'Akina Mzee Mwanakijiji' ni wavivu kufikiri

Uyu bwana MMK nilishamuondoa kati ya GT wa umu JF, japo mie sio mwana siasa na siungi mkono upande wowote ule but napenda mabadiliko ya dhati. Anajiona elite sana kisiasa na hasa za umu javini. Nafikiri watu wanafikiri yeye ni political strategist mwenye vision ya kuona mbali kumbe ni wale wale wachumia matumbo yao.ningekuwa na uwezo ningemdelete asiweke tena post zake umu ndani.
 
Ntatumia matokeo ya kata kama 8 hivi as a Benchmark Ku msupport Tuko
Hii inaonesha kama ungekuwa ni uchaguzi wa Rais, CDM wangepiga Bao kubwa mno

KataCHADEMACCM
Kilema Kusini797736
Najara Rehan23701128
Mnero Miembeno818138
Myovizi17261498
Momba903310
Mahenge444710
Mtibwa30961372
Daraja Mbili21931324
SUM
123477216
Someone is torturing the numbers......the confession is at the bottom.
 
kama anao mwongozo na wewe umeuona na una chembe za ubongo kwanini usiutumie? au na wewe mvivu wa kufikiri? kichwa kama andazi lililoungua.

Hakyamungu Mod mwanakijiji asipopigwa BAN kwa matusi haya utakuwa unaipotezea heshima JF na itakuwa ni ubaguzi wa hali ya juu.
 
hahahah...leo mzee mwanakijiji sijui kanywa konyagi...kichwa kama ANDAZI LILILOUNGUA
ndaga fijo gwa kukaja gwe beno a.k.a mzee mwanakijiji..kali ukwesile makambo lilino
mwanakijijiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
nahisi kunatatizo kubwa dhidi ya mwanakijiji au account yake.all latest started threads haziko sawa,mods na members tusaidiane.
 
Kuna uzi uliwahi kutoka hapa wiki jana kuhusu kubadilika kimsimamo kwa mzee mwanakijiji.mimi nilimuomba aeleze mapungufu ya mbowe na slaa ktk harakati zao za kisiasa.hakujibu.anasema wanataka kuingia ikulu bila kuwa na mikakati yoyote.lakini anajichanganya anaposema alimuunga mköno jk mwaka 2005 kwa sababu tu alikubalika na watu wengi.kwa mtu makini kama yeye kuwa na tabia hiyo ni hatari.mimi nilimpinga jk wakati ule na najivunia kwa hili.hata hivyo cdm wanastahili pöngezi kwa kujiongoza vizuri na kusimamia halmashauri wanazoongoza kwa ufanisi
 
Ni mwongozo mzuri wa kupima mwelekeo wa CHADEMA,lakini hii isiwe assignment ya watu fulani ila wote ili tujadili kwa ushahidi.
 
Mmmmmmm!! Samahani naomba kujua kama kuna Mzee Mwanakijiji zaidi ya mmoja humu, maana nimeshutushwa na hii comment kama kweli ni ya Mwanakijiji niliyemzoea kama mwelimishaji, mchambuzi mwenye busara kabisa katika kujega mstakabari wa jamii yetu, bado siamini kama ndo ameandika mwenyewe hii reply, Mwanakijiji nihakikishie kama kweli ni wewe mwandishi wa zile makala ndo umeshusha hii kitu hapa tafadhali........!!!!

kama anao mwongozo na wewe umeuona na una chembe za ubongo kwanini usiutumie? au na wewe mvivu wa kufikiri? kichwa kama andazi lililoungua.
 
Mada nyingine za kichokozi kumtafutia mtu ban bure,mbona mnatoka nje na kwenda kushitaki kwa mods kwenye malalamiko?gt hawako hivo wanapambana kwa hoja na never give up
 
Sasa nani ni mvivu wa kufikiri? kama wewe unazo majibu ya hayo maswali yaweke hapa siyo utake wengine wakufanyie kazi halafu wewe uje kuchambua! Ili kuonesha kuwa hoja zako ni dhaifu fanya hii kazi wewe mwenyewe, tuwekee matokeo ya uchunguzi wako halafu watu wachambue kuona kama yana ukweli au yanakubaliana na ukweli au mantiki. Vinginevyo, uvivu wetu sisi wengine kufikiri una uwezo zaidi kuliko ujasiri wa kutupuuzia.

Ili kukusaidia, majibu ya maswali yote hayo unaweza kuyapata kwenye Tovuti ya Tume ya Uchaguzi ya Taifa.

Acha kukimbia hoja ya msingi ,mambo mengi umekuwa ukiandika na kuyapamba kwa lugha ya kusadikika bila kuwa na data. Wewe leo hii unathubutu kumwambia atoe majibu! Unastaabisha sana. Mbona kwanye thread yako ya kutaka kujua idadi ya wanachama wa CDM ulikuwa unakwepa kutoa majibu ,iweje uwe na nguvu ya kumtaka huyu atoe majibu!

Matola alikuasa uache majibu magumu kwa maswali mepesi.
 
Namtaja Mzee Mwanakijiji kwa kuwa yeye ni legend wa 'uchambuzi wa mambo ya kisiasa' katika vyombo vya habari. Wapo baadhi ya watu hapa Jf na kwenye magazeti ambao walitumia matokeo ya uchaguzi mdogo wa madiwani juzi kuchambua uwezekano wa CDM kufanya vizuri au vibaya kwenye uchaguzi wa 2015. Ni jambo zuri, na wala siwapingi kwa kuwa ni mojawapoya namna ya uchambuzi wa kisiasa...

Sasa kama mtu anataka kujenga hoja na anataka hoja yake ieleweke, kuhusisha matokeo ya uchaguzi mdogo wa udiwani na matokeo tarajiwa ya uchaguzi mkuu ujao, naomba afanye home work yake kama 'mchambuzi wa kisiasa' kweli na aje na data zilizokamilika. Maana mi Tuko nikiandika uchambuzi hapa, hakuna mtu atakayehangaika sana na kuangalia nimechambuaje, maana nani anamfahamu Tuko? (hapa Tuko anawakilisha undergrounds wengine wote wa uchambuzi wa siasa). Lakini nikiona uchambuzi umeandikwa na Mwanakijiji, au Slaa, au Zitto, au Mnyika, na wengine (Nape hayupo kwenye hili kundi tafadhali, ndio maana hata post yake iliyowekwa hapa juzi sikuisoma) ambao ni members wa JF, masupastaa wa kisiasa wanaojitokeza kwenye hoja za siasa hapa, haraka sana ntakimbilia kusoma post yake na kuirudia mara mbilimbili kutafuta 'point' iko wapi...

Sasa naamini Mwanakijiji na wenzake wana uwezo wa kufanya uchambuzi wa kisayansi zaidi, kuipima CDM sasa na uwezo wake sasa na kuuhusisha na 2015 kwa kutumia matokeo ya chaguzi ndogo za udiwani. Katika uchambuzi, nitaomba waje na data na majibu ya mambo yafuatayo...
  1. Mwaka 2005 CDM ilipata asilimia ngapi ya viti vya udiwani (tuiite R), na asilimia ngapi ya kura za udiwani (tuiite S)?
  2. Kati ya mwaka 2005-2010, kama kulikuwa na chaguzi ndogo za udiwani, CDM ilipata asilimia ngapi ya viti hivyo (T), na asilimia ngapi ya kura zote (U)?
  3. Mwaka 2010, katika uchaguzi mkuu, CDM ilipata asilimia ngapi ya viti vya udiwani (V), na asilimia ngapi ya kura za udiwani? (W)
  4. Mwaka 2010, katika uchaguzi mkuu, CDM ilipata asilimia ngapi ya viti vya ubunge (X), na asilimia ngapi ya kura za ubunge (Y)?
  5. Mwaka 2010, katika uchaguzi mkuu, CDM ilipata asilimia ngapi ya kura za uraisi (Z)?
  6. Je, R, S, T, na U, zilikuwa na correlations zozote na V, W, X, Y na Z? Kama zilikuwa na correlations, watuambie zilikuwa za aina gani, na watupatie 'factors' za hizo correlation. Kwa kutumia factors za correlations ambazo wamepata, nawaomba ma-legends hawa wakokotoe matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2015.

Hata hivyo, naomba wazingatie confounding factors kama vile, impacts za daftari la wapiga kura mwaka 2004 kutengenezwa, na mwaka 2009/2010 kuboreshwa, impacts za demographical changes, impacts za kushuka ama kupanda kwa vyama vingine vya kisiasa, n.k...

Naamini hii ni kazi ndogo sana kwa watu ambao wapo kwenye tasnia ya habari na uchambuzi, lakini ina umuhimu sana ku-predict matokeo na mustakabali wa taifa letu baada ya uchaguzi wa 2015.
Naamini, ikifanyika kazi hii, matokeo ya uchaguzi ujao hayatatanguliwa na vichwa vya habari kwenye magazeti; ..."Katika hali ambayo haikutarajiwa, matokeo ya uchaguzi yanaonyesha kwamba"...

