Zanzibar: Polisi wajitafakali, mtu anagonga mtu anaachiwa bila mawasiliano na ndugu wa aliyegongwa

DREAMBOY

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
2,050
1,220
Inahuzunisha sana !Sijui ni ubaguzi au nini?

Ipo hivi, Kuna kijana yupo zanzibar, kwa muda sasa.

Jumapili aligongwa na gari akiwa pembeni ya Barabara, baada ya kumshusha mkewe kwenye kibaiskel chake abaki kibandani, ili yeye akafuate mzigo wa kuongeza kitandani chake.

Madhara aliyoyapata ni makubwa, na hii ilisababishwa na dereva wa gari ile maana baada ya kumpamia aligundua hajafa hivyo akarudisha gari nyuma nadhan alitaka kumuua kabisa, hivyo ndipo alipopita juu ya mkono na akaamua kuondoka. Hali hiyo ndiyo ilisababisha kuvunjika mkono.

Wasamalia bado wapo wakati yule dereva anafanya hayo kuna gari ilikuwa inakuja kwa mbele, kumbe yule dereva wa gari ya mbele aliliona tukio lile vizuri hivyo akakinga gari barabarani, jambo lilosaidia kukamatwa kwa dereva yule.

Sasa mkewe kaenda polisi kufuatilia,kaambiwa wamemuachia kwa kujidhamini,

Lakini polisi wamemuachia bila hata kuwasiliana na waliotendewa uovu huo, na upo usemi kuwa mbara ni ngumu kupata haki vituo vya polisi. Ndivyo ndungu wanavyoambiwa na mwenyeji.

Jeshi la polisi tendeni haki ,ulinzi ni suala la muungano.
 
Hiyo jamii hatukupaswa kuungana nayo, waasisi wa Tanganyika walitukosea sana. Hao watu wamejaa ubinafsi na ubaguzi, picha linaanza wao kwa wao wanabaguana kwa vyama, asili na maeneo watokayo!
Jambo ambalo nna uhakika nalo: siku wakitoka kwenye muungano Zanzibar hakutakalika, watamalizana.
 
Haya mambo ya ajabu yapo sana unguja,kama hujawahi kuishi unguja kwa muda mrefu unaweza kuhisi labda wazanzibari wanasingiziwa,ila hawa jamaa ni wabaguzi na wana roho mbaya sana nadhani pia sababu ya ukosefu wa elimu miongoni mwao kwa asilimia kubwa
Anyway salamu za pole ziende kwake huyo jamaa inaumiza sana.
 
Dhamana siyo lazima ajulishwe alietendewa kosa maana dhamana ni haki ya mtuhumiwa wa makosa yanayo dhaminika, kumbuka mtuhumiwa hatakiwi kukaa zaidi ya masaa 24 kituo cha polisi bila dhamana au kufikishwa mahakamani kama kosa linadhaminika

Kama amedhaminiwa ni haki yake, ingekua kafutiwa kesi kabla ya majeruhi kupata haki yake hiyo ndo ingekua ni uonevu na kinyume na sheria
 
Vipi kama aliyegongwa baadae alikwenda kufa na huku mtuhumiwa kashaachiwa kwa dhamana
 
Hiyo jamii hatukupaswa kuungana nayo, waasisi wa Tanganyika walitukosea sana. Hao watu wamejaa ubinafsi na ubaguzi, picha linaanza wao kwa wao wanabaguana kwa vyama, asili na maeneo watokayo!
Jambo ambalo nna uhakika nalo: siku wakitoka kwenye muungano Zanzibar hakutakalika, watamalizana.
Wazanzibari Wana ubaguzi gani wakati rais wao tunawachagulia huku Dodoma. Akimaliza kutawala anarudi Tanzania kuendelea kula mema ya nchi.
 
Vipi kama aliyegongwa baadae alikwenda kufa na huku mtuhumiwa kashaachiwa kwa dhamana
Atakamatwa tena maana kaachiwa kwa dhamana, kuachiwa kwa dhamana maana yake wakikuhitaji wanakupata, hata asipokufa bado ataendelea na kesi yake akiwa nje
 
Hiyo jamii hatukupaswa kuungana nayo, waasisi wa Tanganyika walitukosea sana. Hao watu wamejaa ubinafsi na ubaguzi, picha linaanza wao kwa wao wanabaguana kwa vyama, asili na maeneo watokayo!
Jambo ambalo nna uhakika nalo: siku wakitoka kwenye muungano Zanzibar hakutakalika, watamalizana.
Inahudhunisha sana, hugo kijana kaandikiwa oparesheni kichwa ,mpaka sasa kalazwa. Ana maumivu ya kichwa sana.
 
Nani ataisimamia hiyo kesi, maana ndugu zake wamekwenda kituo cha polisi . Wanaambiwa sisi tunachojua yupo nje kwa dhamana mambo ya mahakama sisi ndo tunajua cha kufanya

Atakamatwa tena maana kaachiwa kwa dhamana, kuachiwa kwa dhamana maana yake wakikuhitaji wanakupata, hata asipokufa bado ataendelea na kesi yake akiwa nje
 
Back
Top Bottom