Tabia ya Kuvimbiana.(Cheo + Uwajibikaji)

Tman900

Senior Member
May 30, 2017
174
343
Leo Mida ya asubuhi Niko njiani na kibaskeli changu uchwala mala Kuna Gari imekuja nyuma Yetu Kasi Sana, mpaka ikataka kutugonga sie waendesha Vibasikeli visivyoheshimika mjini.

Kwa kua barabara Ni Finyu Jamaa katanua na kule Mbele Kuna Gari kubwa Kama tatu zimeongaza Jamaa amebrock barabara ya kulia, na kushoto tuko kwenye Foreni.

Bonge jam pande zote, Trafik alipokuja anagonga kwenye hile Gari, Jamaa katuria tu.

Anaenda Mbele ya Gari anagonga kioo Jamaa katulia tu.

Trafik ikabidi asimame tu awe ametulia tu.

Baada ya 1 dakika au 2 Dakika Jamaa kashuka kwenye gari.

Kwa kua nilikua kwa Mbali kidogo inaonekana Kama kuliukua na mgongano wa kauli. Yule Trafik alipotoka pale alionekana kufyonya alipokua anakuja upande wetu alisema " UKU NI KUZARAULIANA KIKAZI"

# Wote tuliobarabarani tulikua tunashangaa tu.

Ila yule Trafik alionekana kushushwa uthamani wake Mbele za watu.

***Kwa Mtazamo wangu naomba tueshimu kazi za watu Hata Kama umemzidi Cheo, Kipato Mali tuheshimu na Tufuate utaratibu.

Kitu alichotendewa yule Trafik Leo sio Cha Kinidhamu na hakionyeshi Utu na ustarabu wa kazi na Nidhamu ya kuheshimu Uwajibikaji wa watu walio Chini kivyeo na kimajukumu. Tujifunze kuheshimu jukumu la mtu.

Kuna Baadhi ya Mambo tunayatenda yanaonyesha dhahiri kua Kuna Baadhi ya watu hawajitambui kimajukumu na kiutendaji.

Bila hao wadogo mnao wadharau hadharani Hata nyinyi mlioko Juu msingekuepo.

TUHESHIMIANE WATANZANIA HATA KAMA MTU UMEMZIDI
 
Trafik akidharauliwa poa tu.mbona hao wanamadharau Sana Tena wanakula wasipopanda.
 
Back
Top Bottom