Ahsante mheshimiwa Zitto, lakini huyo ni mbuzi kwenye gunia!

Wakati ambapo bajeti yetu ni tegemezi kiasi cha kushindwa hata kugharamia matumizi ya kawaida 100% kutoka pato letu la ndani bado kuna watu wanapiga kelele kutetea huu ulaji!!
Si bure tumerogwa......
 
bwana willy gamba (ni sifa kubwa kukufananisha na mtunzi maharufu)

kuna tofauti kati ya haya maneno mawili, posho na mshahara. Natumaini unaelewa hoja zitto kuwa ni posho na sio mshahara lakini wewe umeamua kuvichanganya pamoja sijui kama huelewi utofauti wake au ni kwa maksudi kabisa.

kuna pande mbili hapa kwenye hizi posho moja ikiwa bunge na nyingine serikalini.

bunge
Wabunge tiyari wanalipwa mishahara mizuri na ambayo ni ya juu kufanya kazi zao, kwa hiyo hii hoja ya kusema wabunge wanamshahara mdogo haipo. watu wanacholalamika ni juu ya posho wanazolipwa ilihali mishahara yao ni mikubwa tiyari. kwa nini wapewe posho wakati mishahara yao inajitosheleza, zitto hataki posho kwa ajili mshara unatosha. Ukiondoa posho wabunge watabakia kuwa ni watu wanaolipwa mshahara wajuu na sio wachini kama unavyotaka watu waamini.

serikalini/watumishi wa umma

watumishi wa umma wamegawanyika katika makundi mawili, wajuu na wakati kwenye kundi moja na wa chini ambao ndio wengi kwenye kundi jingine. watumishi wote wa serikali wana tatizo moja nalo ni mshahara mdogo.
wakati kundi la chini ndio ambalo linagoma kutaka kuongezewa mishahara kundi la juu haligomi ilihali mishahara yao nayo ni midogo. Hii inatokana na ukweli kwamba kundi la juu pamoja kuwa na mishahara midogo take home yao imekua ikiongezeka mwaka hadi mwaka kutokana na posho zao kuongezeka mwaka hadi mwaka. ukijumlisha posho na mishahara unakuta watu wa juu wanawanyonya sana watu wa chini, sina maana mishahara yao au total ya kipato chao kilingane hapana bali kuwe kuna fair pay kutokana na position mtu aliyenayo kazini na sio wingi wa vikao utakavyofanya.
wafanyakazi wakundi la chini hawapati kuhudhuria vikao lakini sio kama hawafanyi kazi, wafanyakazi wengi wa juu wao wanchofikiria ni idadi ya vikao atakavyohudhuria ambavyo vitamlipa na sio majukumu yake mengine ya kazi.
ukifuta posho wafanyakazi wa chini wataweza kuongezewa mishahara sambamba na wafanyakazi wa juu, uta creating level playing field.
leo hii mfanyakazi wa kati hawezi kumpinga bosi wake kwa ajili ataondolewa kwenye list ya watu wanaotakiwa kwenda kwenye vikao.

kuna mtu mmoja nadhani smu amesema kitu kimoja muhimu sana, posho zinawaathiri sana hawa watumishi wakistaafu. kwa ajili mishahara yao ni midogo na 10% contribution yao ya penshion ni ndogo, akistaafu unamsikia akilalamika pension yake ni ndogo simply because alikuwa anakula posho nyingi na mshahara mdogo.

tunachotaka ni kwamba total income yako itokane na position yako kazini na sio idadi ya vikao utakavyohudhuria. mbali na posho wanazolipwa wabunge bado mshahara wao ni mkubwa.
 
Mkuu @New York City; US.

Tatizo ni kwamba hizo Posho zinawafaidisha watu wachache sana
 
Kwa wale wapigia debe posho kama wanazihitaji sana basi waongeze mishahara ya watumishi wa umma halafu wafute posho. Tatizo la posho ni sehemu mbili:-
a. Hazikatwi kodi.
b. Zinalipwa kutokana na kazi nyengine ambazo umepewa katika job description yako.

