'Akina Mzee Mwanakijiji' ni wavivu kufikiri

Ntatumia matokeo ya kata kama 8 hivi as a Benchmark Ku msupport Tuko
Hii inaonesha kama ungekuwa ni uchaguzi wa Rais, CDM wangepiga Bao kubwa mno

KataCHADEMACCM
Kilema Kusini797736
Najara Rehan23701128
Mnero Miembeno818138
Myovizi17261498
Momba903310
Mahenge444710
Mtibwa30961372
Daraja Mbili21931324
SUM
123477216

Sawasawa; now lets go a little further:

a. Kuna wapiga kura wangapi waliojiandikisha katika eneo hilo, wangapi walijitokeza kupiga kura

b. Kuna watu wangapi ambao wako eligible kuandikishwa kupiga kura.

c. CDM ina wanachama wangapi katika eneo hilo na CCM ina wanachama wangapi

Thanks.
 
Sawasawa; now lets go a little further:

a. Kuna wapiga kura wangapi waliojiandikisha katika eneo hilo, wangapi walijitokeza kupiga kura

b. Kuna watu wangapi ambao wako eligible kuandikishwa kupiga kura.

c. CDM ina wanachama wangapi katika eneo hilo na CCM ina wanachama wangapi

Thanks.

majibu ya (a) na (b) yanapatikana kwenye Daftari la Wapiga Kura.

hapo kwenye (c) ngoja nipavutie kasi.
 
kama mtu hataki washinde anatakiwa kusubiri baada ya 2015; kama mtu anataka CDM ifanye vizuri anatakiwa kuanza jana kuwafuatilia..

kuwafuatilia ni process lakini kuwahukumu ni event!hatukatai kuwafuatilia lakini kuwahukumu...kabla ya wakati si sahihi.
Kama tuliwapa malengo ya kuchukua kata 29 wakapata 5 definetly they have to go!lakini kama tuliwapa malengo ya kusimamisha mgombea kila kata na kuzoa kura zaidi ya nusu huku wakikabiliwa na vikwazo basi wana haki za kupongezwa.
 
Hoja za Tuko zipo sahihi sina doubt nae;
pia kwa upande mwingine Mzee Mwanakijiji kamjibu vizuri sana.. Na tuko kuonyesha validity ya thought afuate ushauri wa mwanakijiji
- bravo mzee mwanakijiji hao mashabiki wengne walioanza kukukashifu ni umewajibu VIZURI SANA
 
Last edited by a moderator:
tatizo watu wanafikiria takwimu tu zinasema kila kitu; kuna msemo kuwa takwimu ni kama sketi zinadokeza tu kilichopo lakini zinaficha kilicho muhimu zaidi.

Wengine wamewahi kusema "torture numbers and they will confess to anything"...

Au kama William Watt alivyowahi kusema "Do not put your faith in what statistics say until you have carefully considered what they do not say" na mwingine akasema akitolea mfano kuwa "I abhor averages. I like the individual case. A man may have six meals one day and none the next, making an average of three meals per day, but that is not a good way to live. "

Labada nitoe mfano hai to support your argument that "Do not put your faith in what statistics says until you have carefully considered what they do not say." Katika matokeo kamili ya uchaguzi wa Udiwani wa kata ya Daraja Mbili, CHADEMA wamepata kura 2,193 , CCM kura 1,324, CUF kura 162, TLP kura 42 na NCCR mageuzi kura 22. Kura zilizoharibika ni 27.

Ukisoma taarifa na statistics nyingi za matokeo ya hii kata, hazighusii kabisa ni watu wangapi walijiandikisha kupiga kura kwenye hii kata. Idadi ya watu waliojiandikisha kupiga kura inafichwa sana kwenye hizi statistics bila sababu ya msingi.

But the naked fact is that waliojiandikisha kupiga kura Daraja mbili ni watu 16,295. Waliopiga kura ni watu 3,770 tuu. Sasa hapo hebu fikiria hii ni ngome ya Chedema lakini watu zaidi ya 10,000 hawakupiga kura. Wafuasi wa Chadema bila hata kufikiria wanaona ni sawa kabisa kwa Chadema kupata kura 2,193 kati ya kura possibly 16,295 votes. Kama ungekuwa ni uchaguzi mkubwa unafikiri CCM wangeshindwa kuchakachua huo uchaguzi na kupata extra 1,000 votes?

Hapa nilidhani Chadema wangeumiza kichwa kujua ni kwa nini watu zaidi ya 10,000 hawakupiga kura japokuwa walikuwa wanajaa kwenye mikutano ya kampeni na ile ya M4C. Watu wako tayari kupigwa mabomu lakini hawapigi kura? Hapa ndiyo Chadema walitakiwa kukaa chini na ku-assess whether M4C is actually working, ku-address tatizo la watu kutopiga kura as a matter of urgency kabla uchaguzi mwingine whether mdogo au mkubwa haujaja.

