Ahsante mheshimiwa Zitto, lakini huyo ni mbuzi kwenye gunia!

Watu wengi nimegundua kuwa wanaingia kichwa kichwa kwenye hii issue. Kwanza lazima wajue kuwa hii issue siyo ya zitto ila zitto amevalia njungu (Mungu akubariki). Hii issue imekuwa inaongelewa na donors miaka nenda miaka rudi na ni moja ya chanzo cha utendaji mbovu serikalini. CCM na wabunge wake na wale wwanaofaidika na huu unyama always watapenda hii issue iendelee kwa sababu ina wagawa wafanyakazi na kufanya watawalike kirahisi na hawa manjangili.

Issue wenyewe: Hizi posho haramu (sitting allowance) amabzo zitto anazivalia njunga ni posho ambayo mfanyakazi wa serikali analipwa kwa kutekeleza wajibu amabao pia analipwa mshahara kwa mfano. Procurement officer amabye kazi yake ni kuhakikisha kuwa kuna manunuzi yenye tija katika idara yake analipwa posho kwa kukaa kwenye eavaluation board. Huyu procurement officer muda wake anaolipwa mshahara ni saa moja na nusu asubuhi mpaka saa kumi jioni. evaluation board ina kaa saa nne mpaka saa nane mchana, ndani ya muda wake wa kazi anaolipwa mshahara lakini anapewa tena posho. Hii pratice ya serikali inaleta mazara makubwa sana kwa utendaji serikalini na nchi kama kawaida kwa mfano
  • Kuna tija gani kwa daktari kwenda kufanya operation kwa mgonjwa ambako hapati allowance yoyote wakati akitafuta workshop ya customer care analipwa allowance na anaweza kuhudhuria workshop hizo kwa mara 5 kwa 3 years sababu posho haramu
  • Hizi posho zimeweza kutumiwa na serikali kuweza kuwa retain technical staff. Lakini ni kwamba baada ya kuacha ujamaa( mpango wa shetani kuwadanganya watu) salaries siku hizi zinategemea soko na hizi allowance aziwatendei haki wafanyakazi wa nchi hii kwa kuwa ina fanya mishahara iwe chini sana kwa Tanzania. Ukiwa unafanya kazi katika shirika ambalo lina ofisi nchi za kenya na uganda, ni watanzania ndiyo watakao lipwa kidogo kwa kuwa salary marjetyetu imefunikwa na hizi posho.
  • Watanzania wachache wanaolipwa hizi posho mara kwa mara il waendelee kuwepo kwenye hii circle wamekuwa wakiwaabudu viongozi wao ili kuwepo kwenye hii ciecle. kumbuka kuwa si wafanyakazi wote ambao wanafaidikia na hizi posho.
  • mabosi wamekuwa wanatumia hizi posho kama rushwa kwa nyumba ndogo kwa sabubu ni bosi anayetoa ruhusa kwenda kuhudhuria hivi vikao na workshop.

- Mkuu talking about kuingia kichwa kichwa na ishus, ungaeuliza kwanza poshoo za wabunge zilishinikizwa na nani huko nyuma, thenutagundua ni hao hao donors hasa the Scandnavians ambao toka int he 90s wamekua wakihaha sana kuona CCM inaondolewa kwenye power, they thought kwamba Mrema alikuwa na nguvu kubwa ya kuiondoa CCM walipolilia kuongezwa kwa hayo maposho kwa wabunge wapya na kumfanya Mrema Rais anayekubalika sana na wabunge, na infact ni wewe unayeingia kichwa kichwa na ishu kwa sababu, sio siri kwa maelezo yako hata huelewi nani hasa anatoa hizo hela za posho kwa Wabunge wetu, vipi ungeuliza kwanza kabla ya kuingia kichwa kichwa!

- CCM wanafadika na mfumo wetu wa utawala ambao ni rukhsa kwa chama chochote kinachoshinda uchaguzi, mfumo wa Winner takes all, lakini si mfumo uliotengenezwa kwa ajili ya CCM tu ni mawazo potofu sana!