Chukulia mfano mshahara wa mbunge ni Milioni 2.5 halafu mbunge huyo huyo hulipwa kila mwezi posho ya ubunge ya milioni 5 (wakati analipwa mshahara wa kuwa mbunge wa milioni 2.5). Posho hii pengine hata katika kodi haikatwi. Weka na posho za kikao cha bunge (kazi ambazo ndio mbunge anatakiwa kuzifanya). Unakuta mbunge anapata karibia milioni 12.5

Sasa tujadili ajira ya kawaida je wanalipwa hivyo hivyo. Tutolee mfano mwalimu wa primary analipwa Shs 400,000 . Kwa mantiki ya mshahara wa wabunge inabidi nao tuwawekee posho ya kuwa mwalimu kama Tshs 500,000, ikisha tuwawekee posho kila vikao wanavyokaa kujadili maendeleo ya wanafunzi. Matokeo ya mwenendo kama huu ni kuongeza ukubwa wa matumizi ya serikali na kupelekea serikali kufilisika!!!! Wabunge na washabiki wa CCM endeleeni kupigia debe kwani kufilisika kwa nchi sasa sio jambo la ajabu (mifano hai ipo kama ugiriki na ureno). Tanzania tukijisahau ndiko tunakoelekea na kasi hii ya kukopa. Jilipeni maposho manono ila muwepo tu wakati wa kulipa madeni ya nchi tu!!!!
 
Kutetea posho kwa misingi ya kwamba tutapoteza wataalam ni kupotosha. Hakuna anayesema wataalam wasilipwe vizuri, tunapenda tulipwe vizuri. lakini sio posho. Tatizo la posho ni kwamba inawahusu watu wachache tena wa juu na linaua morali ya kufanya kazi maana semina ni za kujuana.Kama huna urafiki au ukaribu na bosi wako inabidi usahau kupata posho. Kuna kazi kama za ualimu, hawa lini wanapewa posho? Kitu cha msingi ni kuboresha mshahara na maslahi mengine ambayo ni rasmi kama nyumba, matibabu, nauli wakati wa likizo n,k-yaani vitu ambavyo kila mtu atapata bila kujipendekeza kwa bosi.

Katika taasisi nyingi za serikali, kinachoangaliwa ni posho halafu ndio kikao au semina. Nina maana, semina zinatafutwa ili kupata posho na sio maarifa. Sio ajabu kukuta mtu mmoja amehudhuria semina ya ukimwi mara 4 kwa mwaka. Sasa kipi kisichoeleweka kuhusu ukimwi? Watu walipwe mishahara mizuri, ndipo tutaweza kuwa-retain. Kila mwaka mshahara wa mwalimu na askali unaongezwa, lakini wanaongeza elfu nne(4,000) mpaka kumi (10,000) na hawa hawapati posho-haya sio matusi?

Tatizo la posho za wabunge ni kwamba,hayo wanajipangia wenyewe na rais anapitisha. Rais lazima apitishe maana naye hapendi serikali yake ikimbizwe mchakamchaka (kama wa Richmond) na wabunge.Hawaandamani kama TUCTA na CWT kudai haki zao. Wanajiongezea mara kwa mara kadiri wanavyoona inafaa na hamna wa kuwaambia jamani nchi yetu ni maskini, mnachodai hakiendani na hali yetu. Lakini pia, ukishapewa per diem kwakuwa umesafiri na upo kwenye kikao dodoma, posho za kikao ni za nini?
 
Ndugu yangu pamoja na hoja zako nzuri, lakini tukubaliane kwamba kama hawa hawa waliopo kwenye uongozi ndio wanashindwa kusimamia hizo sheria zilizopo na at the same time wanatumia nafasi hizo hizo kujihalalishia posho haramu. Kwa mfano kwenye halmashauri fulani hapa nchini, unakuta mtu mmoja anaandikwa kwenye warsha 3 hadi 5 kwa siku au wiki. Kwamba unakuta wiki moja kuna semina 3 tofauti, watu wa ardhi, watu wa idara ya elimu na wana semina yao, Mazingira nao, n.k. Hapo unakuta treasurer anaandikwa kwny hizo semina zote na asipoandikwa anakuwa na turufu ya kukubali kwamba semina hii ina posho au la! Na kingine unakuta wahudhuriaji hapa ni wale wale wa level moja/fulani siku zote, je wale ambao wako marginalized na huu mfumo haramu wako condemned to abysmal poverty?

