'Akina Mzee Mwanakijiji' ni wavivu kufikiri

Haiwezekani chama ambacho kinajinadi ndio chama mbadala na chama kinachojinadi kuchukua uongozi wa nchi 2015 ..lakini uchaguzi mdogo tu wa madiwani viti 29 kinapata viti 5 na huku kampeni zake zimefanywa na viongozi wa kitaifa kina babu slaa,mbowe.
Mi napata tabu sana na hiki chama
 
ww unaonekana ni miongoni mwa watu wanaoleta hapa hoja dhaifu na kusahau kuwa hili ni jukwaa la gt, sasa mwenzio kakupatia dondoo unazopaswa kuzijibu kwa ushahidi makini, bila hivyo usiendelee kupost hoja dhaifu kuhusu CDM kutochukua dola 2015. hivi nikuulize unajua matokeo halisi ya uchaguzi wa 2010. hekima ni kuwa kama hujui omba kuelimishwa utafaidika kuliko kujifanya unajua kila kitu

wewe kama unajua si ubandike; mnayouliza leo wenzenu tulishayafanya miaka imeshapita. Mngekuwa siyo wavivu wa kutumia kitufye cha "search" mngejikuta mmeshapata majibu!
 
sina uhakika na anayetumia user name ya Mzee Mwanakijiji kwa kipindi cha kama wiki tatu hivi!

Oh ni mimi ndugu yangu wala usiwe na shaka; watu wakileta hoja watajibiwa kwa hoja; wakileta vioja watajibiwa kwa vioja. Kuna watu wanataka tuitendee CDM kama mwali fulani hivi. Wana mapenzi ya ajabu kwa chama badala ya kanuni kiasi kwamba mtu akikosoa CDM tu mishipa inawatoka wanaona kama tunaiharibia hawaoni kuwa tunaisaidia sana. Wengine wangependa ukosoaji wa CDM ufanyike sirini lakini wa CCM ufanyike hadharani. CDM ni kama chama kingine cha kisiasa; inataka kushika madaraka.

Tatizo ni kuwa madaraka yana tabia mbaya sana kwa wanaoyataka; yana tabia ya kuwaharibu. Kuna watu wanafikiria CDMM wakiingia madarakani hawatoharibiwa. Tayari tumeshaona dalili za baadhi ya watu ndani ya CDM kuharibiwa vibaya sana na tumadaraka tudogo waliko nako hadi inaudhi wakipata na vyombo vya dola watakuwaje.
 
Torture numbers, and they'll confess to anything - G. Easterbrook

Wakuu nadhani hapa tatizo letu ni kuwa mediocre..

Ni kweli Chadema imefanya vyema kuliko miaka ya nyuma.., lakini all in all imefanya vibaya kwa Chama kinachotaka kuchukua nchi 2015...., Now je mtaridhika 2015 mkishindwa kwa 0.5% ?

Tuache kuwa mediocre and lets strive for the best...; Lets not settle for less...
 
Torture numbers, and they'll confess to anything. ~Gregg Easterbrook

of course wataridhika; watasema walikuwa na 0.1 mwaka 2010 na 2015wana 0.5... watakuambia ni ongezeko la asilimia.... na hivyo watasema wajiandae kwa 2020
 
sasa nani ni mvivu wa kufikiri? kama wewe unazo majibu ya hayo maswali yaweke hapa siyo utake wengine wakufanyie kazi halafu wewe uje kuchambua! Ili kuonesha kuwa hoja zako ni dhaifu fanya hii kazi wewe mwenyewe, tuwekee matokeo ya uchunguzi wako halafu watu wachambue kuona kama yana ukweli au yanakubaliana na ukweli au mantiki. Vinginevyo, uvivu wetu sisi wengine kufikiri una uwezo zaidi kuliko ujasiri wa kutupuuzia.

Ili kukusaidia, majibu ya maswali yote hayo unaweza kuyapata kwenye Tovuti ya Tume ya Uchaguzi ya Taifa.

...dah!...hapa kisu kimegonga mfupa...je huu ndo mliowake?...
 
hoja ipo sana tu!mwenzetu katoa changamoto,hata kama hana data ni vyema wale waliobobea katika chambuzi za siasa zetu mkamuwekea hizo data na kupangua hoja yake.mleta mada anaamini wakongwe mnazo data anazphitaji,msaidieni basi!

sasa kama hana data anaweza vipi kusema wengine tuna uvivu wa kufikiri. Angekuwa ameweka data na kuzinyambulisha tungeziangalia na kuanza kuzitorture...
 
Lazy mind bwana... If you want to hide something from a black man, put it in writing or numbers... What's so hard with you finding the respective data and present it here instead unaita wenzio WAVIVU wa kufikiri?! Does taking ready-made data from an identified source require thinking?!
 