William @ NYC, USA.
 
nimekushangaa sana leo...yanni nimekushaanga kweli kijana wangu..........nadhani huijua dhana nzima ya hizi posho........kulipana posho hakulirudishi taifa zama za ujamaa ala ujima....posho hizi kwa mbali zimekuwa na harufu ya wizi(kuwaibia wananch)....

wewe willy wacha nikuulize mbona mwl akiingia darasani halipwi posho? bali anasubiri mwisho wa mwezi!!!

wala usifikiri ni mtu kutafuta umaarufu hapa ili ni kuwa mzalendo zaid maana amekaa na kuinagalia namna ilivyo na kuona sio hakii na ndio maana hata jana lukuvi wakati anahojiwa na tbc alikiri kuwa kweli posho zinachukua sehmu kubwa ya pesa za walipa kodi........ hata wabunge wa ccm wenyewe baadh yao wanakiri na dhamira zinawasuta (soma wamananchi ya jana online)....jaribu kuelewa mantiki ya hoja kijana wangu

- Unasema ujira wa Waalimu uwe sawa na Viongozi wa taifa? Lukuvi amesema posho zinachkua kodi ya taifa toka lini posho za Wabunge zimelipwa na kodi zetu? Acha hoja wengine wanasema sema wewe unasema na mimi nitakujibu ninasema nini, sio Lukuvi wala wabunge wengine wa CCM, si Demokrasia mkuu kila mwananchi anakuwa na mawazo yake, kinachopimwa ni faida ya mawazo ya mwananchi sio mbona wengi wamesema! Pleaase!

William @ NYC, USA.
 
- Ningeelewa kama tungetaka wabunge wasiokuwa active katika kuwakilisha wananchi waliowachagua basi wawe wanapunguziwa ujira, labda ningeelewa, lakini kupunguza ujira eti ni mwingi sana, pleaase!

William @ NYC, USA.
nina wasiwasi na uelewa wako.kwanza posho si ujira,ujira ni mshahara ambao upo kwenye mfumo unaoeleweka.
hakuna mtu aliyesema ujira upunguzwe.labada akili yako ina shida kila aliyechangia hapa anapendekeza ujira uongezwwe ili posho ziondolewe.
najua umekula haramu mpaka unachanganya mambo.
posho=wizi
ujira=malipo yanayotokana na ajira kwa mujibu wa sheria yanayokatwa kodi na malipo ya shirika la hfadhi ya jamii,yanayo akisi malipo yako ya uzeeni.
 
Hivi mmeshagundua kwa nini viongozi wengi wanaoishi kwa hizi allowance, mara wakiacha kazi huwa wanakufa haraka?

Hii kitu inalemaza sana. Hizi pesa hata wake zao nyumbani hawazioni na ndiyo maana Dodoma imeshamiri UFUSKA.

Hizi pesa zinaongeza tu magonjwa ya ajabu na anasa pale Dodoma. Wengi sana wamelisema hili hapa JF.

Watu wanalalamika kuwa vikao vikianza, chunga sana Mkeo au Girlfriend wako.

Pia kwa sababu posho hazikatwi kodi, wafanyakazi huwa wanaishi maisha ya juu sana na siku akiacha kazi aanze kuzipwa hela za uzeeni, unakuta maisha yanawashinda kabisa. Na ndiyo maana wengi sana hufa within 5 years tangu waache kazi.

Mtani wangu Willy, acha kuendekeza hiki kilema kwa hawa watu. Acha miashahara ipande sana tu. Ikibidi Mbunge apate hata 5.M kwa mwezi na akiacha kazi, akiba yake itakuwa nono sana na ataendelea kuishi maisha karibu sana na aliyokuwa akiishi zamani.

Ndiyo maana unaona hata pesa za kutibiwa huwa hawana mara wakiacha kazi. Watu kama Mrema alikuwa kaishiwa kabisa maana watoto kibao. Kuna yule mama wa CCM alitokea kwenye magazeti akiwa hoi kitandani na huku hana hela ya kutibiwa. Mifano ipo mingi sana...... Hiki kilema unachotaka kiendelee, kinawauwa wao na kuliuwa Taifa kwa ujumla.

Ngoja siku ifike na Tanzania iwe kama Wagiriki. Wanakula zaidi ya wanavyozalisha............... Anytime watatangaza nchi IMEFILISIKA. Na sijui sasa hao wataalamu wako unaotaka walipwe sana tutaona kama wataendelea kubaki.....
 
@New York, USA
, naomba usiskip ili swali langu ningepependa unijibu kiufasaha.
1. kwa miaka hii 10 umewahi kukaa Tanzania kwa siku ngapi? ukijurimsha vizuri ushindwi kunipa jibu.
2. umejiridhisha kabisa unachokipinga ni kipi?
3. unakumbuka wakati wa mtikisiko wa uchumi diuniani Kansela wa Ujerumani aliamuru serikali yake ibane matumizi?
4. una nia ya kuja kugombea ubunge Tanzania? kama jibu ni ndio kwahiyo inakuuma ulaji unaanza kupunguzwa kabla ujaingia bungeni?

Kweli sasa naanza kupata mantiki ya wale uvccm wa mkoa wa pwani waliosema kwamba nyinyi mmshakula mpaka mmevimbiwa sasa ni zamu yao kula, ni kweli naamini na wewe umevimbiwa.
kama unataka kuja kuwa kiongozi hapa nyumbani na mtazamo huo nakushauri endelea kubeba box tu huko huko na maisha yakikushinda ni bora uje kuwa moderator hapa JF.
umenisikitisha sana, selfishness mind.

- Yaaani mkuu kwa sababu tu mawazo yangu hayakubaliani na yako on the ishu, basi ndio kunirushia mahukumu yote haya as if nimeua mtu, sasa nyinyi Chadema kweli mkishika hili taifa kweli itakuwaje? I mean kila mwananchi ni lazima afikirie kama mnavyofikiria tu akiwa tofauti basi anataka ubunge, amevimbiwa, ni fisadi, abebe mabox tu, selfish mind, mkuu wangu ndio maana ninakiogopa sana hicho chama! Duh!

Ww kijana wa Kwiro jibu maswali acha blah blah.
 
Mkuu,

Long term solution kwa tanzania ni kwamba kuwapo na utaratibu wa kusimamia vizuri matumizi ya pesa za umma. Hata huko marekani kila pesa huwa inasimamiwa vizuri na ndio maana Senator wako mmoja anaitwa Edward sasa jasho linamtoka kwa kutumia hela za umma vibaya hivyo basi utaratibu huo ndio unaotakiwa sasa hivi Tanzaniai. Unaposema mtu ujira wake alipwe ujira anaostahili na sio ufisadi wa kiidara. Mfano unapomlipa mbunge posho ya kuwa mbunge halafu hapo hapo unamlipa mshahara wa ubunge huo ndio ufisadi wa kiidara. Pia kila kikao unamlipa kwa kuhudhuria kikao wakati ndio kazi yake. Wewe ukiajiriwa kazi huko ulaya unalipwa mshahara wa kuwa mfanyakazi na sio na posho ya kuwa mfanyakazi.

Tabia hii ndio inachangia kuwapo kwa matumizi makubwa serikalini. Kukuwa kwa matumizi makubwa serikali kunaharibu ukuaji wa uchumi kwa kupitia kodi, ushuru kwani mapato ya serikali hutokea katika kodi na ushuru. Serikali ikiwa na matumizi mazuri ya kodi basi na uchumi nao unakuwa vizuri venginevyo uchumi utakua na maskini vile vile wataongezeka nchini.

- Kama ninakuelewa vizuri hapa unaongelea the enforcement of the poshos rules, sio viwango vya ajira as of the ishu at hand!, they have nothing to do with each other!

William @ NYC, USA.
 
Malecela na Lole lenu ni moja tu. Mna haki ya kukataa hoja hii lakini argument yenu is completely crap hadi inanichefua. How could you support this kind of very an informal spending ambapo hata serikali yenyewe haina control nayo? kama issue ni motivation why dont we adopt private sector policy? kwani huko kuna sitting allowance? lakini mbona watu ndiko wanakopendelea kufanya kazi tena kwa ufanisi zaidi.
Suala la Lukuvi kusema Zitto kapersonalise haina tija coz wengine wanasikika wakisema hizo allowance ziko kisheria, what sheria? sheria ndio kitu gani??? wanaotunga sheria ni akina nani?? plz msinisababishie hasira za kutukana hapa.
 
- Yaaani mkuu kwa sababu tu mawazo yangu hayakubaliani na yako on the ishu, basi ndio kunirushia mahukumu yote haya as if nimeua mtu, sasa nyinyi Chadema kweli mkishika hili taifa kweli itakuwaje? I mean kila mwananchi ni lazima afikirie kama mnavyofikiria tu akiwa tofauti basi anataka ubunge, amevimbiwa, ni fisadi, abebe mabox tu, selfish mind, mkuu wangu ndio maana ninakiogopa sana hicho chama! Duh!

William @ NYC, USA.

Kwanza mkuu mimi sio CHADEMA ila siwezi kuisupport CCM over my dead body, lakini Willy sikutegemea mtu kama wewe kuja na hoja za kipuuzi kama hizi, sina haja ya kukuorodheshea maslahi ya wabunge nina uhakika unayafahamu vizuri ndio maana umevutiwa na hiyo ajira unayoinyemelea, mimi nasema huku ni kuvimbiwa ndio maana hujui kwamba Mtanzania wa kawaida anaishi kwa chini ya dolla 1.
Hivi hizo shillingi 70,000/= zikiondolewa wabunge watakosa nini? ni kwa nini wabunge walipwe sitting allowance? na ni kwa nini wananchi wasilipwe listen allowance?
By the way,Willy haujajibu maswali yangu katika bandiko langu la kwanza hapo juu.
 
Malecela na Lole lenu ni moja tu. Mna haki ya kukataa hoja hii lakini argument yenu is completely crap hadi inanichefua. How could you support this kind of very an informal spending ambapo hata serikali yenyewe haina control nayo? kama issue ni motivation why dont we adopt private sector policy? kwani huko kuna sitting allowance? lakini mbona watu ndiko wanakopendelea kufanya kazi tena kwa ufanisi zaidi.
Suala la Lukuvi kusema Zitto kapersonalise haina tija coz wengine wanasikika wakisema hizo allowance ziko kisheria, what sheria? sheria ndio kitu gani??? wanaotunga sheria ni akina nani?? plz msinisababishie hasira za kutukana hapa.

- Duh! What a genius!

Willie @ NYC, USA.
 
Kwanza mkuu mimi sio CHADEMA ila siwezi kuisupport CCM over my dead body, lakini Willy sikutegemea mtu kama wewe kuja na hoja za kipuuzi kama hizi, sina haja ya kukuorodheshea maslahi ya wabunge nina uhakika unayafahamu vizuri ndio maana umevutiwa na hiyo ajira unayoinyemelea, mimi nasema huku ni kuvimbiwa ndio maana hujui kwamba Mtanzania wa kawaida anaishi kwa chini ya dolla 1.
Hivi hizo shillingi 70,000/= zikiondolewa wabunge watakosa nini? ni kwa nini wabunge walipwe sitting allowance? na ni kwa nini wananchi wasilipwe listen allowance?
By the way,Willy haujajibu maswali yangu katika bandiko langu la kwanza hapo juu.

- Well, mkuu ukimaliza hizi hukumu against mawazo yangu, nifahamishe ili tuweze kujadili tena taifa, maana naona badala ya taifa wewe so far una tatizo na mimi mtoa maoni badala ya maoni yenyewe, haya ukimaliza matusi yako na hizo hukumu, nifahamishe!

William @ NYC, USA.
 
Hivi mmeshagundua kwa nini viongozi wengi wanaoishi kwa hizi allowance, mara wakiacha kazi huwa wanakufa haraka?

Hii kitu inalemaza sana. Hizi pesa hata wake zao nyumbani hawazioni na ndiyo maana Dodoma imeshamiri UFUSKA.

Hizi pesa zinaongeza tu magonjwa ya ajabu na anasa pale Dodoma. Wengi sana wamelisema hili hapa JF.

Watu wanalalamika kuwa vikao vikianza, chunga sana Mkeo au Girlfriend wako.

Pia kwa sababu posho hazikatwi kodi, wafanyakazi huwa wanaishi maisha ya juu sana na siku akiacha kazi aanze kuzipwa hela za uzeeni, unakuta maisha yanawashinda kabisa. Na ndiyo maana wengi sana hufa within 5 years tangu waache kazi.

Mtani wangu Willy, acha kuendekeza hiki kilema kwa hawa watu. Acha miashahara ipande sana tu. Ikibidi Mbunge apate hata 5.M kwa mwezi na akiacha kazi, akiba yake itakuwa nono sana na ataendelea kuishi maisha karibu sana na aliyokuwa akiishi zamani.

Ndiyo maana unaona hata pesa za kutibiwa huwa hawana mara wakiacha kazi. Watu kama Mrema alikuwa kaishiwa kabisa maana watoto kibao. Kuna yule mama wa CCM alitokea kwenye magazeti akiwa hoi kitandani na huku hana hela ya kutibiwa. Mifano ipo mingi sana...... Hiki kilema unachotaka kiendelee, kinawauwa wao na kuliuwa Taifa kwa ujumla.

Ngoja siku ifike na Tanzania iwe kama Wagiriki. Wanakula zaidi ya wanavyozalisha............... Anytime watatangaza nchi IMEFILISIKA. Na sijui sasa hao wataalamu wako unaotaka walipwe sana tutaona kama wataendelea kubaki.....

- Duh!

Willie @ NYC, USA.
 
Mkuu nimekusoma na nilivyokuelewa ni kwamba hujamuelewa MHE. ZITTO. Posho zinazofutwa ni sitting allowance. sasa tujiulize hizi sitting allowance wanalipwa wafanyakazi wote wa kila kada? kiuhalisia posho hizi zinaishia kwa Makatibu Wakuu, Wakurugenzi na wajumbe wa Bodi, kwenye vikao vya menejimenti na tender board!! Hivi ni lini, walimu, maaskari, manesi, madereva na wahudumu nao watakaa vikao walipane posho? sasa unamlipa posho ya kikao mkurugenzi wakati hiyo ndiyo kazi yake ya kujadili na kupitisha maamuzi hapohapo analipiwa nyumba, gari au mafuta ya gari, simu maji umeme na mshahara juu na unamuongezea na posho!!! hii si haki hata kidogo!!

Wataalam wanaondoka, si wakurugenzi, ni wataalam wa kawaida, anaona ametumia muda mwingi kusoma, mshahara mdogo, halafu wengine wanalipana maposho tu!! umeshasikia mkurugenzi yoyote kaacha kazi tanzania eti kwa sababu ya maslahi madogo? huwezi kumkuta. Sasa kwa mujibu wa zitto anasema ni bora hizo posho za vikao zifutwe, then ziongezwe kwenye mishahara ya watumishi, kuanzia wahudumu madereva mpaka maafisa wa juu. Kima cha chini cha 350,000/- kinawezekana. Maana kwa mujibu wa bajeti posho hizi jumla yake yote kwa mujibu wa bajeti ni billion karibu 900.

Unafikiri William hajaelewa au anataka kusikia maoni ya hapa Jamvini? Kwa uelewa wake hasa kutokana na ufuatiliaji wa issues na hoja kadhaa hapa kwenye jamvi naamini kabisa upeo wake ni mkubwa mno wa kuielewa hii hoja ila naona kama anafanya makusudi mazima....
Mnatikiswa kwa hiyo hoja halafu mnatikisika... Sio toka kwa William, labda ingekuwa Nape au baadhi ya wabunge waliokuwa huko Dodoma but not William at all...

@ William, acha kuwachemsha watu.... Wananchi waha hasira sana na mambo mengi, sasa kuleta mizaha kama hii ndio utaishia kutukanwa na kukashifiwa for no good reason while knowing what you are up to
 
- Well, mkuu ukimaliza hizi hukumu against mawazo yangu, nifahamishe ili tuweze kujadili tena taifa, maana naona badala ya taifa wewe so far una tatizo na mimi mtoa maoni badala ya maoni yenyewe, haya ukimaliza matusi yako na hizo hukumu, nifahamishe!

William @ NYC, USA.

Mkuu sioni kama kuna sehemu ambayo nimekutukana, na bado nasisitiza i value to differ lakini hii thread ni ya kipuuzi kabisa, na hizi ni dalili za wazi za kuvimbiwa.
Na kuhusu Taifa huna hoja yoyote kwa leo ya kujadili kuhusu Taifa. Nakushauri nenda kapige box tu saa hizi maana @ New York, sasa hivi ni asubuhi, usije ukatuchefuwa bure hapa jamvini.
 
Jamaa anakuja kugombea ubunge 2015 kule mtera kumnyanganya yule mchungaji, sasa mkitoa posho yeye pesa atakazotumia kwenye kampeni walizozibatiza jina la "TAKRIMA" zitarudije?

Kama vijana wa CCM ndiyo hawa, wenye mawazo na hoja zao kama ni hizi, na navyojua mimi nguzo cha chama chochote cha siasa ni vijana, basi CCM - kwisha habari...Kwisha habari...

Ngoja nihamie kwa NAPE nione naye kaandikaje kuhusu hotuba ya Upinzani kama nitapata chochote cha kuondoka nacho ...... baadaye kidogo.
 
Unafikiri William hajaelewa au anataka kusikia maoni ya hapa Jamvini? Kwa uelewa wake hasa kutokana na ufuatiliaji wa issues na hoja kadhaa hapa kwenye jamvi naamini kabisa upeo wake ni mkubwa mno wa kuielewa hii hoja ila naona kama anafanya makusudi mazima....
Mnatikiswa kwa hiyo hoja halafu mnatikisika... Sio toka kwa William, labda ingekuwa Nape au baadhi ya wabunge waliokuwa huko Dodoma but not William at all...

@ William, acha kuwachemsha watu.... Wananchi waha hasira sana na mambo mengi, sasa kuleta mizaha kama hii ndio utaishia kutukanwa na kukashifiwa for no good reason while knowing what you are up to

- Kwa hiyo unasema kwamba wewe kwa kuogopa kutukanwa na kukashifiwa, ndio maana unafuata tu upepo wa bendera? Na unashauri na mimi niwe hivyo?

William @ NYC, USA.
 
Mkuu sioni kama kuna sehemu ambayo nimekutukana, na bado nasisitiza i value to differ lakini hii thread ni ya kipuuzi kabisa, na hizi ni dalili za wazi za kuvimbiwa.
Na kuhusu Taifa huna hoja yoyote kwa leo ya kujadili kuhusu Taifa. Nakushauri nenda kapige box tu saa hizi maana @ New York, sasa hivi ni asubuhi, usije ukatuchefuwa bure hapa jamvini.

- Duh! what a great thinking!

William @ NYC, USA.
 
Back
Top Bottom