayodai kuungana nayo ni ya kufikirika haijawahi kuunga na Tanganyika.
 
Ni ukweli ambao utandelea kusemwa kuwa Wazanzibari waliuza bandari za Tanganyika lakini wakaziacha za kwao.

Ni ukweli ambao hautaacha kusemwa kuwa kuna hila imefanywa na watu wa Zanzibar dhidi ya Tanganyika kwenye rasilimali zilizopo Tanganyika.

Ni ukweli kuwa kama Muungano huu hautawekwa vizuri ili mipaka ya kila upande iwe sawia, lazima Mungano huu utakuja kuleta uhasama mkubwa baina ya pande hizi mbili ambazo awali zilikuwa katika ukaribu mkubwa japo hazikuwahi kuchanganyika.
 
Ni ukweli ambao utandelea kusemwa kuwa Wazanzibari waliuza bandari za Tanganyika lakini wakaziacha za kwao.

Ni ukweli ambao hautaacha kusemwa kuwa kuna hila imefanywa na watu wa Zanzibar dhidi ya Tanganyika kwenye rasilimali zilizopo Tanganyika.

Ni ukweli kuwa kama Muungano huu hautawekwa vizuri ili mipaka ya kila upande iwe sawia, lazima Mungano huu utakuja kuleta uhasama mkubwa baina ya pande hizi mbili ambazo awali zilikuwa katika ukaribu mkubwa japo hazikuwahi kuchanganyika.
Wacheni kopotosha watu Bandari sio suala la muungano by Juma Duni Haji
 
Wengi wanaopiga kelele kujiita wazanzibari ni wale makapuku wanaodanganywa na waarabu wa Oman kuwa umasikini wao unaletwa na muungano.

Akina Bakhressa, SSH, Masauni, Mbarawa n.k wanakula matamu ya muungano, hawawezi kujiita wazanzibari. wamejenga majumba ya kifahari Dar 😁.
 
Kama bandari sio suala la muungano kwa nn mkataba unaohusiana na bandari usainiwe na wazanzibar?
Ni hivi mfumo wa Muungano uliopo umefanya vitu vya Tanganyika vyote kuwa vya muungano hao wazanzibari waliosaini huo mkataba wamesaini kwa jina la jamhuri ya Muungano wa Tanzania sio Tanganyika
 
Hakuna Mzanzibari ameuza ardhi, si ya Tanganyika wala ya Tanzania na hakuna Mzanzibari anakataa kuitwa Mzanzibari, ila inapokuja swala la uraia, Wazanzibari ni Watanzania kama ambavyo 'Watanganyika' ni Watanzania.
Wazanzibar baada ya kuuza bandari za Tanganyika wanataka wasiitwe wazanzibar kwa nini?
Na ukiwa na akili timamu huwezi kuamini kuwa kuna raia wa Tanzania. Urai wa Tanzania ni wa kufikirika tuu bali kuna raia halali wa Tanganyika na wa Zanzibar.
Unaota ndoto za mchana, amka kumekucha.
Afadhari kidogo Watanganyika wanaweza kujikomba kizuzu kuwa raia wa Tanzania kwa kulipoteza taifa lao kijinga jinga tuu lakini hiyo nchi wanayodai kuungana nayo ni ya kufikirika haijawahi kuunga na Tanganyika.
Si haba angalau unajidanganya. Fanya tu maisha yaende. Sasa huu muungano ni kitu gani?


Umejitahidi kutuonesha wewe ni nani, nasi tumekuelewa.
 
Kama ambavyo wewe ni kapuku unayedanganwa na Wazungu kwamba Uafrika wako utakuwa mzuri kwa kuiga uzungu na bado hujajitambua.
Wengi wanaopiga kelele kujiita wazanzibari ni wale makapuku wanaodanganywa na waarabu wa Oman kuwa umasikini wao unaletwa na muungano.
 
Tulia wew kibwetele dawa ikuingie hizi bandari si za wazanzibar mtazinyaa.
Hakuna bandari za Tanganyika zinagawiwa kwa wajomba zenu huko kienyeji hivi mtajutaa.
Kama ni kujuta kwanini msijute nyinyi? Wazanzibari wamepoteza nini?
 
Back
Top Bottom