Amini usiamini, CCM ina jukumu la kutupatia Rais bora mwaka 2015...

Watanzania tuna background mbovu kabisa, siasa na maisha tuliyoishi yametuharibu na hatufai hata kidogo, hapa tukisema chadema hawafai tutapigwa mawe mchana mchana, kuna watu wanalinda kwa gharama yoyote ile chadema iendelee mbele bila sisi wanachama kuona upande wa pili wa shilingi, by the way wewe Rutashubanyuma si mmojawapo wa warundi mliochukua uraia kienyeji hapa tanzania,nimesoma post zako nyingi inaonekana kama huna uzalendo na nchi yetu, hata mambo ya east africa unavyoongea ni kama una maslahi na wakenya.

Sitaki kuongea mengi kwenye post hii kwa sababu imeletwa na wewe,ila nipo busy naandaa post ya kutaka mambo yote ya chadema yawekwe wazi ili tuweze kuwajua,nafanya hivyo kwa sababu najua chadema imetoka kwa watanzania hao hao waliandaliwa na ccm na hakuja kutoka mbinguni,nipe muda kidogo
 
Last edited by a moderator:
Huyu Ruta atakuwa miongoni mwa madiwani waliofukuzwa; nasema maana nimefuatilia mijadala wakati wa uchaguzi alikuwa comrade hasa katika kupigania haki za wananchi tena mtetezi wa kweli; tulipata kila update kutoka arusha na mikutano ya Lema, siku hizi adui namba moja wa LEMA, acha kupotosha umma kama ulipata mlungula kwa kutegemea huruma ya kura za maoni huo ujuha; mimi nitakuwa mpinzani daima hata sasa wakija chadema wakachukua nchi come 2015, nitashangilia for few months then nitawapinga maana wao ndio jicho letu na hapo watakuwa na makosa.

NASEMA RUTA ni miongoni mwa madiwani waliofukuzwa, nina uhakika na nitafuatilia amekuwa mpotoshaji wa demokrasia kisa upepo haupo upande wako
 
Ukitaka kuipima demokrasia ya chadema kwanza tazama wabunge wa kuteuliwa kwa upendeleo. Kwi kwi kwi teh teh teh.

Ukimaliza msome TUNTEMEKE uone madudu yaliyo Ikulu Kivuli (ofisi za chadema). Hapo utapata picha halisi ya chadema.

Rutashubanyuma, nahisi sasa hivi utaambiwa "umenunuliwa". Tatizo kubwa la Watanzania huwa hatuupendi ukweli na kubadilishana mawazo tunakokupenda ni kupakana mafuta tu lakini si kugusia maswala ya msingi.

Nikiyatazama kwa mtazamo chanya uliyoyaainisha hapa na madudu mengine tunayoyasikia kutoka kwa kina TUNTEMEKE, kila mwenye kuupenda ukweli ataona ni bora "zimwi likujualo".
 
Labda wagombea watokee mbinguni!

Sometimes tatizo la khoja hii ni kuwa inavihusu vyama vyote na hainyesh mapungufu ya mgombea ccm kama wakibadilisha mfumo wa kumpata..............na vyama vinginevyo vikabaki vilivyo......
 
Ukitaka kuipima demokrasia ya chadema kwanza tazama wabunge wa kuteuliwa kwa upendeleo. Kwi kwi kwi teh teh teh.

Ukimaliza msome TUNTEMEKE uone madudu yaliyo Ikulu Kivuli (ofisi za chadema). Hapo utapata picha halisi ya chadema.

Rutashubanyuma, nahisi sasa hivi utaambiwa "umenunuliwa". Tatizo kubwa la Watanzania huwa hatuupendi ukweli na kubadilishana mawazo tunakokupenda ni kupakana mafuta tu lakini si kugusia maswala ya msingi.

Nikiyatazama kwa mtazamo chanya uliyoyaainisha hapa na madudu mengine tunayoyasikia kutoka kwa kina TUNTEMEKE, kila mwenye kuupenda ukweli ataona ni bora "zimwi likujualo".

zomba mie ninatetea mifumo ya utawala bora...........naona upinzani wamekalia kuti kavu tu.atayasema nimenunuliwa nitamwabisha na makala yangu ijayo ambayo nitailima ccm vilivyo........hapo ndipo atajua mie sifungamani na upande wowote ule.........
 
Naungana na mtoa mada!

Ni kweli kabisa vyama vya upinzania havina democrasia ndani ya vyama vyao ndio maana CDM walimshambulia sana Zitto na Shabuda kwa kuonyesha nia yao ya kugombea Urais 2015.

Kama mtakumbuka huyu huyu Zito aliwahi kukataliwa na kulazimishwa asigombee Uenyekiti wa Chadema amuachie Mbowe ambae ni Chaguo la Mzee mwenye chama Mtei ili kuendeleza ukanda. Pia hakuna utaratibu mzuri wa kupata Wabunge na hata Wabunge wa viti maalum achilia mbali udiwani.

Kwa mfano kuna watu wameanza kuonesha nia ya kugombea ubunge Arusha kupitia CDM lakini wanapigwa zengwe eti hiyo ni nafasi ya LEMA sasa kweli hawa jamaa wakipewa uongozi wa nchi itakuwaje?

Nionavyo mimi bila kuweka nafasi sawa na haki kwa kila mgombea wa nafasi ktk vyama pinzani wasahau kushika dola kwani ni CCM pekee yenye mfumo mzuri wa kushirikisha wananchi na wanachama wao kupiga kura ya maoni hiyo lazima wapenda haki na usawa wakipe ushindi wa kishindo ccm 2015.
 
Huyu Ruta atakuwa miongoni mwa madiwani waliofukuzwa; nasema maana nimefuatilia mijadala wakati wa uchaguzi alikuwa comrade hasa katika kupigania haki za wananchi tena mtetezi wa kweli; tulipata kila update kutoka arusha na mikutano ya Lema, siku hizi adui namba moja wa LEMA, acha kupotosha umma kama ulipata mlungula kwa kutegemea huruma ya kura za maoni huo ujuha; mimi nitakuwa mpinzani daima hata sasa wakija chadema wakachukua nchi come 2015, nitashangilia for few months then nitawapinga maana wao ndio jicho letu na hapo watakuwa na makosa.

NASEMA RUTA ni miongoni mwa madiwani waliofukuzwa, nina uhakika na nitafuatilia amekuwa mpotoshaji wa demokrasia kisa upepo haupo upande wako
Malunde-Malundi

....kama kitu hujui uliza kuuliza siyo ujinga...... hivi hao madiwani waliofukuzwa kunamwenye upeo nilionao? Wanaweza kuunganisha khoja zangu hizi au unajiroipokea....... kwanza mie siyo chadema na wala sitakwenda huko... mie CCM Daima.... ila nachukia dhuluma za aina yoyte ile na kwa mtu yeyote yule siyo mfungwa wa vyama vya siasa....

Khalafu siyo mfuatiliaji wa nyuzi zangu na ndiyo maana unazungumzia mambo ya mwaka 2005........nina nyuzi nyingi humu jamvini za kuisagia ccm kwa hiyo nitendee haki siyo kunisigina kwa kunitungia uongo.....................lol
 
Last edited by a moderator:
viongozi hawapaswi kutenguliwa na vikao ambavyo havikuwachagua.........kama viongozi wa matatazo basi tuulizwe siye na wala siyo kamati Kuu ya Chadema ambayo hakuna hata mpigakura wetu kule........wa jiji la Arusha..........hiyo ndiyo misingi ya demokrasia.......haiwezekani wakaazi wa nje ya jiji la Arusha watuchagulie nani anafaa kutuongoza huo ni uwakilisha haramu tu................usiutetee............... Filipo

Lakina haudhani kuwa madiwani hao walibanwa na katiba ya chama......wangepataje dhamana ya kuwatumikia wananchi kama si kupitia kwa chama na je wewe ungeshauri wafanyweje? Kama unashindwa ku abide na sheria za chama si kuna kanuni zimewekwa kwa ajili hiyo?
 
Last edited by a moderator:
"Have your say too...unaridhika na demokrasia ndani ya vyama vya siasa hasa hivi vya upinzani hata sasa kuviamini kutupatia Raisi na viongozi wengineo bora bila ya kutushirikisha grassroots?"

Hakuna chama kisichotumia WANANCHI kupata viongozi isipokuwa jinsi wanavyowatumia wewe ndiyo hujui!.

DEMOKRASIA unayoiona ndai ya CCM huijui pia na nasema hukufanya hicho inachoita UPEMBUZI YAKINIFU. Kama kweli ungegundua udikteta tena dhidi ya watu juu ya maamuzi yao ndani ya CCM sina haja kukutajia maana najua unalielewa hili. Ndilo limetufikisha kwenye kuzalisha MIKOA na WILAYA ili kuwabembeleza waathirika wa UDIKTETA huo.

Kifupi nikwambie rafiki yangu kuwa hiyo DEMOKRASIA ndani ya CCM ni DEMOKRASIA ya fisi kuwatawala mbuzi! na ndiyo maana kumekuwepo na kubadirishwa kwa matokeo ya kura za maoni sehemu mbalimbali ndani ya CCM. Wanaopendwa na WANANCHI wanaonekana hawana
magamba ya kweli.

Mkuu Rutashubanyuma,

Pamoja na yote hayo unayoyasema lakini kwa sasa C.C.M. imezeeka tunataka chama kingine chochote kije kitawale mkuu hatupo sisi Urusi tupo Afrika Mashariki hatupo Zimbambwe tupo Tanzania Mkuu tunataka mabadiliko na Maendeleo C.C.M. tangu iundwe sasa yapata miaka 35 hakuna Maendeleo yoyote yale Chama cha C.C.M kimesha pitwa na wakati tungoje chama kingine Tuyavue Mkuu Magamba tuvae People in Power Mkuu kila lilio na Mwanzo halikosi kuwa na mwisho. Waswahili wamesema Ngoma ikivuma sana mwisho hupasuka C.C.M hu ndio mwisho wao imekalia kuti kavu mkuu samahani kama nitakukwaza.

MziziMkavu suala hapa siyo kama ccm imetuchosha au la bali je ccm ikilinganishwa na vyama vya upinzani inamfumo bora wa kutupatia viongozi wanaofaa kwa maana ya demokraasia shirikishi?

Tukishabikia vyama sana tutasahau ya kuwa hata kule Zambia akina chiluba walichukua nchi kwa miaka 20 na baadaye mbona raia haohao walikuja kuwatema?........mambo siyo chama kipi kipo madarakani lakini kina mikakati ipi ya kutupatia viongozi bora.....................hiki ndicho kiini cha mada hii..ukienda nje ya mda michango yako nayo itakwend nje....................na hutatusaidia sana.........
 
Ulichosema ni kwamba CCM inajukumu hilo, hukusema wana nafasi ya kutupatia Rais bora kama ni suala la nafasi kila chama kina nafasi, ila kwasababu CCM imepewa hiyo nafasi miaka mingi na haijaitumia vizuri uwezekano wa kupewa nafasi hiyo tena ni mdogo sana watu tupo tayari ku-take risk kwa chama kingine hata TLP

Ezan.....jukumu hilo wanalo lakini watalitumia? Hilo ndilo swali wanalo kwa sababu ndicho chama komavu na kimeonyesh ania ya kujirekebisha na vyama vinginevyo vimekuwa vikiangalia kwa kuigiza maigizo yao kama ya kikatiba n.k kimuundo n.k...usitegemee chadema pamoja na kujiita chama makini kama kinaumakini ya kuwaondoa wabunge kwenye ngazi za uongozi ndani ya chama....wataendelea akina Mbowe kushika nyadhifa kebekebe yey na wabunge wenzie.............and that is not democracy......
 
Last edited by a moderator:
Ezan sijasem marasis wa ccm waliotangulia walikuwa bora ila sasa wanayo nafasi ya kutupatia raisi bora kama watapanua wigo la demokrasia.......ungelikuwa umenielewa ungelifahamu hao wote waliotangulia walikuwa ni bomu kwa sababu wanachama wa kawaida wa ccm hawakushiriki katika kuchagua kiongozi bora............. Ezan

Rutashubanyuma i see where you are going with this halafu unaji contradict kidogo..,CCM kwa mfumo wao watatoa mgombea bora really? Halafu at the same time wapinzani wameiga mfumo wa CCM.....kwanini Upinzani usitoe mgombea bora? Kwanini unakuwa na haraka ya Mgombea bora toka CCM iliyoshindikana duniani na Mbinguni? Ebu tujadili njia za kumpata mgombea bora wa Upinzani kama una mapenzi kweli na nchi yako.....
 
Last edited by a moderator:
"Have your say too...unaridhika na demokrasia ndani ya vyama vya siasa hasa hivi vya upinzani hata sasa kuviamini kutupatia Raisi na viongozi wengineo bora bila ya kutushirikisha grassroots?"

Hakuna chama kisichotumia WANANCHI kupata viongozi isipokuwa jinsi wanavyowatumia wewe ndiyo hujui!.

DEMOKRASIA unayoiona ndai ya CCM huijui pia na nasema hukufanya hicho inachoita UPEMBUZI YAKINIFU. Kama kweli ungegundua udikteta tena dhidi ya watu juu ya maamuzi yao ndani ya CCM sina haja kukutajia maana najua unalielewa hili. Ndilo limetufikisha kwenye kuzalisha MIKOA na WILAYA ili kuwabembeleza waathirika wa UDIKTETA huo.

Kifupi nikwambie rafiki yangu kuwa hiyo DEMOKRASIA ndani ya CCM ni DEMOKRASIA ya fisi kuwatawala mbuzi! na ndiyo maana kumekuwepo na kubadirishwa kwa matokeo ya kura za maoni sehemu mbalimbali ndani ya CCM. Wanaopendwa na WANANCHI wanaonekana hawana
magamba ya kweli.

Kyaiyembe......tuanza na nafasi ya upatikanaji wa wabunge uchaguzi wa 2010............je tofauti ya ccm na chadema ilikuwa ni nini?..................mwezetu ambaye unajua............
 
Nimevipima vyama vya upinzani kwenye mizania yangu ya upembuzi yakinifu na kubaini bila ya mashaka yoyote yale bado havipo tayari kimfumo kutupatia Raisi bora na hizi ndizo nondo zangu zilizonifikisha hapo..:-

a) Vyama vyote vya upinzani vimeiga mfumo mbovu wa kidemokrasia wa ccm na vinaendeshwa kibabe-kibabe mno na huku wenzao wa ccm kuanzia 2010 walianza kujivua gamba la udikteta pale waliporuhusu wabunge wake wachaguliwe na wananchi moja kwa moja...ingawaje bado wana safari ndefu kwenye hili lakini lazima niwapongeze ccm kwa angalau kujaribu....rushwa na kuingiliwa na ngazi za juu katika maoni ya wananchi ni changamoto ambazo ccm itabidi waendelee kuzitafutia muarobaini wake.

Kwenye hili vyama vya upinzani wapo nyuma na tumeona hata chadema bila ya kupitisha kura ya maoni kwa wapigakura wa Arusha wakitumia kauli za kidikteta kukejeli kura za wanachama wao Arusha pale kamati kuu yao ilipotengua madiwani wakaidi wa Arusha...well, chadema worshippers...that was not democracy at all...it was dictatorship.........face it now before it is too late.....Only the truth will set you free

b) Vyama vyote vya siasa vyenye wabunge Bungeni vimekumbwa na dhoruba kali la wizi na ubadhirifu wa ruzuku ya hazina na hakuna uthibiti wa aina yoyote ile!!!!!

Kwa mtazamo wangu kama wapinzani wameshindwa hata kusimamia kidogo ambacho tumewapa ni kwa upuuzi upi utushawishi kuwakabidhi nchi yote?

Njaa ya viongozi wa upinzani ni kali kulikoni ya viongozi wa ccm ambao pamoja na bandubandu kweli humaliza gogo lakini ccm hawana uchu wa kututafuna kama upinzani walionao.....

c) Mchakato wa katiba mpya umenifungua macho hila na upofu wa wapinzani ambao waliipinga tume kwa vile wao hawajaweka mrija wao ndani yake na kunyonya Hazina baada ya CCM kuwaingiza kingi - au niseme mkenge? - hakuna anayehoji uhalali wa Tume ya kukusanya maoni.

You know the words BUT you miss their meaning!! pole sana; kama upembuzi yakinifu ndio kama huu, then no wonder Tanzania is in the 21st century but her peoples are living like in the old stone age!! for lack of analytical capability of our situation.
 
Hawezi Rais Bora kutoka tena C.C.M. You Forget it. Tunataka Rais atoke sehemu yoyote ile sio tena Rais atoke C.C.M imesha zeeka Mkuu .............................. .. Rutashubanyuma

MziziMkavu.........ccm imezaliwa 1977 na haina hata miaka 40 sasa yawaje kuwa imekuwa imezeeka? Tofautisha matatizo ya kimfumo na chama chenyewe.....kwalugha nyingine.tatizo siyo ccm bali mifumo ambayo ccm imejiwekea na sasa inaendelea kuiboresha..................ongelea mifumo ya chadema ambayo wameiiga kutoka ccm sasa wafikiri wakiingia madarakani si wataiga u-ccm tu wa wizi na ubadhirifu?

nchi yaongozwa na mifumo na wala siyo vyama chambua mifumo na khoja yako itaeleweka.................
 
Last edited by a moderator:
You know the words BUT you miss their meaning!! pole sana; kama upembuzi yakinifu ndio kama huu, then no wonder Tanzania is in the 21st century but her peoples are living like in the old stone age!! for lack of analytical capability of our situation.

MTK ninashukuru kwa kukiri hizi nondo zangu huna majibu yake...........because it is a gospel truth.............wewe unayelewa misingi ya "words" and tehir "meanings" hebu tuchambulie mapungufu ya nondo zangu/........lol
 
Last edited by a moderator:
Rutashubanyuma i see where you are going with this halafu unaji contradict kidogo..,CCM kwa mfumo wao watatoa mgombea bora really? Halafu at the same time wapinzani wameiga mfumo wa CCM.....kwanini Upinzani usitoe mgombea bora? Kwanini unakuwa na haraka ya Mgombea bora toka CCM iliyoshindikana duniani na Mbinguni? Ebu tujadili njia za kumpata mgombea bora wa Upinzani kama una mapenzi kweli na nchi yako.....

lemonade.........acha kukufuru ccm ingelikuwa imeshindikana hadi binguni na duniani yote si nchi ingelikuwa kwenye vurugu kubwa.............asubuhi unakaa na kunywa kikombe cha chai khalafu unatoa mahuzuniko.................au wadaia gharika ya chadema ikufikie kama kule zambia ilivyotokea khalafu baadaye turudi tena ccm?
 
Last edited by a moderator:
Ruta kuna kitu unakitafuta, kutoa hoja kama hizi kuhusu 2015 unataka kujiletea matatizo!
maana CCM wakigundua malengo yako, WAFA! unadiriki kusema waliotangulia wote BOMU!
Sasa mabomu waliwekwa na mabomu wenzao na katika mabomu hayo hayo hata wakitumia wananchi atatoka humohumo tu.
Yaani sasa umewasiliba ungesema wamo wachache wazuri tungesema watabaahatisha tena 2015,
Lakini umesema MABOMU.
Na nikiangalia wanavyolipuana ndani ya chama Duh Kweli ni MABOMU.
Na sisi tu nasema tumechoka kulipuka wamelipua vyakutosha sasa basi.

Sina shaka unalo lako jambo weye!.
 
Sikubaliani asilani na hoja za Watanzania wengi wenye uoga wa kubadili mfumo wa utawala kwa maelezo chapwa eti heri tuendelee na wezi hawa hawa tuliowazoea (Chama Cha Magamba) kuliko kuleta wezi wapya wa Upinzani. Astaghfilullah!! Hivi ndo kusema wizi ni sifa kuu ya Watanzania? Kwamba kila anayeingia madartakani lazima aibe?

Kama hivi ndivyo bado tunadhani ipo haja ya kuwabadili 'wezi' kwa sababu wapinzani wana sera ya kuunda serikali ndogo na hivyo kupunguza mianya ya wizi kuliko hawa Chama Cha Magamba ambao ukubwa wa serikali hauelezeki maana wapo viongozi rasmi na wasio rasmi. Wasio rasmi ni kama watoto, mashemeji, vidosho, mabest, makada, nyumba mbhoke.......Na woote hawa ni wezi kama alivyobainisha Rutashubanyuma
Omonto wa-hene,

....BIG POINT..... Chadema kunionyesha ni chama makini waachane na mifumo ya kiubabebabe walioiiga kutoka ccm........ charity begins at home....... hawezi kudai wakiingia madarakani watarekebisha mifumo wakati wao ni carbon paper ya ccm....
 
Last edited by a moderator:
Ruta kwa hili sikubaliani nawewe japo kuna some point la kishibisha matumbo.
Mimi ningependa kwasababu ccm imeonyesha kushindwa na wapinzani wanafanana basi tumpate raisi asiyetoka chama cha siasa, independent candidate.
 
Back
Top Bottom