Kuna watu wanataka tuitendee CDM kama mwali fulani hivi. Wana mapenzi ya ajabu kwa chama badala ya kanuni kiasi kwamba mtu akikosoa CDM tu mishipa inawatoka wanaona kama tunaiharibia hawaoni kuwa tunaisaidia sana. Wengine wangependa ukosoaji wa CDM ufanyike sirini lakini wa CCM ufanyike hadharani. CDM ni kama chama kingine cha kisiasa; inataka kushika madaraka.

Kaka hapo umenena, asante sana!!
 
Watanzania Mungu ametujalia utamaduni wa pekee na wa ajabu sana,kukosoa/kushauri ni utovu wa nidhamu na dhambi pia,ata kama unaona kabisa hii ni mbili ili kuwafurahisha wakubalie kuwa ni tano watakusifu sana wakati kamwe ile mbili itabaki vile vile,katika vyama vya siasa vyetu mapungufu ni mengi sana lakini hayafanyiwi kazi,mtu akiona tatizo na kuliweka atashambuliwa utafikiri kakojolea msaafu.
 
Haa ha haa!! Duh! We ni noma!! Bonge la GT!!

Btw, ni busara ndogo sana inipasayo kuitumia kukujibu!!

Nasubiri data kiongozi!!

ukisubiri kutoka kwangu utachoka hadi miguu ionde magamba; muulize mleta mada alete data tuzijadili tumuoneshe kama kweli ni wavivu wa kufikiri.
 
Oh ni mimi ndugu yangu wala usiwe na shaka; watu wakileta hoja watajibiwa kwa hoja; wakileta vioja watajibiwa kwa vioja. Kuna watu wanataka tuitendee CDM kama mwali fulani hivi. Wana mapenzi ya ajabu kwa chama badala ya kanuni kiasi kwamba mtu akikosoa CDM tu mishipa inawatoka wanaona kama tunaiharibia hawaoni kuwa tunaisaidia sana. Wengine wangependa ukosoaji wa CDM ufanyike sirini lakini wa CCM ufanyike hadharani. CDM ni kama chama kingine cha kisiasa; inataka kushika madaraka.

Tatizo ni kuwa madaraka yana tabia mbaya sana kwa wanaoyataka; yana tabia ya kuwaharibu. Kuna watu wanafikiria CDMM wakiingia madarakani hawatoharibiwa. Tayari tumeshaona dalili za baadhi ya watu ndani ya CDM kuharibiwa vibaya sana na tumadaraka tudogo waliko nako hadi inaudhi wakipata na vyombo vya dola watakuwaje.

naelewa na ninaheshimu maoni na busara zako kwa chadema na watanzania kwa ujumla.hata mimi natambua chadema kama iliivyo chama kingine cha siasa inahitaji kukosolewa sasa na baadae.natambua tabia ya wanasiasa ni ile ile.

Lakini naamani unatambua ni wakati gani wa kutoa maoni gani ,kwa lengo gani na kwa faida gani na ya nani na hadhira ipi?

Tukubaliane kuwa kama kweli tumedhamiria kuleta mabadiliko ni lazima tuchague kuusadia upande unaotaka mabadiliko.hatuwezi kuusaidia upande huo kwa kutoa maoni ya kuumiza na kusaidia adui huko ni kumpa nguvu adui.kwa maneno mengine tusilazimishe mtoto kwa kumpa matonge ya ugali(ndani ya mwezi mmoja) huku anatakiwa aendelee kunyonya kisa anatakiwa kula ugali baada ya miezi sita.
Kimsingi tumuwekee lengo la kula ugali ndani ya miezi sita huku tukimzoesha uji,matonge madogo madogo na hatimaye matonge makubwa.
Unachojaribu au ulichajaribu kufanya ni kumpa mtoto huyu ugali mkubwa na unataka aanze kuumeza from day 1 to six months!ili uweze kunyanyua kilo 100 ni lazima uanzie kumi!

Nasisitiza lengo la cdm kushika nchi ni 2015 leo wamenyanga'nya tatu kesho wayanyanga'nya kumi lakini 2015 ni lazima wafikie lengo.

Sio wakati wa Maoni ya kuwalaumu viongozi wa chadema na kuona wameshindwa ndio maana reaction ya watu hapa jamvini imekuwa kali dhidi yako.

Nadhani wewe(stand to correction) ni mmoja wa walioshauri cdm ipeleke nguvu zake mikoani na vijijini,chadema ilisikia na leo imepata matokeo haya,sasa unayabeza tukuelewe/tuwaelewe vipi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom