AJABU: Chenge aitetea DOWANS ilipwe!

Mafisadi wa kizalendo wasamehewe na wapewe nafasi ya kutubu, mbona wa kihindi wanapeta? kwa sababu wanatoa zawadi nono kwa wakubwa? au wanalindwa na serikali za countries of origin? ndio maana wana passport zaidi ya 3
 
Chenge kaombwa ushauri, mlitaka adanganye? Mna nini nyinyi? Khaaa, mnashangaza.

Mtu aliyetumwa utamfahamu tu we cheki

Join Date : 9th May 2011
Posts : 537
Thanks81Thanked 32 Times in 29 Posts

Rep Power : 22

Umekuwa na chungu ghafla, fedha uliyopewa ikiisha tu basi. Wenye akili wamekushtukia long time utakuwa unaongea kitu wanakucheki wala hakuna atakayepoteza muda na wewe
 
Mtu aliyetumwa utamfahamu tu we cheki

Join Date : 9th May 2011
Posts : 537
Thanks81Thanked 32 Times in 29 Posts

Rep Power : 22

Umekuwa na chungu ghafla, fedha uliyopewa ikiisha tu basi. Wenye akili wamekushtukia long time utakuwa unaongea kitu wanakucheki wala hakuna atakayepoteza muda na wewe
Ni kweli wametumwa JF na sidhani kama ni sawa kuwasamehe!
Pamoja na waTZ kupelekwa utumwani na masaibu mengine, miaka 50 baada ya uhuru tunashuhudia kizazi kisicho na uchungu na utumiaji mzuri wa akili kikizidi kuongezeka! Very sad!!! Wasiwasi wangu ninajaribu kuangalia miaka 50 ijayo, tusijeona ajabu miti na wanyama wakaonekana kuwa na akili zaidi ya "WADANGANYIKA".
Acheni mashihara jamani, amkeni! Mzee Chenge si raia tena anayestahili kutoa ushauri kama huo, maana amepewa zaidi ya miaka 10 (1/5 ya uhuru wetu) kufanya kazi ya uanasheria mkuu na inaelekea dhamira yake haikumtuma kutumikia mamilioni ya Watanzania bali watu wachache tu! Ni bora akawaongelee hao hao aliowatumikia na sio sisi! KUKAA KIMYA PIA NI USTAARABU badala ya kutonesha machungu!
Mungu "asimbariki" Mh. Chenge ....Mungu Ibariki Tanzania na Watanzania wote Wazalendo!
 
Kimsingi Dowans imeshinda kesi kihalali kutokana na weakness za contract baina ya TANESCO nao

The fact kuwa sheria iliyotumika kubomoa hoja za TANESCO ya PPRA haikuwa na mshiko kwenye ICC what Chenge is reminding us all ni kuwa, ametuingiza kwenye kusaini mikataba ambayo dispute ikitokea hawaamini mahakama zetu...kumbuka Dowans walivunja mkataba baada ya kupokea letter of intent iliyotoa notice from TANESCo ya kusitisha, ambayo kimkataba ni halali kwa pande zote kufanya hivyo...

Madai wanayoidai TANESCO ni malimbikizo ya capacity charges etc etc...sasa since Chenge ndie aliyedesign na kudraft hizo int legal jargons....he's also poised to challenge everything in his mighty breath provided his party is dropping him like hot potatoes, his big frigging ego is spreading even to issues which will crash the nation's coffers..he might be right..but does he really care?? His fat swiss account is bulging with money he had plundered all along...

Have mercy Chenge O'mighty!
 
Kuna jopo la wanasheria wa CCM waliojitolea kuitetea Serikali ndidi ya mzigo huu wakiongozwa na Mh. Nimrodi Mkono; ina maana Mh. Chenge hakuwa mmoja wa hilo jopo?

Kwa kumteua huyo Mkono kuongoza hilo jopo la wanasheria wa ccm ili waisaidie nchi iepukane na hilo deni la Dowans ni sawa na kumuachia nyani shamba la mahindi!! Inaelekea tunasahau kuwa Mkono pia alikuwemo kwenya list ya Dr. Slaa ya mafisadi wanaoihujumu nchi!!
 
Kwa kumteua huyo Mkono kuongoza hilo jopo la wanasheria wa ccm ili waisaidie nchi iepukane na hilo deni la Dowans ni sawa na kumuachia nyani shamba la mahindi!! Inaelekea tunasahau kuwa Mkono pia alikuwemo kwenya list ya Dr. Slaa ya mafisadi wanaoihujumu nchi!!

Mkono ndie anaemtetea Jeetu Patel, na ameshafanikiwa na pia ana cheo cha juu kwenye Bank ya Jeetu Patel Bank M Limited, na eti imepewa jukumu la kukusanya kodi za taifa. ngoja aje simba wa kweli Lowassa, watashika adabu
 
Nakumbuka Bunge lililopita, Mbunge mpya kwa tiketi ya cdm, Tundu Lissu, alipokuwa anajitafutia umaarufu Bungeni kwa kufanya u"tundu" na kuzua malumbano kwa kila hoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, alisimama Chenge na kumpa Tundu hoja moja tuu ya kisheria ambayo ilimfanya Tundu kuwacha utundu wake wa kulumbana, kwani kwa pale ilidhihirika wazi kuwa Tundu ni katoto kwa Chenge kisheria. Nani anaekumbuka?

Kwa mantiki hiyo, ikiwa Chenge kasema fedha ya Dowans walipwe, basi ujuwe kaiona sheria kwa jicho la wazi na anajuwa kutokuwalipa Dowans kunaweza kuleta utata zaidi na kuliingiza Taifa kwenye utata zaidi, Jee, inawezekana kuwa hata Symbion hawatakubali kulipia mitambo ambayo bado ina deni?

Mwanasheria yoyote makini whether Chenge or not atakuambia kisheria hatuna ujanja. Kisheria deni lazima lilipwe. Imetokea tuu bahati mbaya aliyetoa huo ushauri ni Chenge, lakini kisheria nakubaliana na ushauri aliotoa japokuwa sijaelewa ametoa in what capacity. Kwa mfano, Tanesco wanapinga mahakama ya ICC kutumia sheria za Texas kwenye maamuzi yake. Lakini kwenye mkataba kati ya Tanesco na Dowans walikubaliana kuwa in case of any dispute sheria za Texas zitatumika. Sasa how come Tanesco wanahoji uhalali wa kuzitumia sheria hizo? Kusema kweli, hoja ya Tanesco ya kuhoji maamuzi yaliyofikiwa kwa kutumia sheria za Texas haina mashiko.

Pia kuna masuala ya ushahidi ambayo Tanesco inalalamikia. Lakini sidhani kama Mahakama itaweza kupokea ushahidi mpya. Suala la ushahidi ni la ushahidi na mahakama haina uwezo wa kisheria kuingilia. Suala tusilipe kwa sababu za public interests, halina mshiko. Tumelijadili sana hii issue kwenye jukwaa la sheria. Kusema kweli sheria inatubana. Tulisaini na kukubaliana na terms za ule mkataba. Kama tulisaini mkataba mbovu then, tutavuna tulichopanda. Ukipanda kokoto usitegemee kuvuna mahindi.

Kuna watu wanauliza wapi uzalendo wa viongozi kwa Taifa lao. At the same time utakuta hawa hawa ndio wanaodai utawala wa sheria. Linapokuja suala la uzalendo na sheria, the former should prevail. Wangeonyesha uzalendo kabla ya kusaini mikataba mibovu not after. Suala la Symbion na kesi ya Dowans ni gumu kulijua unless tupate mkataba wa mauzo.
 
Huyu Baba ni Mtanzania kweli?
Paul huyu ni Mtanzania kweli lakini naungana nawewe kuwa na mshaka na utanzania wake inawezekana alisha ukana huo uraia wake na sasa ni mtu wa Saudia kwa Alli Hadaiwi, haiwezekani kwa mzalendo wa kweli kufanya haya anayoyafanya Andrew John Chenge.
"Chenge tugwililage ng'holo abatanzania tuleluha!"
 
Huyu jamaa wa vijisenti mwizi halafu ana dharau sana, dawa yake siku akishuka Kariakoo kumpigia kelele za mwizi mwizi halafu apate kisago cha angry mob kama kibaka na polisi wakichelewa avishwe tairi.......(maliza mwenyewe!) moto!
 
Nakumbuka Bunge lililopita, Mbunge mpya kwa tiketi ya cdm, Tundu Lissu, alipokuwa anajitafutia umaarufu Bungeni kwa kufanya u"tundu" na kuzua malumbano kwa kila hoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, alisimama Chenge na kumpa Tundu hoja moja tuu ya kisheria ambayo ilimfanya Tundu kuwacha utundu wake wa kulumbana, kwani kwa pale ilidhihirika wazi kuwa Tundu ni katoto kwa Chenge kisheria. Nani anaekumbuka?

