Aliponisaidia tu akafa! Nina mkosi?

Pole sana ndugu yangu. Si kweli kwamba una mkosi hapana, kwani sote hatujahi kinachokuja ndani ya dakika 1 mbele, kwani Mungu ndiye ajuaye.
 
Nashukuru sana kutushirikisha kwenye experience hii. Ushauri wote uliotolewa ni wa nia njema. Deni la msaada wa marehemu ulilipe hapa hapa kwa kuwasaidia wengine hasa uliotajiwa na marehemu
 
Sio mkosi bali wewe unabahati ya kuweza kupata maneno ya mwisho ya marehemu na yenye busara "msaidie mwenye shida bila kujali malipo nawe utasaidiwa kwenye shida zako"
Umebarikiwa sana kwa kuuleta ujumbe huu hapa na kuwafikia wengi
 
Hata wewe ulionesha roho ya ubinadamu maana angekuwa mwingine angekimbia na kumuacha
 
Mkuu usisikitike sana umepata bahati kubwa sana ya kuachiwa zawadi ya muhimu,zawadi yenyewe ni huo ujumbe,na katika maisha yako kuna siku itatokea utakutana na mtu mwenye shida make sure unamsaidia bila kudai malipo yeyote,wewe jaribu siku moja kutembelea familia ya marehemu you never know sio ajabu huo ujumbe ukautekeleza hapohapo inawezekana wakawa na shida fulani,we watembelee tu,sio lazima uwaelezee kisa kilichotokea.
 
Pole sana. Amani yako ipo katika kuwa karibu na familia ya marehemu. Usisahau kuwajulia hali kila uwezapo. Pia kufanyia watu wema kama alivyokuasa marehemu.
 
Inasikitisha daah, jitahidi kufuata walichokushauri wengine, kama bado unapakumbuka nyumbani kwake jitahidi ukaijulie hali familia yake!
 
Ni kisa cha kusikitisha sana, pole mkuu,
Kwa imani yangu ni kuwa wote tunaokolewa kwa NEEMA tu, ule msaada aliokupa marehemu inaweza kuwa ilikuwa ibada yake ya mwisho,
Kuna ushauri umetolewa hapo juu, kuwa ni heri uende nyumbani kwa marehemu na upate ndugu wa karibu na umsimulie KISA chote kwani inaonekana bado una mzigo mkuu wa jambo hili,
Kwa kuwaeleza ndugu wa karibu wa marehemu inawezekana ukautua huo mzigo,
Nakupa moyo Mkuu nenda kawaone punde.
Pole sana
 
Sio mkosi bali wewe unabahati ya kuweza kupata maneno ya mwisho ya marehemu na yenye busara "msaidie mwenye shida bila kujali malipo nawe utasaidiwa kwenye shida zako"
Umebarikiwa sana kwa kuuleta ujumbe huu hapa na kuwafikia wengi

Yaani bwana, ninasaidia mno watu sometimes hadi inanicost.....!! lkn nadhani la kwenda kwenye familia yake ni la msingi zaidi ntaenda.....
 
Pole sana ndugu na hongera kwa kuachiwa ujumbe mzuri kama walivyosema wengine tembelea familia yake kuonyesha upendo kwa rafiki yako marehemu
 
pole sana mkuu, ni habari ya kusikitisha.
fuata ushauri wa wadau nenda kaitembelee familia aliyo iacha jamaa.
 
Hapo hakuna mkosi mkuu....umepata bahati sana ya kujifunza kwa uhalisia ulio wazi kabisa .mafunzo unayoyapata wewe na sisi ni haya;
1.Tuwe karibu na MWENYEZI MUNGU.kwani hatujui siku wala saa.
2.Kujitahidi kuwa wakweli kwani ukweli humsaidia mtu hata baada ya kifo.asingesema ukweli nani angewatafuta ndugu zake?
3.Tuwe na huruma na moyo wa kusaidia watu wote bila kujali dini wala kabila.
4.Tusipende malipo kwa kazi zisizo rasmi.
Umepata bahati ya kujua madhaifu ya binadamu MBELE YA MWENYEZI MUNGU.HAPO HAKUNA MKOSI WALA NUKSI.HILO NI FUNZO..
 
Hapo hakuna mkosi mkuu....umepata bahati sana ya kujifunza kwa uhalisia ulio wazi kabisa .mafunzo unayoyapata wewe na sisi ni haya;
1.Tuwe karibu na MWENYEZI MUNGU.kwani hatujui siku wala saa.
2.Kujitahidi kuwa wakweli kwani ukweli humsaidia mtu hata baada ya kifo.asingesema ukweli nani angewatafuta ndugu zake?
3.Tuwe na huruma na moyo wa kusaidia watu wote bila kujali dini wala kabila.
4.Tusipende malipo kwa kazi zisizo rasmi.
Umepata bahati ya kujua madhaifu ya binadamu MBELE YA MWENYEZI MUNGU.HAPO HAKUNA MKOSI WALA NUKSI.HILO NI FUNZO..

Umeniongezea mafunzo mkuu,.....
Lakini ukweli ni kwamba baada ya kupata ushauri wenu wadau naona kama mzigo unapungua uzito hivi..... asanteni wooote!
 
Naomba nami niongezee hili, siku ile Mungu alikuwa anamchukua aliyekuwa mfadhili wako na alitaka akushirikishe sehemu ya huduma yake kama Mungu. Kumbuka siku zote Mungu hufanya kazi na watu wake, maneno aliyoyasema ingawa yanaonekana yalikuwa ni mengi hayakuwa yake, Mungu alimwamuru ayaseme na yalikuja kwake kwa makusudi maalum. Hivyo haikuwa mkosi ila kuna wajibu unapewa, ingawa wakti huo hukuelewa sasa chukua hatua. Wale aliowaacha marehemu ambao walikuwa wanamtegemea, sasa wamehamisha mategemeo yao moja kwa moja kwa Mungu na kama nilivyoeleza kwanza Mungu hufanya kazi na watu wake, hili ni jukumu ambalo Mungu anataka akushirikishe nawe utamuona jinsi Mungu alivyo wa ajabu.
Nenda kawatafute, hata kama wamehama jitahidi kuwatafuta naye atakuongoza utawapata tu. Baada ya kuwapata atakuonyesha ufanye nini, usiache kwenda kwa maana ndio sababu ilikusukuma utafute ushauri hapa.
 
Mkuu Kisigino, Mungu anapokuja kwetu ni kwa umbo la binadamu.
Yule alikuwa ni malaika wa Mungu, alifanya alichoweza kufanya na mengine muachie Mungu na mshukuru kwa kila jambo.
Muhimu ni kutafakari ujumbe wa upendo aliokuacia,mpende jirani yako Kama unavyojipenda.
Msaidie jirani aliye matatizoni kama wewe mwenyewe unavyoweza kupata matatizo
 
Pole sana najua hiyo picha ya tukio hilo litaishi nawe milele.

Ulifanya vizuri kwenda kwenye msiba, ila kwa mie naona kama polisi alikushauri usiseme kitu jitahidi na Mungu anajua why hadi leo hujasema kitu. Kwa mie naona nenda kawaone ila usiongee nini ilikuwa vipi haraka kama unataka sema ongea mbeleni sana ila uwe unahuakika kuwa polisi bado wanajua kilichotokea.

Kwa nini nasema hivi, hii dunia ni ya ajabu na ina watu wa ajabu inaweza kuwa sio immediate family watakusumbua bali ndugu wa karibu wasio na mbele wala nyuma shit happens na kujuta huwa ni mbeleeeeeeee

kwenda kwako kunaweza hata elfu chache kusaidia watoto wake wasome au ushauri wako ukasaidia familia.

Pia yeye kukuambia yote juu yake labda angepatwa na kifo familia yake wasingejua yupo wapi, labda pia kuhisi amepotelea safarini labda alipata ya haraka bila kuweza kuwafahamisha yaani labda wasingeona hata uo mwili wa kuzika na kuhisi labda kafia huko nchi za watu etc yaani anyithing.

I believe tendo kubwa ulilomtendea siku hiyo na atakuwa anafurahia hadi leo ni wewe kujitolea na hilo hilo gari lako kumbeba, kutaafifu familia

Chukulia hili lilikuwa ni jambo kubwa ambalo ulimtendea that day. Ukiwasalimu tujulishe ila kaa kimya for now or forever (wengi wana imani za ushirikina etc na wanaweza kupa matatizo kuzani ulihusika as haswa ile point ya aligeuka kukuaga... utaweza singiziwa mengi sanaaaaa hata ambayo hujawahi jua yamo duniani)

Mungu awe nawe,na ndie atakayekuongoza. Omba.
 
Back
Top Bottom