- Well, people tusiwaruhusu viongozi wetu kutu-limit our Natioanl scope kwa kuangalia short terms political solutions, Tanzania ni bigger than hawa viongozi wetu, sasa wasitu-short site na kutufikisha kwenye quick reactionary political solution kwa masuala muhimu kama ya uchumi wa taifa which kwa maoni yangu is the heart also ya hoja ya Zitto, tutafute majibu magumu ambayo ni long term National solution, kama viongozi hawawajibiki kwenye kusimamia sheria za uchumi makazini, siamini solution ni kupunguza ujira as I understand to be your concern here mkuu!

- Tufikirie solutions ambazo zinatakuwa ni good kwa taifa for the next 100 years, sio tu good kwa ajili ya uchaguzi wa Rais 2015!

William @ NYC, USA.
 
- Well, people tusiwaruhusu viongozi wetu kutu-limit our Natioanl scope kwa kuangalia short terms political solutions, Tanzania ni bigger than hawa viongozi wetu, sasa wasitu-short site na kutufikisha kwenye quick reactionary political solution kwa masuala muhimu kama ya uchumi wa taifa which kwa maoni yangu is the heart also ya hoja ya Zitto, tutafute majibu magumu ambayo ni long term National solution, kama viongozi hawawajibiki kwenye kusimamia sheria za uchumi makazini, siamini solution ni kupunguza ujira as I understand to be your concern here mkuu!

- Tufikirie solutions ambazo zinatakuwa ni good kwa taifa for the next 100 years, sio tu good kwa ajili ya uchaguzi wa Rais 2015!

William @ NYC, USA.

Mkuu,

Long term solution kwa tanzania ni kwamba kuwapo na utaratibu wa kusimamia vizuri matumizi ya pesa za umma. Hata huko marekani kila pesa huwa inasimamiwa vizuri na ndio maana Senator wako mmoja anaitwa Edward sasa jasho linamtoka kwa kutumia hela za umma vibaya hivyo basi utaratibu huo ndio unaotakiwa sasa hivi Tanzaniai. Unaposema mtu ujira wake alipwe ujira anaostahili na sio ufisadi wa kiidara. Mfano unapomlipa mbunge posho ya kuwa mbunge halafu hapo hapo unamlipa mshahara wa ubunge huo ndio ufisadi wa kiidara. Pia kila kikao unamlipa kwa kuhudhuria kikao wakati ndio kazi yake. Wewe ukiajiriwa kazi huko ulaya unalipwa mshahara wa kuwa mfanyakazi na sio na posho ya kuwa mfanyakazi.

Tabia hii ndio inachangia kuwapo kwa matumizi makubwa serikalini. Kukuwa kwa matumizi makubwa serikali kunaharibu ukuaji wa uchumi kwa kupitia kodi, ushuru kwani mapato ya serikali hutokea katika kodi na ushuru. Serikali ikiwa na matumizi mazuri ya kodi basi na uchumi nao unakuwa vizuri venginevyo uchumi utakua na maskini vile vile wataongezeka nchini.
 
Nimesikitishwa sana na mtoa hoja malecela juu ya dhana hii ya posho kwa watumishi wa umma. Nadhani hajaiangalia kwa kina au ameangalia ki misingi ya kisiasa zaidi kwa kuwa imetolewa na Zitto, CDM!! Zitto (Mhe.) anakubakiana na dhana ya kuboresha masilahi ya watumishi wote wa umma-mishahara! Anapinga kulipana posho kwa watumishi wa umma hususan viongozi wa juu kwa kazi ambazo ndo majukumu yao; na kuacha wafanyakazi wengine (polisi, walimu, madakitari, wauguzi, ma bwanashamba,usala wa taifa n.k) wakiwa hawana posho ili hali nao hufanya vikao vingi tu vya kazi zao pasina kulipwa posho. Wabunge wanatumia uweO wao wa kupisha au kutunga sheria kujilimbikizia wenyewe na hivyo kuwafanya viongozi wengine seriakli (mawaziri, makatibu wakuu, wakurugunzi wa idara,wakuu wa mikoa/wilaya, nk) kutumia mwanya huo nao kujilipa kila wanapokuwa na vikao vyao vya kazi za kila siku. Hawa ni wachache sana katika asilimia ya wafanyakazi wa tanzania, bali wanachukuwa kiwango kikubwa cha fedha za umma kwa posho, ambacho kama kingetumika vema wangeweza kupandisha masilahi ya wafanyakazi wote wa umma kwa kiwango kikubwa (kumbuka posho katika budget hii ni karibu 25% ya budget). Hii ndo argument ya Zitto (mhe.) posho zote zifutwe na ikiwezeka zielekezwe kuboresha masilahi ya wafanyakazi na shughuli zingine za maendeleo ya nchi. Kama ni lazima kulipana posho wabunge na viongozi wa juu; basi kuwe na posho kwa kila mtumishi ya kazi yake (staffic-standing allowance-akiwa kwenye jua mchana kutwa; mwalimu-teaching alllowances; nurse; caring allowances, n.k ya kila siku wafanyazo kazi!!!!!!!!! Hoja siyo kupunguza masilahi ya watu, bali kutotoa mwanya kwa wachache wenye mamulaka kufaidi keki ya taifa peke yao kwa masilahi yao wala si ya watanzania, period!!