Kama kweli uongozi wa Chadema unafikiria kama mleta mada, wasifikirie kabisa kukanyaga Ikulu within the next 25 years. Lakini kitu ambacho nimejifunza hapa jamvini siku tatu zilizopita ni kwamba wafuasi wengi wa Chadema hawana tofauti yoyote na wafuasi wa CCM. Hata Chadema wakifanya kosa, they will attempt to justify it by whatever means. Copy kwa Ritz
 
kwi kwi kwi kwi, mambo mengine ni kwamba mnataka tucheke au, JF burudani daaa; inanikumbusha shule ya msingi ..... '' twende kaka' twende kaka'' Mgongo kama meza ya kolokolo...

Uwiiii,yaani mmenichekesha hapa leo!kweli jf stressless zone
 
  • Thanks
Reactions: MC
Leo Mzee Mwanakijiji ni sawa na ule usemi 'USIMSHIKE MANGI ****' leo umeshikwa mwanakijiji kwikwikwikwiwkjiwkwi umeshikwaaaaaaa tia uchambuzi mkuu Tuko sio mchambuzi thats why kaleta hoja mbona unajifaragua na kejeli angalia jf haijali shareholder mzee utakula ban kwikwikwi
 
Last edited by a moderator:
Ntatumia matokeo ya kata kama 8 hivi as a Benchmark Ku msupport Tuko
Hii inaonesha kama ungekuwa ni uchaguzi wa Rais, CDM wangepiga Bao kubwa mno

KataCHADEMACCM
Kilema Kusini797736
Najara Rehan23701128
Mnero Miembeno818138
Myovizi17261498
Momba903310
Mahenge444710
Mtibwa30961372
Daraja Mbili21931324
SUM
123477216
Mkuu kuna TAKWIMU zako hapo juu zinapotosha.....Baadhi hazina ukweli....

Fanya upitie habari hii hapa chini...

Udiwani: CCM chapoteza viti vinne


LICHA ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kunyakua viti 22 kati ya 29 vya udiwani katika uchaguzi uliofanyika juzi, chama hicho tawala kimepoteza kata nne kilichokuwa kinazishikilia kabla ya uchaguzi huo.
Uchaguzi huo ulifanyika kuziba nafasi zilizoachwa wazi na madiwani walioondoka kutokana na sababu mbalimbali zikiwamo vifo.

Matokeo ya uchaguzi huo yanaonyesha kwamba katika Kata 29, Chadema wameshinda katika kata tano na kukifanya kuongeza madiwani watatu. TLP na CUF kila kimoja kimepata kata moja.
Kabla ya uchaguzi huo, Chadema kilikuwa na Kata mbili za Rombo na Mvomero ambazo kimefanikiwa kuzitetea na kuongeza nyingine tatu, ambazo ni Mlangila (Ludewa), Ipole (Tabora) na Daraja Mbili (Arusha) ambazo awali, zilikuwa zikishikiliwa na CCM.

TLP kilitetea kiti chake katika Kata ya Vunjo (Kilimanjaro) wakati CUF kilitwaa Kata ya Newala ambayo awali ilikuwa ikishikiliwa na CCM.
CCM kimetetea viti vyake vingine vilivyobaki ambavyo ni Msalato (Dodoma), Bang'ata (Arumeru Magharibi), Mletele (Songea), Mwawaza (Mjini Shinyanga), Lwezera (Geita), Bugarama (Kahama) na Bagamoyo mkoani Pwani.

Viti vingine ni Mnero na Miembeni (Nachingwea), Myovizi (Mbozi), Mpapa (Momba), Mahenge (Ulanga), Vugiri (Korogwe), Tamota (Lushoto), Makata (Liwale), Mpepai (Mbinga), Kiloleli (Sikonge), Miyenze (Tabora), Karitu (Nzega), Lubili (Misungwi), Kilema Kusini (Moshi), Nanjara/Neha (Rombo), Lokokona (Nanyumbu) na Kitangiri (Newala).

Katika Kata ya Rwezera, Misango Jeremiah alishinda baada ya kupata kura 1,309 dhidi ya wapinzani wake, Ibuga Mussa (Chadema) aliyepata kura 933 na Mussa Mtagala (CUC) aliyepata kura 317. Uchaguzi huo ulifanyika kujaza nafasi hiyo iliyokuwa wazi baada ya aliyekuwa Diwani wa Kata hiyo, Anatory Mkufu kufariki dunia kwa ajali ya gari Februari 23, mwaka huu.