Kazi kwenu

Hesabu za kawaida tu kama algebra na log ni msiba wa kitaifa. Je linear regression si ndo janga kabisa!?
 
sasa kama hana data anaweza vipi kusema wengine tuna uvivu wa kufikiri. Angekuwa ameweka data na kuzinyambulisha tungeziangalia na kuanza kuzitorture...

Lazy mind bwana... If you want to hide something from a black man, put it in writing or numbers... What's so hard with you finding the respective data and present it here instead unaita wenzio WAVIVU wa kufikiri?! Does taking ready-made data from an identified source require thinking?!

point yangu ni kuwa inawezekana hana data lakini ameweka vipengele vya data muhimu za uchambuzi.
Ataridhika iwapo magwiji wa uchambuzi mtajadili kwa kutumia vipengele tajwa.ameamini mna uwezo wa kupata data husika.naomba tumuache mtoa mada na tutafute data hizo ili mjadala uwe mtamu.kama amekosea kuwasilisha tumsahihishe na turudi kwenye hoja ya msingi.

Mada nyingine za kichokozi kumtafutia mtu ban bure,mbona mnatoka nje na kwenda kushitaki kwa mods kwenye malalamiko?gt hawako hivo wanapambana kwa hoja na never give up

Mi nikiambiwa kuwa ni mvivu wa kufikiri, sitakataa moja kwa moja kwa sababu sina uhakika kwa nini nami sijawa legend wa 'uchambuzi wa mambo' Kama kina Mwanakijiji... inawezekana ni kutokana na uvivu wangu wa kufikiri

Hata hivyo, pamoja na uvivu wangu wa kufikiri, natambua kuwa mtu anatakiwa atoe takwimu kusapot hoja aliyojenga. Namaanisha kwamba mtu anatafuta data kusapot hypothesis yake.
Mimi sijajenga hoja yeyote kuhusiana na uwezo wa CDM, kutokana na uchaguzi mdogo wa madiwani uliopita. Sijasema kama CDM imeimarika, au imeporomoka, au imebaki vile vile kwa kuangalia matokeo hayo. Kwa hiyo wanaonidai mimi nikatafute takwimu eti kusupport au kucrash hoja ambayo sikuijenga mimi, wananipa kazi ambayo sikuona umuhimu wa kuifanya tangu mwanzo. Akina Mwanakijiji ndiyo waliokuja na hoja hapa, na wao ndio wanatakiwa waje na data kusupport hoja zao.
Hoja niliyojenga mimi, ambayo ndiyo ninatakiwa kuiwekea takwimu ni "Akina Mzee Mwanakijiji" ni wavivu kufikiri... thats my null hypothesis, na kuthibitisha hypothesis yangu, nikapoint out udhaifu wa hoja zao dhidi ya CDM. Au mnataka hadi niattach posts zao walizotoa kusema kuwa CDM haitafanya vizuri 2015?
 
Namtaja Mzee Mwanakijiji kwa kuwa yeye ni legend wa 'uchambuzi wa mambo ya kisiasa' katika vyombo vya habari. Wapo baadhi ya watu hapa Jf na kwenye magazeti ambao walitumia matokeo ya uchaguzi mdogo wa madiwani juzi kuchambua uwezekano wa CDM kufanya vizuri au vibaya kwenye uchaguzi wa 2015. Ni jambo zuri, na wala siwapingi kwa kuwa ni mojawapoya namna ya uchambuzi wa kisiasa...

Sasa kama mtu anataka kujenga hoja na anataka hoja yake ieleweke, kuhusisha matokeo ya uchaguzi mdogo wa udiwani na matokeo tarajiwa ya uchaguzi mkuu ujao, naomba afanye home work yake kama 'mchambuzi wa kisiasa' kweli na aje na data zilizokamilika. Maana mi Tuko nikiandika uchambuzi hapa, hakuna mtu atakayehangaika sana na kuangalia nimechambuaje, maana nani anamfahamu Tuko? (hapa Tuko anawakilisha undergrounds wengine wote wa uchambuzi wa siasa). Lakini nikiona uchambuzi umeandikwa na Mwanakijiji, au Slaa, au Zitto, au Mnyika, na wengine (Nape hayupo kwenye hili kundi tafadhali, ndio maana hata post yake iliyowekwa hapa juzi sikuisoma) ambao ni members wa JF, masupastaa wa kisiasa wanaojitokeza kwenye hoja za siasa hapa, haraka sana ntakimbilia kusoma post yake na kuirudia mara mbilimbili kutafuta 'point' iko wapi...

Sasa naamini Mwanakijiji na wenzake wana uwezo wa kufanya uchambuzi wa kisayansi zaidi, kuipima CDM sasa na uwezo wake sasa na kuuhusisha na 2015 kwa kutumia matokeo ya chaguzi ndogo za udiwani. Katika uchambuzi, nitaomba waje na data na majibu ya mambo yafuatayo...
  1. Mwaka 2005 CDM ilipata asilimia ngapi ya viti vya udiwani (tuiite R), na asilimia ngapi ya kura za udiwani (tuiite S)?
  2. Kati ya mwaka 2005-2010, kama kulikuwa na chaguzi ndogo za udiwani, CDM ilipata asilimia ngapi ya viti hivyo (T), na asilimia ngapi ya kura zote (U)?
  3. Mwaka 2010, katika uchaguzi mkuu, CDM ilipata asilimia ngapi ya viti vya udiwani (V), na asilimia ngapi ya kura za udiwani? (W)
  4. Mwaka 2010, katika uchaguzi mkuu, CDM ilipata asilimia ngapi ya viti vya ubunge (X), na asilimia ngapi ya kura za ubunge (Y)?
  5. Mwaka 2010, katika uchaguzi mkuu, CDM ilipata asilimia ngapi ya kura za uraisi (Z)?
  6. Je, R, S, T, na U, zilikuwa na correlations zozote na V, W, X, Y na Z? Kama zilikuwa na correlations, watuambie zilikuwa za aina gani, na watupatie 'factors' za hizo correlation. Kwa kutumia factors za correlations ambazo wamepata, nawaomba ma-legends hawa wakokotoe matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2015.

Hata hivyo, naomba wazingatie confounding factors kama vile, impacts za daftari la wapiga kura mwaka 2004 kutengenezwa, na mwaka 2009/2010 kuboreshwa, impacts za demographical changes, impacts za kushuka ama kupanda kwa vyama vingine vya kisiasa, n.k...

Naamini hii ni kazi ndogo sana kwa watu ambao wapo kwenye tasnia ya habari na uchambuzi, lakini ina umuhimu sana ku-predict matokeo na mustakabali wa taifa letu baada ya uchaguzi wa 2015.
Naamini, ikifanyika kazi hii, matokeo ya uchaguzi ujao hayatatanguliwa na vichwa vya habari kwenye magazeti; ..."Katika hali ambayo haikutarajiwa, matokeo ya uchaguzi yanaonyesha kwamba"...

Kazi kwenu

Uchambuzi wako nimeupenda sana. Kina Mzee Mwanakijiji ni wakusamehewa kwani bado uandishi wao ni wa kusadikika na usio na mahusiano na mambo halisi. Wanafanikiwa kuteka hadhira na kuwaaminisha wasomaji kuwa wanachokiandika ni sahihi kwa kupamba maneno kwa misemo mingi inayokinzana na ukweli ,kwani ni dhahiri kuwa ukweli unauma na wanadamu hatupendi kuambiwa ukweli.

Hawa ni watu wasiothamini takwimu halisia kama msingi wa maoni na michango yao ,kwani hawataki kujua mahusiano halisi ya vichocheo vinavyoshawishi mambo mbalimbali kwenye jamii. Inashangaza kuona mabandiko yao hayana mahusiano na uhalisia ila wamekuwa mahiri wa kutabiri mambo ,kwa ufupi huwa nawaona hawana tofauti na wapiga ramli kina Shekh Yahaya/Prof. Maji Marefu.
 
Last edited by a moderator:
Si kila wakati TAKWIMU zinahitajika ku-proove jambo fulani!
Data si za pande moja tu, yaani si FACTS tu, bali pia na LOGIC, hivyo si kila HOJA inaweza kuombwa Facts kui-proove, bali nyingine huhitaji MANTIKI tu(REASONING)
Mungu wetu anaita sasa!
 
What's your problem, sir? And why you singled me out when I'm not the only one using English?

Tatizo langu ni wewe na hao wenzio mnaojifanya mnajua kingereza hoja ya Kiswahili unachangia kingereza na je ingekuwa ya kingereza siunge changia kichina sasa? Waambie na wenzako wenye ulimbukeni Kama wako waache mara moja ulimbukeni wa kudandia lugha za watu au unaamini kingereza ndio kitambulisho cha usomi Kama wenzako wanavoamini?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom