Ajali ya kutisha: Zaidi ya watu 40 wahofiwa poteza maisha!

Kwa hali halisi ya bas jinsi linavyoonekana ni vigumu kujua ni basi gani. Kwa walio kuwa karibu na eneo la tukio watatupa habari kamili
 
moto ulikuwa ni mkubwa ajabu nimeshuhudia kwa jirani aliyebahatika kupiga picha
 
Oooh my God! I now start being so curious that there could be SATANIC WORSHIP in our country.



25th October 2011 18:15 shabibiby.jpg

Umeona eeh. Freemason hao wako kazin kwa ushirika wa ccm. Watanyonya mpaka tukome
 
hapa napata wakati mgumu, nasikia tyre ilipasuka sasa basi lilichukua muda gani mpaka kusimama na moto kuanza kuwaka au lilipinduka na kulipuka ghafla? mpaka watu washindwe hata kutokea dirishani?

may god rest you all in peace. Amen.
 
Sijui ni chombo gani hasa kinahusika na utoaji wa leseni kwa magari ya abiria. Hicho chombo/taasisi ni ya kupelekwa mahakamani ili waeleze wanatumia vigezo gani kutoa leseni kwa mabasi mabovu kama haya. Yapo mengi mengi tu na mengine wanachakachua body & engine ili mradi linatembea lakini mwisho wa siku ni kuzika watu. Kwenye hii ajali sijui hata kama miili itatambulika bila DNA. RIP na poleni wafiwa.
 
Wakuu nasikia basi la deluxe limeanguka na kuwaka moto maeneo ya misugusugu mkoani pwani na kuua watu zaidi ya 21. Source: ni channel 10-habari
 
Jana Sumry,
Leo Shabiby,
Kesho nani sijui!!!
Hapa kuna kitu, hii nchi inahitaji kiongozi mmoja mkubwa tu atolewe kafara ndio haya majanga yatapungua!!!
 
Tatizo ya hizi ajali ni kwa wale tuliowapa dhamana kuiendesha hii nchi, wanaruhusu rushwa, wanaingiza nchini na kuhalalisha bidhaa feki yakiwemo matairi yasiyokidhi na kulingana na barabara zetu pamoja na mazingira ili maradi waboreshe maisha yao na familia zao.
Ndugu zangu Watanzania tutakwisha na hizi Ajali. Usiku si Mchana ni ajali, nimeshuhudia kila wakati Jeshi la Polisi (police traffic) mnapokea rushwa kwa ajili ya umaskini wenu na tamaa ambazo zinagharimu maisha ya watanzania wengi. R.I.P wote mliotutoka ktk ajali hii.
 
Nilishasema hapo siku za nyuma kuwa ajali hizi haziwezi kuzuilika lakini tunaweza kuzuia maafa yatokanayo na ajali hizi. Kwa mfano, bus kupasuka tairi hutokea mara nyingi katika nchi nyingine pia, lakini huwezi kusikia kuwa basi linapinduka na kuua watu na kama hili limeshatokea ni mara chache. Je, ni kwa nini hakuna maafa kwa wenzetu? Madereva wanaendesha mwendo ambao kama kuna dharura wanaweza ku-control bus na kuepusha maafa. Madereva wa mabasi yetu haya hawayafikirii kabisa. Poleni wajeruhiwa na Mungu awapumzishe mahali pema peponi waliopoteza maisha yao.
 
Back
Top Bottom