Alishaileta humu, ilisikitisha sana mkuu... I hope atakusimuliailikuwaje mkuu?
Sio mkosi bali wewe unabahati ya kuweza kupata maneno ya mwisho ya marehemu na yenye busara "msaidie mwenye shida bila kujali malipo nawe utasaidiwa kwenye shida zako"
Umebarikiwa sana kwa kuuleta ujumbe huu hapa na kuwafikia wengi
Hapo hakuna mkosi mkuu....umepata bahati sana ya kujifunza kwa uhalisia ulio wazi kabisa .mafunzo unayoyapata wewe na sisi ni haya;
1.Tuwe karibu na MWENYEZI MUNGU.kwani hatujui siku wala saa.
2.Kujitahidi kuwa wakweli kwani ukweli humsaidia mtu hata baada ya kifo.asingesema ukweli nani angewatafuta ndugu zake?
3.Tuwe na huruma na moyo wa kusaidia watu wote bila kujali dini wala kabila.
4.Tusipende malipo kwa kazi zisizo rasmi.
Umepata bahati ya kujua madhaifu ya binadamu MBELE YA MWENYEZI MUNGU.HAPO HAKUNA MKOSI WALA NUKSI.HILO NI FUNZO..