- Unapaswa kusikitishwa na hoja yangu sio mtoa hoja, HOWEVER; kama taifa letu tunataka kufuata Demokrasia ya kweli huwezi kupunguza poshos za wabunge ukaacha za watumishi wengine kwenye taifa, kama ninakuelewa kilio chako ni kile kile cha wananchi wengi on this ishu kwamba usmamiaji wa sheria za posho makazini, now that has nothing to do na viwango ambavyo mimi nido hasa ninaposiamamia, huu ujira tumetoka nao mbaali sana hili taifa mpaka kuufikisha hapa ulipo, ninakataa hoja ya aina yoyote ile inayoshauri kurudi tena kule tulikotoka zamani, tunatka kusonga mbele! Kugusua ujira sasa ni kuigusa The Middle Class, we can't afford that for the good of our our future as a nation!

- Kukimbilia ajira as solution to our problems ni kutafuta majibu mepesi kwa ajili ya maswali magumu sana!


William @ NYC, USA.
 
Toto la fisadi at work. huna point wewe. wangesema hao CCM, usingesema maneno hayo. ungewasupport 100%. Akili topetope. Wewe ngoja tukichukua nchi, nyinyi wasaliti tutawashughulikia tu. I hate you.

- Ni mambo ya territory, karibu sana mkuu!

Willie @ NYC, USA.
 
Ningependa mishahara ya watumishi wa umma iboreshwe,posho zote zifutwe kabisa.
 
Mkuu William,
Katika hili ninatofautiana na wewe kwa 100%. Kwanza naona mada ya posho kwako ni msamiati unaodhihirisha welfare (Flourishing life eg labda kwa mbunge, etc). Lakini ukiangalia hili suala la posho Mfano kwa wabunge, linapelekea kuwa na ushindani wa hali ya juu katika kugombea kwani mtu anaona kuwa akipata ubunge basi malupulupu ni mengi including POSHO. Hii inapelekea kuingia kwenye ubunge hata watu wasiokuwa na dhamira ya kweli ya kutetea wananchi Mfano Mbunge wa Kahama-Lembeli. Na pia hili hili suala watu wanafanya kila mbinu kusacrifice chochote (mfano kulogana a.k.a uchawi a.k.a ndumba) ili mtu awe mbunge kwa sababu kuna mshiko mkubwa. Kwa ufupi wabunge wengi kuwa ni wauza sura, njuka (Halima Mdee), yaani wengi wao utakuta wapo pale kwa ajili ya posho tu. Ila endapo mfano utitiri wa posho ukipunguzwa na watu kweli wawe accountable kwa kazi zao, basi lile wimbi la maprof, ma Dr, wenye tamaa na utajiri wa haraka hawataingia bungeni, bali tutapata watu wenye uchungu na wananchi. Na hapa nimechambua upande mmoja tu, sijasemea kuhusu kuprioritize gov expenditure Mfano mabweni shule za kata, maji vijijini n.k.
Kwa hiyo kaka hili suala ni multifaceted, na siyo ujamaa kwani hili ni suala la accountability kwa wafanyakazi wa umma.

- Ningeelewa kama tungetaka wabunge wasiokuwa active katika kuwakilisha wananchi waliowachagua basi wawe wanapunguziwa ujira, labda ningeelewa, lakini kupunguza ujira eti ni mwingi sana, pleaase!

William @ NYC, USA.
 
- Unapaswa kusikitishwa na hoja yangu sio mtoa hoja, HOWEVER; kama taifa letu tunataka kufuata Demokrasia ya kweli huwezi kupunguza poshos za wabunge ukaacha za watumishi wengine kwenye taifa, kama ninakuelewa kilio chako ni kile kile cha wananchi wengi on this ishu kwamba usmamiaji wa sheria za posho makazini, now that has nothing to do na viwango ambavyo mimi nido hasa ninaposiamamia, huu ujira tumetoka nao mbaali sana hili taifa mpaka kuufikisha hapa ulipo, ninakataa hoja ya aina yoyote ile inayoshauri kurudi tena kule tulikotoka zamani, tunatka kusonga mbele! Kugusua ujira sasa ni kuigusa The Middle Class, we can't afford that for the good of our our future as a nation!

- Kukimbilia ajira as solution to our problems ni kutafuta majibu mepesi kwa ajili ya maswali magumu sana!


William @ NYC, USA.


Mkuu,

Watumishi wa umma wanaweza kuongezewa mshahara wakaondolewa posho hilo litasaidia kwanza kuongeza pato la kodi la nchi (kwani PAYE na contribution nyenginezo zitaongezeka), pia itasaidia kuwaweka wataalamu unaohofia kukimbia. Hata hivyo unapowalipa mshahara vile vile utafuta posho zisizo na msingi kama vikao. Nitakupa mfano wakurugenzi wa BOT hulipwa posho za kikao zinasemekana ni nono. Vile vile kama wakurugenzi wanapokea karibia milioni 11 kama mshahara (sina uhakika but watu wa chini yao ndio wanavyodai ni mshahara wao). Sasa mkurugenzi wa BOT analipwa mshahara wa milioni 11 halafu hapo hapo kila kikao analipwa posho nono ya karibia milioni 1 sasa huoni huo ni ufisadi!!!!! Utamlipaje mkurugenzi allowance ya kikao wakati katika job description yake inasema pia atakuwa anahudhuria kikao cha idara au bodi????

Middle class wanatengenezwa na kuwapo na viwanda vya kutosha, elimu na mzunguko wa fedha na sio mishahara kama unavyodai. Posho zilizopo zinatengeneza sio middle class bali concentration katika uchumi ambapo kuna watumishi wa umma ni matajiri wa kutupwa wakati watanzania wengine wengi ni maskini mno. Tungelikuwa na viwanda vya kutosha, elimu kwa vijana wetu tungeliweza kuzalisha middle class, sio sasa unemployment amongst graduate is more than 20%, amongst youth ni 70% halafu unasema posho zinasaidia kutengeneza middle class I beg differ my comrade!!!
 
Sina wasi wasi kwamba SOONER RATHER THAN LATER,Wale wabunge wanaoshabikia posho zibaki watakumbana na ZOMEA ZOMEA MAJIMBONI MWAO.Ni suala la muda tu,watu wakiielewa hoja hii Nyie akina MREMA etal mnaozipigia chapuo mtakosa kukubalika,JIVUENI MAGAMBA MAPEMA.JOIN ZITO UPESI na tusaidieni kufutilia mbali dhana ya POSHO ati kuboresha maisha ya mfanyakazi,mshahara ndo uboreshwe.COME ON!

- Mkuu kuna historia moja ndani ya serikali yetu inayomuhusu kiongozi mmoja alikuwa juu sana kwenye awamu ya kwanza, kwenye kikao kimoja cha Cabinet wajumbe wengi walilalamika sana kwamba penshion ya Viongozi wa juu ya wakati ule mbele ya safari ya maisha itakuwa ni ndogo sana, yule kiongozi akapigana kufa na kupona kukataa zisiongezwe, yeye alipostaafu mpaka sasa posho yake ni Shillingi 50, 000, sina sababu ya kukueleza maisha ya sasa ya huyu kiongozi, ndio faida ya kulilia short term solution kwa maswali magumu!

William @ NYC, USA
 
- Unapaswa kusikitishwa na hoja yangu sio mtoa hoja, HOWEVER; kama taifa letu tunataka kufuata Demokrasia ya kweli huwezi kupunguza poshos za wabunge ukaacha za watumishi wengine kwenye taifa, kama ninakuelewa kilio chako ni kile kile cha wananchi wengi on this ishu kwamba usmamiaji wa sheria za posho makazini, now that has nothing to do na viwango ambavyo mimi nido hasa ninaposiamamia, huu ujira tumetoka nao mbaali sana hili taifa mpaka kuufikisha hapa ulipo, ninakataa hoja ya aina yoyote ile inayoshauri kurudi tena kule tulikotoka zamani, tunatka kusonga mbele! Kugusua ujira sasa ni kuigusa The Middle Class, we can't afford that for the good of our our future as a nation!

- Kukimbilia ajira as solution to our problems ni kutafuta majibu mepesi kwa ajili ya maswali magumu sana!


William @ NYC, USA.

Willy vp kaka! Wewe umeshaambiwa kuwa zikifutwa kwa hawa wafanyakaz wa chini mishahara yao itaongezwa na hii itawasaidia hata watakapokuja kustaafu kwa kupata mafao mazuri.
Mbona unatetea uovu na ufisadi mtu wangu! Hv humuonei huruma mwalimu anaelipwa 180,000 (laki moja na themaninini t. shs) huku ana mke na watoto wawili. Hv kweli mwalimu huyu anatendewa haki kwa ujira anaopewa? Je mwalimu hana umuhimu katika taifa?
Kuwa mzalendo Willy japo baba yako amenufaika na hizo posho na ndio zimekusomesha pale Kwiro ila usizitee. Otherwise na ww nitakuweka kundi moja nachumia tumn wa magamba tu!
 
- Unapaswa kusikitishwa na hoja yangu sio mtoa hoja, HOWEVER; kama taifa letu tunataka kufuata Demokrasia ya kweli huwezi kupunguza poshos za wabunge ukaacha za watumishi wengine kwenye taifa, kama ninakuelewa kilio chako ni kile kile cha wananchi wengi on this ishu kwamba usmamiaji wa sheria za posho makazini, now that has nothing to do na viwango ambavyo mimi nido hasa ninaposiamamia, huu ujira tumetoka nao mbaali sana hili taifa mpaka kuufikisha hapa ulipo, ninakataa hoja ya aina yoyote ile inayoshauri kurudi tena kule tulikotoka zamani, tunatka kusonga mbele! Kugusua ujira sasa ni kuigusa The Middle Class, we can't afford that for the good of our our future as a nation!

- Kukimbilia ajira as solution to our problems ni kutafuta majibu mepesi kwa ajili ya maswali magumu sana!


William @ NYC, USA.

@New York, USA
, naomba usiskip ili swali langu ningepependa unijibu kiufasaha.
1. kwa miaka hii 10 umewahi kukaa Tanzania kwa siku ngapi? ukijurimsha vizuri ushindwi kunipa jibu.
2. umejiridhisha kabisa unachokipinga ni kipi?
3. unakumbuka wakati wa mtikisiko wa uchumi diuniani Kansela wa Ujerumani aliamuru serikali yake ibane matumizi?
4. una nia ya kuja kugombea ubunge Tanzania? kama jibu ni ndio kwahiyo inakuuma ulaji unaanza kupunguzwa kabla ujaingia bungeni?

Kweli sasa naanza kupata mantiki ya wale uvccm wa mkoa wa pwani waliosema kwamba nyinyi mmshakula mpaka mmevimbiwa sasa ni zamu yao kula, ni kweli naamini na wewe umevimbiwa.
kama unataka kuja kuwa kiongozi hapa nyumbani na mtazamo huo nakushauri endelea kubeba box tu huko huko na maisha yakikushinda ni bora uje kuwa moderator hapa JF.
umenisikitisha sana, selfishness mind.
 
Uliyoyaandika hapo embu jaribu kusoma mwenyewe then utaelewa wapi ulipokosea

Ndugu yangu mada zako sometimes huwa zinakingana zenyewe ndo hapo huwa nashindwaga kuzielewa nimekuwa mfatiliaji wa jamii forums daily lakini
sichangiagi kutokana na kwamba mada nyingine ni kuchafuana na mambo mengine ni ushabiki usio wa msingi.

Malecela hoja yako iyo ya kusema posho zisipunguzwe elewa kwanza pendekezo la zito lielewe na usikurupuke kama Nape huwa haelewi anakurupakaga nini na kuongea mabo then badae anabaki kimya anajishangaa mwenyewe

Huwa najiulizaga uelewa wa viongozi na makada wa CCM elimu zao na jamii wanazotoka mpaka leo sijapata jibu sijui mpaka sasa kama we mwenyewe ukikaa na kutafakari kama
kuna mwana CCM yeyote ambaye ana akili timamu kuanzia mwenyekiti hadi wanaoishabikia CCM nadhani wote wana ulakini na mambo yao so next time unapokua uanaandika kitu kisome kwanza then upost

- Duh! mkuu inaonekana una akili sana maana haya maneno ni lazima yameandikwa na a genius tu! heri yako mkuu sana! ila for a genius like you kupoteza muda kujibu watu kama mimi wasio na akili timamu, hebu iangalie tena hiyo mkuu imekaaje!

- Have a nice day!


William @ NYC, USA.
 
William unachokisema nadhan ni sawa kabisa. Lakini nadhani hujaelewa vizuri hoja ya Mh. Zitto, na ili uelewe vizuri jaribu kupitia hotuba yake ya bajeti. Mimi pia ntajaribu kukuelewesha kuhusiana na hoja yake hii ya posho.

Kwanza, Zitto anasema kuwa posho ya kikao (Sitting Allowance) haifai kulipwa kwa wabunge na watumishi wengine wa Umma. Kukaa vikao au kuhudhuria vikao vya Bunge na Kamati zake ni kazi ya msingi kabisa ya wabunge. Niambie ni vipi mbunge anaweza kutekeleza majukumu yake bila kuhudhuria vikao hivyo? Unamtenganisha vipi mbunge na vikao vya Bunge? Sasa Zitto anasema mbunge kuhudhuria vikao vya bunge ni kazi yake ambayo katika hiyo analipwa mshahara. Sababu ya yeye kulipwa tena posho ya vikao haipo kabisa na huo ndo ukweli.

Pili, Kwenye utendaji wa Umma, maamuzi hufanywa kupitia vikao na kufanya maamuzi ni jukumu la msingi la wakuu wa idara na taasis za Umma. Wanapofanya maamuzi hayo kupitia vikao hivyo wanatekeleza majukumu yao ya msingi kabisa katika nafasi zao. Fikiria pia kuwa wanalipwa mishahara mikubwa kwa kushika nafasi hizo. Sasa posho ya kukaa kikao cha kutekeleza majukumu yako inakujaje hapo?

Tatu, hoja ya kusema kuwa yeye ni mdogo na hajui nchi hii imetokea wapi sijui inatokea wapi. Lakini ni kawaida ya watu wasio na hoja kujaribu kutumia vitu visivyo vya msingi ili kuwadivert watu kutoka kwenye hoja ya msingi. Jiulize ni kwanini maprofesa, ma-doctor na wahadhiri wengine wanavyokimbilia kwenye siasa. Hapo achia mbali wahandisi, wahasibu, madaktari na wengine wote. Unadhani wote wanapenda kuwatumikia wananchi?

Nne, Nchi inabidi iondokane na ulipaji wa mambo yasiyokuwa na msingi ili fedha zitakazookolewa ziweze kuboresha maisha ya wananchi. Serikali imeshindwa kuwalipa watumishi kima cha chini cha 315,000 lakini inatenga 900 bilioni kwa ajili ya posho. Wataalam wa nje watakuja nchini kwa ajili ya maslahi mazuri na wala sio posho zisizokuwa na maana.

Tano, kwa upande wangu naona hata bei za bidhaa muhimu zinaweza kushuka baada ya posho kuondoshwa kwan sasa viongozi wetu watafanya maamuzi ambayo hata wao yatakuwa yakiwaumiza. Kwani wamekuwa hawaoni uchungu wa ongezeko la bei za bidhaa kwa sababu wao wana upenyo wa kupata fedha rahisi kupitia vikao.

Mwisho, Tujaribu kutoa mada ambazo zinalenga katika kuimarisha maisha ya wananchi wote. Nchi hii ni yetu sote na inatubidi wote tufaidike kutokana na matunda yake. Pia jaribu kuelewa hoja ya mtu pasipo kuwa na macho ya upendeleo. Tushirikiane katika kujenga nchi hii jamani.
 
Back
Top Bottom