Ajali ya kutisha: Zaidi ya watu 40 wahofiwa poteza maisha!

Wajameni ni vp naweza kuweka hzo pcha humu kwa kutumia simu? Ninazo picha za ajali ya hlo bus ila nashndwa kuziweka humu.. Msaada wenu unahtajika.
 
Hii inasikitisha, ukiangalia kwamba ajali Tanzania zinaweza kuzuiliwa tunaweza kuokoa maisha ya watu kwa kutumia mabasi yenye ubora nchini. Uwekezaji katika usafiri unasababisha wamiliki wa mabasi kuagiza mabasi ya bei ya chini na kuajiri madereva ambao hawana uzoefu.

Kipindi usafiri ulivyokuwa unamilikiwa na serikali miaka ya 1970 ni nadra kuona mabasi ambayo hayana ubora barabarani.
 
Which is which jamani, ni gari ya Shabiby au Deluxe? Plz tujuzeni vzr. R.I.P wahanga wote.

Mi mwenyewe wananichanganya jana TBC1 taarifa ya habari wamesema Delux rafiki yangu kanitaarifu shabib so which is which?
 
inasikitisha sana kupoteza ndugu zetu wengi kwa uzembe wa mtu mmoja.
pole sana kwa wafiwa, na majeruhi Mungu awasaidie wapone haraka.
 
Nilibahatika kupita eneo la ajali majira ya saa moja na nusu jioni leo.....hakika hali inatisha, Bus limeteketea kabisa...nimeshuhudia vijana wa maeneo jirani wakisomba mabati na vyuma vinavyobebeka kutoka kwenye Bus lililopata ajali huku wengine wakiendelea kung'oa mabati na kukongoa vyuma...imenisikitisha..imenikera na imenichefua sana! Huu utamaduni wa kufa kufaana haufai..ni aibu!

Nimejiuliza maswali mengi kuhusu wepesi wa mamlaka za uokoaji katika hali kama hii...hivi tuna helikopta hata moja ya uokoaji? Tuna helikopta hata moja ya kusaidia kuzima moto? Nini vipaumbele vya nchi yetu?sherehe tu? Ziara za nje za viongozi? Au ununuzi wa vifaa vya kukandamiza demokrasia?

Tuache kukaa kama maboya, tufikirie namna ya kujenga mazingira ya kupunguza vifo katika ajali kama hii ya leo, inawezekana tukiacha uvivu wa kufikiri!

na ingekuwa ni kampeni za uchaguzi viongozi wote wa serikali na helkopta wangehamia
 
Naona na hili ni janga la kipekee la taifa. Nina wasiwasi basi hili lilibebe petroli. Haiwezekeni gari ya dizeli iteketee kwa muda mfupi. Serikali ina nyenzo zote. Sasa mabasi yote ya abiria yazianze safari bila ya ukaguzi na udhibitisho wa ukaguzi huo. Askari wote wa barabarani wafanye kazi na wenye vitambi wapewe meza za kufanyia kazi kama kuwafukuza itakuwa tabu.
 
Yah, nimesikia hii ajali toka redio ya clouds FM. Kuna jamaa alikuwa anaripoti live akiwa eneo la tukio. Pole sana kwa waliopata ajali na ndugu na jamaa zao!
Hii radio sio tena ya kuburudisha?
Taarifa zao zinatangulia kuliko za radio station zenye majukum zaid yao! Tbc radio vip?
 
Nimeckia mda mfupi kutoka radio free kwny kipind cha darubini ya leo kuwa watu walikua km 65 na walookolewa ni km 15,walobak wote wameteketea kwa moto.polen sana wafiwa kwa msiba huu mkubwa,Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema peponi amina.
Innalillahi wainna ilayhi rajiuun.
Poleni wafiwa.
Uchungu waujua nyie kwa ndugu na jamaa zenu.
Nasi tupo pamoja nanyi...wenye nafsi za huruma.
 
Mie mbona sielewi idadi kamili ya waliopoteza maisha,kuna taarifa za kuchanganya kidogo kuwa waliopelekwa hospitali ni majeruhi 36 wameruhusiwa 35 amebaki 1.waliofariki ni 5 watatu ndio afadhali hawakuungua sana hao 2 hawatambuliki ni majivu.walioshuhudia ajali wanasema polisi waliweza kupata majeruhi si zaidi ya 10 kwenye tukio.hiyo idadi ya 36 ilitokea wapi? Mara wengine waliruhusiwa kurudi makwao leo mkuu wa mkoa anaomba watu walewale walioruhusiwa wakatoe taarifa kwenye vituo vya police kwani hawakuchukuliwa taarifa kabla ya kuruhusiwa?inaonekana idadi kubwa ya watu imeteketea.kunanini cha kuficha hapo hebu wawe wazi tujue moja
 
Nilibahatika kupita eneo la ajali majira ya saa moja na nusu jioni leo.....hakika hali inatisha, Bus limeteketea kabisa...nimeshuhudia vijana wa maeneo jirani wakisomba mabati na vyuma vinavyobebeka kutoka kwenye Bus lililopata ajali huku wengine wakiendelea kung'oa mabati na kukongoa vyuma...imenisikitisha..imenikera na imenichefua sana! Huu utamaduni wa kufa kufaana haufai..ni aibu!

Nimejiuliza maswali mengi kuhusu wepesi wa mamlaka za uokoaji katika hali kama hii...
hivi tuna helikopta hata moja ya uokoaji? Tuna helikopta hata moja ya kusaidia kuzima moto? Nini vipaumbele vya nchi yetu?sherehe tu? Ziara za nje za viongozi? Au ununuzi wa vifaa vya kukandamiza demokrasia?

Tuache kukaa kama maboya, tufikirie namna ya kujenga mazingira ya kupunguza vifo katika ajali kama hii ya leo, inawezekana tukiacha uvivu wa kufikiri!
Mkuu unaulizia Helicopter kwani kuna uchaguzi mdogo sehemu?? au EL keshavua nae Gamba?
 
Back
Top Bottom