Aliye jirani na Kocha Mbovu kuwahi kutokea Taifa Stars Amunike anisaidie Kuniulizia Kwake haya Maswali yangu 11 tu tafadhali

Kwahiyo tulihangaika ili tufuzu tukashiriki au tufuzu tukashindane kama wengine?
Punguza kiherehere na kujifanya una uchungu kama mama mjamzito, Amunike awachukie wachezaji wa Simba kwani anakaa nao mtaa mmoja tuseme wanagombea demu?

Hao wachezaji unaoorodhesha hapa, si siku zote wanacheza na tunafungwa? Yaani hii nchi kila mtu kocha.
 
Ishukuru CCM kwa kufanya mafekeche na Uganda ili kulainisha Mambo.

Kumbuka Tz na Ug zina historia ndefu.
Wewe ni mwepesi sana kusahau, umesahau hao Uganda kwao walinusurika kula kichapo tukatoa draw,na kwenyewe CCM ilienda kuongea nao? Uganda tuliwafunga kihalali kabisa na walikuja kupambana kwelikweli
 
Mbona Uganda kwao hawakutufunga. .acheni hizo huyo Mkude away game zote za Simba alifanya nini?
Mimi sijasema Mkude wala nani wote ni walewale tu sijui Fey Toto mimi kwangu bado kupambwa na magezeti tu sasa jana ilikuwa reality check kila mtu kajuwa level yake, Uganda level sio yetu hata kama tulitoka draw kikubwa hapa sababu ya sisi kuwa Egypt kuruhusu team 24 ingekuwa 16 tungesubiri miaka 39 mingine huo ndio ukweli.
 
Acha uprimitive,porojo na kukaririshwa wewe,kwani pamoja na kuongezwa timu in mataifa mangapi makubwa kisoka kuliko sisi hayajafuzu? Wapi ivory coast, wapi Zambia, wapi Gabon, Wapi Bukinabe, wapi jirani zetu Rwanda n.k? Au wenyewe hawakutaka kushiriki kwa sababu Misri kuna joto sana!?

Kocha akosolewe tena siyo kwa kujidanganya kwamba ameacha wachezaji wazuri,labda namna ya ufundishaji na mipango lakini apongezwe pia kwa kukufanikishaia wewe na Mimi kuiangalia timu yetu ya taifa kwenye TV ktk mashindano makubwa haya.
Yaani Rwanda, Burkina na Gabon nchi kubwa kisoka? sasa leo South Africa anacheza na nani sio Ivory? ungesema Zambia sawa. Team kubwa zote Africa zipo. Egypt, Tunisia, Morocco, Nigeria, Algeria, Senegal, Ghana na Cameroon hawa ndio wafalme wa soka la Africa hao wengine wapo hawapo. Kwa hiyo kama kuna joto ndio maana Zambia alijitoa au? mashindano yote yanachezwa kipindi cha joto kwa taarifa yako mechi ya jana ilikuwa ni 28 Temp hata Dar joto.
 
Mimi sijasema Mkude wala nani wote ni walewale tu sijui Fey Toto mimi kwangu bado kupambwa na magezeti tu sasa jana ilikuwa reality check kila mtu kajuwa level yake, Uganda level sio yetu hata kama tulitoka draw kikubwa hapa sababu ya sisi kuwa Egypt kuruhusu team 24 ingekuwa 16 tungesubiri miaka 39 mingine huo ndio ukweli.
Ila ndugu nadhani ongezeko la timu limeziathiri timu kubwa kubwa kama Ivory coast, S.A,Gabon, Zambia,jirani zetu Rwanda n.k mana imebidi zisubiri. Au unasemaje?
 
kiukweli hili Kocha ni bovu kuliko yaan linakera ningekuwa na bunduki ningekusubiri Airport nikupige risasi. watanzania kila siku tunasononeka ni lini tutafurahi?

Nilidhani ninayemchukia sana Tanzania nzima nipo peke yangu kumbe tupo wengi! Halafu hata Jana ile Makocha wenzake wakisimama unaona kabisa wanavyohangaika Kuwaelekeza huku na kule Wachezaji wao na Midadi juu muda mwingine lakini lenyewe ( Amunike ) jana lilikuwa linaamka muda mchache na muda mwingi linakaa tu na Mpua wake na Mbichwa wake Mkubwa kama Madafu ya Mafia na Kilwa.
 
Kwahiyo tulihangaika ili tufuzu tukashiriki au tufuzu tukashindane kama wengine?
Mbali ya madhaifu ya kocha Amunike, lkn upumbavu wa Mkude kaeni nao nyie. Hakuna kocha anayejitambua akaingiza kambini timu kwa siku 6 mchezaji anaripoti siku ya 5 jioni.
 
Yaani Rwanda, Burkina na Gabon nchi kubwa kisoka? sasa leo South Africa anacheza na nani sio Ivory? ungesema Zambia sawa. Team kubwa zote Africa zipo. Egypt, Tunisia, Morocco, Nigeria, Algeria, Senegal, Ghana na Cameroon hawa ndio wafalme wa soka la Africa hao wengine wapo hawapo. Kwa hiyo kama kuna joto ndio maana Zambia alijitoa au? mashindano yote yanachezwa kipindi cha joto kwa taarifa yako mechi ya jana ilikuwa ni 28 Temp hata Dar joto.
Nlikosea hapo S.A na ivory coast. Ila nnachosema hapa ni kwamba kuongezeka kwa timu siyo factor kubwa sana mana kuna nchi hazijafuzu pamoja na onhezeko hilo.
Burkinafaso,Zambia na Gabon wametuzidi mbali tu kisoka. Na Rwanda hapo nlitolea mfano tu kwamba nao kwa nn wasitumie daraja la ongezeko la timu?
 
Ila ndugu nadhani ongezeko la timu limeziathiri timu kubwa kubwa kama Ivory coast, S.A,Gabon, Zambia,jirani zetu Rwanda n.k mana imebidi zisubiri. Au unasemaje?
Katika hizo Ivory coast wako na wanacheza na South Africa leo hawa kina Rwanda wa kawaida tu hawana ukubwa wowote Africa wala Gabon. Zambia ndio wa kushangaa kakosa vipi lakini super power wote wako huko na ushindani ni mkubwa. Turudi katika mada kuongezwa team imesaidia kama sisi kupata nafasi na ni nzuri kupata ujuzi ili isiwe mwaka huu tu na mashindano yajao tuwepo tatizo letu kubwa ni lazima tukubali bado mpira wetu kuna changamoto nyingi katika uelewa wa tactic wa wachezaji wetu. unaweza kuwa wametuzidi lakini nidhamu muhimu jana hata defence line walikuwa wanashindwa kukaa line moja
 
Naunga mkono hoja
Huyo jamaa maswali yake hayajibiki kamwe kama tukiamua kuchukua kiwango cha mchezaji mmoja mmoja kwa kuwafananisha na wale senegali......
Namshukuru kocha Amunike kwa kuiwezesha timu yetu kushiriki michuano ya afcon ..... Ni miaka 39 imepita tangu mara ya mwisho kushiriki
 
We mpira hutaujua kamwe
1. Kikosi cha jana dhidi ya Senegal alikipinga Yeye au alisaidiwa na akina Karia pamoja na Mwakyembe?

2. Ni kwanini ana Chuki sana na Wachezaji Nyota wanaotoka Klabu ya Simba Sports Club?

3. Kwanini alimpanga Beki David Mwantika ambaye alimuita kutoka Tanzania, hakuwa na Mazoezi ya pamoja na Wenzake, wala match Fitness na akampanga huku akimpanga Benchi Mchezaji Kiraka Erasto Nyoni?

4. Anaweza kunipa sababu ya Yeye kupenda kuwatumia Wachezaji kama Himid Mao na Mudathiri Yahaya katika Kiungo cha Ukabaji huku akimuacha na Kumchukia kabisa Natural Defensive Midfielder na ambaye yupo katika Kiwango cha juu Tanzania nzima kwa miaka kadhaa sasa Jonas Gerald Mkude?

5. Je zile Rafu za Kipumbavu ( Kiduduna ) walizokuwa wakizicheza akina David Mwantika, Faisal Salum na Himid Mao Yeye ndiye aliwatuma hivyo walikuwa wakitekeleza Maelekezo yake?

6. Je mpaka hivi sasa Kichwani mwake ana Kikosi chake cha Kwanza kiasi kwamba hata nikimuamsha tu Usiku wa Manane atanitajia bila matatizo yoyote?

7. Je baada ya Beki wake Aggrey Morris Kuumia alipaswa amuite Beki Abdi Banda ambaye alikuwa nae huko huko Kambini Misri au alipaswa amuite Beki David Mwantika ambaye hapo mwanzoni hakumjumuisha katika Kikosi chake kile cha Wachezaji 33 alioondoka nao?

8. Ni kwanini anawapenda sana Wachezaji Thomas Ulimwengu na Himid Mao kiasi kwamba hata kama wakiwa hawako katika Form au Majeruhi lakini Yeye ni lazima tu atawaita na kwenda nao popote pale ambapo Taifa Stars itaweka Kambi yake?

9. Je kati ya Thomas Ulimwengu na Rashid Mandawa ni Mchezaji gani ambaye Kiuhalisia na jinsi Mechi ilivyokuwa Jana alitakiwa ndiyo amuingize ili aweze kuleta Uhai au Mabadiliko katika Timu?

10. Kama tukiamua Kuangalia Mchezaji ambaye amepata Uzoefu wa Michuano mikubwa mikubwa ya Kimataifa je Kwake Yeye kati ya Mohammed Hussein Tshabalala kutoka Simba SC na Gadiel Michael kutoka Yanga SC ni nani angefaa na pengine hata Kumuanzisha katika Mechi ya Jana?

11. Tanzania tunajivunia sana Wachezaji wanaocheza Ligi Kubwa tena za Ulaya kama Samatta anayecheza KRC Genk ya Ubelgiji na Yousuf anayecheza Blackpool ya Uingereza ni kwanini ameamua tu Kumtumia Samatta na Wachezaji wengine wa Kulipwa ila wanacheza Klabu za hapa hapa barani Afrika zisizo na Mafanikio akina Msuva, Himid na Ulimwengu na akimuacha Yousuf benchini?

Mwisho kabisa akishanijibu haya Maswali yangu Kumi na Moja ( 11 ) naomba anisaidie pia kuniambia ni lini atatuachia Timu yetu ya Taifa Stars ili waje Makocha wenye Kuujua Mpira kuliko Yeye, wasio na Chuki wala Visasi kwa Wachezaji kabla Mimi na Wenzangu wenye Uchungu na Hasira kali dhidi yake hatujaamua Kumvizia pale Uwanjani JNIA akirudi na Timu kisha tumpopoe na Mawe na aione Tanzania hii Chungu Kwake!

Msisahau kumwambia kuwa mwana JamiiForums Mimi An Eagle a.k.a BRAINIAC namsalimia ila simkubali kabisa na aondoke tu.
 
Nlikosea hapo S.A na ivory coast. Ila nnachosema hapa ni kwamba kuongezeka kwa timu siyo factor kubwa sana mana kuna nchi hazijafuzu pamoja na onhezeko hilo.
Burkinafaso,Zambia na Gabon wametuzidi mbali tu kisoka. Na Rwanda hapo nlitolea mfano tu kwamba nao kwa nn wasitumie daraja la ongezeko la timu?
Mimi nakubaliana na wewe Zambia siku zote wamekuwa zaidi ya sisi ila Gabon ni level yetu wala hao Rwanda kawaida sana, Burkina wao wamekuwa wazuri ila sio kuwa wakubwa kisoka maana hawajahi kufanya vitu vya ajabu. Hao niliowataja North na West Africa ndio wamekuwa vinara wa soka letu huyo South Africa tu ilikuwa tabu kupata nafasi
 
Katika hizo Ivory coast wako na wanacheza na South Africa leo hawa kina Rwanda wa kawaida tu hawana ukubwa wowote Africa wala Gabon. Zambia ndio wa kushangaa kakosa vipi lakini super power wote wako huko na ushindani ni mkubwa. Turudi katika mada kuongezwa team imesaidia kama sisi kupata nafasi na ni nzuri kupata ujuzi ili isiwe mwaka huu tu na mashindano yajao tuwepo tatizo letu kubwa ni lazima tukubali bado mpira wetu kuna changamoto nyingi katika uelewa wa tactic wa wachezaji wetu. unaweza kuwa wametuzidi lakini nidhamu muhimu jana hata defence line walikuwa wanashindwa kukaa line moja
Timu jana ilicheza kama timu ya Shule flani inayoshiriki mashindano ya Umitashumta. Nilimuonea sana huruma Mbwana Samatta kuwa ktk kundi la wachezaji waliocheza namna ile
 
Mbali ya madhaifu ya kocha Amunike, lkn upumbavu wa Mkude kaeni nao nyie. Hakuna kocha anayejitambua akaingiza kambini timu kwa siku 6 mchezaji anaripoti siku ya 5 jioni.

Faisal Salum ( Fei Toto ) anahitaji Kucheza Mechi 1000 ili aweze Kuufiki uwezo mkubwa na Kiwango Kikubwa cha Mtalaam na Fundi wangu Kipenzi Kiungo Bora wa Ukabaji kwa Tanzania kwa miaka takribani Mitatu Minne iliyopita Jonas Gerald Mkude. Kama Yanga SC mnamtaka Kocha Emanuel Amunike ili asaidiane na Mpuuzi wenu mwingine Mwinyi Zahera mchukueni ila kwa Timu yetu ya Taifa Stars hatumtaki na asipoangalia Siku akirejea pale JNIA tutampopoa na ama Mawe au Mayai Viza.
 
Back
Top Bottom