Kwa mantiki hiyo, ikiwa Chenge kasema fedha ya Dowans walipwe, basi ujuwe kaiona sheria kwa jicho la wazi na anajuwa kutokuwalipa Dowans kunaweza kuleta utata zaidi na kuliingiza Taifa kwenye utata zaidi, Jee, inawezekana kuwa hata Symbion hawatakubali kulipia mitambo ambayo bado ina deni?

Du, kweli Taznaia tuna vila za wengi. Poa Faizah, sikutegemea kama Pesa ya huyu jamaa unaitafuana.
 
Tatizo ni kwamba Sehemu ambayo akili inapaswa kuingilia Umeifunika. Nenda kavue huo ujinga kwanza ndipo ubongo wako ufunguke na kuchangia points zenye akili. Nyau we!!
Matusi na kashfa ya nini kiongozi? au ndio uoenekane unauchungu sana wa nchi hii,tumia busara walau kidogo ili uonekane una akili timamu za kiungwana huna haja ya kutukana mawazo ya mtu.
 
U wapi uzalendo wa viongozi kwa Taifa lao.,bila hata aibu unaisaidia kampuni 'inayoidai' serikali unayoitumikia ili iweje?.Nilitegemea angesaidia serikali na nchi yake isiingie au jinsi ya kujitoa katika katika migogoro ya kisheria...

Kwani maana ya uzalendo ni usisaidie kampuni zinazoidai serikali unayoitumikia? Au huoni kuwa mkweli na kutenda haki ndio kuisaidia serikali unayoitumikia?

Watu wenye fikra kama zako ndio wanao-uwa hii nchi kwa kudhani tu wanaisaidia.
 
Mbona Mende ana wadai waingereza wamrudishie chenji Chenge aliyo isahau BAE? Umelogwa kuichukia Tanzania wewe, siyo bure!

Mwenye kuipenda Tanzania hatotaka kudhulumu kwa sababu ati anaipenda Tanzania. Kuipenda Tanzania uwe mkweli na utende haki kila panapo stahiki.

NB. Umelogwa = Umerogwa.
 
Du, kweli Taznaia tuna vila za wengi. Poa Faizah, sikutegemea kama Pesa ya huyu jamaa unaitafuana.

Kwanza kajifundushe kuandika na kusoma kisha ndio uje hapa kutaka kulumbana na hoja. Hicho ulicho kiandika unakielewa?
 
Mtu aliyetumwa utamfahamu tu we cheki

Join Date : 9th May 2011
Posts : 537
Thanks81Thanked 32 Times in 29 Posts

Rep Power : 22

Umekuwa na chungu ghafla, fedha uliyopewa ikiisha tu basi. Wenye akili wamekushtukia long time utakuwa unaongea kitu wanakucheki wala hakuna atakayepoteza muda na wewe

Hizo tarehe zisikutishe waulize ma mods, sisi wengine tupo JF toka enzi za Jambo. una nini wewe?
 
Chenge amesoma jengo moja na Obama, HARVARD, chuo baba wa dunia, huyu tungemchukua tukampa TAKUKURU aiendeshe, tutawanyonga wangapi? basi tuanze na Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Karume na wote, nina uhakika asilimia 100 viongozi wetu wameiba japo mara 3 kila mmoja, ok Chenge amepokea asante ya dola mil 1, tunamsumbua, na Jeetu Patel amechota Billioni 400 za BOT na sehemu ya pesa hiyo ndio imeanzisha bank yake ya M, huyu anatetewa na Nimrod Mkono ndugu yake Mwalimu Nyerere, sasa fisadi ni nani? jamani mi kichwa kinanizunguuka tu. Chenge amenuna sasa apewe TAKUKURU amalizie hasira zake lakini tujue hatapatikana wa kuongoza nchi

Chenge hana haja yakununua TAKURURU, Chenge ndio aliyempigia ndogo ndogo HOSEA kwenye hiyo nafasi akatolewa uhakimu akawekwa TAKURURU. Sijui kama ni blood relation au mzizi wa uhusiano wao uko wapi; lakini ni wakabila moja. So huu mtandao uliwekwa tayari mapema mno.
 
Chenge asaidia Dowans ilipwe

Na Waandishi wetu
1st June 2011

headline_bullet.jpg
Awasilisha ushauri mkali wa kisheria Uingereza
headline_bullet.jpg
Asema kesi ya kupinga tuzo nchini haina nguvu


Chenge1%2831%29.jpg

Mwanasheria Mkuu wa zamani wa serikali, Andrew Chenge

Mwanasheria Mkuu wa zamani wa serikali, Andrew Chenge, ameamua kuitetea kampuni ya Dowans ilipwe na serikali ya Tanzania Sh. bilioni 94 kama ilivyoamriwa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro (ICC).

Chenge ametoa utetezi kwa niaba ya mlalamikaji kwenye shauri la usuluhishi kati ya walalamikaji wawili ambao ni Dowans Holdings SA akiwa ni mlalamikaji wa kwanza na Dowans Tanzania Limited mlalamikaji wa pili dhidi ya Kampuni ya Umeme nchini (Tanesco) ambaye ndiye mdaiwa.

Mbali ya kuwa mwanasheria mkuu wa serikali, Chenge pia amekuwa waziri katika serikali ya awamu ya nne, akianzia Ushirikiano wa Kimataifa, kisha Ujenzi (wakati huo Miundombinu) ambako alijiuzulu kwa sababu ya sakata la rada.

Katika sakata la rada, Chenge alikuwa mtuhumiwa muhimu, na sakata hili liliisha kwa Kampuni ya BAE ya Uingereza kukubali kulipa fidia kwa uzembe wa kuweka kumbukumbu, na kukwepa kigingi cha rushwa.

Katika maelezo ya Chenge ambayo yameelezwa kuwa ni ushauri wa kitaalam, uliotolewa kwa maandishi Mei 6, mwaka huu katika Mahakama Kuu ya Uingereza, kitengo cha Biashara unalenga kuhalalisha malipo ya tuzo kwa kampuni ya Dowans iliyoamriwa kulipwa na ICC.

Katika maelezo yake hayo yanayorejewa kuwa ni ‘Ripoti ya kitaalamu ya Andrew Chenge', anaanza utangulizi wake kwa kueleza kuwa yeye ni Andrew Chenge anayeishi katika kiwanja namba 240, Nyumba namba 546, Barabara ya Ghuba, eneo la Oysterbay jijini Dar es Salaam Tanzania Anaendelea kueleza katika maelezo yake kuwa, anatoa maelezo hayo kufuatia ombi la Stephenson Harvard, wakili wa walalamikaji na katika kuitikia barua yao ya Aprili 15, mwaka huu ambayo bila ya viambatanisho vyake imenakiliwa kama ushahidi namba "AJC 1"

Aliendelea kueleza kuwa alipata Shahada yake ya Sheria (LLB) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1972.

Alisema baada ya hapo alijiunga na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali na baada ya hapo kwa muda wa miaka minne alikwenda Harvard Marekani, Benki ya Dunia na katika kazi za kibinafsi, kisha alirejea kwenye idara ya sheria za kiraia na za kimataifa iliyokuwa katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali mwaka 1978.

Chenge alisema aliteuliwa kuwa Mwanasheria Mwandamizi wa serikali mwaka 1988 na Naibu Mwanasheria Mkuu na Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria mwaka 1991.

Alisema aliteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa serikali ya Tanzania mwaka 1993 ambapo alishikilia nafasi hiyo hadi Desemba mwaka 2005. Alisema alichaguliwa kuwa Mbunge wa Bariadi Magharibi mwaka 2005 na hadi leo anaendelea kuishikilia nafasi hiyo.

Alisema nakala ya wasifu wake (CV) imetolewa kama kielelezo "AJC2"

"Sasa nitashughulika na hoja na maswali yaliyojitokeza kwenye barua ya Stephenson Harwood. Ninaitoa katika kielelezo"AJC3" taarifa ambayo nimeirejea katika ripoti yangu hii ambayo marejeo yake katika namba za kurasa kwenye AJC 3 zimekolezwa," anasema Chenge.

Katika maelezo yake ya utetezi ya kuzifafanua hoja na maswali yaliyojitokeza katika barua waliomwandikia walalamikaji, Chenge ameangalia ‘utawala wa kisheria wa kuipinga tuzo iliyotolewa katika Mahakama za Tanzania' akiitumia sheria ya usuluhishi ya mwaka 2002.

Alisema pamoja na vifungu vyote vilivyoondolewa, vilivyorejewa na vilivyorekebishwa kuhusiana na suala linalohusu tuzo, kanuni ambazo bado zipo lazima zisomwe pamoja na sheria ya usuluhishi ya mwaka 2002 ambapo nakala ya sheria hiyo na kanuni za usuluhishi za Tanzania za mwaka 1957 anaeleza kuziambatanisha.

Chenge alisema sababu pekee zinazoweza kuifanya tuzo hiyo ikapingwa zimeelezwa katika sheria hiyo ya mwaka 2002 na hasa katika kifungu cha 16 ambacho kinaruhusu tuzo kupingwa ikiwa tu limetolewa kutokana na mwenendo mbaya au kama imepatikana isivyo kihalali.

Alisema chini ya kifungu cha 15, tuzo inaweza kurudishwa kwa ajili ya masahihisho katika mahakama iliyotoa maamuzi hayo.

Akizungumzia namna ya kuipinga hukumu ya tuzo chini ya kutolewa kwa mwenendo mbaya (misconduct), Chenge alisema neno hilo halikutolewa maana yake kwenye sheria ya usuluhishi ya mwaka 2002 na kwamba hakuna mamlaka yoyote Tanzania ambayo imetafsiri neno hilo na kwamba kwa maoni
yake mahakama za Tanzania zitaliangalia suala hilo kwa ufinyu na kutilia mkazo kama mahakama au mjumbe wake hakutenda haki au isivyo sawa.

Baada ya hapo, Chenge alizungumzia pingamizi dhidi ya tuzo lililowasilishwa na Tanesco na wadau wengine na hasa maswali manne yaliyotolewa katika aya ya 10 iliyotolewa kama kilelezo "AJC 1"

Alisema kwa kuangalia alichopewa yeye, pande hizo mbili katika mgogoro huo zilikubaliana kutumia sheria za Texas katika mgogoro wao na kwamba wakati wanakubaliana Tanesco hawakuhoji uhalali wa kuzitumia sheria hizo, hivyo anaona hoja ya Tanesco ya kuhoji maamuzi yaliyofikiwa kwa kutumia sheria za Texas haina mashiko.

Akizungumzia aya ya sita ya pingamizi la Tanesco, Chenge alisema kwamba ' inaonekana aya hiyo inakubaliana na maoni yake kwamba kinachounda mwenendo mbaya ni mapungufu ya taratibu za haki. "Kwa hiyo siamini kama sababu hizo 11 walizotoa zinaunda mwenendo mbaya."

Akizungumzia pingamizi la Tanesco la aya ya tisa lisemalo kwamba tuzo iliyotolewa ina makosa kisheria katika macho ya kumbukumbu, Chenge alisema hilo ni suala la ushahidi na si la sheria kwa msingi kwamba mahakama ina mamlaka ya kuingilia.

Alisema kesi ya D.P Shapriya imeshalifafanua vizuri sana suala hilo.

Alimalizia kwa kusema kwamba maoni yake kwa aya ya 10 ya pingamizi la Tanesco kwamba tozo iko kinyume cha sera ya umma haina nguvu ya kushinda kwa sababu zilizoelezwa katika aya ya 15.

NIPASHE ilimwuliza Chenge anajisikiaje anapotaka kuibana nchi yake ilipe kampuni hiyo ya kigeni na alijibu kuwa hawezi kuzungumzia mambo yasiyomhusu na alimtaka mwandishi kuendelea na shughuli zake.

"Nimesema siwezi kuzungumza masuala ambayo hayanihusu na naomba uendelee na shughuli zako inamaana hunielewi?" alisema Chenge kwa kifupi na kuhoji kisha akakata simu.


CHANZO: NIPASHE


that is where we can see the big nonsense most of Tanzanian's by using their professional's or whatever to ruin their own country either for their own sake of interest or whatever despite using their motherland identity for country protection in either case!....But all in always hii inasababishwa na sisi jamii kwani we still hanging around with him/them..at the same time we dare crying life is tough???"it sounds like waiting a soup from a cooked empty pot of beans''......cdm alone still nt enough turning things on the right truck..a big promo and support required in case we are serious don't like buying sukari 1,700-2,500/=and so on.....while inazalishwa hapo morogoro...!
advice if we won't take measures on the ground....we must realize and forget about development..!sometimes it's a shame to be called a Tanzanian..?we are so weak as our government for implying ni nchi ya amani...insteady is a poorest country?
No matter what you hold or reacher you are...someone will judge what you do with them for your nation..?
Pls may i submit...?
 
Back
Top Bottom