Kilimanjaro
Katika Kata ya Kilema Kusini, Joseph Rubega wa TLP alishinda kwa kura 1,044 wakati Peter Temu (CCM) alipata kura 797 akifuatiwa na Serafine Mbuya (Chadema) kura 736 na Paul Shirima wa DP kura 13.
Katika Kata ya Nanjara Reheha, Rombo, Frank Salakana (Chadema) alishinda kwa kura 2,370 na kumshinda mpinzani wake pekee kutoka CCM, Dismas Silayo aliyepata kura 1,128.

Lindi
Katika Kata ya Mnero Miembeni, Gervas Ungele (CCM) alipata kura 818 wakati Jumanne Ali (CUF) alikuwa wa pili kwa kura 611 na Sinji Ali (Chadema) alipata kura 138.

Mbozi na Momba
Katika Kata ya Myovizi, Mbozi Cosmas Nzowa (CCM) alipata kura 1,726 huku Musa Mtakati (Chadema) akipata kura 1,498.

Katika Kata ya Mpapa, Momba, Nolatico Simbeye (CCM) alishinda kwa kura 903 na mpinzani wake, Ladius Kasonso (Chadema) alipata kura 310.

Morogoro
CCM kilishinda katika Kata ya Mahenge kwa Mark Asenga, kupata kura 710 , dhidi ya Baltazar Kizee (Chadema) aliyepata kura 444.

Katika Kata ya Mtibwa, Mwakambaya Edward (Chadema), alishinda kwa kura 3,096 na Musa Kingu (CCM) alipata kura 1,372.


Arusha
Kata ya Daraja Mbili, iliyokuwa ikishikiliwa na CCM kabla ya diwani wake, Bashiri Msangi kufariki dunia ghafla mapema mwaka huu, Chadema kiliibuka na ushindi baada ya mgombea wake, Prosper Msofe kupata kura 2,193 dhidi ya Philip Mushi wa CCM aliyepata kura 1,324. Mgombea wa CUF, Zani Hassan Zakaria alipata kura 162, William Msuyakura (TLP) alipata 42, Mohamed Msuya wa NCCR Mageuzi alipata kura 22. Uchaguzi huo, unafanyika wakati bado kuna viti sita vya
udiwani katika Manispaa ya Arusha, vikiwa wazi. Madiwani watano kati yao walitimuliwa na Chadema na diwani mwingine wa Kata ya Sombetini, Alphonce Mawazo alijiondoa CCM na kujiunga na Chadema.

Udiwani: CCM chapoteza viti vinne - Habari - mwananchi.co.tz
 
kuwa great thinker haina maana unafikiri namna wengine wanapenda iwe. Lakini pia haina maana utapinga hata jambo lililo wazi kabisa kwa sababu tu watu wametofautiana na wewe. Mwanakijiji ni mchambuzi mzuri wa siasa nilivosoma makala zake. Tuko pia katoa maelezo mazuri tu tuseme kama direction kuelekea kwenye truth. Ambacho hakikumpendeza MM ni kichwa cha habari; akina mzee mwanakijiji ni wavivu wa kufikiri Ah!
 
-Hizi fikra tegemezi ndizo zinazotufanya tujenge taifa la ajabu.Ndiyo maana akisimama waziri akamwaga takwimu tu tunaishia kumtangaza " Caesar for presidency" au unasikia "Wow,......such a brilliant leader"

Duh ila leo nimecheka kweli.JF Rocks!

Thank you Ben

Tatizo letu ni kutaka fulani afanye, na sie tuseme.... Tuko angenifurahisha kama angefanya hiyo analysis kuliko kuniwekea postulates zake. Jamaa ana hoja nzuri lakini anataka wengine wafanye la sivyo basi ni wavivu wa kufikiri...

Nadhani kwa sasa wote tu tumekuwa wavivu wa kufikiri:bowl:
 
umekubali kuwa kikwete ammebadilisha mawaziri wake lakini sio yeye kuwajibika!
Je kwa upande wa cdm ulitaka wawajibike kina mbowe,slaa,zitto,mnyika,lema and other top figures au wenyeviti wa matawi?(make it clear)kama ni wenyeviti wa matawi kwa nini maoni yako yalielekea kwa viongozi hawa wakuu wa chama?

2010 walifanya vibaya?kikata,kibunge au kirais?naona kama unalinganisha mambo yasiyolinganishwa mkuu.

Ungesubiri 2015 uwahukumu comprehensively!


Mkuu, hapa unampigia mbuzi gitaa!!

Rejea baada ya uchaguzi Igunga alisemaje, kabla ya uchaguzi Arumelu alisemaje, na urejee kauli yake ya juzi!!

"Ogopa kichwa cha kumbikumbi hakisagwi na meno!!"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom